Search This Blog

Tuesday, May 8, 2012

KOCHA WA AZAM FC: STEWART HALL ASEMA RUSHWA NDIO KIKWAZO CHA MAENDELEO YA SOKA TANZANIA


KOCHA wa Azam, Stewart Hall amelia na wadau wa Simba na Yanga wanavyoipiga vita timu yake, ambayo imeibuka kuwa kigogo cha Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na Mwanaposti katika mahojiano maalumu, Hall anasema anashangazwa na mashabiki hasa wa Simba na Yanga kwa kuijengea chuki timu yake kutokana na kutishia ubabe wao.

Hall anaonya kuwa tabia ya wadau wa Simba na Yanga wanaotaka kuona ligi ya Tanzania ikitawaliwa na timu mbili zao tu kitu ambacho si sahihi kwa maendeleo ya soka.

"Timu hizi zimekuwepo kwa miaka mingi sana lakini nashangaa zimeshindwa kusaidia kukuza soka la Tanzania.

"Ninachokiona katika soka la Tanzania kinanisikitisha na kinachonikera zaidi wameingia watu makini wa Azam, ambao wameingiza fedha lakini wanapigwa vita," anasema Hall, ambaye ni raia wa Uingereza.

Anasema Watanzania wanapaswa kuruhusu ushindani na kutolea mfano Ligi Kuu Scotland inavyoshindaniwa na timu mbili tu za Rangers na Celtic na kufanya soka la sehemu hiyo kuwa chini.

Ligi Kuu Tanzania Bara
Hall anasema anafurahia timu yake kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa miaka chache tangu kuanzishwa kwake.

Anaeleza ni kitu kizuri kuona timu yake iliyoanzishwa mwaka 2004, imeipiku Yanga iliyoasisiwa katika miaka ya 1930.

Azam safari hii imenyakua nafasi ya pili na mwakani itashiriki katika mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Hall anaonya Watanzania wanapaswa kubadilika kama kweli wanataka soka la nchi hii ibadilike.
Anasema kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatakiwa kuwa makini katika kuendesha katika ligi hiyo.

Analalamikia vitendo vya rushwa kwenye ligi hiyo na viwango duni vya uchezeshaji miongoni mwa waamuzi.

Hall anaeleza kuwa anashangaa kuona rushwa na upangaji matokeo vinakubalika kama sehemu ya soka la Tanzania.

"Ni hatari kwa soka la nchi yenu kama mtakubali masuala ya upangaji matokeo," anasema Hall, ambaye timu yake ililazimika kurudiana na Mtibwa kwenye mzunguko wa pili baada ya mechi ya kwanza kukatizwa kutokana na makosa ya mwamuzi Rashid Msangi.

Pia mechi za Yanga na Polisi Dodoma zilimalizika kwa waamuzi kupigwa kutokana na timu hizo kudai mwamuzi alikuwa anaibeba Azam.

Kocha huyo anakanusha vikali madai hayo na kudai kuwa watu wanaionea wivu tu timu yake kutokana na kuwa na fedha nyingi.

Hall anasema TFF kwa kushirikiana na wadau wa soka la Tanzania wanapaswa kupiga vita kwa nguvu zote masuala ya rushwa.

Anatahadharisha ni ndoto kwa timu za Tanzania kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa kama wadau wa soka watakumbatia rushwa kama sehemu ya soka la Tanzania.

Anasema wapangaji matokeo wanapaswa kuchukua hatua kali kama Marseille ya Ufaransa ilivyoadhibiwa mwaka 1993 baada ya kubainika ilikuwa inanunua baadhi ya mechi za Ligi Kuu Ufaransa au ile kashfa ya upangaji matokeo ya Italia iliyokuja kujulikana kwa jina la Calciopoli.

Anaonyesha kuwa ubaya wa timu kununua mechi unasababisha Tanzania kuwakilishwa na timu dhaifu kwenye michuano ya Afrika.

"Bwana mwandishi jiulize, timu gani ya Tanzania imetwaa kutwaa taji la Afrika? Jibu linafahamika na ni wazi kuwa linasababishwa na rushwa ndani ya Ligi Kuu," anaeleza Hall, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Birmingham.

Hall, hata hivyo, anadai anategemea ushindani mkali zaidi msimu ujao kwenye Ligi Kuu kwani ameona timu kama Mtibwa na Coastal Union ziko juu.

Mashabiki wa Simba na Yanga
Hall anaeleza pia mashabiki wa Simba na Yanga kwa kiasi kikubwa nao wanachangia kwa kiasi kikubwa kuvuruga soka la Tanzania.

Anasema mashabiki hao wanaweka presha kubwa kwa wachezaji na viongozi wa soka kuhakikisha timu zao zinashinda.

