Search This Blog

Thursday, January 26, 2012

JE MANCHESTER UNITED INAPASWA KUMREJESHA OLD TRAFFORD CARLOS QUEIROZ?




Carlos Queiroz amekuwa akionekana mtu ambaye hafai katika siku za hivi karibuni. Amefeli akiwa timu ya taifa ya Ureno, pamoja na kupata matatizo ya kisheria nchini kwao, amekuwa akifukuzwa kazi mapema. Hana yale mafanikio kama kocha mkuu, ni mtu ambaye amekuwa underrated hata na baadhi ya washabiki wa Man United. Mafanikio pekee kama kocha mkuu ni pale aliposhinda kombe la vijana na kikosi cha vijana cha Ureno, pamoja na kushinda kombe la Super Cup akiwa na Los Blancos Real Madrid. Queiroz anasifika kwa kuendeleza kizazi cha dhahabu cha wachezaji wa Ureno, ambacho Luis Figo alikuwa mmoja wao.

Wakati wake akiwa kocha msaidizi @Old Trafford huwa hauongelewi mara kwa mara; kutokana na nature ya nafasi ya ukocha msaidizi. Ambayo ni mara chache sana kutokea kuona wasaidizi wa makocha wakuu kuwa wanatambuliwa na kupewa heshima kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Queiroz alikuwa moja ya makocha bora kabisa wasaidizi at United. Anakumbukwa na wachezaji kwa mapinduzi yake ya mbinu za ufundishaji. Gary Neville anakumbuka moja ya training sessions kupitia makala anazoandika.

“Routine za kila siku za Queiroz kabla ya Champions league semifinal dhidi ya Barcelona mwaka 2008 ilikuwa ni kuweka sit-ups mats (vitambaa vigumu vya kufanyiwa mazoezi ya kukata tumbo) uwanjani ili kuweka alama kwenye sehemu ambapo alitaka mabeki wawe wanasimama kwa ukaribu zaidi.

“Hatukuwahi kuona attention ya namna ile. Tulifanya mazoezi kwa utaratibu ule na baadae tukawa tunatembea na mipira kwa kufuata namna zoezi lile lilivyokuwa linapaswa kuwa.

“Matokeo yake United tuliwatoa Barcelona na katika michezo yote miwili Barca hawakufanikiwa kugusa nyavu zetu.”

Of course, haya yote hayakuwa yakijulikana na mashabiki wa United,.

Ingawa, mashabiki wa United wanapaswa kujua kwamba Queiroz alikuwa msaidizi wa Fergie katika kipindi muhimu zaidi katika klabu yao. Alipokuja , Manchester United walikuwa wameachwa nyuma wakikimbiza upepo wa kikosi kisichofungika cha Arsenal kwa pointi 15. Kikosi cha United kilikuwa kimeanza kudhoofika, huku Ruud Van Nistelrooy na Paul Scholes hawapo kwenye form baada ya kuwa na msimu mzuri wa nyuma yake. Keane alikuwa anakaribia kustaafu, na matumaini pekee yalikuwa winga mchanga aliyeitwa Cristiano Ronaldo (ambaye aliletwa na Queiroz, alipokuwa Old Trafford kwa mara ya kwanza, in 2002-03, msimu ambao United pia walichukua ubingwa).

Tangu kuja kwa Queiroz, United walifanya usajili wa wachezaji mablimbali, lakini wengine wanaweza kuwa wamestuck kwenye minds zaidi ya wengine.

MSIMU WA 2004-05 :

DatePos.NameFromFee
1 July 2004DF Gerard PiquéSpain BarcelonaUndisclosed
6 July 2004FW Giuseppe RossiItaly ParmaUndisclosed
31 August 2004FW Wayne RooneyEngland Everton£27m

Wachezaji wote hawa sasa hivi ni maarufu sana ulimwenguni. Pique sasa anatajwa kama moja ya mabeki bora wa kati. Giuseppe Rossi ambaye kwa sasa yupo nje ya uwanja kwa majeraha alikuwa lulu katika dirisha usajili summer iliyopita. Rooney ndio kafunika kabisa, mchezaji bora England pamoja na Manchester United.

