Search This Blog

Tuesday, November 29, 2011

Azam msimlazimishe Chombo kwenda Moro Utd..


Nimeamka asubuhi ya leo kama ilivyo kawaida yangu kabla ya hata kunywa chai huwa naingia kwenye mitandao mbali mbali pamoja na kusoma magazeti kuona yaliyojili kwenye ulimwengu wa michezo, kwenye mtandao wa BBC nikakutana na habari ya AC Milan kusisitiza kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Carlos Tevez toka klabu ya Manchester City.
Wakati napitia kwenye magazeti ya michezo nikakutana na habari ya Azam kumpeleka kwa mkopo kunako klabu ya moro utd kiungo wao mchezeshaji Ramadhani Chombo ‘Redondo’.
Sports Management and Administration ni maeneo yenye mapungufu makubwa kwenye soka la bongo! leo nimeshangazwa sana na taarifa eti Azam wamempeleka kwa mkopo Ramadhan Chombo ' Redondo ' kwa Moro Utd.

ninachokijua ni kwamba hakuna uhamisho wa mchezaji unaofanyika pasipo pande husika kukubaliana au kuridhiana! kwa maana ya mchezaji na klabu kukaa chini na kukubaliana kabla ya maamuzi ya kuuzwa au kuhamishwa kutolewa kwenda kucheza sehemu husika.
haiwezekani na haijawahi tokea mchezaji kuuzwa ama kuhamishwa pasipo kupewa taarifa na yeye mwenyewe kuwa na ridhaa na timu atakayoenda kuchezea...kwa mujibu wa Redondo mwenyewe hajapewa taarifa hizo na hayupo tayari kwenda Moro Utd,haya mambo ya kienyeji yamekua yakifanyika sana hapa bongo na inanisikitisha sana hasa klabu kama AZAM inapofanya maamuzi kama haya...

Redondo kwa Azam ni kama David Silva kwa Man City, Mario Goetze pale Dortmund, Xavi pale Barcelona na wengine wengi tu. Redondo ni super star wa Azam kwasasa,kama Azam waliona hana msaada kwao basi wangemwambia mapema kabla ya hata dirisha dogo kufunguliwa ili atafute timu na si kumlazimisha kujiunga na timu wanayotaka wao..hili jambo la kuwauza wachezaji kama kuku au mbuzi naona limezidi sasa na linatakiwa kukemewa kwa nguvu zote na kupigwa vita..hii terminology ya 'by mutual consent' kwa maana ya makubaliano ya pande zote husika,imekua ikitumika sana pindi mkataba unapotaka kuvunjwa au vinginevyo...kuna mchezaji mtovu wa nidhamu kwasasa kama Carlos Tevez ? tusubiri tuone january kama City watamlazimisha Tevez kwenda Wolves kwa mkopo.. ninachokiamini pamoja na City kutomuhitaji tena Tevez pale Etihad Stadium lakini hawawezi kumlazimisha kwenda klabu wanayoitaka wao na ndio maana hata hivi tunavyozungumza Tevez yuko kwao Argentina lakini City wameheshimu mkataba walioingia naye na analipwa mshahara wake kama kawaida hadi usuluhishi wa suala lake utakapopatikana.
Kwahiyo basi nawaomba viongozi wa Azam wakae chini na Redondo hatimae yatoke maamuzi yatakayozinufaisha pande zote mbili huku wakitambua fika dirisha linafungwa ndani ya masaa 24 yajayo.

4 comments:

  1. Shaffih ulichokisema ni sahihi kabisa "Sports Management and Administration ni maeneo yenye mapungufu makubwa kwenye soka la bongo" na hii inapelekea wachezaji wengi wa kibongo kuburuzwa tu. Ifike mahali hawa wanaojiita viongozi wa mpira wajue kuwa Mpira ni kazi kama kazi nyingine na mchezaji anapaswa kuheshimiwa, hivi wanafikiri kucheza mpira ni kazi rahisi sana, mimi nilifikiri ligi ya bongo imeanza kuwa professional league kumbe wapi, Simba nao walifanya uhuni kama huo kwa banka siku si nyingi sina uhakika kama walikwishamlipa fedha zake ama la ila kwa kweli si haki hata kidogo, na huyu Redondo mbona bado ana kiwango kikubwa sana jamani huyo jamaa ni kiungo wa ukweli wakati yupo simba alikuwa akiingia kama super sub lazima aletee balaa kwa timu pinzani.
    Azam kaeni chini muangalie vizuri mnataka kumpoteza mmoja wa wachezaji bora kabisa mmenunua magarasha kutoka Ghana na Ivory Coast naona yamewachanganya sasa. Azam mmeanza kukurupuka.
    Mike.

    ReplyDelete
  2. Azam wakimtoa kwa mkopo Ridondo watajuta!!

    nazani wanababaika na hao wageni!!!

    ReplyDelete
  3. Nikweli soka la bongo sijui tuna nia nalo gani ki ukweli Azam fc ndio tuliwategemea sana kuja kuleta mapinduzi ya undava wa simba na yanga dah kumbe gonjwa ile ile baba moja mama moja..
    unamlazimisha redondo kwenda moro huku mwenyewe hajui lolote huu c utumwa ktk soka jamani kwann,mbona huyo mchezajo mwenyewe anatakiwa na simba na yy yupotayar ss kwann mnambania azam hamfanani na mambo yenu banaaa...

    ReplyDelete
  4. Shaffih uko sawa kbs bip up! Mzaz wa2 km nyiny 2nawahitaj sn hapa bongo bila hvyo ha2end, mana kuna wa2 wanaendesha soka la bongo km vile baba mlev alirud home!

    ReplyDelete