Search This Blog
Thursday, April 19, 2012
RAUL: NAONDOKA SCHALKE SIONGEZI MKATABA
![]() |
| BYE BYE BYE |
Taarifa iliyotolewa na klabu ya Gelsenkirchen kupitia webiste yao imethibitisha kuwamba Raul, 34, ambaye alijiunga na tiu hiyo akitokea Real Madrid miaka miwili iliyopita, ameamua kutoendelea kuichezea timu hiyo.
Mshambuliaji huyo amesema atatoa sababu zake katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Gelsenkirchen jioni hii. Raul kwa haraka zaidi aliweza kuteka mioyo ya mashabiki wa Schalke baada ya kufunga magoli 13 katika msimu wake wa kwanza, zikiwemo hat tricks mbili.
Na msimu huu tayari ameshatupia kambani magoli 14 na kuwasogeza The Royal Blues kukaribia kupata nafasi ya kushiriki Champions league msimu ujao, lakini baada ya miezi mitatu ya tetesi sasa Raul ameamua kuondoka katika klabu hiyo.
TAARIFA KUTOKA TFF
25 TWIGA STARS KAMBINI APRILI 20
Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa ameita wachezaji 25 watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa Aprili 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Twiga Stars kabla ya mechi ya mashindano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia itakayochezwa Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa kabla ya timu hizo kurudiana jijini Dar es Salaam wiki mbili baadaye.
Baada ya kuripoti kambini jioni, wachezaji hao watafanyiwa vipimo vya afya (medical examination) siku inayofuata (Aprili 21 mwaka huu) na kuanza mazoezi Aprili 22 mwaka huu. Kambi ya timu hizo itakuwa kwenye hosteli za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani.
Wachezaji walioitwa ni Amina Ally kutoka Sekondari ya Lord Baden, Asha Rashid, Aziza Mwadini (New Generation, Zanzibar), Etoe Mlenzi (JKT Mbweni), Evelyne Sekikuto (Mburahati Queens), Fadhila Hamad (Uzuri Queens), Fatuma Bashiri (Simba Queens), Fatuma Khatib (Mburahati Queens) na Fatuma Mustafa (Sayari).
Wengine ni Fatuma Omari (Sayari), Hanifa Idd (Uzuri Queens), Maimuna Said (JKT Mbweni), Mariam Aziz (Tanzanite), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens), Mwapewa Mtumwa (Sayari) na Rehema Abdul (Lord Baden).
Kikosi hicho pia kina akina Rukia Khamis (Sayari), Semeni Abeid (Tanzanite), Siajabu Hassan (Evergreen), Sophia Mwasikili (Luleburgaz Spor Kulubu, Uturuki), Veneranda Mtamo (Tanzanite), Zena Khamis (Mburahati Queens) na Zena Said (Uzuri Queens).
KUONA NGORONGORO HEROES, SUDAN 3,000/-
Kiingilio cha chini cha mechi ya kuwania kucheza Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan itakayochezwa Jumamosi (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na viingilio vingine vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati VIP itakuwa ni sh. 15,000.
Sudan inatarajia kuwasili leo mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu 30 na itafikia hoteli ya Rungwe iliyoko maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam. Jioni itafanya mazoezi Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Ngorongoro Heroes tayari iko kambini chini ya Kocha Kim Poulsen, na leo inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Sudan yenyewe itafanya mazoezi kwenye uwanja huo kesho.
Kesho (Aprili 20 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutakuwa na mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili na Waandishi wa Habari.
MKUTANO MKUU TFF APRILI 21, 22
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika kwa siku mbili (Aprili 21 na 22 mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano huo watawasili jijini kesho (Aprili 20 mwaka huu) na watafikia kwenye hoteli ya Royal Valentino. Wajumbe wanatoka katika vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom.
Mkutano huo utakaoanza saa 3 asubuhi utakuwa na ajenda kumi na moja. Baadhi ya ajenda hizo ni hotuba ya Rais wa TFF, taarifa ya utendaji ya mwaka 2011, bajeti ya mwaka 2012 na taarifa ya ukaguzi wa hesabu (audited accounts).
JKT RUVU, SIMBA ZAINGIZA MIL 30/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Simba lililochezwa jana (Aprili 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 30,095,000.
Jumla ya watazamaji 8,362 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000. Watazamaji 7,310 kati ya hao walishuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,590,762.71 kila klabu ilipata sh. 4,455,551.19, uwanja sh. 1,485,183.73.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 1,485,183.73, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 297,036.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 297,036.75.
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 742,591.86, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 148,518.37 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 1,485,183.73.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000 na nauli ya ndani kwa mtathmini wa waamuzi sh. 10,000.
Mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna, mtathmini wa waamuzi na waamuzi sh. 120,000, gharama ya tiketi sh. 3,750,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 585,340 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 510,720.
SIMBA, MORO UNITED KUCHEZA USIKU
Mechi ya Ligi ya Vodacom kati ya Simba na Moro United iliyokuwa ichezwe Aprili 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imerudishwa nyuma hadi Jumatatu ya Aprili 23 mwaka huu kwenye uwanja huo huo na itaanza saa 1 kamili usiku.
