Search This Blog

Friday, June 15, 2012

SHOMARY KAPOMBE MWANAMICHEZO BORA WA MWAKA 2011


TUZO ZA TASWA ZILIVYOFANA USIKU HUU DIAMOND JUBILEE

Rais wa TFF, Leodegar Tenga wa pili kulia akiwa na Jellah Mtagwa kushoto kwake


Familia ya ndondi


Wadau wa ndondi
Tedi Mapunda kulia na bosi wake 


Eiphraim Mafuru kulia


Maswahiba wa siku nyingi, Shaaban Mkongwe kulia akiwa Waziri Mahadhi


Beki wa Mtibwa Salum Swedi 'Kussi'


Kaburu kulia akikabidhi tuzo


Daud Salum 'Bruce Lee' kulia akikabidhi tuzo


Athumani Hamisi akikabidhi tuzo


Asha Baraka akikabidhi tuzo


Mafuru akikabidhi tuzo


Ridhiwani Kikwete kulia akiwa na Benny Kisaka kushoto, cheko la maana


Dioniz Malinzi kushoto akikabidhi tuzo


Kapombe akipokea tuzo ya Mwanamichezo Bora Chipukizi kutoka kwa Salim Amir


Mzee Matumla akimkabidhi Kaburu tuzo ya Emmanuel Okwi


Mwenyekiti wa RT, akimkabidhi tuzo Mwanahamisi Gaucho


Aggrey Morris kushoto akipokea tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka 


Ally Choky akikabidhi tuzo


Mafuru akipakia msosi


Kim Poulsen kulia akiwa na nani sijui


Jamal Rwambow kulia na Kaburu wakati wa maakuli


Serengeti Beer inapokolea, mambo huwa hivi...


Mzee El Maamry akimkabidhi tuzo George Tarimo


Mzee Mwinyi akimkabidhi tuzo Adolph Rishard


Mzee Mwinyi akimkabidhi tuzo Peter Tino


Mzee Mwinyi akikabidhi tuzo


Waziri Mahadhi akimpokelea tuzo marehemu baba yake, Omar Mahadhi


Kaburu akimsaidia Kapombe kupokea tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwaka 2011 


Juma Pinto akikabidhi tuzo


Zena Chande na swahiba zake


Shaffih Dauda kulia, Amour Hassan na Michael Maluwe


Tullo Chambo na bosi wake


Akina nani sijui hawa


BIN ZUBEIRY kulia na Shaffih Dauda


MAJINA YA WASHINDI

1: OLIMPIKI MAALUM-Zanzibar
Ahmada Bakar:

2:OLIMPIKI MAALUM-TANZANIA BARA
HERITH SULEIMAN

3: PARALIMPIKI: WANAUME
ZAHARANI MWENEMTI

4:PARALIMPIKI: WANAWAKE
FAUDHIA CHAFUMBWE

5: KIKAPU: WANAUME
GEORGE TARIMO:

6:  KIKAPU WANAWAKE
EVODIA  KAZINJA:-

7: NETIBOLI:
LILIAN SYLIDION

8:  GOFU WANAWAKE:
MADINA IDDI

9: GOFU WANAUME:
Frank Roman:

10: NGUMI ZA RIDHAA
SULEIMAN SALUM KIDUNDA

12:  WAOGELEAJI MWANAMKE
MAGDALENA MOSHI     

WAOGELEAJI MWANAUME
AMMAAR GHADIYALI  -  MEN

13:JUDO...
AZZAN HUSSEIN KHAMIS (ZANZIBAR)
14:JUDO BARA: . MBAROUK SELEMANI

14: WAVU WANAWAKE
THERESIA ABWAO  

15: WAVU WANAUME
MBWANA ALLY

16: NGUMI ZA KULIPWA
 Nasibu Ramadhan

17. TENISI:Wanaume
WAZIRI SALUMU

18. TENISI WANAWAKE: 
REHEMA ATHUMANI

20: BAISKELI (Wanawake)
Sophia Hussein
-
21: BAISKELI WANAUME
Richard Laizer

22: WACHEZAJI WA TANZANIA WANAOCHEZA NJE
Mbwana Samatta-

23: MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI
SHOMARI KAPOMBE- (soka) SIMBA

24: MCHEZAJI WA NJE ANAYECHEZA TANZANIA
Emmanuel Okwi-Simba

25: SOKA (WANAWAKE)
MWANAHAMISI OMARI

26: SOKA WANAUME
Aggrey Morris-Azam:

27: RIADHA
WANAWAKE
Zakia Mrisho:

28: RIADHA WANAUME
Alphonce Felix:

