Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya
miaka 17 ya Serengeti Boys wakishangilia bao lililofungwa na Mudathiri Yahaya
Abbas wakati timu hiyo ilipopambana na Congo Brazzaville katika mchezo wa
kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika
mwakani nchini Morocco. Serengeti Boys imeshinda 1-0. (Picha zote na Habari
Mseto Blog)
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Jacob Michelsen
na msaidizi wake Jamhuru Kihwelo wakipongezana baada ya mchezo
kumalizika.
Mshambuliaji wa timu ya
taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys, Hussein Twaha akiwatoka
mabeki wa timu ya Congo Brazzaville katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za
Afrika kwa vijana wenye umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Mchezo
huo ulifanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Serengeti Boys
imeshinda 1-0.
Mshambuliaji wa
timu ya Srengeti Boys, Faridi Mussa (katikati) akiwania mpira huku beki wa Cpngo
Brazzaville, Tmouele Ngampio akijaribu kumzuia. Kulia ni Golipika wa Congo
Brazzaville, Ombandza Mpea akijaribu kuokoa hatario langoni mwake.
Waamuzi wa mchezo huo wakitoka baada ya kwisha
kwa pambano hilo
Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Tumain Baraka
akichuana na beki wa Congo Brazzaville, Okombi Francis
Heka heka katika lango la Congo
Brazzaville
Wachezaji wa Serengeti Boys, Hussein Twaha
(shoto), Joseph Lubasha na Selemani Hamis Bofu wakibadilioshana mawazo wakati
wakitoka mapumziko
Selemani Hamis Bofu akitafuta mbinu za kumtoka beki
wa Congo Brazzaville, Tmouele Ngampio
Picha zote kwa hisani ya :www.francisdande.blogspot.com
No comments:
Post a Comment