Mabadiliko hayo yamefanyika ili kuipa Simba fursa ya kujiandaa vizuri kwa mechi yao ya Kombe la Shirikisho la Afrika dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa Aprili 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Pia mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Aprili 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam imesogezwa mbele hadi Aprili 22 mwaka huu kupisha mechi ya U20 kati ya Tanzania na Sudan itakayochezwa Aprili 21 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi nyingine mbili zimefanyiwa marekebisho; Coastal Union na Kagera Sugar zilizokuwa zicheze jijini Tanga, Aprili 29 mwaka huu, mechi yao imesogezwa hadi Aprili 30 mwaka huu ili kupisha shughuli za Mei Mosi kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Nazo Azam na Toto Africans zilizokuwa zicheze Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Chamazi, sasa zitacheza Aprili 28 mwaka huu.
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
MANCHESTER UNITED WAENDELEA KUONGOZA KWA UTAJIRI DUNIANI KWA MWAKA WA 8 MFULULIZO - YAZIFUNIKA REAL NA BARCA.
Manchester United wametajwa tena kama timu ya soka tajiri zaidi duniani - wakitajwa kuwana thamani ya £1.39billion.
Mabingwa hao wa Uingereza wamekaa kileleni mwa listi ya jarida la kimarekani la Forbes kwa miaka 8 mfululizo kufuatia mwaka mwingine wa mafanikio chini ya Sir Alex Ferguson.
Majirani zao Manchester City wenyewe pamoja na matanuzi yote ya Fedha hawajaweza hata kuingia Top 10 - wakishika nafasi ya 13.
Timu nyingine ya kiingereza iliyofuata nyayo za United ni Arsenal waliopo nafasi ya nne, wakifuatiwa na Chelsea katika nafasi ya saba, Liverpool wapo nafasi ya 8 na Tottenham wakiwa nafasi ya 11.
Giants wa Spain Real Madrid wapo nafasi ya pili, wakifuatiwa na wapinzani wao Barcelona. Bayern Munich wamekamta nafasi ya tano.
LISTI KAMILI TIMU TAJIRI DUNIANI BY FORBES MAGAZINE
| Rank | Team | Current Value ($mil) | 1-Yr Value Change (%) | Debt/Value (%) | Revenue ($mil) | Operating Income ($mil) |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | Manchester United | 2,235 | 20 | 32 | 532 | 178 |
| 2 | Real Madrid | 1,877 | 29 | 13 | 695 | 214 |
| 3 | Barcelona | 1,307 | 34 | 54 | 653 | 96 |
| 4 | Arsenal | 1,292 | 8 | 32 | 364 | 98 |
| 5 | Bayern Munich | 1,235 | 18 | 13 | 466 | 90 |
| 6 | AC Milan | 989 | 18 | 9 | 341 | 29 |
| 7 | Chelsea | 761 | 16 | 22 | 362 | 76 |
| 8 | Liverpool | 619 | 12 | 8 | 295 | 45 |
| 9 | Juventus | 591 | -8 | 15 | 223 | -38 |
| 10 | Schalke 04 | 587 | 56 | 40 | 293 | 101 |
BAADA YA RUFAA YAO KUTUPWA - YANGA WATAFAKARI CHA KUFANYA
SIKU moja baada ya kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutupilia mbali rufaa ya timu ya Yanga kupinga kupokwa pointi tatu na mabao matatu, uongozi wa klabu hiyo umesema bado unatafakari cha kufanya.
Kamati ya nidhamu chini Mwenyekiti wake kamishna mstaafu wa Polisi Alfred Tibaigana iliyokutana juzi ilitupilia mbali rufani hiyo ya Yanga iliyowasilishwa na Yanga ikilalamikia kamati ya kamati ya Ligi kuipoka pointi hizo na mabao matatu baada ya kumchezesha beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye alikuwa akitumikia adhabu ya kukosa mechi tatu.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu alisema jana kwamba wamezipata taarifa za rufaa yao kutupiliwa mbali lakini kwa sasa wanaendelea na mambo mengine kwanza ambayo yana manufaa na klabu hiyo huku wakiliweka kiporo suala hilo.
Alisema kwa sasa viongozi wengi wa klabu hiyo wapo nje ya jiji la Dar es Salaam kwa majukumu tofauti lakini bado kuna nafasi ya kukata rufaa kwa kamati ya Rufaa kama itabidi kuwa hivyo kwa kuwa muda bado upo.
“Tumepata taarifa za rufaa yetu kushindwa, hivyo ni mapema mno kutoa uamuzi tutkaochukua baada ya hatua hiyo, kwa sasa tunaendelea kuchapa kazi kwanza,”alisema Sendeu.
Aprili 2 mwaka huu Kamati ya Ligi ya TFF iliipa Coastal Union ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Yanga kumchezesha Cannavaro kwenye mechi ya Ligi Kuu bara kati ya timu hizo iliyofanyika Machi 31 mwaka huu wakati akiwa na adhabu ya kukosa mechi tatu.
MATUKIO YA PICHA UWANJA WA KAITABA YANGA NA KAGERA SUGAR
anaitwa sajid shabiki wa kagera sugar.
Abdulraz Majid mtangazaji kasibante fm radio
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Fabian Masawe ndiye alikua mgeni rasmi pembeni ni Athmani Chama katibu wa chama cha soka mkoa
Mwamedi Hussen msemaji wa kagera
sadik galiatano kushoto, enock na kulia ni mc baraka wa bukobawadau.
