Search This Blog

Wednesday, April 18, 2012

HAYUPO WILSHARE, HAYUPO ROONEY WALA KOCHA MKUU=HAKUNA MATUMAINI: MIPANGO YA ENGLAND IMEHARIBIKA KABLA YA MICHUANO YA EURO KUANZA.

Mashabiki wa Arsenal tayari wameshafahamu kwamba watamaliza msimu pia bila kombe, na sasa na hizi habari za Jack Wilshare kwamba hatosafiri kwenda Euro, mashabiki wa England nao itabidi waelewe hakuna taji.

Baada ya kufungwa na Wigan Jumatatu usiku, Arsene Wenger alitoa za msiba kwa Three Lions na matumaini yao ya kufanya vizuri nchini Ukraine na Poland. Alisema: "Wilshare hatoenda kwenye Euro kwa hakika."

Katika msimu wa 2011, Wilshare alionyesha uwezo mkubwa, pamoja na ubunifu uliokomaa katika sola la daraja la juu, lakini majeraha ya mara kwa mara yameharibu malengo yake ndani  ya England na Arsenal katika msimu huu wa 2011-2012.

Wilshare akiwa na miaka 20 aliwatawala viungo wa Barcelona Xavi na Andres Iniesta katika uwanja wa Emirates mwezi February 2011 - hii ilithibitisha kiasi gani ana potential ya kuwa mchezaji mzuri.

Pia aliendelea kucheza kwa kiwango cha juu katika timu ya taifa ya England, hasa katika mechi dhidi ya Denmark, Wilshare akiwa amevaa jezi namba 10 alicheza katikati ya safu ya kiungo na ushambuliaji na kung'ara sana katika mechi dhidi ya Switzerland. - Versatility.

Wilshare kwa sasa yupo nje ya dimba kwa muda mrefu kiasi, na kutokuwepo kwake kunzidi kuumiza vichwa vya mashabiki wa timu yake ya Taifa, kwa kuwa anazidi kuongeza ugumu wa ndoto za England kufanya vizuri katika Euro 2012.

Huku zikiwa zimebakia wiki chache kabla ya michuano kuanza, England bado hawana manager wa kuelewaka, watamkosa roho yao Wayne Rooney kwa mechi mbili za kwanza, na sasa wanaambiwa Wilshare hatocheza michuano hiyo.

Kocha wa muda Stuart Pearce amekaririwa akisema anatumia mipango ile ile ambayo ilikuwa tayari imeshawekwa na Fabio Capello, lakini mipango yote hii inaweza ikatupwa pembeni pale kocha mpya atakapowasili.

Na huku msimu wa Tottenham ukiwa umeenda mlama mara tu baada ya Harry Redknapp kuanza kuhusishwa na kazi ya benchi la ufundi la timu ya taifa lake, sasa kumeanza kuwepo na mashaka juu ya bosi huyo wa Spurs kwamba ni mtu sahihi wa kuleta matumaini mapya ndani ya England.

Hili inamuacha Stuart Pearce, ambaye hawezi kuwa kocha wa moja kwa moja, na Roy Hodgson, ambaye alifeli katika kazi yake ya mwisho kwenye timu kubwa, kama wabadala wa Harry Redknapp ambao FA itakuwa inawaangalia.

England inakosa manager, ubunifu katika kiungo na pia wana options chache katika mashambulizi kwa mechi dhidi ya Sweden na France, huku Wayne Rooney akiwa amefungiwa hivyo kuweka matumaini ya England kwenye Euro kuwa madogo.

Pia giz a linazidi kuongezeka katika anga la England baada ya mbadala sahihi kwa kiasi fulani wa Wayne Rooney, Darren Bent  akiwa katika hali mbaya ya majeraha.

Wabadala wengi wa Rooney na Bent bado wanatia mashaka katika mioyo ya wengi.
Danny Welbeck ana potential kubwa lakini anakosa utulivu mbele lango ambalo litakuwa linalindwa na mabeki wa level ya juu katika Euros.

Peter Crouch, lile goli alilomfunga Joe Hart pembeni, kijana huyo amekosa consistency itakayomfanya aweze kuitwa tena na Jermain Defoe anaweza akawa mfungaji bora wa Spurs msimu huu, lakini magoli dhidi ya Stevenage, Cheltenham na Shamrock Rovers hayawezi kiujumla, kuwapa wachezaji nafasi ya michuano ya kimataifa.

Wengine kama Bobby Zamora, Andy Carroll na Grant Holt aidha wapo nje ya form au bahati, kiufupi  hawajathibitisha kama wanafaa kuiongoza safu ya mashambulizi ya England.

Of course, mambo yanaweza yakabadilika. Paul Scholes, ndio mtu pekee ambaye anashabihiana na impact ya Wilshare, anaweza kaamua kurudi kuilisadia taifa lake, Andy Carroll nae anaweza akaendelea kuwa kwenye form aliyopo nao sasa na Liverpool, na Redknapp anaweza akarudisha focus aliyopteza ndani ya muda, labda haya yanaweza yakabadilisha hatma ya England in Kiev.

Lakini kwa jinsi mambo yalivyo sasa, inaonekana mambo yatakuwa mabaya na itakuwa summer ya maumivu kwa Three Lions na mashabiki wake. 

No comments:

Post a Comment