29: MIKONO WANAUME
Kazad Monga-Magereza Kiwira
Faraji Shaibu  Khamis-Nyuki Zbar

30:  MIKONO WANAWAKE
Zakia Seif-Ngome Dar

31: Kriketi WANAWAKE
Miss. Monika Pascal

32; KRIKETI WANAUME
Mr. Kassimu Nassoro

33: TUZO YA HESHIMA:
KIKOSI KILICHOFUZU FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA 1980

34:MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA MWAKA 2011-
SHOMARI KAPOMBE
 
 

THE RETURN OF ELNINO: TORRES AWAFUNGASHA VIRAGO IRELAND - SPAIN IKIKAA KILELENI MWA KUNDI C


Spain 4-0 Rep. of Ireland (Euro 2012 - Group C)... by fasthighlights-2012

ITALY 1-1 CROATIA - PIRLO NA MODRIC WATOKA NGOMA DROO


Italy 1-1 Croatia (Euro 2012 - Group C) Highlights by fasthighlights-2012

Thursday, June 14, 2012

DIDIER DROGBA AMFUNIKA YAYA TOURE: ASHINDA TUZO YA UCHEZAJI BORA WA MWAKA WA IVORY COAST

Didier Drogba ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ivory Coast, akimfunika mchezaji wa Manchester City Yaya Toure na mshambulaiji wa Aroune Kone kwenye kura zilizopigwa na waandishi wa nchi hiyo pamoja na watumiaji wa internet.

Mshambuliaji huyo aliye njiani kuondoka Chelsea alipata kura 110 kutoka kwa waandishi wa habari na kura 17, 863 kwa internet, na kwa ujumla akapata asilimia 37.69 za kura zote, huku mchezaji bora wa Africa Yaya Toure akimaliza kwa kupata asilimia 30.16%, huku mchezaji wa Sevilla akimalizia kwa kupata asilimia 12.29%.

Drogba anapata tuzo hii kwa mara ya pili, baada ya kushinda kwa mara ya kwanza mwaka 2007.

Nahodha huyo wa The Elephants aliisadia kucheza mpaka kwenye fainali ya AFCON 2012 nchini Gabon na Equatorial Guinea.

Ingawa alikosa peanti muhimu kwenye mechi ya fainali dhidi ya Zambia.

Drogab, 34, alitangaza uamuzi wa kutaka kuondoka Chelsea siku 3 baada ya kushinda kombe la mabingwa wa ulaya mwezi uliopita, baada ya kuisadia The Blues kwa kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Bayern Munich kabla ya kufunga penati ya ushindi iliyoipa Chelsea ubingwa wa kwanza wa ulaya.

 

MIAKA 10 ILIYOPITA YA USHUJAA WA IKER CASILLAS ULIANZIA KWENYE MECHI DHID YA IRELAND - HISTORIA KUJIRUDIA USIKU HUU?


Iker Casillas, Spain
Iker Casillas sasa hivi anacheza kwenye michuano ya sita mikubwa ya kimataifa akiwa na Spain. Golikipa wa Real Madrid amekuwa akitajwa ni mmoja ya magolikipa bora duniani tangu alipocheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa chini ya Jose Antonio Camacho mwaka 2002, na tangu wakati huo amekuwa hana mpizani kwenye milingoti mitatu ya Spain.

Na ilikuwa miaka 10 iliyopita, dhidi ya wapinzani wao watakaocheza nao leo usiku Ireland, siku ambayo Casillas aliweka jiwe la msingi la kujenga historia yake ndani Spain na kwenye soka kwa ujumla, aliokoa penati tatu kwenye raundi ya pili ya michuano ya kombe la dunia na kuipeleka Spain kwenye robo fainali.

Hivyo katika kuelekea mchezo wa leo usiku dhidi ya Ireland, ebu tuangalie historia ya kishujaa ya Iker Casillas ilivyojengwa kwa matukio makubwa.

2002 WORLD CUP: SPAIN 1-1 IRELAND: THE PENALTY LEGEND BEGINS

Michuano ya World Cup ya Japan na Korea ndio yalikuwa jiwe la kwanza la msingi wa ushujaa wa Casillas kwenye timu ya taifa. Kipa wa Madrid, alikuwa chaguo la pili nyuma ya Santiago Canizares, Iker alipata nafasi ya kucheza baada ya golikipa Santiago kuumia. Casillas, ambaye mwezi mmoja kabla alicheza kwa mafanikio na kuisadia Madrid kushinda kombe la ulaya dhidi ya Bayern Leverkusen baada ya kumbadili majeruhi na Cesar Sanchez katika hatua za mwisho, ambaye pia Casillas alimbadili kwenye kikosi cha Spain baada ya kuumia.