Wednesday, April 18, 2012
SIMBA YAZIDI KUCHANUA MAKUCHA NA KUTAMBA KILELENI - YANGA YAPIGWA TENA HUKO KAGERA
Simba imendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania baada ya kuichapa JKT Ruvu kwa mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Kwa matokeo hayo, Simba imejiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua ubingwa huo baada ya kujikita zaidi kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 56 ikiwazidi, pointi 13 mabingwa watetezi, Yanga.Simba ilianza kwa kasi mchezo na kufanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya kwanza ya mchezo lililofungwa na Uhuru Selemani kwa kichwa baada ya kuunganisha kona iliyopigwa na Emnuel Okwi.
Simba walizidi kulisakama lango la JKT Ruvu ambapo katika dakika ya saba, Amir Maftah alitoa pasi ambayo Seleman alichelewa kuunganisha na kutoka nje.
Simba waliendelea kulisakama lango la JKT ambapo katika dakika ya 17, Haruna Moshi ‘Boban’ aliipatia timu yake bao la pili baada ya uzembe uliofanywa na Emanuel Pius wa JKT na kupachika wavuni mpira.
Wekundu hao wa Msimbazi, walifanya mashambulizi tena katika dakika ya 26 ambapo Seleman alikosa bao baada ya kupaisha juu mpira aliopasiwa na Maftah huku Gervas Kago naye akikosa akikosa bao baada ya kushindwa kumalizia pasi ya Seleman katika dakika ya 39.
JKT walicharuka na kuliandama lango la Simba ambapo katika dakika ya 42, Hussein Bunu alikosa bao baada ya kushindwa kumalizia pasi ya Pius.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kusaka bao, lakini katika dakika ya 64, Mwinyi Kazimoto aliipatia Simba bao la tatu baada ya kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa JKT, Aman Simba.
JKT walifanya mabadiliko katika dakika ya 71 kwa kutoka Mohamed Banka na nafasi yake kuchukuliwa na George Mketo.
Kwa upande wa Simba alitoka Juma Nyoso na kuingia Obadia Mungusa, huku Kago akitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Edward Christopher.
Kwa upande mwingine mambo yamezidi kuwa mabaya kwa klabu ya Yanga baada ya kupokea kipigo kingine kutoka kwa Kagera Sugar leo hii katika uwanja wa Kaitaba.
Goli la Kagera lilifungwa na Shija Mkina katika kipindi cha kwanza cha mchezo., na mpaka filimbi ya mwisho inalia Kagera 1-0 Yanga.
LEO NI MIAKA 5 TANGU MESSI ALIPOMLIPA MARADONA.
miaka mitano iliyopita siku kama ya leo Leo Messi alifunga moja kati ya mabao yake bora katika maisha yake ya kucheza soka.ilikua ni kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe ya mfalme ugenini dhidi ya Getafe.
Maradona vs England kwenye robo fainali ya kombe la dunia mnamo mwaka 1986.
REAL MADRID NDIO ILIYOPIGA MASHUTI MENGI YALIYOLENGA GOLI KWENYE LA LIGA NA CHAMPIONS LEAGUE.
Kikosi cha Jose Mourinho kimepiga mashuti mengi langoni mwa wapinzani kuliko timu yoyote katika la liga na Champions league, wana wastani wa 8.1 na 8.5 kwa mechi katika kila michuano hiyo.
Real wamepiga mashuti 270 yaliyo lenga langoni mwa wapinzani katika mechi 33 msimu huu katika La Liga, kuliko Barcelona, Atletico Madrid na Sevilla. Mechi ambazo walipiga mashuti mengi yaliyolenga lango msimu ni dhidi ya Zaragoza (17), ikifuatiwa na mechi dhidi ya Granada walipiga mashuti 12.

| SHOTS ON GOAL IN LA LIGA | ||||||||
| TEAM | TOTAL SHOTS | PER MATCH | ||||||
| Real Madrid | 270 | 8.1 | ||||||
| Barcelona | 256 | 7.7 | ||||||
| Atletico Madrid | 200 | 6 | ||||||
| Sevilla | 188 | 5.7 | ||||||
Real katika Champions leaguendio wanatisha zaidi. Wamepiga mashuti 94 katika mechi 11, wastani wa 8.5 kwa maechi, na kati ya hayo 3.2 yamekuwa magoli.
| SHOTS ON GOAL IN UCL | ||||||||
| TEAM | TOTAL SHOTS | PER MATCH | ||||||
| Real Madrid | 94 | 8.5 | ||||||
| Bayern Munchen | 83 | 7.5 | ||||||
| Barcelona* | 82 | 8.2 | ||||||
| Chelsea* | 77 | 7.7 | ||||||
OFFICIAL: RUFAA YA YANGA YAPIGWA CHINI !
| Cannavaro |
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Aprili 17 mwaka huu) imetupa rufani ya Yanga iliyowasilishwa mbele yake kupinga uamuzi wa kupokwa pointi tatu kwa kumchezesha mchezaji asiyestahili.