Hall anatolea mfano vurugu za mechi ya Yanga na Azam kuwa zilichangiwa zaidi na viongozi na mashabiki wa Yanga kuwapa shinikizo wachezaji wao kushinda.

"Unajua tulikuwa tumeifunga Yanga mara kadhaa, sasa safari hii wakaona hapana wanapaswa kushinda kwa njia zozote. Basi baada ya kuona mambo hayaendi vizuri wakampiga mwamuzi," anasema Hall, ambaye pia ni Mshauri wa Ufundi wa timu ya Zanzibar.

Hall anasema anaelewa mashabiki wa soka wa Tanzania wamegawanyika kushabikia timu hizo lakini amesema zinapaswa kubadilika.

Anaeleza mashabiki wa timu hizo wanapaswa kuhakikisha timu zao zinaendeshwa kisasa zaidi ndani na nje ya uwanja badala ya kuendekeza siasa za nje ya uwanja.

Hall anaeleza kutokana na presha na wingi wa mashabiki wa Simba na Yanga kumefanya wababaike wanapochezesha mechi za baina ya timu hizo.

Pia ameponda mashabiki hao kwa kukosa uzalendo na kuzishabikia timu za kigeni zinapokuja kucheza Tanzania.

"Nimefundisha soka katika nchi mbalimbali duniani lakini sijawahi kuona timu ya kigeni inashabikiwa," anasema Hall.

Katika miaka ya karibuni, imekuwa kitu cha kawaida kwa mashabiki wa Simba na Yanga kushangilia timu za kigeni zinapocheza na mahasimu wao.

Hall anasema ameshangazwa kuwa tabia hiyo imeingia katika timu ya taifa.
"Mashabiki wa Simba na Yanga wanaua soka lenu kwani wameingiza siasa zao kwenye timu ya taifa," anaeleza Hall, ambaye alikuwa anazungumzia vituko vya Kombe la Chalenji mwaka jana wakati mashabiki wa Yanga walipokuwa wanaizomea timu ya Bara kutokana na kuwa na wachezaji wachache wa Yanga.

Pia anatolea mfano jinsi mashabiki hao walivyokuwa wanamsakama mshambuliaji wake John Boko na kumfanya ajitoe kwenye kikosi cha timu ya taifa.

"Boko ni mchezaji mdogo sana lakini ameacha kuchezea Stars kutokana na kujengewa chuki na mashabiki hawa. Watu hawa wanaua soka la Tanzania," anaeleza Hall.

Pia anaeleza kuwa mashabiki hao wamejenga chuki kubwa dhidi ya timu yake kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na matajiri wa timu hiyo.

Azam imejenga uwanja na hosteli ya wachezaji na ina mfumo mzuri wa timu kuanzia watoto wenye umri wa miaka 12.

Pia wachezaji wa timu hiyo wanaangaliwa vizuri kwa kulipwa mishahara na marupurupu kwa wakati.

"Mimi nilitegemea kuwa mashabiki hawa wangetuunga mkono na kushinikiza viongozi wao kubadilika na kuendesha timu zao vizuri lakini badala yake wanatupiga vita," anaeleza Hall kwa mshangao.

Hall anatoa mwito kwa wadau wa soka la Tanzania kuiangalia Azam kama kioo cha soka la Tanzania badala ya kuichukulia kama adui.

Maendeleo ya Azam
Hall anaeleza kuwa anasema licha ya changamoto za waamuzi lakini anapongeza timu yake kwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Simba iliyotwaa ubingwa.

Amesema amefurahia kuona malengo yao yametimia msimu kwani walikuwa wanataka kuvunja ubabe wa Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Lengo letu kubwa lilikuwa kushika nafasi mbili za juu, kitu ambacho tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

"Sasa msimu ujao tunataka kupigania ubingwa jambo ambalo ninaamini tuna ubavu nalo," aliongeza Hall, ambaye amewahi kuzifundisha timu za taifa za St.Vincent, Grenada na Pune ya India.

Hall anafichua kuwa timu hiyo imeandaa programu ya miaka 10 yenye lengo la kuifanya timu hiyo kuwa miongoni mwa timu kubwa Afrika.

"Tunataka tufikie hatua kutoa upinzani kwa timu kama TP Mazembe au Al-Ahly ya Misri," anaongeza Hall.

Amesema kuwa anasikitishwa na kuona timu yake inapigwa vita na wadau wa soka.
Hall anasema kutokana na haya yanayowakuta Azam yatafanya watu wengine wenye fedha kuogopa kuingiza fedha zao kwenye soka.

"Unajua kuna watu wanaangalia tunayofanya sasa watu wenye fedha zao wakishuhudia jinsi Azam inavyonyanyasika basi hawatataka kushiriki katika mchezo huu," anasema Hall, ambaye anaongeza fedha ni muhimu kwa maendeleo ya soka.
 
www.mwanaspoti.co.tz
 

TAARIFA KUTOKA TFF!