Kwenye hatua ya 16, Spain wakakutana na Ireland na pamoja na kuongoza kwa goli la mapema la Fernando Morientes, lakini mechi hiyo ilikuwa ngumu sana. Casillas aliiokoa Spain kwenye kipindi cha pili baada ya kuokoa penati ya Ian Harte, lakini hakuweza kumzuia Robbie Keane kusawazisha na kupelekea mechi kwenda mpaka kwenye mikwaju ya penati.

Na Casillas alikuwa shujaa tena, akiokoa penati za David Connolly na Kevin Kilbane na kuipeleka Spain hatua ya mbele.

EURO 2008: SPAIN 0-0 ITALY: REWRITING HISTORY

Miaka 6 baadae, Casillas akaisadia Le Roja kuandika historia nyingine kwenye Euro 2008, akiwa nahodha kwa upande Spain kwenye michuano hiyo, wakafanikiwa kupata mafanikio kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1964. Na golikipa wa Real Madrid alicheza vizuri sana, akiokoa penati ya Di Natale na Daniele De Rossi kwenye mikwaju ya penati kufuatia dakika 120 kushindwa kutoa mshindi kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Italia.

2010 WORLD CUP: SPAIN 1-0 PARAGUAY: TAKING REINA'S ADVICE

Wakiwa njiani kwenda kubeba kombe la dunia mwaka 2010 nchini South Africa, Spain wakakutana na Paraguay kwenye robo fainali. Kikosi cha Paraguay kikiongozwa na Gerardo Martino walijipanga vizuri hasa kwenye nafasi ya kiungo na kuwafanya wachezaji wa Vicente Del Bosque kushindwa kucheza vizuri. Gerard Pique akacheza rafu kwenye box na kusababisha penati kwenye kipindi cha pili na kusababisha safari ya La Roja kwenda nusu fainali kutia mashaka.

Pepe Reina alijua kabisa wapi Oscar Cordozo angepiga mpira wa penati kick, baada ya kuwa tayari alikuwa ameshakutana na mparaguay huyo kwenye mechi kati ya Liverpool na Benfica na Cordozo kumfunga kwa penati, Reina akampa ushauri Casillas jinsi amjuavyo Cordozo na penati zake, kwa bahati nzuri Iker akafuata ushauri wa kipa mwenzake na kufanikiwa kuudaka mpira wa Cordozo na kuisadia timu ya kufika hatua iliyofuatia.

2010 WORLD CUP: SPAIN 1-0 NETHERLANDS: CASILLAS TWO; ROBBEN NIL

Katika dakika ya 61 ya mchezo wa fainali ya kombe la dunia, Arjen Robben aliiichambua kama karanga safu ya ulinzi ya Spain na kisha akaingia mpaka kwenye eneo la penati na kukutana uso kwa uso na Casillas, ambaye alizuia mpira uliokuwa ukitinga nyavuni kwa mguu.

Na kwenye dakika ya 90 ya mchezo, wawili hao wakajikuta wakikutana tena ana kwa ana. Matokeo yake yalikuwa yale yale: Robben akanyimwa bao tena na Casillas na mpira ukaenda kwenye muda wa  nyongeza kwa dakika 30, ambapo Andres Iniesta aliibuka shujaa kwa kufunga bao pekee na la ushindi kwa Spain.

Lakini tungekuwa tunaongea mengine bila kuwepo kwa shujaa Casillas.

Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’-Episode 7

*Apata balaa jingine, Wasauz wamkatia rufaa
*Yanga yapita, azuiwa kucheza nane bora Afrika
Na Saleh Ally
WIKI ILIYOPITA, tuliishia wachezaji wa Yanga akiwamo Bakari Malima wakiwa wameomba mechi yao ya marudiano dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda ichezwe mjini MWanza kwa lengo la kukimbia presha kubwa ya mashabiki jijini Dar es Salaam. Uongozi ukakubali na maandalizi yakaanza. Endelea.
TULIENDELEA na maandalizi siku kadhaa tukiwa jijini Dar es Salaam, baada ya hapo tukafunga safari kwenda Mwanza kwa ajili ya kuweka kambi huku tukiisubiri mechi dhidi ya Rayon Sports.
Wachezaji tulijua ugumu wa Wanyarwanda lakini tulipania kushinda na kuweka rekodi ya kuifikisha Yanga kwenye hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mashabiki wengi wa soka walifunga safari kutoka Dar es Salaam kuja Mwanza kutuunga mkono.
Siku ya mechi, kama ambavyo tulitarajia, ilikuwa ni ngumu na wapinzani wetu walionekana walikuwa wamejiandaa vilivyo kushinda ugenini na kusonga mbele. Walijitahidi wakapata bao lakini nasi tulifunga bao zuri lililopachikwa kimiani na mshambuliaji wetu, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’.