Aprili 2 mwaka huu Kamati ya Ligi ya TFF iliipa Coastal Union ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Yanga kumchezesha beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu hizo iliyofanyika Machi 31 mwaka huu wakati akiwa na adhabu ya kukosa mechi tatu.
Yanga katika rufani hiyo iliwasilisha sababu nane za kupinga kupokwa pointi hizo, kubwa zikiwa Cannavaro hakustahili kutumikia adhabu ya kukosa mechi tatu, si aliyempiga refa Israel Nkongo, ripoti za refa na kamishna wa mechi yao dhidi ya Azam zilionesha dalili ya njama (conspiracy) kwani zilifanana.
Pia Cannavaro alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao adhabu zao zilisimamishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Kamishna mstaafu wa Polisi, Alfred Tibaigana.
Katika uamuzi wake, Kamati imesema adhabu ya Cannavaro ya kukosa mechi tatu kwa mujibu wa Kanuni ya 25(c) ya Ligi Kuu ya Vodacom ilitolewa na refa na si Kamati ya Ligi kama ambavyo inalalamikiwa na Yanga, na kanuni hiyo haikatiwi rufani.
Pia barua ambayo TFF iliiandikia Yanga kuhusu adhabu ya mchezaji huyo ilikuwa wazi kwani ilikariri kanuni ya 25(c), hivyo kitendo cha klabu hiyo kumtumia mchezaji huyo ulikuwa ni uzembe wa kutoheshimu kanuni. Kama Yanga haikufahamu vizuri kanuni hiyo ilikuwa na fursa ya kuiandikia TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 25(f) ili kupata ufafanuzi kabla ya kuamua kumtumia mchezaji huyo.
Vilevile adhabu zilizokuwa zimesimamishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ni zile ambazo zilikuwa zimetolewa na Kamati ya Ligi, na si zile zilizotolewa uwanjani na refa.
Kuhusu madai ya conspiracy kwa ripoti za kamishna wa mchezo huo na refa, Kamati imebaini kuwa hazifanani, na suala lililokuwa likibishaniwa (contentious issue) lilikuwa ni kunyang’anywa pointi tatu.
Pia Kamati ilikariri Ibara ya 50 ya Kanuni za Nidhamu za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuwa mchezaji anayembughudhi refa kwa njia yoyote ile anastahili kufungiwa kwa angalau mechi sita.
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
AFRICAN SPORTS YASUSIA MASHINDANO YOTE YA TRFA
Husika na kichwa cha habari hapo juu , sisi kama uongozi wa klabu ya African Sports kwa pamoja tumeamua kutokushiriki mashindano yoyote yatakayoandaliwa na chama cha soka mkoa wa Tanga.
Tumefikia uwamuzi huo kutokana na viongozi wa chama hicho chini ya mwenyekitik wake bwana Said Sud na katibu mkuu wake mama Beatric Mhina pamoja na wajumbve wa chama hicho Juma Mgunda mwakilishi wa vilabu, Salim Amir, Khalid Abdalha kutokututendea haki na kuikandamiza klabu yetu kila mwaka tunaposhiriki mashindano ya mkoa.
Tumetafakari kwa muda mrefu na kupata maoni na mawazo ya waasisi wa klabu hii tumeamua kuachana na masuala ya kucheza mashindano yoyote mpaka viongozi hawa watakapoacha kuongoza soka mkoani hapa hata kama ni miaka elfu kumi ijayo.
Kila mpenda soka amesikitishwa na kitendo ambacho klabu yetu imefanyiwa ila hatuna cha kufanya tunamwachia mungu, tunajua fika uamuzi wetu huu wa kujiondoa kwenye mashindano yanayoandaliwa na chama cha mkoa ni uamuzi mgumu, ila tukumbuke kuwa mpira sio ibada kama ukiacha basi utapata dhambi.
Mwisho wito kwa wajumbe wa mkoa wawe makini kwani wao ndio wanaotuletea viongozi ambao hawataki kufuata kanuni.bali mapenzi ya mioyo yao.
AFISA HABARI AFRICAN SPORTS
SAID KARSANDAS PANDRAM

HAYUPO WILSHARE, HAYUPO ROONEY WALA KOCHA MKUU=HAKUNA MATUMAINI: MIPANGO YA ENGLAND IMEHARIBIKA KABLA YA MICHUANO YA EURO KUANZA.
Mashabiki wa Arsenal tayari wameshafahamu kwamba watamaliza msimu pia bila kombe, na sasa na hizi habari za Jack Wilshare kwamba hatosafiri kwenda Euro, mashabiki wa England nao itabidi waelewe hakuna taji.
Baada ya kufungwa na Wigan Jumatatu usiku, Arsene Wenger alitoa za msiba kwa Three Lions na matumaini yao ya kufanya vizuri nchini Ukraine na Poland. Alisema: "Wilshare hatoenda kwenye Euro kwa hakika."
Katika msimu wa 2011, Wilshare alionyesha uwezo mkubwa, pamoja na ubunifu uliokomaa katika sola la daraja la juu, lakini majeraha ya mara kwa mara yameharibu malengo yake ndani ya England na Arsenal katika msimu huu wa 2011-2012.
Wilshare akiwa na miaka 20 aliwatawala viungo wa Barcelona Xavi na Andres Iniesta katika uwanja wa Emirates mwezi February 2011 - hii ilithibitisha kiasi gani ana potential ya kuwa mchezaji mzuri.
