Search This Blog

Wednesday, November 30, 2011

COUNTDOWN DIRISHA DOGO LA USAJILI BONGO: AFRICAN LYON

Wakati dirisha dogo la usajili wa Bongo likielekea kufungwa hivi punde klabu ya African Lyon imefanikiwa kumsajili kiungo Justus Anene kutoka klabu ya URA ya nchini Uganda,pia timu hiyo imefanikiwa kumnasa beki Obinna Mustafa raia wa Nigeria toka klabu ya Zanzibar Ocean View.

WALIONGIA:

SAMUEL NGASA-HURU
JUSTUS ANENE-kutoka URA ya Uganda
Mbera Mike- Lugazi Utd ya Uganda
Erick Majaliwa- kutoka JKT RUVU
Mohamed Hamad-kutoka Mwanza Utd
Obinna Mustafa- Kutoka Ocean View ya Zanzibar.

WALIOTOKA

Shabani Aboma-ameachwa
John Njama -amekwenda Police Central ya Dar Es Salaam
Bakari Nzige- Polisi Dodoma

OFFICIAL:DERRICK WALUYA AREJEA SIMBA

TAARIFA NILIZOZIPATA HIVI PUNDE SIMBA IMEMREJESHA RASMI KIKOSINI BEKI WAKE RAIA WA UGANDA DERRICK WALUYA.
WAKATI HUO HUO DIRISHA DOGO LA USAJILI LIKIELEKEA UKINGONI KLABU HIYO IMEDHIBITISHA KUWATOA KWA MKOPO WACHEZAJI WAKE WATATU KWENDA VILABU MBALI MBALI.
WACHEZAJI HAO NI:
BEKI WA PEMBENI SALUM KANONI - AMEKWENDA MORO UTD
KIUNGO SHIJA MKINA- AMEKWENDA KAGERA SUGAR
KIUNGO AMRI KIEMBA -AMEKWENDA POLISI DODOMA

BREAKING NEWS: UHAMISHO WA RAMADHANI CHOMBO 'REDONDO' KWENDA MORO UTD WAKWAMA



UHAMISHO WA KIUNGO RAMADHANI CHOMBO KWENDA MORO UTD KWA MKOPO KUTOKEA AZAM FC UMESHINDIKANA, TAARIFA AMBAZO BLOG HII IMEZIPATA HIVI PUNDE ZINASEMA KWASASA KIUNGO HUYO ATABAKI AZAM AU ATAHAMIA SIMBA IWAPO OFA YA SIMBA KUMCHUKUA KWA MKOPO KWA ADA YA TSH MILIONI 10 ITAKUBALIWA,PAMOJA NA SIMBA KUIPA AZAM MILIONI 10 PIA IPO TAYARI KUMLIPA MSHAHARA KIUNGO HUYO ALIYEBAKISHA MWAKA MMOJA NA NUSU KWENYE MKATABA WAKE NA AZAM FC. WAKATI HUO HUO UONGOZI WA AZAM UPO KWENYE KIKAO WAKIIJADILI OFA HIYO TOKA KLABU YA SIMBA.

SAMIR NASRI NUSURA AZICHAPE NA FRIMPONG


Samir Nasri jana nusura apigane na mchezaji wa Arsenal Emmanuel Frimpong wakiwa njiani kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo katika uwanja wa Emirates baada ya kipenga cha mwisho cha mchezo uliozikutanisha Manchester City dhidi ya Arsenal.


Kumekuwa na uhusiano mbaya kati yao tangu Frimpong alipo react juu ya uhamisho wa £24m wa Nasri kujiunga na City in August baada ya kutweet: “Pesa ndio mzizi wa ushetani”

Wachezaji hawa wawili walipokutana jana katika mechi ya Carling cup ambayo Arsenal walifungwa waliendelea kuzozana mara tu baada ya mchezo huo.