MSIMU WA 2005-06:

DatePos.NameFromFee
1 July 2005GKNetherlands Edwin van der SarEngland FulhamUndisclosed
8 July 2005MFSouth Korea Park Ji-SungNetherlands PSV Eindhoven£4m
19 September 2005GKEngland Ben FosterEngland Stoke CityUndisclosed
5 January 2006DFSerbia and Montenegro Nemanja VidićRussia Spartak MoscowUndisclosed
10 January 2006DFFrance Patrice EvraFrance AS Monaco

Undisclosed

Edwin Van Der Sar sasa anafikiriwa kuwa golikipa bora wa pili au tatu kuwahi kuichezea United katika historia, akitoa mchango mkubwa ambao uliisadia United kucheza fainali 3 za Champions league. Park Ji Sung ni moja ya wachezaji bora wa United leo hii, na siku zote amekuwa akisifika kwa kazi kubwa anayoifanya ndani ya squad ya United. Vidic leo anatajwa kuwa ndio beki wa kati duniani. Evra pia anatajwa kwamba ndio beki bora wa kushoto duniani. Ben Foster ni mchezaji ambaye ameweka historia ya kuwa man of tha match mara 2 katika fainali tofauti za Carling cup.

During the 2007-08 season (Queiroz's last):

DatePos.NameFromFee
1 July 2007MFEngland Owen HargreavesGermany Bayern MunichUndisclosed
2 July 2007MFBrazil AndersonPortugal Porto£30m
(combined)
2 July 2007MFPortugal NaniPortugal Sporting
2 July 2007GKPoland Tomasz KuszczakEngland West Bromwich AlbionUndisclosed
1 January 2008FWAngola ManuchoAngola Petro AtléticoUndisclosed
30 January 2008MFBrazil Rodrigo PossebonBrazil InternacionalUndisclosed
13 June 2008FWItaly Davide PetrucciItaly Roma£200k

Ndio, Manucho na Rodrigo Possebon na pia Petrucci hawakuwa good signings, lakini Anderson, Nani na Owen Hargreaves wamekuwa wachezaji wazuri ndani ya United. Anderson bado ni mchezaji mzuri akiwa katika form, na Nani sasa ni moja ya mawinga bora katika dunia ya soka. Hargreaves alikuwa ndio nguzo na kiunganishi cha safu ya ulinzi na usahmbuliaji katika kikosi cha United kipindi akiwa ahajapatwa na majeruhi.

MAKOMBE WALIYOCHUKUA UNITED CHINI QUEIROZ

Makombe matatu ya Ligi kuu

Makombe mawili ya Ngao za Hisani

Kombe la champions league

Ama kwa hakika unapoangalia na kusoma kwa umakini unagundua umuhimu wa mreno katika jopo la makocha pale Old Trafford. Je sasa ni wakati muafaka kwa United kumrudisha Theatre OF Dreams Carlos Queiroz ambaye kwasasa ni jobless ili kuweza kupambana na Barcelona na timu nyingine zinazotishia utawala wa Manchester United katika soka la vilabu barani ulaya?

Wednesday, January 25, 2012

KWANINI MOURINHO ALINYIMWA KAZI YA KUIFUNDISHA BARCA: SIRI ZAFICHULIWA



Jose Mourinho angekuwa kocha wa Barcelona leo hii - kama isingekuwa ukorofi, ujeuri na tabia yake ya kutopenda kusikiliza.

The special one alikataliwa na mabosi wa Barca baada ya kufanyiwa interview in 2008 na hatimaye Barca wakamteua Pep Guardiola.

Na leo kupitia blog hii utafahamu kwanini usiku huu anaiongoza Real Madrdi na sio wapinzani wao wakubwa katika mchezo wa kombe la Copa De Relay.

