Search This Blog

Sunday, May 6, 2012

SIMBA YAIKUNG'UTA YANGA GOLI 5-0 NA KUBEBA UBINGWA WA VODACOM PREMIER LEAGUE


Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma baada ya timu ya Simba kuifunga Yanga magoli 5-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar salaam katika mchezo uliokuwa ni wa  kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii  kwenye uwanja wa Taifa, huku ikiwa tayari ni mabingwa wapya wa ligi hiyo, Simba imefanikiwa kutunza heshima yake baada ya kuifunga Yanga magoli 5 kupitia wachezaji wake Emmanuel Okwi, goli la kwanza. 

Goli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu , Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga  goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari 
Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi akishangilia goli mara baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza
Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe  leo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimvisha Medali mtoto wa mchezaji Uhuru Selemani wa Simba.
Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimvisha medali mshabuliaji wa Simba Emmanuel Okwi.
Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia na kocha wao kwa kumbeba juu juu.
Luninga kubwa ya uwanjani ikionyesha magoli yaliyofungwa na Simba
Mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akiwania mpira mbele ya Shadrack Nsajigwa wa Yanga katika mchezao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania inayomalizika leo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiangalia kitu jukwaani haikufahamika lilikuwa ni tukio gani.
Wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi cha timu ya Simba ambao ndiyo mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2011-2012 kikiwa katika picha ya pamoja na Kocha wao Milovan.
Manahodha wa Simba na Yanga Juma Kaseja kushoto na Shadrack Nsajigwa wakisalimiana mbele ya waamuzi kabla ya kuanza kwa mpambano huo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika uwanjani hapo.

2 comments:

  1. Hongera sana kwa simba kwa kutoa kipigo hicho kwa kweli ni kipigo kikubwa ambacho mimi sikukitegemea hata kidogo, 5 bila is too much for yanga hasa ukizingatia wana timu nzuri kwa kweli hayo matokeo yamenishtua sana, yamenifanya nifikirie sababu nyingi sana ambazo huenda zikawa ziko nyuma ya kipigo hiki cha aibu kabisa.
    Najua mengi yataibuka muda si mrefu ila Yanga sasa wakae chini na kujenga klabu yao haya ndio madhara ya kutokuelewana klabuni watu wanajenga klabu moja lakini ngumi mkononi muda wote wenzao wametumia udhaifu wao kuwabonda kisawasawa, unampiga mtu kipigo ambacho ataendelea kukukumbuka daima.
    Niwasihi yanga kipigo hiki kiwe mwanzo wa mabadiliko na si mwanzo wa vita kamili kama ni makosa yamekwisha tokea waangalia walipojikwaa na kurekebisha mambo bado wanatimu nzuri tu.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete
  2. Kaka shaffih chonde chonde kama kuna uwezekano ukatuwekea clip za magoli ya simba tutashukuru sana kwani wengine hatukupata nafasi ya kuangalia mpira mkuu.
    Natanguliza shukrani.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete