Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes
sasa watawakabili Nigeria katika mchezo wa raundi ya pili kusaka tiketi
ya kucheza mataifa Afrika machi Mwakani, baada ya kuwaondosha Sudan kwa
matokeo ya jumla ya 4-3.
Katika mchezo wa leo usiku uliochezwa katika uwanja wa Khartoum baina ya
Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan ulimalizika kwa Sudan kuibuka na
ushindi wa goli 2-1, wakati mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam ulishuhudia Tanzania wakíibuka na ushindi wa
goli 3-1 na kupelekea matokeo ya jumla kusomeka Tanzania 4-3 Sudan.
Usiku wa leo Sudan walikuwa wa mwanzo kuandika goli katika dakika ya 10
kupitia kwa Mohammed Abdelrahman na dakika mbili mbele Mshambuliaji wa
TP Mazembe Thomas Ulimwengu aliisawazishia Ngorongoro Heroes na
kupelekea timu kwenda mapumziko zikiwa sare ya goli 1-1.
Vijana wa Sudan waliokuwa wanasaka ushindi wa hudi na uvumba waliandika
goli la pili katika dakika ya 65 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Ahmed
Nasr na kupelekea mchezo kumalizika kwa Sudan kushinda kwa goli 2-1.
Ngorongoro Heroes iliyofuzu kwa raundi ya pili itaivaa Nigeria julai 28
mwaka huu jijini Dar es Salaam kabla ya kusafiri kwenda Nigeria kwa
ajiri ya marejeano kati ya Agosti 10 na 12 mwaka huu.
Ngorongoro Heroes ambayo inatarajia kurejea nchini jumapili saa 3
asubuhi, ikifanikiwa kuitoa Nigeria, itacheza mechi ya raundi ya tatu na
mshindi kati ya Afrika Kusini na Congo Brazzaville. Mechi ya kwanza
itakuwa ugenini kati ya Septemba 21 na 23 mwaka huu wakati ya marudiano
itakuwa nyumbani Oktoba 6 mwaka huu.
Nzuri sana Ngorongoro.
ReplyDeleteVile vile natoa shukrani zangu za dhati kwa kuwa habarisha wa-Tanzania kuhusu michezo kwa wakati. Big up bro.
Hongera sana ngorongoro. nimegundua biashara iwe inamalizika hapa uwanja wa taifa kama ilivyofanya simba kwa setif na simba na elly ahal shandy tukishinda. hapa nyumbani kwakushinda mabao.mengi. inakuwa rahisi kwa mechi ya marudiano tujifunze kupitia matokeo ya hivi karibuni
ReplyDeletehivi kwann wanashindwa kumwita samata na adam nditi wa chelsea kwenye timu za vijana
ReplyDelete