Pia aliendelea kucheza kwa kiwango cha juu katika timu ya taifa ya England, hasa katika mechi dhidi ya Denmark, Wilshare akiwa amevaa jezi namba 10 alicheza katikati ya safu ya kiungo na ushambuliaji na kung'ara sana katika mechi dhidi ya Switzerland. - Versatility.
Wilshare kwa sasa yupo nje ya dimba kwa muda mrefu kiasi, na kutokuwepo kwake kunzidi kuumiza vichwa vya mashabiki wa timu yake ya Taifa, kwa kuwa anazidi kuongeza ugumu wa ndoto za England kufanya vizuri katika Euro 2012.
Huku zikiwa zimebakia wiki chache kabla ya michuano kuanza, England bado hawana manager wa kuelewaka, watamkosa roho yao Wayne Rooney kwa mechi mbili za kwanza, na sasa wanaambiwa Wilshare hatocheza michuano hiyo.
Kocha wa muda Stuart Pearce amekaririwa akisema anatumia mipango ile ile ambayo ilikuwa tayari imeshawekwa na Fabio Capello, lakini mipango yote hii inaweza ikatupwa pembeni pale kocha mpya atakapowasili.
Na huku msimu wa Tottenham ukiwa umeenda mlama mara tu baada ya Harry Redknapp kuanza kuhusishwa na kazi ya benchi la ufundi la timu ya taifa lake, sasa kumeanza kuwepo na mashaka juu ya bosi huyo wa Spurs kwamba ni mtu sahihi wa kuleta matumaini mapya ndani ya England.
Hili inamuacha Stuart Pearce, ambaye hawezi kuwa kocha wa moja kwa moja, na Roy Hodgson, ambaye alifeli katika kazi yake ya mwisho kwenye timu kubwa, kama wabadala wa Harry Redknapp ambao FA itakuwa inawaangalia.
England inakosa manager, ubunifu katika kiungo na pia wana options chache katika mashambulizi kwa mechi dhidi ya Sweden na France, huku Wayne Rooney akiwa amefungiwa hivyo kuweka matumaini ya England kwenye Euro kuwa madogo.
Pia giz a linazidi kuongezeka katika anga la England baada ya mbadala sahihi kwa kiasi fulani wa Wayne Rooney, Darren Bent akiwa katika hali mbaya ya majeraha.
Wabadala wengi wa Rooney na Bent bado wanatia mashaka katika mioyo ya wengi.
Danny Welbeck ana potential kubwa lakini anakosa utulivu mbele lango ambalo litakuwa linalindwa na mabeki wa level ya juu katika Euros.
Peter Crouch, lile goli alilomfunga Joe Hart pembeni, kijana huyo amekosa consistency itakayomfanya aweze kuitwa tena na Jermain Defoe anaweza akawa mfungaji bora wa Spurs msimu huu, lakini magoli dhidi ya Stevenage, Cheltenham na Shamrock Rovers hayawezi kiujumla, kuwapa wachezaji nafasi ya michuano ya kimataifa.
Wengine kama Bobby Zamora, Andy Carroll na Grant Holt aidha wapo nje ya form au bahati, kiufupi hawajathibitisha kama wanafaa kuiongoza safu ya mashambulizi ya England.
Of course, mambo yanaweza yakabadilika. Paul Scholes, ndio mtu pekee ambaye anashabihiana na impact ya Wilshare, anaweza kaamua kurudi kuilisadia taifa lake, Andy Carroll nae anaweza akaendelea kuwa kwenye form aliyopo nao sasa na Liverpool, na Redknapp anaweza akarudisha focus aliyopteza ndani ya muda, labda haya yanaweza yakabadilisha hatma ya England in Kiev.
Lakini kwa jinsi mambo yalivyo sasa, inaonekana mambo yatakuwa mabaya na itakuwa summer ya maumivu kwa Three Lions na mashabiki wake.

Washindi ya Promosheni ya Tick Tock ya Zantel waendelea kupata mkwanja.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Zantel Ahmed Mokhles (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Champ Enterprises Shazin Remtullah (katikati) wakimkabidhi zawadi ya milioni 1 kwa SHABANI SAID NJECHELE aliyeshinda kwenye promosheni inayoendelea ya Tick Tock & Win kutoka Zantel.
Mshindi wa siku wa milioni 1 kwenye promosheni ya Zantel ya Tick Tock & Win SHABANI SAID NJECHELE akiifurahia Zawadi yake punde baada ya kukabidhiwa fedha hizo makoa makuu ya Zantel yaliyopo Dar es Salaam. Zantel kila siku inatoa Zawadi ya milioni 1 pamoja na simu aina ya Nokia kila saa na mteja anahitaji kuongeza salio la TSH 1000 na kuendelea na namba yake itaingizwa kwenye droo ya siku hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel Deepak Gupta akimkabidhi mshindi wa simu aina ya Nokia KAISI MASOUD MOHAMMED wa Magomeni Dar es Salaam aliyoshinda kwenye promosheni ya Zantel ya Tick Tock & Win. Zantel kila siku inatoa Zawadi ya milioni 1 pamoja na simu aina ya Nokia kila saa na mteja anahitaji kuongeza salio la TSH 1000 na kuendelea na namba yake itaingizwa kwenye droo ya siku hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel Deepak Gupta akimkabidhi mshindi wa simu aina ya Nokia SAUMU SHARIF MOHAMMED wa Kigamboni Dar es Salaam aliyoshinda kwenye promosheni ya Zantel ya Tick Tock & Win. Zantel kila siku inatoa Zawadi ya milioni 1 pamoja na simu aina ya Nokia kila saa na mteja anahitaji kuongeza salio la TSH 1000 na kuendelea na namba yake itaingizwa kwenye droo ya siku hiyo.