TWIGA STARS KUJIPIMA KWA ZIMBABWE
Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) itacheza na Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Mei 12 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Twiga Stars hivi iko katika ziara ya mechi za kirafiki katika mikoa ya Dodoma na Mwanza. Leo (Mei 8 mwaka huu) itacheza na kombaini ya Mkoa wa Dodoma ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.

Kesho (Mei 9 mwaka huu) itaondoka kwenda jijini Mwanza ambapo pia itacheza mechi moja ya kirafiki Mei 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, na kurejea Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Zimbabwe.

Zimbabwe inatarajia kuwasili kesho (Mei 9 mwaka huu) jioni kwa ndege ya South African Airways (SAA) ikiwa na msafara wa 25 na wataondoka Mei 14 mwaka huu alfajiri.

 atazamaji 41,733 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga iliyochezwa jana (Mei 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

KAMATI YA MASHINDANO KUPANGA VITUO LIGI YA TAIFA
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana leo (Mei 8 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine itapanga vituo vya Ligi ya Taifa na tarehe ya kuanza ligi hiyo.

Mikoa nane imeomba kuwa wenyeji wa ligi hiyo itakayochezwa katika vituo vitatu. Mikoa hiyo kupitia kwenye vyama vyao vya mpira wa miguu ni 
Mikoa iliyoomba vituo ni Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Mara, Mbeya, Shinyanga na Singida.

Timu zinazoshiriki ligi hiyo ni mabingwa wa mikoa. Timu hizo ni Ashanti United ya Ilala (Dar es Salaam), Aston Villa (Singida), Bandari FC (Kagera), CDA (Dodoma), Flamingo SC (Arusha), Forest FC ya Siha (Kilimanjaro), JKT Kanembwa (Kigoma), Korogwe United ya Korogwe (Tanga), Kurugenzi ya Mafinga (Iringa), Lindi SC (Lindi) na Majimaji (Tabora).

Mighty Elephant (Ruvuma), Mkamba Rangers ya Kilombero (Morogoro), Mpanda Stars ya Mpanda (Rukwa), Mwadui FC (Shinyanga), Nangwa VTC (Manyara), Ndanda FC (Mtwara), Pamba SC (Mwanza), Polisi Mara (Mara), Red Coast ya Kinondoni (Dar es Salaam), Super Star ya Bagamoyo (Pwani), Tenende SC (Mbeya) na Tessema FC ya Temeke (Dar es Salaam).

KILA LA KHERI SIMBA, PONGEZI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Simba kwenye mechi yake ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa Jumapili (Mei 13 mwaka huu).

Mechi hiyo itachezwa katika mji wa Shandy kuanzia saa 2 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Simba inaondoka kesho kwenda huko kwa ndege ya Kenya Airways.

Msafara wa timu hiyo utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Hussein Mwamba, na unatarajia kurejea nyumbani Mei 15 mwaka huu.

Pia TFF inaipongeza Simba kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo Mei 6 mwaka huu ilifunga msimu wa 2011/2012.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


UONGOZI MBOVU: GODFREY NYANGE KABURU AMSAJILI MCHEZAJI BILA KOCHA WALA KAMATI YA UFUNDI YA SIMBA KUJUA.

Moja ya chanzo kikubwa kinachookwamisha maendeleo ya soka la Tanzania ni kuwa na viongozi wasiojua mipaka ya madaraka na majukumu yao. Huu ni ugonjwa mkubwa unaolikabili soka la Tanzania hususani katika vilabu vikubwa nchini kwetu ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa ndio uti wa mgongo wa soka letu  - yaani Simba na Yanga.

Hili suala limeendelea kujidhihirisha leo pale ambapo kumetokea sintofahamu kati ya kamati ya ufundi ya klabu bingwa ya Tanzania Simba Sports Club na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Godfrey Nyange Kaburu baada ya bwana Kaburu kuamua kumsajili mshambuliaji kutoka klabu ya Ruvu Shooting Abdallah Juma bila kufuata taratibu za usajili ndani ya klabu zinavyojieleza na kupaswa kuwa.

Nyange bila kupata maoni ya kocha wala jopo zima la kamati ya ufundi leo hii amekamilisha usajili wa mchezaji huyo kwa maamuzi yake binafsi - jambo ambalo kamati nzima ya ufundi imeona na uingiliwaji wa majukumu alioufanya kiongozi huyu mkubwa wa Simba.

NO WONDER SOKA LA TANZANIA LIMEENDELEA KUDUMAA FOR THE LACK OF PROFESSIONALISM!!!!