Mechi iliisha kwa sare ya bao 1-1, maana yake Yanga tulikuwa tumefanikiwa kuvuka hadi hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati huo tulikuwa tunasema Klabu Bingwa Afrika. Sherehe zilianzia pale CCM Kirumba hadi sehemu mbalimbali za mji wa Mwanza.
Sherehe hizo zilikuwa ni za aina yake, kwani ziliendelea jijini Dar es Salaam na sehemu nyingine nchini. Tulikuwa tumeweka rekodi mpya kwa Yanga. Binafsi nilijisikia vizuri kwa kuwa nilikuwa nimetimiza malengo ya kuilipa Yanga mazuri kwa kuwa viongozi walionyesha mapenzi kwangu.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, tulianza mara moja maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo pamoja na mingine iliyokuwa inakabiri Yanga. Kwangu, angalau niliona kama maisha yalianza kwenda vizuri tena, nilianza kuishi kawaida.
Ingawa suala la mahakamani hukumu ilishatolewa na nikaonekana sina hatia, bado wako ambao waliamini kama haikuwa sawa. Hali hiyo iliniumiza sana, kwani kila aliyejaribu kukumbushia alitonesha jeraha nililopata kwa kupata matatizo kwa kitu nisichokijua hata kidogo. Bado niliendelea kumuachia Mungu.
Niliendelea na maisha yangu ya kawaida, mara kadhaa nilikuwa nikiwasiliana na uongozi wa Vaal Professional kuhusiana na suala la kurejea Afrika Kusini. Niliona ningeweza kufanya hivyo kwa kuwa pamoja na kupata matatizo walionyesha ustaarabu kwangu.
Lakini niliona ni vizuri kama ningemaliza jukumu la kupambana kwa ajili ya Yanga kwenye michuano hiyo mikubwa ya Afrika. Maana tayari ratiba ilishatoka na tulipangiwa kuanza mechi dhidi ya Maning Rangars ya Afrika Kusini.
Nilijua ingekuwa ni mechi ngumu kwa kuwa Wasauz wana kila kitu, hivyo lazima wangejiandaa vya kutosha kwa ajili ya mechi hiyo. Lakini binafsi nilikuwa nikifanya mazoezi kuhakikisha nakuwa fiti sawasawa.
Balaa likaibuka tena, Maning Rangers kwa kuwa walikuwa wananijua wakanikatia rufaa kwamba sitakiwi kucheza michuano hiyo kwa kuwa mkataba wangu wa miaka mitatu na Vaal ulikuwa haujamalizika. Nilichanganyikiwa, lakini nikawa na matumaini huenda Shirikisho la Soka Afrika (Caf), litapuuzia.
Ingawa niliingia hofu ya kutoichezea Yanga, lakini niliamua kuweka pamba masikioni na kuendelea na mazoezi kwa nguvu kama vile nilikuwa na uhakika ningeichezea Yanga kwenye michuano hiyo hatua ya nane bora.
Siku chache kabla ya kuivaa Maning Rangers, Yanga ilipokea barua kutoka Chama cha Soka Tanzania (Fat), ilikuwa inatokea Caf. Barua hiyo ilitoa maelekezo kwamba nisingeruhusiwa kucheza, si mechi dhidi ya Wasauz pekee, badala yake zote.
Kwangu ilikuwa ni kama kisu moyoni, niliona maisha yangu yalikuwa yamejaa misukosuko. Ilikuwa kama wamenikumbusha upya matatizo yaliyonipata wakati ninatokea Sauz. Niliamua kwa mara nyingine kumuachia Mwenyezi Mungu.
Nikakaa kando na kuwa mtazamaji, bahati mbaya Yanga haikufanya vizuri katika michuano hiyo, ilitolewa mapema sana. Nilisikia uchungu kwa kuwa niliona huenda kuwepo kwangu kungekuwa msaada kwa kushirikiana na wenzangu na tungeweza kuikoa Yanga. Kukosekana kwangu ni kama kulipunguza nguvu, sikuwa na namna.
Baada ya hapo, niliichezea Yanga kwenye ligi na tulifanikiwa kuwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Afrika Mashariki na Kati iliyofanyika nchini Uganda. Nakumbuka sana, hiyo ni mwaka 1999, safari yetu ilikuwa ni ya kubangaiza.
Tulisafiri kwenda Uganda kwa usafiri wa kuungaunga. Nakukumbusha sisi ndiyo tulitwaa ubingwa kwenye michuano hiyo, lakini safari yetu kwenda ilikuwa ni ngumu kupindukia na hakukuwa na posho, lakini wachezaji tukawa tayari kupambana.
Tulisafikirishwa kwa mafungu mawili kwa basi. Awali uongozi ulitaka kuitoa timu lakini sisi tukasema tutacheza. Tuliondoka tukiwa na pea moja tu ya jezi, maandalizi yetu yalikuwa mabovu kuliko timu yoyote iliyoshiriki michuano hiyo.

