Search This Blog

Wednesday, April 18, 2012

KAMATI YA TIBAIGANA YAITUPILIA MBALI RUFAA YA YANGA.

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeitupili mbali rufaa ya Yanga,  kupinga kopokonywa pointi tatu ilizozivuna kwenye mechi na Coastal Union ya Tanga.
Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana chini ya Mwenyekiti wake, Alfred Tibaigana, kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam zimesema rufaa ya Yanga imetupwa.

Yanga iliifunga Coastal 1-0, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga bao pekee la Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza, lakini Kamati ya Ligi Kuu ikawapokonya pointi kwa kosa la kumtumia beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyekuwa anatumikia adhabu.

Kupokwa pointi hizo, kunamaanisha Yanga sasa iko hatarini kukosa nafasi ya kucheza michuano ya Afrika mwakani, kutokana na Simba SC sasa kuwa inaongoza ligi kwa pointi zake 53 na Azam yenye pointi 50 inashika nafasi ya pili.

Yanga yenye pointi 43 inashika nafasi ya tatu na leo itakuwa mgeni wa Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.

5 comments:

  1. Hii kitu ilikuwa wazi mno!Uongozi ulifanya maamuzi ya kip**mbavu kwani kulikuwa na ulazima gani wa kumchezesha canavaro wakati alikuwa na utata unamzunguka?hakuna watu wengine wa kucheza nafasi yake? Afu kitu kingine ni kuwa maagizo ya tibaigana yalieleza wazi sana alisema maamuzi ya kusitisha adhabu zilizotolewa na kamati ya ligi hayaingilli maamuzi yaliyotolewa na mwamuzi uwanjani na inajulikana ukitolewa kwa vurugu 'violence' unakwenda nje mechi 3.mbona ni kitu cha wazi sana hata kwa mtu mwenye ufahamu wa kawaida kukibaini iweje viongozi wa yanga hayakuliona hili au wana ajenda yao ya siri?mie ni mpenzi wa timu hii na kiukweli nimechukizwa sana na maamuzi mabovu ya uongozi ya kumchezesha canavaro,matokeo yake yameigharimu sana timu yetu.

    By the way,kaka shaffi nashauri uendelee kuiboresha hii yetu blog yetu ili iweze kuwa na mtazamo wa kuvutia zaidi.si maanishi kuwa kwa sasa blog haina mvuto la hasha,naamini blog hii unaweza kuipimp zaidi ili iweze kuwa na mvuto zaidi kwa sisi wasomaji na wafuatiliaji wa masuala ya michezo.kwa mfano ukifungua blog unakutana na vitangazo vidogovidogo vinazungumizia cjui al shabaab,radioraage…sina hakina kama vitu hivi vina baraka yako au vinatokea tu vyenyewe!lakini nina hakika ukionana na watalaam wako wa IT watakusaidia kuondoa hizi nuisance chache nilizoziona mimi kwa jicho la kawaida na zingine za kitaalam kwa lengo la kunogesha majamboz hapa…isije kuwa siku moja blog ikatuhumiwa kuwa inachukua mshiko wa al shabaab (joke)

    ReplyDelete
  2. hili lilikua ni wazi, ni suala tu la muda ulikua unasubiriwa!!!. nchi hii ina matatizo mengi katika soka, umbumbumbu wa viongozi, wanachama, mashabiki na waandishi wa habari za michezo pia huchangia matatizo ya soka la nchi hii. viongozi huwadanganya wanachama hata kwa kitu ambacho kiko wazi, hatuna viongozi ambao wanaweza kukemea ujinga wa wachezaji hata kwa suala kama hili walilofanya wachezaji wa yanga. Ni jambo la aibu!!! lakini kwa sababu viongozi nao ni wajinga basi wanatengeneza mazingira ili timu ionekane imeonewa.
    nikija kwa waandishi wa habari. hapa kuna upuuzi mkubwa!!! hatuna waandishi wenye kuandika kwa maslahi ya mpira wa nchi hii. wengi wanaandika kwa kukidhi UNAZI wao. mfano suala la straight red card. sidhani kama lina mjadala. ni wazi mchezaji atakosa mechi tatu, lakini mfano wa upuuzi wa waandishi ni huyu wa dimba BIN ZUBERI, kwa kuwa anaipenda yanga alifika hata kuandika kwamba canavaro hakua na hatia ya red card kwa kuwa hakwenda kwa ajili ya kumshambulia mwamuzi!!!!. sijui kilichomtoa kanavaro mpaka kwa rewfa nini kitu gani? au ile kazi alikyokua anafanya nsajigwa ya kumzuia kanavaro ilikuwa ya nini? mimi ninasema huu ni upuuzi. tunahitaji waandhishi wenye uwezo wa kuelimisha, kukemea, kuelekeza nini kifanyike. huu upuuzi wa kina bin zuberi hautatufikisha mbali!!!!

    ReplyDelete
  3. Ifike wakati TFF wajivue gamba coz kama Canavaro alimpiga Nkongo mbona Mwasika kafungiwa? Pili,walimshusha daraja kamisaa wa game ya Cost Union Vs Yanga kwa kusubmit weak report.. now what about Nkongo ambaye hakuumudu mchezo wa Yanga Vs Azam kwa kushindwa kumpa RED CARD Mwasika?

    ReplyDelete
  4. Kwanza nishukuru michango ya wachangiaji waliopita kwani wamezungumza yote na umbumbumbu wa viongozi wetu wa vilabu na jinsi ambavyo wanachama wa vilabu hivi nao walivyo na upeo mdogo, suala la Canavaro lilikuwa wazi sana adhabu umepewa ndani ya uwanja na si nje ya uwanja na ilikuwa staight red card, mimi nilishtuka kusikia canavaro amechezeshwa Tanga na maelezo ya Papic anadai yeye aliambiwa amchezeshe lakini yeye binafsi alijua si sahihi ila kwa sababu viongozi ndio wanapanga timu basi akatekeleza maagizo.
    Mimi si shabiki wa YANGA ila naamini hao viongozi wa Yanga walikuwa wanajua fika wanachokifanya naamini pia kuna makundi ndani ya uongozi wa klabu ya Yanga na natumai muhusika atawajibishwa na Yanga kwani wanamfahamu fika.

    Kuhusu ushiriki wa Yanga kimataifa mwakani ndio bye bye, hawana nafasi hilo liko wazi imeshakula kwao.
    Wakajipange tena.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi nakubali maoni yako na yana ukweli sana. Yanga waliambiwa Msimchezeshe Nadir, Kocha alielewa na akamuweka nje. Bhinda akasema kuwa "lazima acheze sisi ni ndio Yanga Afrika tutapambana nao huko mbele". Huu ndio mtazamo wa Yanga hata katika mambo mengine yanayohusu usajili. Kuna watu pale TFF wanapinda sheria na kanuni kwa ajili ya Yanga. Yanga wote waliungana kutetea hata kwa vitisho. Hivi ndivyo Yanga walivyo. walijua Tangu mwanzo hawana haki katika hili, lakini wao wanataka wapewe hata kama si haki yao. Angalia, lugha na vitisho walivyotumia kila mahali inafanana, wao wamezoea na TFF wanafahamu na hata Yanga ikitishia kuvunjika amani mchezoni na ikavunjika hawatachukua hatua yoyote. Hiyo ndiyo lugha ya Yanga. Hakuna timu yoyote inayoongea lugha hii na ikavumiliwa.

      Delete