OFFICIAL: AZAM WAMSAJILI BLACKBERRY - MCHEZAJI BORA WA KENYA

 Kama una kumbukumbu nzuri takribani wiki moja iliyopita mtandao huu ndio ilikuwa ya kwanza kukuletea taarifa juu ya ujio wa mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya George Blackberry Odhiambo kuja Tanzania kufanya mazungumzo na majaribio na klabu ya Azam FC.

Sasa taarifa rasmi kutoka Azam FC ni kwamba George Blackberry Odhiambo amemwaga wino kuichezea Azam FC msimu ujao. Blackberry aliyekuwa mchezaji bora wa KPL msimu wa 2010/11 na baadaye kuelekea Denmark ataichezea Azam FC kwa misimu miwili.

Monday, May 7, 2012

LULU AOMBA KUPELEKWA JELA YA WATOTO - MAHAKAMA YAMKATALIA


Lulu (katikati) akiingia mahakamani na askari magereza wa k***.
Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
Kamera zikimfuata kwa shauku.

Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na mshitakiwa huyo.
Hapa ni karibu na mlango wa kuingia katika chumba cha mahakama.

                                            (PICHA: RICHARD BUKOS / GPL)

MBWANA ATUPIA -TP MAZEMBE WAKIUA 6-0

AZAM YATOA TUZO KWA WACHEZAJI WAKE - YASEMA LENGO MWAKA HUU NI KUKAA KATI YA WATANI WA JADI - MWAKANI NI KUCHUKUA UBINGWA


JOHN BOCCO AKICHUKUA TUZO YAKE



WASHINDI WA TUZO ZA AZAM:
1) OUTSTANDING PLAYER OF THE YEAR
Sr Team- ABUBAKAR SALUM (SUREBOY)
Jr Team – KELVIN FRIDAY

2) BEST ATTITUDE IN TRAINING
Sr.Team – LUCKSON KAKOLAKI
Jr.Team – ISMAIL ADAM GAMBO

3) BEST DISCIPLINED PLAYER ON /OFF THE FIELD
Sr.Team- VAZIRI OMARI
Jr.Team – ASSAD MUSA 
 
4) MOST PROMISING PLAYER
Sr.Team – HAMIS MCHHA (Vialli)
Jr.Team – ALLY KAIJAGE

5) MOST INSPIRATIONAL PLAYER
Sr.Team – AGREY MORRIS
Jr.Team – ABDUL MGAYA

6) MOTIVATIONAL PLAYER OF THE CLUB
Sr.Team -IBRAHIM S CHIMWANGA(Shikanda)
Jr.Team – REYNA ELLY & MUDHATIR YAHAYA
ERASTO NYONI
7) FUNNIEST CHARACTER IN TRAINING
Sr.Team – ERASTO NYONI
Jr.Team –HAMADI JUMA
SAID MORAD
8) FITTEST CHARACTER IN TRAINING
Sr.Team – SAID MORADI
Jr.Team –MOHAMMAD HUSEIN

JOHN BOCC0
9) PLAYER OF THE YEAR
Sr.Team – JOHN BOCCO
Jr Team – JOSEPH KIMWAGA

HARUNA MOSHI BOBAN NA BONDIA FRANCIS CHEKA WAKITOA MAONI YAO BAADA YA USHINDI DHIDI YA YANGA

BHINDA NA MINZIRO WASEMA HATA NCHUNGA NA UONGOZI WOTE UKING'OKA 5-0 ZINABAKI PALE PALE

Training Program for the Youth

Bhavesh Raccha ,Akshay Pinjani and Ganesh Dere from India ,Pune for advanced football training at AZAM FC for a month.The players are from AIYFA,(All India Youth Football Academy ) from Pune,India.

41,733 WASHUHUDIA MECHI YA SIMBA, YANGA

Watazamaji 41,733 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga iliyochezwa jana (Mei 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 VIP C, sh. 30,000 VIP B na sh. 40,000 VIP A. Watazamaji 36,980 walinunua tiketi za sh. 5,000 wakati 203 walikata za sh. 40,000.

Mechi hiyo ambayo ni moja kati ya saba zilizochezwa siku hiyo kufunga msimu wa 2011/2012 iliingiza sh. 260,910,000. Kila klabu ilipata sh. 62,646,395.85. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 39,799,830.51 wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilipata sh. 19,908,361.95.

Gharama za mechi kabla ya mgawo ni nauli ya ndani ya waamuzi na kamishna sh. 20,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, mwamuzi wa akiba sh. 30,000, gharama za tiketi sh. 8,539,950, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.