KAMATI YA TIBAIGANA YAITUPILIA MBALI RUFAA YA YANGA.
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeitupili mbali rufaa ya Yanga, kupinga kopokonywa pointi tatu ilizozivuna kwenye mechi na Coastal Union ya Tanga.
Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana chini ya Mwenyekiti wake, Alfred Tibaigana, kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam zimesema rufaa ya Yanga imetupwa.
Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana chini ya Mwenyekiti wake, Alfred Tibaigana, kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam zimesema rufaa ya Yanga imetupwa.
Yanga iliifunga Coastal 1-0, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga bao pekee la Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza, lakini Kamati ya Ligi Kuu ikawapokonya pointi kwa kosa la kumtumia beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyekuwa anatumikia adhabu.
Kupokwa pointi hizo, kunamaanisha Yanga sasa iko hatarini kukosa nafasi ya kucheza michuano ya Afrika mwakani, kutokana na Simba SC sasa kuwa inaongoza ligi kwa pointi zake 53 na Azam yenye pointi 50 inashika nafasi ya pili.
Yanga yenye pointi 43 inashika nafasi ya tatu na leo itakuwa mgeni wa Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
Tuesday, April 17, 2012
EXCLUSIVE INTERVIEW: RONALDO DE LIMA - AMTAJA MRITHI WAKE, TIMU ANAYOISHABIKIA NA NAFASI YA BRAZIL KOMBE LA DUNIA 2014
Akiwa na miaka 35, kuna vichache sana ambavyo bado havijazungumzia kuhusu mbrazili Ronaldo. Mafanikio aliyoyapata mtupia nyavuni huyu yanaongea kwa sauti kubwa sana, O Fenomena ndio mfungaji bora wa muda wote wa FIFA World Cup, ameshinda medali mbili za kombe la dunia, ameshinda mara tatu tuzo ya FIFA World Player na mara mbili tuzo ya Ballon d'Or.
Ronaldo ambaye kwa sasa amestaafu soka ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya 2014 FIFA World Cup.
Pamoja na kuwa busy sana kuitumikia nafasi yake katika kamati hiyo, mchezaji huyo wa zamani wa PSV Eindhoven, Barcelona, Inter Milan, na Real Madrid aliongea na mtandao wa FIFA.com kuhusu career yake, presha iliyopo dhidi ya Selecao na nafasi yake kwenye kombe la dunia la mwaka 2014.
FIFA.com: Kama mmoja ya kamati ya maandalizi ya FIFA World Cup, je una mategemeo yapi kwa michuano hiyo?
Ronaldo: Tunajisikia fahari sana kuandaa kombe la dunia hapa Brazil. Tutakuwa na nafasi kubwa ya kukua, ambayo ni muhimu kutokana wingi wa watu waliopo nchini kwetu ambao wamesongwa na ukosefu wa ajira. Kupitia michuano hii kutakuwa na uwezekezaji mkubwa katika miundombinu. viwanja vya ndege, barabara, hospitali na hoteli. Kutakuwa na manufaa ambayo yatainufaisha Brazil na maisha yetu wote, na hilo linawezekana pekee kwa sababu ya Kombe la dunia.
Unadhani Brazili wapo tayari kwa ajili ya michuano hii?
Kuna mabadiliko makubwa katika kikosi cha timu ya taifa, kizazi kipya ambacho kiukweli bado hakichezi soka zuri bado. Na nafikiri itachukua muda kidogo ili kuweza kufikia kucheza soka la kibrazili asilia. Lakini kati ya sasa na 2014 kuna muda mzuri kupata consistency, kuelewana, na kuwa katika hali ya kuweza kushindana na kuwa na kikosi ambacho kitakuwa na uwezo kulinda heshima ya nyumbani na kuchukua kombe.
Neymar, Alexandre Pato na Ganso ndio wachezaji ambao wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika kizazi hiki kipya cha Brazil. Je una maoni gani juu watatu hawa?
Ni wachezaji watatu ambao wana vipaji sana, wabrazili ambao wanang'ara katika vilabu vyao. Nadhani Neymar ndio aliyebarikiwa zaidi, na akiwa ndio kwanza ana miaka 19, tayari ameshakuwa na uwezo wa ajabu. Anafunga magoli mengi na tayari ameishakamata Brazil, mashabiki wanampenda. Uzoefu wa kimatifa alioupata katika michauno ya dunia ya vilabu haukuwa mzuri sana, lakini nina hakika bado na muda wa kujifunza zaidi. Pato kwa upande wake, tayari ameshadhirisha kipaji chake barani ulaya, wakati Ganso pia ni mzuri sana anachohitaji na kupata bahati ya kuepeukanana majeraha.
