Polisi wanaochunguza madai dhidi ya John Terry kutoa mananeo ya kibaguzi dhidi ya Anton Ferdinand walimuita na kumfanyia mahojiano nahodha wa England na Chelsea.
Wapelelezi kutoka Hammersmith na Fulham walimfanyia mahojiano nyumbani kwa Terry Ijumaa iliyopita.
Terry anatuhumiwa kumtolea maneno ya kibaguzi Ferdinand wakati Chelsea walipofungwa na Queens Park Rangers mwezi uliopita.
Polisi wanaendelea kuuchunguza mkanda wa video wa mchezo uliofanyika katika uwanja wa Loftus Road.
Terry, ambaye pia anashatakiwa na FA, amekataa kwamba alimtukana mlinzi wa QPR lakini amekiri alitumia maneno ya kuudhi.
Alisisitiza alitoa maneno aliyoyatoa Ferdinand ameyatafsiri vibaya lakini hakuwa amemaanisha kumbagua. John Terry anaamini kamati ya FA itakayochunguza kesi yake ndio itakuwa nafasi pekee kwake kusafisha jina lake.
Wachezaji inabidi wawe na nidhamu nje na ndani ya uwanja, hasa matusi sio mazuri maana yana washushieni heshime wote.
ReplyDeletePia pata links mbalimbali kama za michezo na nyinginezo za kitanzania katika http://www.tanzaniakwetu.com