Husika na kichwa cha habari hapo juu , sisi kama uongozi wa klabu ya African Sports kwa pamoja tumeamua kutokushiriki mashindano yoyote yatakayoandaliwa na chama cha soka mkoa wa Tanga.
Tumefikia uwamuzi huo kutokana na viongozi wa chama hicho chini ya mwenyekitik wake bwana Said Sud na katibu mkuu wake mama Beatric Mhina pamoja na wajumbve wa chama hicho Juma Mgunda mwakilishi wa vilabu, Salim Amir, Khalid Abdalha kutokututendea haki na kuikandamiza klabu yetu kila mwaka tunaposhiriki mashindano ya mkoa.
Tumetafakari kwa muda mrefu na kupata maoni na mawazo ya waasisi wa klabu hii tumeamua kuachana na masuala ya kucheza mashindano yoyote mpaka viongozi hawa watakapoacha kuongoza soka mkoani hapa hata kama ni miaka elfu kumi ijayo.
Kila mpenda soka amesikitishwa na kitendo ambacho klabu yetu imefanyiwa ila hatuna cha kufanya tunamwachia mungu, tunajua fika uamuzi wetu huu wa kujiondoa kwenye mashindano yanayoandaliwa na chama cha mkoa ni uamuzi mgumu, ila tukumbuke kuwa mpira sio ibada kama ukiacha basi utapata dhambi.
Mwisho wito kwa wajumbe wa mkoa wawe makini kwani wao ndio wanaotuletea viongozi ambao hawataki kufuata kanuni.bali mapenzi ya mioyo yao.
AFISA HABARI AFRICAN SPORTS
SAID KARSANDAS PANDRAM
No comments:
Post a Comment