Kitabu kipya cha kusisimua kiitwacho, “Barca: The Making of the Greatest Team in the World” kinaelezea namna ambavyo ilikuwa Mourinho alivyokosa kazi @Nou Camp baada ya kufanya mkutano wa siri wan a viongozi wa Barca.

Makamu wa raisi wa zamani wa Barca Marc Ingla na mkurugenzi wa Michezo Txiki Begiristian walikuwa wapo radhi kumpa kazi lakini Jose aliharibu mwenyewe nafasi ya kukaa katika benchi la Catalan giants.

Ingla anasema: “January 2008 tulikuwa katika presha kubwa ya kumuona Jose kutokana na msukumo tulioupata kutoka kwa wakala wake.

“Alikuwa anatuambia, ‘Jose anaijua klabu hii, na amejiandaa, anaelewa style na uwezo mkubwa wa kufundisha.

“Txiki na mimi tulichagua mji wa Lisbon kuwa eneo la kufanyia mkutano wetu na Mourinho

“Kufikia kipindi hicho tulikuwa tumeshamfuata Pep, ambaye alikuwa tayari amefundisha nusu msimu katika kikosi cha Barca B, ili kujua kama atapenda kuifundisha timu ya wakubwa. Lakini ilikuwa ni lazima kumpambanisha na Mourinho.”

Chelsea walimfukuza Mourinho in September 2007 lakini Ingla na Begiristain walikuwa wamevutiwa na uwezo wake aliounyesha.

Pia Jose alifanya kazi @Nou Camp kama mkarimani chini ya Bobby Robson katika miaka ya 1990s.

Lakini Ingla akaongeza: “Nilimwambia Jose, tatizo lako ni kwamba pamoja na ufundishaji mzuri lakini una tabia ya kulumbana na vyombo vya habari na kutokea ukorofi mkubwa ndani yake.

“Nilimwambia, kocha ni nembo ya klabu, huwezi kuanzisha vita kila mahala, hii ni kinyume na utamaduni wetu.

“Mourinho alijibu, ‘Nafahamu, hii ndio staili yangu. Siwezi kubadilika. Alikuwa ndio chaguo letu namba 1 lakini hakuwa msikivu.”

Makamu wa raisi wa sasa Ferran Soriano alielezea mood waliyorudi nayo Ingla na Begiristian waliporudi kutoka Ureno. Alisema: “Walitumia masaa matatu kuongea na Jose, na mwishowe wote walikubaliana kwamba hakuwa mtu sahihi.

“Ingla alisema Mourinho alikuwa anaongea muda wote yeye, asilimia 90 ya maongezi ilitaliwa na Jose na hakuwa akisikiliza. Aliniambia , hakumpenda Mourinho’.”

Watu wa catulunya walimtaka Mourinho - lakini viongozi wa Barca wakafanya maamuzi ya kumchagua Pep Guardiola mchezaji wa zamani wa klabu hiyo.

Ingla alisema: “Mwisho wa mazungumzo yetu na Pep alituambia: “Kwanini msimuajili Mourinho? Ingekuwa kazi rahisi kwenu.”

Nilimjibu: “Hapana, kuna vigezo Fulani yule jamaa hakuwa navyo na tabia yake haikuwa inatufaa kabisa.”

Baada ya hapo Mourinho alienda na akashinda kombe la mabingwa wa ulaya akiwa na Inter Milan – akiwafunga Barca katika nusu fainali.

Tangu Mourinho alipojiunga na Madrid in 2010, kumekuwepo na kadi za njano 66 na nyekundu 9 katika michezo ya El classico.

Uadui unaendelea leo huku Madrid wakiwa wanautetea ubingwa wao wa Spanish Cup – walioupata kwa kuwafunga Barca last April – wanaenda Nou camp wakiwa nyuma kwa goli 2-1 kutoka katika mchezo wa kwanza.