Unafikiri kuna nafasi kwa wachezaji wazoefu kama Ronaldinho na Kaka?
Ni wachezaji muhimu, ofcourse. Kwa majukumu yao nje ya dimba, na itategemea na fomu zao na kama wanacheza vizuri kipindi kombe la dunia likiwa linakaribia then wana nafasi. Lakini pia bado wana majukumu nje ya dimba, uzoefu wao utakuwa kitu muhimu kwa ajili ya kikosi ambacho kitakuwa na wachezaji wengi wenye umri mdogo.
Je unaiweka Brazili nafasi ngapi kwa ubora wa soka duniani kwa sasa?
Kiukweli kwa sasa hatupo katika Top 3, lakini nafikiri tupo katika top 5 ya timu bora duniani, hata kama hatupo on fire kwa sasa. Kufanya mabadiliko haijawahi kuwa rahisi na hawa wachezaji wadogo wanahitaji kuimarika. Hakuhitaji kupaniki, wanahitaji kupewa muda ili kufanya vizuri.
Unadhani ni mchezaji gani ambaye unaona ndio mrithi sahihi wa Ronaldo?
Leandro Damiao, kutoka Internationa de Porto. Ni mrefu, ana nguvu, na pia ni mfungaji mzuri, anatisha sana hewani na uwezo mkubwa katika miguu yote miwili. Atkauwa mchezaji muhimu sana katika michuano ya 2014.
Ebu tuangalie siku za nyuma kipindi unacheza soka. Ulicheza Brazil, Spain, Uholanzi na Italy, wapi unadhani kuna mashabiki wenye mapenzi makubwa na soka?
Nafikiri mashabiki wa nchi zote ni vichaa wa soka, japokuwa wana staili tofauti za usangaliaji.
Katika timu zote ulizocheza ni timu gani bado ipo moyoni mwako na itaendela kuwa hivyo?
Naangalia muda wangu niliokuwa pale Real Madrid jinsi kulivyokuwa na upendo. nafikiri ndio ulikuwa muda wangu mzuri zaidi katika maisha yangu ya soka. Pia nilipenda maisha yangu pale Inter Milan, niliipenda timu na mashabiki wa mji wa Milan.Lakini kote nilipocheza nilikuwa na marafiki wengi na kuwa muda mzuri.
Je safari yako ya kwenda na timu katika World Cup 1994 USA, ilikuwa na umuhimu gani tena ukizingatia ulikuwa na miaka 17?
Ilikuwa muhimu sana. Kuwaona wachezaji wa kariba ya Romario na Bebeto kwa ukaribu na kuwajua vizuri. Niliweza kujifunza mengi kutoka kwao, pia kupata maelezo kadhaa, kama jinsi gani wanafanya mazoezi, na mengine mengi. Romario alikuwa akinituma sana, kama kwenda kumchukulia viatu vyake na kumletea kahawa - yaani kama mwanae vile, lakini siku zote alikuwa akiniheshimu .
Tuambie katika miaka ya sasa ni timu gani inakufurahisha inavyocheza?
Napenda sana jinsi Madrid wanavyocheza soka lao, lakini huwezi kuiacha Barcelona, ambao wana timu nzuri sana. Kila mchezaji wa kila eneo wa anajua nini afanye katika muda muafaka. Pia wana uwezo mkubwa kukaa na mpira huku wakipasiana vizuri kwa kwenda mbele kwenye goli la wapizani. Ni kazi nzuri sana ambayo Pep Guardiola ameifanya, Barcelona ni moja ya timu nzuri sana ambayo nimewahi kuishuhudia katika maisha yangu ndani ya sayari hii. Inauma kusema hivi ukizingatia mimi ni Madridista, lakini nafikiri tunaweza kushinda mataji mbele yao msimu huu.
Haya sasa tutajie perfect eleven yako ya kikosi cha Brazil.
Mmmh hi ngumu kidogo lakini hawa watastahili. Taffarel, Cafu, Aldair, Lucio, Roberto Carlos, Junior Zico, Rivelino, Pele na mimi mwenyewe. Hi ni timu ya hatari ingeweza kusambaratisha timu yoyote duniani.

WAGANDA KUCHEZESHA NGORONGORO VS SUDAN
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua waamuzi kutoka Uganda kuchezesha mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan itakayofanyika Aprili 21 mwaka huu.
Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni ni Brian Miiro. Waamuzi wasaidizi ni Mark Ssonko na Lee Patabali wakati mwamuzi wa mezani ni Denis Batte.
Ejigu Ashenafi wa Ethiopia ndiye ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi hiyo namba 15. Kamishna na waamuzi hao watawasili nchini Aprili 19 mwaka huu kwa ndege za Ethiopian Airlines na Air Uganda.
KINYANG’ANYIRO VPL KUENDELEA APRILI 18
Kinyang’anyiro cha Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kinaendelea tena kesho (Aprili 18 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa kwenye miji ya Bukoba, Mwanza, Dar es Salaam, Mlandizi na Dodoma.
Mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba wakati Toto Africans itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Vinara wa ligi hiyo Simba wataoneshana kazi na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Ruvu Shooting na Moro United zitaumana kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi. Nayo Polisi Dodoma itakuwa mwenyeji wa Coastal Union mjini Dodoma.