MALIMA anaongozana na Yanga kwenda Uganda, maandalizi ni mabovu, timu haina fedha lakini mwaka huo wa 1999, Yanga walikuwa mabingwa. Je, ilikuwaje hadi wakafanikiwa huku maisha yao yalikuwa ya kuungaunga? USIKOSE  EPISODE-8

VITA NYINGINE YA MAFUNDI WA SOKA: MODRIC NA PIRLO NA KUIONGOZA VIZURI TIMU YAKE LEO?


VIKOSI VINAVYOTARAJIWA KUANZA
Italy: Buffon, Chiellini, Rossi, Bonucci, Maggio, Motta, Pirlo, Marchisio, Giaccherini, Balotelli, Cassano.

Croatia: Pletikosa, Srna, Corluka, Schildenfeid, Strinic, Perisic, Vukojevic, Rakitic, Modric, Jelavic, Mandzukic








  • Antonio Di Natale anategemewa kuanza usiku wa leo lakini anaonekana kuwa na hatari zaidi kama akiingia kutokea benchi, hivyo Mario Balotelli anaweza kupata nafasi ya kuanza tena akiwa na Cassano.
  • Pengine, Nocerino na Balzaretti wanaweza kuanza kwenye safu ya kiungo ya watu wa tano, huku Giaccherini na Motta wanategemewa kuendelea na nafasi zao walizocheza dhidi ya Spain.
  • Prandelli itabidi aanzishe ukuta ule ule ulioanza dhidi ya Italia, huku De Rossi akiwa katikati ya Chiellini na Bonucci kwa mara nyingine tena.
  • Slaven Bilic hana wasiwasi wa majeruhi kuelekea kwenye dhidi ya Italia na itabidi aanze na kikosi kile kile kilichocheza vizuri dhidi ya Ireland.
  • Perisic alichaguliwa kuanza dhidi ya Kranjcar na kucheza vizuri sana kwenye upande wa kushoto, huku Rakitic akicheza upande wa pili.
  • Kwenye ulinzi, beki mwenye asili ya Ujerumani Gordon Schildenfeld alichaguliwa kuanza mbele ya veteran Josip Simunic kusaidiana na Corluka, huku nahodha Srna akiecheza kwa kuelekea mbele kutokea shavu la kulia.

BREAKING NEWS: MWENYEKITI WA VILLA SQUAD AJIUZULU UONGOZI WA KLABU HIYO

Uongozi wa klabu ya Villa na wachezaji.
Baada ya kufanya vibaya kwenye ligi kuu msimu uliopita na kupelekea timu hiyo kushuka daraja, huku mambo yakizidi kwenda ovyo, mwenyekiti wa klabu ya Villa Squad ya magomeni Dar es Salaam Ramadhani Uledi amejiuzulu kuiongoza klabu hiyo.

Uledi ambaye aliingia madarakani mwaka jana baada ya kufanyika uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo amejiuzulu kwa kwasababu za kuwajibika. Akiongea na www.shaffihdauda.com Uledi alisema: "Wakati naingia madarakani dhamira yangu kubwa ilikuwa ni kuiwezesha Villa kubaki ligi kuu, lakini nimeshindwa kufanya hivyo, kwa maana hiyo kazi imenishinda. Kwa hiyo ni vizuri kujiuzulu ili kuwajibika, nafikiri sasa kazi hii nimuachie mtu mwingine ili aweze kuliongoza jahazi la Villa na kulirudisha kwenye sehemu nzuri."


Klabu hiyo ya Villa sasa imebakia ikiwa haina uongozi zaidi ya kamati ya utendaji chini Binslum, Ally Kindoile, Mohamed Kimbegele, Hassan Sharif na Moris Simon.

EXCLUSIVE: ORLANDO PIRATES WATUMA RASMI BARUA YA KUMTAKA EMMANUEL OKWI

Hatimaye klabu ya Orlando Pirates imetuma rasmi barua ya mualiko kwa mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kufanya majaribio ya kuweza kujiunga na timu hiyo.
Hii ni sehemu ya barua ya Orlando kumualika Okwi.
Nimefanikiwa kuiona barua hiyo ikiwa inatoa maelekezo kwamba Okwi atapewa majaribio ya wiki mbili na Orlando Pirates, huku akihudumiwa kuanzia usafiri, malazi, matibabu pamoja na gharama nyingine zitakazojitokeza kwa wakati atakaokuwa na klabu hiyo.