CHUJI KUANZA MAZOEZI YANGA LEO



Mchezaji Athumani Idd’Chuji’ aliyerudishwa kuichezea timu ya Yanga ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kuanza mazoezi na timu hiyo Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam leo kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chuji ambaye hajacheza mpira kwa muda mrefu sasa aliondoka Yanga muda mfupi baada ya kumalizika Ligi Kuu Tanzania Bara Aprili mwaka huu, kisha akajiunga na Simba aliyochezea Kombe la Kagame Julai mwaka huu, lakini alitemwa na timu hiyo kwenye usajili wa Ligi Kuu msimu huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Yanga Selestine Mwesigwa alisema kuwa wamemrudisha kundini kiungo huyo na kwamba leo atakuwepo mazoezini.

Mwesigwa alisema wamemsajili kiungo huyo kwa kumpa mkataba wa miezi sita, ambao watamuongeza kulingana na uwezo atakaouonesha uwanjani.

“Tutakuwa naye mpaka msimu huu wa ligi utakapokwisha ,tutamuongeza kulingana na uwezo atakaouonesha,”alisema.

Pia alieleza kuwa wamewarudisha wachezaji wao chipukizi Salumu Telela na Omega Seme waliokuwa kwa mkopo Moro United.

Kuhusiana na wachezaji wengine timu hiyo iliowasajili Mwesigwa alisema bado usajili wao haujakamilika na kwamba wataweka wazi pindi utakapokamilika.

“Mimi napenda kuzungumza mambo yaliyokamilika kwani yana uhakika, tutaweka wazi majina ya wachezaji wengine pindi usajili wao utakapokamilika,” alisema.

JUVENTUS 3-3 NAPOLI

BARCELONA WAPUNGUZA PENGO LA POINTI NA REAL MADRID

LIVERPOOL WAENDELEZA UONEVU KWA CHELSEA-WAITANDIKA 2-0 IN CARLING CUP

SERGIO AGUERO AIPELEKA CITY NUSU FAINALI YA CARLING CUP

MIAKA 50 YA UHURU : KOMBE LA GOSSAGE

BAADA ya vita vikuu ya pili vya Dunia (W.W.II) hadi Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961, mafanikio pekee ya Tanganyika katika michezo kwa ujumla na hasa mpira wa miguu ilikua ni katika michuano ya Kombe la Gossage iliyokua ikishindaniwa na makoloni ya Uingereza ya Afrika Mashariki.

Mwanzo wa miaka ya 1950 (1952-53) Tanganyika ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mara mbili kwa msaada wa mshambuliaji wake mahiri, William Nashon.
Nahodha wa Kenya Joe Kadenge akipokea Kombe la Gossage kwenye miaka ya 60
Baada ya hapo, Kombe la Gossage lilikuwa likitwaliwa na Uganda na Kenya kwa miaka mingi. Uganda ilikuwa na wachezaji hatari sana, hasa Kalibala na kipa wao Aggard. Lakini Kenya pia ilikuwa na nyota kadhaa wakiwemo Peter Orange, Elijah Lidonde, Shem Chimoto, Ali Kajo, Joe Kandege aliwahi kumvunja kipa mkono katika mechi iliyochezwa kwenye mvua na mipira ya kizamani ilikuwa inanyonya maji, hivyo shuti lake lilimvunja kipa mkono. Kandege alikua anaogopwa na makipa wengi.

Tanganyika pamoja na kuwa na wachezaji wenye vipaji kama Mwemba, Washokera na kipa bora Afrika Mashariki wakati huo Miraji, haikuweza kuhimili vishindo vya Wakenya na Waganda. Kutambiana kati ya Kenya na Uganda bado kunaendelea hadi leo.

Zanzibar mbali na kuwa ndiyo timu iliyokuwa ikiisumbua sana Uganda, ilibaki kuwa timu ya kupatia mabao na kuwafurahisha watazamaji kwa pasi zao za chini chini na kuvutia.

Hali hii iliendelea mpaka Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961. Baada ya uhuru, kocha kutoka Yugoslavia aitwaye Celebic alipewa jukumu la kuifundisha Tanganyika. Haikuchukua muda kwa Celebic kugundua kuwa, Tanganyika ilikuwa inazidiwa na Kenya na Uganda.

Kuzidiwa huko kwa Tanganyika hakukuwa kwa vipaji au akili pekee, bali hata nguvu ya mwili. Baada tu ya michuano ya Kombe la Taifa iliyokusanya mikoa yote katika Uwanja wa Ilala (Karume), Celebic alichagua wachezaji wengi wapya baadhi yao kutoka mikoa ambayo haikuwahi kutoa wachezaji wa timu ya taifa wakiwemo Kama Chuma na Dini kutoka Mtwara.