TENDA YA TIKETI KUFUNGULIWA APRILI 18
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho (Aprili 18 mwaka huu) itafungua maombi ya tenda zilizowasilishwa na kampuni mbalimbali kwa ajili ya kutengeneza tiketi za elektroniki.
Maombi hayo yatafunguliwa saa 9 alasiri kwenye ofisi za TFF ambapo kampuni zote zilizowasilisha tenda zinatakiwa kuwepo wakati wa ufunguzi huo.
Machi 9 mwaka huu TFF ilitangaza tenda kwa ajili ya kutengeneza tiketi za elektroniki kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na mechi nyingine inazozisimamia.
SIMBA, SHOOTING ZAINGIZA MIL 40/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Simba lililochezwa juzi (Aprili 15 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 40,855,000.
Jumla ya watazamaji 10,824 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000. Watazamaji 8,500 kati ya hao walishuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 6,232,118.64 kila klabu ilipata sh. 7,406,424.41, uwanja sh. 2,468,808.14.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 2,468,808.14, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 493,761.63 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 493,761.63.
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,234,404.07, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 246,880.81 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 2,468,808.14.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000 na nauli ya ndani kwa mtathmini wa waamuzi sh. 10,000.
Mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna, mtathmini wa waamuzi na waamuzi sh. 200,000, gharama ya tiketi sh. 2,460,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 757,680 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 649,440.
Nayo mechi kati ya Villa Squad na Coastal Union iliyochezwa Aprili 15 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam iliingiza sh. 499,000 ambapo kila klabu ilipata sh. 44,374 wakati watazamaji walioshuhudia mechi hiyo ni 451.
Vilevile mechi kati ya Moro United na JKT Oljoro iliyochezwa Aprili 14 mwaka huu Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam iliingiza sh. 410,000 kutokana na washabiki 402. Kila klabu ilipata sh. 39,257.
7,186 WASHUHUDIA MECHI YA TOTO AFRICANS, YANGA
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Toto Africans na Yanga iliyochezwa juzi (Aprili 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ilishuhudiwa na watazamaji 7,186 na kuingiza sh. 15,392,000. Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa jukwaa kuu na sh. 2,000 mzunguko.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 2,347,932 kila klabu ilipata sh. 2,729,060, uwanja sh. 909,686.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 909,686, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) sh. 363,874, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 454,843, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 90,968 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 909,686.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. Mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna na waamuzi sh. 160,000, gharama ya tiketi sh. 2,300,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 503,020 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) kilipata sh. 431,160.
MTWARA FA WAPATA VIONGOZI WAPYA
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA) kimepata viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika juzi (Aprili 15 mwaka huu) ukumbi wa Clinical Officers Training College wilayani Masasi.
Waliochaguliwa ni Athumani Kambi (Mwenyekiti), Vincent Majili (Katibu Mkuu), Kazito Mbano (Mhazini) na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Fredrick Nachinuku.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa MTWAREFA walikuwa 30 ambapo Kambi alipata kura 23 za ndiyo na saba za hapana wakati Majili alipata kura 27 dhidi ya tatu za Charles Haule.
Nafasi nyingine hazikuwa na wagombea ambapo uchaguzi mdogo utaitishwa baadaye.
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
MAXIMO SINA MPANGO WA KUJA KUIFUNDISHA AZAM, YANGA WALA TAIFA STARS. ATOA MBINU ZA KUPATA WACHEZAJI BORA.
Na Anna Nkinda - Sao Paul, Brazil
Vilabu vya soka nchini vimeshauriwa kuwa na timu nzuri kuanzia ngazi ya watoto wenye umri wa miaka nane, vijana na kuendelea ili kupata timu bora ya Taifa.
Wito huo umetolewa jana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Star Marcio Maximo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Sao Paul.
Maximo alisema kuwa timu nyingi ambazo ni bora na zinafanya vizuri katika mchezo wa soka zimekuwa zikiwaandaa watoto wenye vipaji vya mchezo huo wangali wadogo ili waweze kuwa wachezaji wazuri hapo baadaye.
Kuhusiana na uvumi ulioenea kuwa anataka kwenda kufundisha timu za Taifa Stars, Azam na Yanga alisema kuwa siyo kweli na wala hajawasiliana na timu hizo na hawezi kwenda kufundisha kwani hivi sasa anamkataba wa kufundisha timu ya Democrata iliyopo nchini humo.
“Timu ya Taifa Star inakocha mzuri ambaye ninamuheshimu na ninaukubali ufundishaji wake hivyo basi kupitia kocha huyo ninaamini watanzania watazidi kuendelea katika soka na kufika mbali zaidi”, alisema.
Maximo alimalizia kwa kusema kuwa anamawasiliano mazuri na watanzania na anawapenda ndiyo maana kila mahali anapopita anajivuna na kusema kuwa Tanzania ni nchi yake ya pili.
Hivi sasa Maximo ni kocha wa timu ya Democrata iliyopo nchini humo ambapo wiki ijayo inatarajia kuanza mashindano ya taifa yatakayopelekea kupata wachezaji bora watakaoshiriki mashindano ya kombe la Dunia yanayotarajia kufanyika mwaka 2014 nchini Brazil.
source:http://www.mjengwablog.com/
Subscribe to:
Posts (Atom)