Mgawo wa uwanja ni sh. 19,908,361.95, gharama za mechi sh. 19,908,361.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 9,954,180.97, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 1,990,836.19 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 10,467,324.78.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

EXCLUSIVE VIDEOS: MUUAJI EMMANUEL OKWI AKIELEZEA NAMNA ALIVYOPLEKA MSIBA JANGWANI

ADEN RAGE ASEMA ALIHAIDI KUIFUNGA YANGA 5-0 NA AMETIMIZA AHADI - ANGALIA PIA NA VITUKO VYAKE

KOCHA MSAIDIZI WA YANGA FELIX MINZIRO AKIZUNGUMZA KWA HASIRA BAADA YA MECHI

MMILIKI WA MADUKA YA ZIZZOU FASHION ATHUMANI TIPPO AKIWA NA FURHA YA AJABU JUU YA USHINDI WA SIMBA

MWENYEKITI WA KAMATI YA UFUNDI WA SIMBA IBRAHIM MASOUD MAESTRO AKISHANGILIA USHINDI

KATIBU WA SIMBA MTAWALA AKIELEZEA FURAHA YAKE YA USHINDI

KIONGOZI WA YANGA MOHAMED BHINDA AKIELEZEA KWA UCHUNGU JINSI OKWI ALIVYOWADHURU LEO HII - HUKU AKISEMA INAWEZEKANA KUNA MKONO MTU KWENYE KIPIGO HIKI



MWANA FA AKISHANGILIA USHINDI WA BAO 5 WA SIMBA - HUKU MADEGA AKIKIMBIA ...

MUIGIZAJI DOKII AKIWA KWENYE MAJONZI MAKUBWA - HUKU MSEMAJI WA YANGA AKI...

PAPIC AANGALIA MECHI JUKWAANI - MICHO AJA KUWACHUNGUZA MAFISANGO NA NIYONZIMA

Katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF - Fredirick Mwakalebela alikuwepo kuangalia mtanange wa watani wa jadi.

Kocha Mkuu wa Yanga Kostadin Papic alikuwa jukwaani kuangalia timu yake ikifungwa mabao 5-0 kwa sifuri - mserbia huyu inasemekana hayupo katika maelewano mazuri na viongozi wake ndio maana hakuwepo katika benchi la ufundi leo hii.


Azim Dewji akiwa na naibu waziri wa michezo Amos Makalla.

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Rwanda Amavubi - Micho alikuwepo uwanjani kuwaangalia wachezaji wake Patrick Mafisango na Haruna Niyonzima.

MASHABIKI WA SIMBA JUKWAA LA VIP WAKISHANGILIA MOJA YA MAGOLI YA LEO

PIC OF THE DAY: FLOYD MAYWEATHER, 50 CENTS, LIL WAYNE AND JUSTIN BIEBER

JUVENTUS MABINGWA WAPYA WA ITALIA - WAITANDIKA CAGLIARI 2-0 NA KUBEBA SCUDETTO


szólj hozzá: Cagliari 0-2 Juventus Goals

Sunday, May 6, 2012

SCHOLES NA ASHLEY YOUNG WAIZAMISHA SWANSEA CITY HUKU UNITED WAKISUBIRI MIUJIZA YA QPR DHIDI YA MAN CITY


Manchester United 2 - 0 Swansea City by warrant

YAYA TOURE AONGOZA MAUAJI DHIDI YA NEWCASTLE: MAN CITY WAKIUSOGELEA UBINGWA WA EPL


Newcastle United v Manchester City by rookster17

SIMBA YAIKUNG'UTA YANGA GOLI 5-0 NA KUBEBA UBINGWA WA VODACOM PREMIER LEAGUE


Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma baada ya timu ya Simba kuifunga Yanga magoli 5-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar salaam katika mchezo uliokuwa ni wa  kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii  kwenye uwanja wa Taifa, huku ikiwa tayari ni mabingwa wapya wa ligi hiyo, Simba imefanikiwa kutunza heshima yake baada ya kuifunga Yanga magoli 5 kupitia wachezaji wake Emmanuel Okwi, goli la kwanza. 

Goli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu , Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga  goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari 
Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi akishangilia goli mara baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza
Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe  leo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimvisha Medali mtoto wa mchezaji Uhuru Selemani wa Simba.
Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimvisha medali mshabuliaji wa Simba Emmanuel Okwi.
Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia na kocha wao kwa kumbeba juu juu.
Luninga kubwa ya uwanjani ikionyesha magoli yaliyofungwa na Simba
Mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akiwania mpira mbele ya Shadrack Nsajigwa wa Yanga katika mchezao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania inayomalizika leo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiangalia kitu jukwaani haikufahamika lilikuwa ni tukio gani.
Wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi cha timu ya Simba ambao ndiyo mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2011-2012 kikiwa katika picha ya pamoja na Kocha wao Milovan.
Manahodha wa Simba na Yanga Juma Kaseja kushoto na Shadrack Nsajigwa wakisalimiana mbele ya waamuzi kabla ya kuanza kwa mpambano huo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika uwanjani hapo.