Kwa kipindi cha misimu miwili sasa Orlando wamekuwa wakimfuatilia Okwi ambaye klabu yake ya Simba imemuwekea price tag ya Billioni 2 kwa timu inayomtaka, huku pia wapinzani wao wa jadi klabu ya Yanga ikiwa inamfukuzia mshambuliaji huyo wa Uganda ambaye siku za hivi karibuni amekuwa ndio tegemeo la safu ya ushambuliaji ya mabingwa wa Tanzania.

IANDIKIE CAPTION HII PICHA!

SUPER MARIO GOMEZ AMFUNIKA VAN PERSIE EURO: UJERUMANI WAKIINYONGA UHOLANZI


Germany - Netherlands 2-1 All Goals - 13/06/2012 by a7mad141991

VARELA AMUOKOA RONALDO NA AIBU URENO IKIIFUNGA KWA TAABU DENMARK


PORTUGAL 3-2 DENMARK 13th JUNE 2012 1080p HD... by eurofootball2012

KIMENUKA TOTTENHAM: HARRY REDKNAPP ATIMULIWA KAZI - DAVID MOYES NJIANI KUMRITHI

Usiku wa leo umekuwa mmbaya kwa kocha Harry Redknapp baada ya kutimuliwa kazi na Tottenhma Hostpur.

Harry mwenye miaka 65 jana alisisitiza kwamba ataendelea kuwepo White Hart Lane, lakini jioni hii alifanya mazungumzo na mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy na hatimaye akatimuliwa.

Kocha huyo wa zamani wa West Ham alifanya mazungumzo na bosi wake Levy ili kuweza kujua hatma yake baada ya mkataba wake kuwa umebakiza miezi 12 uishe, huku akiwa na akiwa anajiamini amefanya kazi nzuri ambayo ingempa nafasi ya kuongezewa mkataba.

Lakini Levy inasemekana hakuwa na furaha na suala la Redknapp kushindwa kuiwezesha timu kupata nafasi ya champions league pamoja na kukaa kwenye nafasi ya tatu kwa muda mrefu kwenye msimamo wa ligi ya msimu uliopita.

Spurs walimaliza nafasi ya nne katika EPL,  kwa maana waliweza kupata nafasi nafasi lakini wakaikosa nafasi hiyo baada ya Chelsea waliokuwa nyuma yao kubeba ubingwa wa ulaya jijini Munich dhidi Bayern.

Mpaka sasa Redknapp bado anafanya mazungumzo ya juu ya mapato yake atakayoyapata baada ya Spurs kumtimua akiwa bado na mkataba wa mwaka 1, na anatagemewa kutangazwa rasmi kutimuliwa hapo kesho.

David Moyes wa Everton anatajwa kuwa ndio kocha anayeweza kumrithi Harry Redkanpp pale White Hart Lane.

OFFICIAL: DI MATTEO APEWA MIAKA MIWILI KUIONGOZA CHELSEA

Roberto Di Matteo leo amethibitishwa kuwa kocha mpya wa kudumu wa Chelsea kwa mkataba wa miaka miwili.

Muitaliano huyo alirudi Stamford Bridge leo akitokea kwenye mapumziko na kukamilisha dili  hilo na mabingwa wa ulaya.

Di Matteo alisema: "Nina furaha kuweza kuchaguliwa kuwa manager mpya. Tulipata mafanikio makubwa msimu uliopita ambayo yalijenga historia kwenye klabu.
"Lengo letu ni kuendelea kutokea hapo tulipofika na tayari nimeanza kupanga maandalizi ya msimu ujao."

Di Matteo, 42, alitajwa kama kocha wa muda wa Chelsea baada ya Andre Villas Boas kufukuzwa kazi mwezi wa 3.

Akafanikiwa kuiongoza The Blues kushinda  kombe la FA na champions league ndani ya kipindi cha wiki 11.

Wednesday, June 13, 2012

wadhamini wazidi kujitokeza shindano la Miss Dar Inter College 2012

baadhi ya warembo watakaoshiriki shindano la Miss Dar Inter College 2012 wakimsikiliza mwalimu wao Marlydia Boniface wakati wa mazoezi yao juzi kwenye hoteli ya Grand Villa.