Baada ya kuwasuka vizuri, kazi ikaanza. Matokeo yake Tanganyika ilichukua Ubingwa wa Afrika Mahariki mara tatu mfululizo hadi Celebic alipoondoka. Hadi leo hajatokea kocha kama yeye hapa nchini.

NINI MAANA YA MCHEZAJI KUHAMA KWA MKOPO ?

Wakati dirisha dogo la usajili wa bongo likiwa linafungwa usiku wa leo,nimeona si vibaya kuandika juu ya utaratibu wa mchezaji kuhamishwa kwa mkopo kutoka klabu moja kwenda nyingine unavyofanyika.
Nimeamua kufanya hivi baada ya kugundua utaratibu wa kuhamisha wachezaji kwa mkopo hapa bongo unafanyika kiholela sana.
Kwenye soka mchezaji kuondoka kwa mkopo maana yake ni kwenda kuichezea timu nyingine ambayo hana mkataba nayo kwa muda maalum. Mikataba ya mikopo huwa inakuwa ya muda husika kama vile wiki kadhaa hadi wakati mwingine msimu mzima.
Wachezaji wanaweza kupelekwa timu nyingine kwa mkopo kwa sababu kadhaa na mara nyingi wachezaji wachanga hupelekwa sehemu nyingine kwa mkopo ili wapate uzoefu na hatimaye watumike baadaye kwenye timu zao .
Katika mfano huu timu ya mchezaji inaweza kuendelea kulipa mshahara wa mchezaji au vinginevyo kuendana na makubaliano yaliyopo baina ya pande tatu husika na baadhi ya timu huweka mazingira maalumu baina yake na baadhi ya vilabu ambapo timu ndogo hutumika kama timu ya kulea wachezaji kwa mkopo yaani feeder club , mfano Man United wana makubaliano na Royal Antwerp ya Ubelgiji na Arsenal wana makubaliano na Beveren.


Mkopo pia unaweza kutumiwa katika mazingira ya kusubiri muda wa dirisha la usajili kufunguka ambapo makubaliano maalum yanaweza kuwekwa ili kuipa timu fursa ya kumsajili mchezaji husika kwa muda mrefu.
Klabu inaweza kumchukua mchezaji kwa mkopo kama haina fedha ya kutosha kufanya usajili lakini wanaweza kulipa mishahara kwa muda na pia wachezaji huchukuliwa kwa mkopo kama mbadala wa wachezaji wanaoumia au kufungiwa kwa muda mrefu.
Klabu ya kwanza ya mchezaji husika inaweza kuhitaji fedha kutumika kama ada ya uhamisho wa mkopo au inaweza kuwapa wanaohitaji mchezaji wake masharti ya kuwalipa wachezaji walioko kwa mkopo huku pia wachezaji hutolewa kwa mkopo endapo kuna wachezaji waliokuwa wameumia wamerejea au kama timu haina fedha za kutosha na inataka kupunguza gharama.
Kuna baadhi ya wachezaji wengine hutolewa kwa mkopo kwa kuwa hawana furaha kwenye klabu walizopo au wameingia kwenye mazingira ya ugomvi na viongozi wao na hakuna klabu inayowahitaji kwa muda mrefu na hapa kuna mifano ya akina Henri Camara akiwa Wolves na Craig Bellamy akiwa na Man City na kabla ya hapo Newcastle United.
Kwenye Ligi kuu ya England wachezaji wanaocheza kwa mkopo hawaruhusiwi kucheza dhidi ya timu zao za msingi au timu zenye usajili wao(hii ni kwa mujibu wa sehemu ya 7.2 ya sheria ya m.6) ambapo hii inamaanisha kuwa klabu kubwa yaweza kumtoa mchezaji wake kijana kwenye timu ndogo huku ikifurahia kushuhudia anachofanya dhidi ya timu nyingine kubwa ambazo ni wapinzani wake huku wakiwa hawaruhusiwi kuidhuru timu ya msingi .
Hata hivyo wachezaji walioko kwa mkopo wanaweza kucheza dhidi ya timu zao kwenye michezo ya vikombe .