Lakini Barca wameshinda mara makombe 13 kati ya 16 tangu walipomuajiri Guardiola na wamefungwa mara 1 tu kati ya michezo 9 waliyokutana na Madrid ya Mourinho.

Je Mourinho leo atafanikiwa kuwatoa Barcelona katika Spanish Cup na kuweza kulipiza kisasi kwa kunyimwa kazi na Barcelona maiak 3 iliyopita.

HAPPY BIRTHDAY XAVI!



LEO KIUNGO XAVI AMETIMIZA UMRI WA MIAKA 32.NA WAKATI HUO HUO ATAKUA ANASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA HUKU AKICHEZA MCHEZO WAKE WA 31 DHIDI YA REAL MADRID NA KUMFANYA KUIFIKIA REKODI YA MCHEZAJI WA ZAMANI WA BARCELONA JUAN SEGARRA ALIYESTAAFU HUKU AKIWA AMECHEZA MICHEZO 32 DHIDI YA REAL MADRID.

VODACOM PREMIER LEAGUE: SIMBA WAITAFUNA COASTAL UNION



Mchezaji wa timu ya Simba akikokota mpira baada ya kumtoka beki wa timu ya Coastal Union ya Tanga Felix Stanley katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom mzunguko wa pili unaoendelea kwenye uwanja wa Taifa jioni hii,Mpira umekwisha Simba imeshinda goli 2-1goli la kwanza limefungwa na mchezaji Haruna Moshi "Boban" katika kipindi cha kwanza na goli la pili likafungwa na mchezaji Gelvas Kago akipokea pasi nzuri ya Haruna Moshi. Timu ya Coastal Union ilifanikiwa kupata goli katika kipindi cha pili kwa njia ya penati lililofungwa na mchezaji Hamis Shengo, mpaka mpira unakwisha simba 2 na Coastal Union 1.




Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia mara baada ya timu yao kupata goli la kuongoza dhidi ya Coastal Union katika mchezo huo.




BARCA VS MADRID: KIPIGO KUTOKA KWA BARCA KUTAWAHARIBU SANA KISAIKOLOJIA REAL MADRID.


Utawala wa Barcelona wa siku za hivi karibuni mbele ya wapinzani wao wa kihistoria Real Madrid utazidi kuwa mbaya kwa Los Blancos ikiwa wakatalunya watawatoa leo katika kombe la Copa del Rey.

Madrid watakuwa katika wakati mgumu kisaikolojia kama Barcelona atawafunga leo katika mechi hii muhimu, na kitu kibaya kibaya zaidi Los Blancos wanaweza kuchukua muda mrefu sana ku-recover.

Barcelona hawajafungwa katika mechi 6 za mwisho za ligi dhidi Real Madrid, huku wakifunga Madrid na kuwatoa katika michuano ya UEFA Champions league katika hatua ya nusu fainali msimu uliopita.

Kufungwa tena na Barcelona na kutolewa katika mashindano muhimu kutaendelea kuwatesa sana Madrid. Klabu itahitaji kufanya mabadiliko makubwa, ambayo mengine yalipaswa kuwa tayari yameshafanyika.

Sehemu ya ulinzi ya Real inahitaji kuwa stronger zaidi, hasa katikati na upande wa kushoto. Marcelo ni overrated na hana uwezo wa kuzuia kama ambavyo anajua kushambulia. Sure, uwezo wake wa kushambulia na kuipandisha timu upo very effective, lakini katika upande wa kukaba na kuzuia hayupo vizuri. Ricardo Carvalho alikuwa ni world –class player, lakini sio sasa.

Kipindi Los Blancos wakiwa busy kusajili watu wakali wa kushambulia kuanzia summer 2009 wakiwajumuisha kundini Cristiano Ronaldo, Kaka na Karim Benzema, walisahau kabisa kuhusu kuimarisha ukuta wao.

Kwa mtu ambaye alikuwa anategemea zaidi kuwa ukuta mgumu akiwa Inter kabla ya kujiunga na Real Madrid last season, manager Jose Mourinho bado hajafanya usajili wa maana na wenye tija uliomletea mafanikio makubwa katika klabu za nyuma alizofundisha.