Na Mwandishi Wetu

WAKATI shindano la kumsaka  Miss Dar Inter College 2012 likitarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) duka la vipodozi la Shear Illusions,pamoja na mbunifu maarufu wa mavazi,Mustafa Hassanali wamejitosa kudhamini shindano hilo .Awali shindano hilo lilipangwa kufanyika juni 8 kabla ya kusogezwa mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya warembo kuwa katika mitihani pamoja na mafunzo yao kwa vitendo ‘Field’.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba Shear lenye matawi yake jengo la Millennium Tower na Mlimani City linajihusha na uuzaji wa vipodozi halisi ‘original’ kutoka nje ya nchi litatoa vipodozi kwa warembo watakaoshiriki,huku Hassanali atatoa zawadi ya magauni ya warembo.
Alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea ambapo juzi warembo hao ambao awali walikuwa wakifanya mazoezi kwenye hoteli ya Lamada, walihamishia kambi yao kwenye hoteli ya Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.Dina aliongeza kuwa mpaka sasa wameshapatikana warembo 13 ambao wapo chini ya ukufunzi wa Marlidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na dansa aliyepata kufanya vema miaka ya nyuma, Bob Rich.“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.Warembo watakaoshiriki shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe

MCHEMSHA BONGO! HUYU NI NANI

EXCLUSIVE: MATOLA NJIANI KUWA KOCHA MPYA WA AFRICAN LYON

Rahim Zamunda akiwa na mmiliki wa klabu ya Portsmouth Suleiman Al-Fahim
Klabu ya African Lyon imemtimua kazi kocha wake Jumanne Chale, baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwenye ligi kuu ya Tanzania bara msimu uliopita.


Kwa mujibu wa mmiliki wa klabu hiyo Rahim Zamunda amesema kwamba wamefikia uamuzi huo ili kuweza kuisuka upya vizuri timu yao itakayoweza kupambana vizuri na mashindano yajayo.


"Huu ni uamuzi tuliofikia ili kuweza kuleta mabadiliko chanya kwenye timu yetu, na kwa sasa tupo kwenye mazungumzo ya mchezaji wa zamani wa Simba, Selemen Matola ili aweze kuwa bosi wa benchi letu la ufundi. Mpaka sasa tumefikia pazuri na lolote linaweza kutokea,"

EURO 2012: UJERUMANI VS UHOLANZI - WAPINZANI WA JADI WA KIHISTORIA NANI KUCHEKA LEO.