Tuesday, November 29, 2011

HAPPY BIRTHDAY GIGGS

BARCELONA WATIMIZA MIAKA 112 TANGU KUANZISHWA

***WENGI WANAAMINI NDIO KLABU BORA KABISA KWA SASA-ILIANZISHWA MWAKA 1899, HIVYO LEO HII INATIMIZA MIAKA 112 TANGU KUANZISHWA KWAKE.**************
************************BEJI YAO YA KWANZA KUITUMIA **************************

***HII NDIO JEZI YA KWANZA KUANZA KUTUMIKA KWA KLABU HII**************

***KOMBE LA KWANZA KUSHINDA KLABU YA BARCELONA MWAKA 1902**
***HUU NDIO UWANJA WA KWANZA KUANZA KUTUMIKA KAMA UWAJA WA NYUMBANI WA BARCA***********

KILIMANJARO STARS YAITANDIKA DJIBOUTI MABAO 3:0

HATIMAE KILIMANJARO STARS IMEFANIKIWA KUPATA USHINDI WA KWANZA KWENYE MASHINDANO YA CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP 2011 BAADA YA KUIFUNGA DJIBOUTI MABAO 3-0.
MABAO HAYO YAMEFUNGWA NA THOMAS ULIMWENGU,MWINYI KAZIMOTO NA YUSUF RASHID.
WAKATI HUO HUO RWANDA IMEIFUNGA ZIMBABWE MABAO 2-0 KWENYE MCHEZO ULIANZA MAPEMA.

Azam msimlazimishe Chombo kwenda Moro Utd..


Nimeamka asubuhi ya leo kama ilivyo kawaida yangu kabla ya hata kunywa chai huwa naingia kwenye mitandao mbali mbali pamoja na kusoma magazeti kuona yaliyojili kwenye ulimwengu wa michezo, kwenye mtandao wa BBC nikakutana na habari ya AC Milan kusisitiza kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Carlos Tevez toka klabu ya Manchester City.
Wakati napitia kwenye magazeti ya michezo nikakutana na habari ya Azam kumpeleka kwa mkopo kunako klabu ya moro utd kiungo wao mchezeshaji Ramadhani Chombo ‘Redondo’.
Sports Management and Administration ni maeneo yenye mapungufu makubwa kwenye soka la bongo! leo nimeshangazwa sana na taarifa eti Azam wamempeleka kwa mkopo Ramadhan Chombo ' Redondo ' kwa Moro Utd.

ninachokijua ni kwamba hakuna uhamisho wa mchezaji unaofanyika pasipo pande husika kukubaliana au kuridhiana! kwa maana ya mchezaji na klabu kukaa chini na kukubaliana kabla ya maamuzi ya kuuzwa au kuhamishwa kutolewa kwenda kucheza sehemu husika.
haiwezekani na haijawahi tokea mchezaji kuuzwa ama kuhamishwa pasipo kupewa taarifa na yeye mwenyewe kuwa na ridhaa na timu atakayoenda kuchezea...kwa mujibu wa Redondo mwenyewe hajapewa taarifa hizo na hayupo tayari kwenda Moro Utd,haya mambo ya kienyeji yamekua yakifanyika sana hapa bongo na inanisikitisha sana hasa klabu kama AZAM inapofanya maamuzi kama haya...

Redondo kwa Azam ni kama David Silva kwa Man City, Mario Goetze pale Dortmund, Xavi pale Barcelona na wengine wengi tu. Redondo ni super star wa Azam kwasasa,kama Azam waliona hana msaada kwao basi wangemwambia mapema kabla ya hata dirisha dogo kufunguliwa ili atafute timu na si kumlazimisha kujiunga na timu wanayotaka wao..hili jambo la kuwauza wachezaji kama kuku au mbuzi naona limezidi sasa na linatakiwa kukemewa kwa nguvu zote na kupigwa vita..hii terminology ya 'by mutual consent' kwa maana ya makubaliano ya pande zote husika,imekua ikitumika sana pindi mkataba unapotaka kuvunjwa au vinginevyo...kuna mchezaji mtovu wa nidhamu kwasasa kama Carlos Tevez ? tusubiri tuone january kama City watamlazimisha Tevez kwenda Wolves kwa mkopo.. ninachokiamini pamoja na City kutomuhitaji tena Tevez pale Etihad Stadium lakini hawawezi kumlazimisha kwenda klabu wanayoitaka wao na ndio maana hata hivi tunavyozungumza Tevez yuko kwao Argentina lakini City wameheshimu mkataba walioingia naye na analipwa mshahara wake kama kawaida hadi usuluhishi wa suala lake utakapopatikana.
Kwahiyo basi nawaomba viongozi wa Azam wakae chini na Redondo hatimae yatoke maamuzi yatakayozinufaisha pande zote mbili huku wakitambua fika dirisha linafungwa ndani ya masaa 24 yajayo.