Ikiwa Madrid watafungwa na Bacelona na kutolewa leo katika mashindano haya ambayo waliwafunga Barca msimu uliopita, kujiamini kwao kutashuka sana na kusababisha matatizo ya kisaikolojia. Mapambano ya kuondoa utawala wa Barca sasa hayatopiganwa uwanjani tu, lakini pia katika minds za wachezaji wa Real, kitu ambacho sio kizuri kwa Los Blancos.

TAYE TAIWO ASAJILIWA QPR



QPR wamekamilisha usajili wa beki wa AC Milan Taye Taiwo kwa mkopo mpaka mwisho mwa msimu.

The 26-year old pia aliripotiwa kuwa katika rada za Arsenal lakini alichagua kujiunga na boss Mark Hughes @Loftus Road.

Mnigeria huyo ambaye alisajiliwa na AC Milan kutoka Merseille kipindi cha kiangazi kilichopita alianza katika mechi 4 katika klabu hiyo San Siro.

Taiwo ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Hughes mara baada ya kumbadili Neil Warnock wiki tatu zilizopita.

MTOTO WA RAISI WA EQUATORIAL GUINEA - AIPA TIMU YA TAIFA ZAIDI BILLIONI 1 KWA USHINDI DHIDI YA LIBYA.


Teodoro Nguema Obiang Mangue, mtoto wa raisi wa Equatorial Guinea, ametimiza ahadi yake ya kutoa kiasi cha dolla million 1 ambayo ni zaidi ya billion moja ya kibongo kwa timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya timu hiyo kuifunga Libya katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika.

Obiang, ambaye pia ni waziri wa kilimo wan chi hiyo, alitoa ahadi ya kutoa kiasi hicho cha pesa kwa wachezaji ikiwa wangeshinda mechi yao ya ufunguzi.

E Guinea walishinda kwa goli 1-0, goli likifungwa na Javier Balboa ambaye katika hafla ya makabidhiano ya zawadi kutoka mtoto wa raisi, yeye pekee alipewa pesa ya ziada $20,000 kwa kufunga bao la ushindi.

Pia mchezaji mwingine Ivan Bolado ambaye alifunga goli kipindi cha kwanza na likakataliwa nae alipewa $20,000 na mtoto huyo wa raisin a waziri wa kilimo wan chi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta lakini wananchi wakikabiliwa na umaskini wa kutupwa.

Tuesday, January 24, 2012

HAPO MNASEMAJE ?



DEBATE:KUFUNGWA KWA ARSENAL NA MAN UTD ILIKUA NI KWASABABU YA ARSENE WENGER KUMTOA ALEX OXLADE CHAMBERLAIN ?

Hizi ni Comments za baadhi ya mashabiki kutoka kwenye mtandao wa kijamii wa FACEBOOK!