Wakati timu ya taifa ya Ujerumani au the Die Menschaff ikiwa imetulia kambini ikisubiri jukumu lililoko mbele ambalo kuwakabili wapinzani wao wa miaka mingi Uholanza, wapinzani wao hao  wamekuwa wakipambana wenyewe kwa wenyewe kama walivyozoea .
Vichwa vya habari vya magazeti ya michezo nchini Uholanzi kuelekea kwenye mchezo huu vimepambwa na kauli mbaya za Rafael Van Der Vart ambaye amekuwa mwepesi kusema yaliyo moyoni mwake dhidi ya kocha Bert Van Marwick, Klaas Jan Huntelaar naye hajabaki nyuma huku wengine kina Nigel De Jong na Wesley Sneijder wakihusika kwenye utata uliokizunguka kikosi cha Oranje .
Upande wa pili wajerumani wameshikama wote wakitambua mtihani ulioko mbele na wamekuwa wakiifikiria timu kwanza kabla ya kufikiria jinsi ambavyo baadhi wamekuwa wakiwekwa benchi na wengine wakicheza.
Hii ndio tofauti ya kwanza ambayo inaweza kuamua mchezo huu wa watani hawa wa jadi kwa miaka mingi.
Kila mmoja akiingia uwanjani na ajenda yake tofauti lakini wote wawili wana agenda ya kufanya vizuri na kuchukua pointi zote tatu huku Uholanzi wakionekana kuzihitaji pointi hizo pengine kuliko Ujerumani .
Ukiingia kwenye idara ya ufundi kujaribu kupata ufumbuzi wa kipigo walichopata Uholanzi toka kwa Denmark utagundua yafautayo, kimsingi kabisa Uholanzi hawakupaswa kupanga mfumo ambao uliwajumuisha viungo wakabaji wawili ambao ni De Jong na Van Bommel. Mfumo huu uliwafanya Uholanzi kukosa ubunifu wa ziada kwenye idara ya ushambuliaji. Tatizo lingine ambalo limeonekana ni kutomjumuisha Klaas Jan Huntelaar . Robin Van Persie alipangwa kwenye sehemu ya ushambuliaji wa kati, hakuna anayeweza kusema kuwa Van Persie si mchezaji mzuri, la hasha lakini kwenye mfumo wa uholanzi sio mara nyingi amekuwa akipangwa kama mtu ambaye anaongoza mstari kwenye ushambuliaji na hapa ndio unagundua tatizo. Ibrahim Affelay hajacheza sehemu kubwa ya msimu huu na kwenye nafasi yake angeweza kupangwa Van Persie halafu Affelay akasubiri kuleta impact kama Supersub huku Huntelaar akicheza kama mshambuliaji wa kati .
 Mchezo dhidi ya Ujerumani hauna budi kushudia mabadiliko haya endapo Uholanzi watataka kuweka hai matumaini yake ya kusonga mbele.
Ujerumani kwa upande wao sio kwamba walicheza vizuri kwa kustahili alama za asilimia mia moja kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ureno, kulikuwa na matatizo sehemu kadhaa, Lukas Podolski alikuwa na matatizo hasa kwenye jinsi ya kuipenya ngome ya Ureno na kwenye umaliziaji pia  kama ilivyokuwa kwa Thomas Mueller. Kilichowapa ufanisi mkubwa wajerumani ni juhudi za wachezaji hawa hasa pale ambapo mambo yalionekana kuwaelekea kombo , walifanya kazi kwa juhudi kubwa na matokeo yake yalikuwa ushindi wa bao moja dhdi ya timu nzuri na ngumu ya Ureno.
Ujerumani wanaweza kufanya mabadiliko endapo watataka kumaliza mchezo mapema, kuna wachezaji kama Andre Schurrie na Marco Reus ambao wanaweza kuingia kwenye nafasi za kina Podolski na Mueller japo hakuna ulazima wa haraka wa kushuhudia mabadiliko haya .
Tatizo kubwa la Uholanzi siku ya jumamosi lilikuwa umaliziaji . Takwimu zinaonyesha kuwa Uholanzi kwenye mechi dhidi ya Denmark walipiga mashuti 22 ambayo hayakulenga lango. Hii ndio idadi kubwa ya mashuti yaliyopotea mwelekeo kuliko timu yoyote ya taifa au klabu yoyote ile kwenye ligi zote kubwa  barani ulaya. Na hapa ndio panaweza kuhitaji mabadiliko. Pamoja na kwenye ushambuliaji mabadiliko mengine yanaweza kuonekana kwenye safu ya Ulinzi ambako Joris Mathijsen amepona na huenda akaingia kwenye nafasi ya Ron Vlaar, hata hivyo mabadiliko ambayo Kocha Van Marwick anapaswa kufikiria kuyafanya ni yale ya kupunguza kiungo mkabaji mmoja na kuongeza kiungo mbunifu kama Rafael Van Der Vart hasa ukizingatia mchezo wa kwanza wa Ujerumani ambapo wajerumani walikuwa wanapitika kiwepesi jambo ambalo linaweza kumpa Bert mawazo kwamba staili ya mchezo ya wajerumani ya kutegemea sana mashambulizi ya counter itakuwa nzuri akiwa na kiungo wa ziada kama Van Der Vart.
Mchezo kati ya Uholanzi na Ujerumani kihistoria ni mchezo ambao utazifanya timu zote ziwe na morali ya ziada kumkabili mpinzani wake. Mara nyingi Ujerumani wamekuwa wakiwanyanyasa wadachi , mazingira ya michezo ya kwanza ya timu hizi yanawafanya wadachi kuwa na sababu ya ziada ya kushinda kwani kitu chochote pungufu ya pointi tatu kitamaanisha kuwa Uholanzi itakuwa ianchungulia kaburi.

EURO 2012: URENO KUACHA UTEJA KWA DENMARK LEO?


VIKOSI VITAKAVYOANZA LEO
Denmark: Lindergaard, Poulsen, Agger, Kjaer, Jacobsen, Zimling, Kvist, Kron-Dehli, Eriksen, Rommedahl, Bendtner


Ureno: Patricio, Pereira, Pepe, Alves, Coentrao, Moutinho, Veloso, Meireles, Nani, Postiga, Ronaldo




MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMU
  • Wakiwa hawana majeruhi mapya, Denmark wanategemewa kutaja kikosi kile kile kilichoshtua watu kwa kuifunga Uholanzi bao 1-0.
  • Kwa maana hiyo kipa Stephen Andersen anaweza akaanza mbele ya Lindergaard huku pia Jacobsen na Zimling wakitarajiwa kuanza mbele ya Wass na Poulsen.
  • Lasse Schone atakuwa na matumaini ya kuanza mbele ya Rommedahl katika winga sambamba na Kronh-Dehli.
  • Ureno nayo haitegemewi kubadili kikosi kilichofungwa na Ujerumani, Paulo Bento hana option kubwa zaidi ya kukianzisha kile kile.
  • Nani alicheza dakika zote 90 japokuwa alionekana kuchoka mwishoni mwa mechi, anategemewa atakuwa fiti na kuanza leo dhidi ya Wadenmark na kucheza kwa dakika zote 90 kutegemeana na kiwango chake.
  • Nelson Oliveira atakuwa akitaka kuanza mbele ya Postiga ambaye ameonekana butu kwa safu ya ushambuliaji, huku Almeida akisubiri kwenye benchi.