DROGBA AKATAA KUSAINI MKATABA MPYA NA CHELSEA - KUONDOKA MWISHONI MWA MSIMU



Didier Drogba yupo tayari kuondoka Chelsea baada ya kukataa kusaini mkataba mpya.


mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33, yupo katika siku za mwisho mwisho za mkataba wake unaomuingizia £120,000 kwa wiki na amekataa nyongeza ya miezi 12 katika mkataba wake.


Sasa anajiandaa kuondoka Stamford Bridge akiwa huru kipindi kijacho cha kiangazi kuelekea Russia au Qatar.


Agent wa Drogba Thierno Seydi, alisema jana usiku: “Didier alipewa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja na Chelsea. Lakini ameona haumfai.


“Tunajua nini tunataka, wapi tunataka kwenda na kwa ofa ya namna gani. AC Milan walikuja na dili la mkopo kwa Didier wakiwa na option ya kumnunua pia, lakini niliwaambia haiwezekani. Ofa yao haikutuvutia.


“Kwa umri huu wa Didier, hana kipya cha ku-prove kama mchezaji. Ataenda mahala ambapo watatoa mkwanja mrefu zaidi. Inaweza kuwa Marekani , Russia, Qatar au popote in Asia.


“Unapokuwa tayari katika umri wa miaka ya 30 unatakiwa uende katika timu ambayo una uhakika utapata pesa ya kuweza kukuwezesha kuishi vizuri. LA Galaxy ni moja ya timu ambazo Drogba anaweza kujiunga nazo. Pia Anzhi, wanalipa vizuri lakini sio mimi wala Didier tumepokea ofa kutoka kwa timu hizo.”


Drogba alisajiliwa na Jose Mourinho kutoka Marseille kwa ada ya £24million in 2004 na amefunga magoli 146 katika kipindi cha miaka 7 aliyokaa Chelsea.


Habari za Drogba kutaka kuondoka zimekuja siku chache baada ya mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Marcel Desailly kusema kwamba klabu hiyo sasa imegawanyika chini ya Andre Villas Boas, timu haina umoja.


CRISTIANO RONALDO AVUNJA REKODI YAKE MWENYEWE


Real Madrid wapo on top of the league wakishinda mechi 11 kati ya 13, na wameshinda mechi zao zote za makundi in Champions league. Cristiano Ronaldo ndio mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio haya. Ndiye anayeongoza kwa ufungaji in La Liga akiwa na magoli 16 na jumla akiwa amefunga magoli 20 msimu huu. So far ndani ya mwaka huu , mreno huyu ameshafunga mabao 48, akiivunja rekodi yake mwenyewe ya magoli 45 aliyotia kambani in 2010.
































































































































CRISTIANO RONALDO'S GOALS



YEAR



CLUB



LEAGUE



UCL



CUP



OTHER



TOTAL







2011



Real Madrid



39



5



3



1



48







2010



Real Madrid



36



5



4



-



45







2009



Real Madrid /Manchester United



17



10



1



1



29







2008



Manchester United



26



3



3



2



34







2007



Manchester United



18



8



3



-



29







2006



Manchester United



18



-



-



-



18







2005



Manchester United



7



1



4



-



12







2004



Manchester United



4



-



-



-



4







2003



Manchester United/Sporting Portugal



1



-



-



-



1







2002



Sporting Portugal



3



-



-



-



3







TOTAL



169



32



18



4



223












JOHN TERRY AFANYIWA MAHOJIANO NA POLISI DHIDI YA KESI YA KUMTUSI FERDINAND


Polisi wanaochunguza madai dhidi ya John Terry kutoa mananeo ya kibaguzi dhidi ya Anton Ferdinand walimuita na kumfanyia mahojiano nahodha wa England na Chelsea.

