Moja ya chanzo kikubwa kinachookwamisha maendeleo ya soka la Tanzania ni kuwa na viongozi wasiojua mipaka ya madaraka na majukumu yao. Huu ni ugonjwa mkubwa unaolikabili soka la Tanzania hususani katika vilabu vikubwa nchini kwetu ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa ndio uti wa mgongo wa soka letu - yaani Simba na Yanga.
Hili suala limeendelea kujidhihirisha leo pale ambapo kumetokea sintofahamu kati ya kamati ya ufundi ya klabu bingwa ya Tanzania Simba Sports Club na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Godfrey Nyange Kaburu baada ya bwana Kaburu kuamua kumsajili mshambuliaji kutoka klabu ya Ruvu Shooting Abdallah Juma bila kufuata taratibu za usajili ndani ya klabu zinavyojieleza na kupaswa kuwa.
Nyange bila kupata maoni ya kocha wala jopo zima la kamati ya ufundi leo hii amekamilisha usajili wa mchezaji huyo kwa maamuzi yake binafsi - jambo ambalo kamati nzima ya ufundi imeona na uingiliwaji wa majukumu alioufanya kiongozi huyu mkubwa wa Simba.
NO WONDER SOKA LA TANZANIA LIMEENDELEA KUDUMAA FOR THE LACK OF PROFESSIONALISM!!!!
Tanzania kama vile tunalaana brother, hivi inakuwaje mtawala (adminstrative) anaingilia majukumu ya ufundi (technical)??? mtu kama Nyange anafahamu kabisa anachokifanya au ndo katumwa na Yanga ili kuanza kuivuruga Simba baada ya kuwa tumetulia muda mrefu??I hate this na achukuliwe hatua haraka sana. majitu kama haya ni kupiga risasi tu kama colombia
ReplyDeleteAnajiona yeye ndie kila kitu,hii ndio shida ya timu kutegemea mbeleko za watu wachache..yeye kama kiongozi anatakiwa kuifanya timu ijiendeshe kisayansi lakini anaendeleza mambo ya kizamani..shame on him..upuuzi tu
ReplyDeletekaka hapa kwetu bongo hakuna soka kuna siasa tu,ila hii itaisha kwa kuwa na timu za kweli za soka kuliko hizi za vyama vya siasa,heti timu zina wanachama hayo ndio matokeo yake kaka,mdau Yahya.
ReplyDeleteTatizo vilabu vya Simba na Yanga vimeingiliwa na watu wasio wa mpira,Kaburu si mtu wa mpira wala hakucheza mpira kapata uongozi Simba kwasababu ya D.Malinzi,Kaburu ni mcheza mpira wa mezani(table tennis)pale Azania Secondary alikuwa tegemeo kwa mchezo huo,yeye na soka wapi na wapi hana utaalam wowote kuhusu soka na watu kama hawa ndiyo wanao didimiza soka la Bongo wamewekwa tu klabu nawatu wao kwasasbabu zao Kaburu ni kama Nchunga wa Yanga sina uhakika kama hata cha ndimu walicheza,wapo kwa maslahi yao si kwa maslahi ya vilabu vyao,uliza sasa mzigo aliopewa huyo mchezaji na mzigo uliochotwa klabu,aa wabongo kaaazi kweli kweli
ReplyDeleteJE HII NI TETESI AU HABARI KAMILI???BRO FANYA CITATION "hoya broh izo habari kwanza ungemuuliza yeye mwenyewe kaburu then ndio ungetoa jibu sasa kutokana na hizo tuhuma sasa hapo hatujui umetoa habari kutoka chanzo gani cha simba...may be angekuwa amezungumza mwenyekiti wa simba au msemaji wao hivyo tungejua uhakika wa hiyo habari au ikishindikana mtafute mchezeji mwenyewe"....maana sasa simba ameongeza uadui kwa yanga hivyo watu wanatumia njia nyingi kuondoa utulivu uliokuwepo simba sports club kwa namna yeyote
ReplyDeleteSasa hivi bundi aliyeko jangwani atahamia msimbazi, hilo jambo alilofanya kaburu halikubaliki katika soka aache wenye kazi zao wazifanye, kama yeye ana pesa asizitumie kufanya kitu anachotaka yeye katika klabu huko ni kuvunja utaratibu, kocha na benchi lake la ufundi wao ndio wanaopaswa kushughulikia mapungufu katika kikosi.
ReplyDeleteHaipendezi kwa mtu Kama Kaburu kuanza kuleta mambo tatanishi hasa katika kipindi hiki ambacho simba inaonekana kutulia.
Mdau
Mike
Unamanisha Abdallah Juma huyu huyu aliyekuwa Mtibwa halafu akaja Simba msimu mmoja baadaye sijui akaenda timu gani, kama ni huyo basi viongozi hatuna, hata kama angekuwa na mamlaka ya kusajili lakini kama ni yule jamaa sijui atasaidia nini Simba, basi ngoja tusubiri tuone.
ReplyDeleteKwa Tanzania sio ajabu kabisa kwa kiongozi kusajili mchezaji hata huyo Nyange na yeye si mjumbe wa kamati ya Utendaji na mahitaji ya Kocha yanajulikana kwamba ni wachezaji wa aina gani wanatakiwa....mbona kina manji wamesajili sana..kina Madega na pia tatizo ni kamati ya ufundi au ni aina ya mchezaji na kiwango chake kikubwa kwa mshabiki yoyote wa Simba akiskia Dullah Juma anatua hapo lazma afurahi na Kaka Shaffii unatakiwa umuulize Nyange kwanini kafanya hivyo na sio kulaumu tu....kuna wachezaji wengine ukiwapata katika angle moja lazma uwasainishe fasta.....kumbuka mtu kama Kasimu Issa Chumu wa Mtibwa alivyosajiliwa au umesahau????
ReplyDeleteACHENI MAMBO YENU..............GODFREY NYANGE KABURU KAIPA MAFANIKIO SANA SIMBA MSIMU HUU KUTOKANA NA WACHEZAJI ALIOWASAJILI YEYE.............MUACHENI AENDELEE KUTUPA RAHA WANA MSIMBAZI....SIIIMBA OIYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE........YANGA FIVE STAR MODERN TAARAB MPO? OKWI ANAWAPA HI...
ReplyDelete