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA 5-0 YANGA FULL TIME


KICK OFF: SIMBA VS YANGA
DK: 1 - Emmanuel Okwi wanawainua Simba vitini
JUKWAA LA MASHABIKI WA YANGA



WANASIMBA


Young Africans inafaya shambulizi dkk ya 8 ya mchezo, shuti linagonga mwamba wa juu na kutoka.

Hamis Kiiza anakosa bao la wazi dakika ya 19 ya mchezo

Dakika ya 25, Simba 1 - 0 Young Africans.

Hamis Kiiza anakosa tena bao la wazi dakika ya 33, baada ya kuwatoka mabeki wote wa timu ya simba.
Shadrack Nsajigwa anaonyeshwa kadi ya njano dakika ya 39 ya mchezo.
Half time: Simba 1-0 Yanga

Mwali wa VPL akisubiri kunyanyuliwa na mnyama



Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza,
Simba SC 1- 0 Young Africans.
Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Said Mohamed anatoka Yaw Berk.


Simba wanafanya mabadiliko dakika ya 48, anaingia Jonas Mkude anatoka Mwinyi Kazimoto.

DK.50 Felix Sunzu anakosa bao la wazi hapa.


DK 55: Simba wanapata penati na Sunzu anaipatia Simba bao la pili. 

Young Africans inafanya mabadiliko dakika ya 56, anaingia Kenneth Asamoah anatoka Davies Mwape.

Emmanuel Okwi anaipatia Simba SC bao la tatu dakika ya 63.

Juma Kaseja anaipatia Simba goli la nne kupitia penati. 

Athumani Idd Chuji anampiga kwanja la makusudi Okwi nna simba wanapewa penati - Patrick Mafisango anaweka mpira kimiani. 
Mpira umemalizika, Simba 5 - 0 Young Africans

LIONEL MESSI AMUAGA GUARDIOLA NOU CAMP NA MABAO MANNE - BARCA WAKIUA ESPANYOL 4-0


Lionel Messi alihakikisha Pep Guardiola anapokea perfect send off pale Nou Camp kwa kufunga mabao manne huku Barcelona wakiitandika  Espanyol 4-0 usiku wa jumamosi.

Katika mechi ya mwisho ya Guardiola akiwa kiwanja cha nyumbani kabla hajampisha msaidizi wake Tito Vilanova, aliipokea zawadi hiyo ya magoli kutoka kwa mchezaji ambaye anatajwa kama mchezaji bora kabisa katika kizazi hiki cha soka.

Messi tena alikuwa hatari jana usiku akifikisha jumla ya mabao 72 ndani ya msimu mmoja - huku akifikisha mabao 50 kwenye La Liga. Sasa ana jumla ya magoli 251 katika mechi 327 alizoichezea Barcelona.


Official Floyd Mayweather-Miguel Cotto scorecard

three judges gave the last four rounds to Mayweather.

PREVIEW SIMBA NA YANGA


Simba


VIKOSI:
SIMBA: Juma Kaseja, Nassor Chollo, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kelvin Yondan, Patrick Mafisango, Uhuru Suleiman, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Emanuel Okwi.
BENCHI: Ally Barthez, Derrick Walullya, Obadia Mungusa, Victor Costa, Ramadhan Singano, Gervais Kago na Salum Machaku.

Yanga


YANGA: Yaw Berko, Nsajigwa Shadrack, Oscar Joshua, Nadir Cannavaro, Athumani Iddi, Juma Seif, Shamte Ally, Haruna Nironzima, Davies Mwape, Kenneth Asamoah na Hamisi Kiiza.
BENCHI: Shaaban Kado, Omega Seme, Zuberi Ubwa, Job Ibrahim, Bakari Mbega, Nurdin Bakari, Idrisa Senga, Pius Kisambale na Geoffrey Bonny.    

WATANI wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga wanashuka dimbani leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa funga dimba, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, huku kila timu ikihitaji kulinda hadhi yake tu.
SImba tayari bingwa- lakini ili sherehe za kukabidhiwa Kombe zinoge lazima wamfunge mtani wa jadi- lakini kwa Yanga, baada ya kupokonywa ubingwa wa Bara na kukosa hata nafasi ya pili, kitu pekee cha kuwafariji mashabiki wao ni kuua mnyama.
Yanga leo itamkosa mshambuliaji wake mzoefu wa mechi za watani wa jadi, Jerry Tegete ambaye anatumikia adhabu ya kutocheza hadi mwisho mwa msimu.
Simba inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa katika mwendo mzuri- ikishinda mechi za ligi na za Afrika- zaidi safu yake ya ushambuliaji inaonekana kuchanganya zaidi katika siku za karibuni.
Hapana shaka, Mserbia Milovan Cirkovick ataendelea kuwapanga pamoja Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ na Felix Sunzu katikati na pembeni yao Emmanuel Okwi kushoto na Uhuru Suleiman kulia- hii maana yake atashambulia na wanaume wanne.
Yanga kadhalika- kuna uwezekano Freddy Felix Minziro akatumia washambuliaji wanne- Kenneth Asamoah na Davies Mwape katikati na pembeni yao Hamisi Kiiza kushoto na Shamte Ally kulia.
Haruna Niyonzima katika kiungo cha Yanga na Mwinyi Kazimoto katika kiungo cha Simba ni burudani nzuri inayotarajiwa Taifa leo.
Patrick Mafisango atacheza kama kiungo wa ulinzi, lakini kwa sababu anapanda sana- inamaanisha Simba inawezaa kuifunika Yanga katika nafasi ya kiungo- itategemea Juma Seif ‘Kijiko’ atakuwa katika hali gani leo na atachezaje, maana jamaa huwa hatabiriki.
Beki wa kulia wa Yanga atakuwa ‘babu’ Nsajigwa Shadrack upande ule ambao atakuwa anateleza Okwi- wakati kulia atakuwapo Oscar Joshua eneo ambalo ni njia ya Uhuru.
Beki wa kulia wa SImba bila shaka atakuwa Nassor Masoud ‘Chollo’ ambako atakuwa anapita Kiiza na beki wa kushoto atakuwa Amir Maftah katika njia ya Shamte Ally.
Katikati Yanga, Minziro anaweza kuamua kumpanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Chacha Marwa au kuendelea kumchezesha pamoja na Athumani Iddi ‘Chuji’.
Simba hapana shaka Milovan ataendelea kuwachezesha pamoja katikati Shomary Kapombe na Kelivn Yondan. Langoni Simba piga, ua atasimama Kaseja tu labda awe mgonjwa wa kushindwa kucheza hata kwa sindano ya ganzi. Yanga bila shaka atadaka Mghana Yawe Berko.     


JE WAJUA?
Mara ya mwisho Simba na Yanga kukutana katika mechi ya kulinda heshima- baada ya tayari kuwa bingwa amekwishapatikana ilikuwa ni Aprili 27, mwaka 2008 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana, Yanga ikiwa tayari imekwishatwaa ubingwa chini ya kocha Mserbia Profesa Dusan Savo Kondic.

Kocha wa Simba katika mechi hiyo ya Aprili 27, 2008 alikuwa ni Profesa Milovan Cirkovic, ambaye baada ya mechi hiyo aliondoka SImba kutokana na uongozi wa klabu hiyo, chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Hassan Daalal kugoma kumuongezea mshahara.

Pambano la kwanza la Ligi Kuu, wakati huo klabu ya bingwa ya taifa baina ya watani wa jadi lilifanyika Juni 7, mwaka 1965 Uwanja wa Ilala (sasa Karume), wakati huo Simba bado inaitwa Sunderland na Yanga ndio walioshinda mechi hiyo, bao pekee la
Mawazo Shomvi dakika ya 15.

Ushindi mkubwa zaidi kwa Yanga dhidi ya watani wao wa jadi, Simba ni wa mabao 5-0 Juni 1, 1968, siku hiyo Maulid Dilunga ‘Mexico’ akifunga mabao mawili katika dakika ya 18 kwa penalti na na 43, wakati mengine yalifungwa na Salehe Zimbwe dakika ya 54 na 89 na Kitwana Manara dakika ya 86.

Simba ililipa kisasi cha 5-0 Julai 19, mwaka 1977 kwa kuwafunga Yanga mabao 6-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam- siku hiyo Abdallah ‘King’ Kibadeni akifunga mabao matatu peke yake katika dakika za 10, 42 na 89 wakati mengine yalifungwa na Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika ya 60 na 73 na beki wa Yanga, Suleiman Sanga akajifunga dakika ya 20.

Sare ya mabao 4-4 Novemba 9, mwaka 1996 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, inabakia kuwa sare ya kihistoria katika mapambano ya watani wa jadi kufungana mabao mengi. Mabao ya Yanga yalifungwa na Edibilly Lunyamila kwa penalti dakika ya 28, Mustafa Hozza alijifunga dakika ya 64, Said Mwamba 'Kizota' dakika ya 70 na Sanifu Lazaro ‘Tingisha’ dakika ya 75. Simba mabao yao yalifungwa na Thomas Kipese dakika ya saba, Ahmed Mwinyimkuu dakika ya 43 na Dua Saidi dakika ya 60 na 90.

Leo Yanga inatarajiwa kuongozwa na kocha mzalendo, beki wake wa zamani Freddy Felix Minziro wakati Simba ina Mserbia, Milovan Cirkovic- hii ni mara ya kwanza benchi la Yanga kuwa na kocha mzawa katika mechi dhidi ya watani tangu alipofukuzwa Kenny Mwaisabula mwaka 2004.