Wapelelezi kutoka Hammersmith na Fulham walimfanyia mahojiano nyumbani kwa Terry Ijumaa iliyopita.

Terry anatuhumiwa kumtolea maneno ya kibaguzi Ferdinand wakati Chelsea walipofungwa na Queens Park Rangers mwezi uliopita.

Polisi wanaendelea kuuchunguza mkanda wa video wa mchezo uliofanyika katika uwanja wa Loftus Road.

Terry, ambaye pia anashatakiwa na FA, amekataa kwamba alimtukana mlinzi wa QPR lakini amekiri alitumia maneno ya kuudhi.

Alisisitiza alitoa maneno aliyoyatoa Ferdinand ameyatafsiri vibaya lakini hakuwa amemaanisha kumbagua. John Terry anaamini kamati ya FA itakayochunguza kesi yake ndio itakuwa nafasi pekee kwake kusafisha jina lake.

NGORONGORO HEROES KWENDA BOTSWANA KESHO

Kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya Taifa kwa vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na viongozi watano kinatarajia kuondoka kesho (novemba 30 mwaka huu) kwa ndege ya PrecisionAir kwenda Gaborone, Botswana.

Ngorongoro Heroes itaondoka saa 20.20 usiku kupitia Johannesburg, Afrika Kusini kwenda huko kushiriki michuano ya umri huo ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA). Michuano hiyo itafanyika kuanzia Desemba 1-10 mwaka huu ikishirikisha timu za mataifa 11 wanachama wa COSAFA na Tanzania inayoshiriki kama mwalikwa.

Wachezaji watakaoondoka ni Saleh Malande (Simba), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Suagr), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Said Samir (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Domayo (JKT Ruvu Stars) na Omega Seme (Yanga).

Wengine ni Atupele Green (Yanga), Jerome Reuben (Moro United), Simon Happygod (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Abdallah Hussein (AFC), Rajab Mohamed (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Emily Josiah (TSC Mwanza), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting Stars). Ngorongoro Heroes iko kundi C pamoja na Zambia, Afrika Kusini na Mauritius na itacheza mechi yake ya kwanza Desemba 2 mwaka huu dhidi ya Zambia.

Mechi ya pili itakuwa Desemba 4 mwaka huu dhidi ya Afrika Kusini wakati ya mwisho katika hatua hiyo ya makundi ni dhidi ya Mauritius itakayochezwa Desemba 6 mwaka huu. Msafara wa timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Muhsin Balhabou. Wengine katika msafara huo ni Kocha Mkuu Kim Poulsen, Kocha Msaidizi Mohamed Rishard, Daktari wa timu Dk. Joakim Mshanga na kocha wa makipa Peter Manyika.

Monday, November 28, 2011

MILOVAN ASAINI MKATABA WA MIEZI SITA KUIFUNDISHA SIMBA..

KOCHA MPYA WA SIMBA MILOVAN CIRKOVIC AKISAINI MKATABA KWENYE HOTEL YA MOVEN PICK JIJINI DAR ES SALAAM.


HAPA AKIWA NA MWENYEKITI WA SIMBA ALHAJ ISMAIL ADEN RAGE.



MWENYEKITI WA KAMATI YA UFUNDI IBRAHIM MASOUD 'MAESTRO ' ALIKUA SHUHUDA WA TUKIO HILO.






Ibrahimovic Afikisha mabao 100 nchini Italia.




HILI NI MOJA YA KATI YA MABAO MAZURI NILIYOWAHI KUYAONA, IBRAHIMOVIC ALIFUNGA BAO HILI WAKATI HUO AKIWA AJAX AMSTERDAM YA NCHINI UHOLANZI.


Juventus
(2004-2006)

Michezo 69


Mabao 23
Inter Milan
(2006-2009)


Michezo 88


Mabao 57

AC Milan
(2010-present)


Michezo 38


Mabao 21


JUMLA


MICHEZO 196


MABAO 101