Juma Kaseja atakuwa ni mchezaji aliyeanza muda mrefu zaidi kucheza mechi za watani wa jadi, mwaka 2003 mechi yake ya kwanza ikiwa ni ya Aprili 20, mwaka 2003 akikaribishwa na kipigo cha mabao 3-0, yaliyotupiwa nyavuni na Kudra Omary dakika ya 30, Heri Morris dakika ya 32 na Salum Athumani dakika ya 47.

Washambuliaji wote wa kigeni wa Yanga, Mghana Kenneth Asamoah, Mganda Hamisi Kiiza na Mzambia Davies Mwape wamekwishatikisa nyavu za Simba- ingawa bao la Kiiza lilikataliwa kwenye fainali ya Kombe la Kagame Julai mwaka jana, kwa madai aliotea, lakini lilionekana kuwa bao salama kabisa.

Ni mshambuliaji mmoja tu wa kigeni wa Simba, Felix Mumba Sunzu Jr katika washambuliaji watatu wa kigeni wa Simba, wengine wakiwa Gervais Kago kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati na Emmanuel Okwi kutoka Uganda aliyeweza kutikisa nyavu za Yanga.

Kiungo Patrick Mutesa Mafisango wa Simba kutoka Rwanda, amekwishatikisa nyavu za Yanga katika msimu wake huu wa kwanza Msimbazi- lakini Mnyarwanda mwenzake Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima anaingia kwenye mechi ya mwisho ya msimu leo- akiwa hajui nyavu za SImba zinatikisikaje.

Hili linakuwa pambano la 11, kwa watani wa jadi kukutana Uwanja mpya wa Taifa tangu ufunguliwe, awali katika mapambano 10, Yanga ilishinda mechi tano, Oktoba 26, 2008 (1-0), Oktoba 29, 2011 (1-0), Julai 10, 2011 (1-0), Desemba 25, 2009 (2-1) na Agosti 18, 2010, iliposhindwa penalti 3-1 baadaye ya sare 0-0, wakati Simba imeshinda mechi tatu tu Oktoba 31, 2009 (1-0), Aprili 18, 2010 (4-3) na Agosti 17, 2011 (2-0) na timu zimetoka sare mara mbili, Aprili 19, 2009 (2-2) na Machi 5, 2011 (1-1).

Kiiza kushoto na Chollo kulia, leo itakuwaje?

Source: Bongostaz.

NGORONGORO WAITOA SUDAN - NGOMA SASA KUPIGWA DHIDI YA WANIGERIA

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes sasa watawakabili Nigeria katika mchezo wa raundi ya pili kusaka tiketi ya kucheza mataifa Afrika machi Mwakani, baada ya kuwaondosha Sudan kwa matokeo ya jumla ya 4-3.

Katika mchezo wa leo usiku uliochezwa katika uwanja wa Khartoum baina ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan ulimalizika kwa Sudan kuibuka na ushindi wa goli 2-1, wakati mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ulishuhudia Tanzania wakíibuka na ushindi wa goli 3-1 na kupelekea matokeo ya jumla kusomeka Tanzania 4-3 Sudan.


Usiku wa leo Sudan walikuwa wa mwanzo kuandika goli katika dakika ya 10 kupitia kwa Mohammed Abdelrahman na dakika mbili mbele Mshambuliaji wa TP Mazembe Thomas Ulimwengu aliisawazishia Ngorongoro Heroes na kupelekea timu kwenda mapumziko zikiwa sare ya goli 1-1.


Vijana wa Sudan waliokuwa wanasaka ushindi wa hudi na uvumba waliandika goli la pili katika dakika ya 65 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Ahmed Nasr na kupelekea mchezo kumalizika kwa Sudan kushinda kwa goli 2-1.


Ngorongoro Heroes iliyofuzu kwa raundi ya pili itaivaa Nigeria julai 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam kabla ya kusafiri kwenda Nigeria kwa ajiri ya marejeano kati ya Agosti 10 na 12 mwaka huu.


Ngorongoro Heroes ambayo inatarajia kurejea nchini jumapili saa 3 asubuhi, ikifanikiwa kuitoa Nigeria, itacheza mechi ya raundi ya tatu na mshindi kati ya Afrika Kusini na Congo Brazzaville. Mechi ya kwanza itakuwa ugenini kati ya Septemba 21 na 23 mwaka huu wakati ya marudiano itakuwa nyumbani Oktoba 6 mwaka huu.

DROGBA AENDELEZA MAAJABU WEMBLEY - AIONGOZA CHELSEA KUIUA LIVER. NA KUBEBA UBINGWA WA FA




Chelsea vs Liverpool 2-1 All Goals & Highlights... by kofiswag