JANA ALIETUFUNGISHA NI ARSENE WENGER NA PIA NIMEGUNDUA ARSENE WENGER HAWEZI KUMFIKIA KWA MBINU SAF HATA ROBO. ARSENE WENGER KWA SASA ANAFA AWE MWALIMU WA ACADEMY NA KUWAIBUA WACHEZAJI KWA SABABU KWA HILO YUPO JUU. ARSENE WENGER SUB ZAKE NYINGI HUWA HAZIONGEZI CHOCHOTE KTK TIMU ZAIDI YA HASARA. HII NI MARA YA 2 NAONA ANAFANYA MAKOSA MPAKA WACHEZAJI WAKE HUWA WANAKASIRIKA NA KUTOPENDA MABADILIKO ANAYOFANYA. FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE YA 2006 ALIFANYA MABADILIKO AMBAYO HAYAKULETA FAIDA NA ANAFANYA HAYO MABADILKO KWA KUMTOA ROBERT PIRES NA KUMWACHA FREDRIK LYUMBERG AMBAYE GAME ILIMKATA. LEHMAN ALIPEWA RED NA LAZIMA ATOLEWE PLAYER ILI AINGIZWE KIPA LAKINI UNA ANGALIA PLAYER GANI WA KUMTOA KTK MAWINGA. NA MAWINGA PIRES NA LYUBERG NI LYUBERG NDIO ILIMKATAA. NA HENRY NA PIRES WALIKUWA WANAELEWANA SANA PALE MBELE. SASA MECHI YA JANA KTK MAPAYER AMBAO GAME ILIMKUBALI MPAKA MAN U WAKAWA WANAMHOFIA ALIKUWA CHERMBALIN. GAME INAENDA KWA KASI NA ANAYEIPELEKA KWA KASI CHERMBERLIN WENGER ANAMTOA ANAMUINGIZA ARSHAVIN AMBAYE FORM YAKE IMEKATAA TOKEA MSIMU ULIOPITA NA MPAKA SASA HIVI FORM YAKE HAIJARUDI. ARSENE WENGER BADO SANA UKILINGANISHA SAF NA MOURINHO NA PIA HATA PEP GURDIOLA. HESABU TOKEA 2000 UEFA NDOGO FAINALI NA GALATASARAI MPAKA SASA HIVI. ARSENAL INAHITAJI KOCHA MWINGINE MTAKE MSITAKE LAKINI BODI ARSENE WENGER NDIO ANAWAFAA>

o If the English Premier League were a classroom, Arsenal would be the boy who works hard throughout the year but fails to make the mark. Manchester City would be the spoilt kid who gets all the expensive and fancy books but is never interested in reading them. Liverpool would be that pupil that is very proud of his father’s academic achievements. As for Man United, it would be that kid who just rides out the term but still emerges top while Chelsea would be the pupil who fails and blames his teachers then his family hires a new teacher every year- RIDHIWAN KIKWETE

o FA charge Manchester City's Mario Balotelli with violent conduct after stamp on Tottenham's Scott Parker
The Italian striker faces a four-game ban after clashing with the midfielder during the 3-2 win over Spurs at the Etihad on Sunday and has until Wednesday evening to respond-HUSSEIN FACT KAPINGA

o We can take out a couple of positives from last nights match against Manchester United. One- RVP's amazing goal-scoring form. The Dutch maestro has 19 goals this season in the EPL and leads the top scorers section by a 5-goal margin! Another positive would be the performance of Alex Oxlade-Chamberlain. The English lad is definitely one for the future!-SOSY DIWANI

o Hiv ile subs: ya wenger jana ya kumtoa Alex oxlade-chamberlain na kumwingiza Andre arshavin alifikiria nin et,n kweli alishauriana na kamati yke ya ufundi pale bechi kweli or n yeye 2 alikurupuka 2 kwa vle yeye ndo mananger wa arsnal bac,kila k2 yeye 2.
Anyway pole sn fans wa arsnal wenger ndo mchawi wenu 2 wachezaj mnao wazur 2,sema kwa vle alex hakuwa mfarance bac wenger akaamua kumtoa asiendelee kushaini uwanjan.-NTANDU BODE

Monday, January 23, 2012

TAARIFA KUTOKA TFF

WABUNGE KUCHANGIA TWIGA STARS

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia timu ya Bunge wameomba kucheza mechi maalumu dhidi ya Twiga Stars kabla ya kuwasilisha mchango wao kwa timu hiyo. Benchi la Ufundi la Twiga Stars kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubali kucheza mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya maonesho tu ambapo baada ya kumalizika ndipo Wabunge watakabidhi kile walichopanga kutoa kwa timu. Mechi hiyo itafanyika Alhamisi (Januari 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume uliopo Ofisi za TFF kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars na Namibia zitapambana Jumapili (Januari 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya marudiano kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.

GHARAMA ZA UWANJA- TWIGA STARS VS NAMIBIATFF

imeiandikia Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuomba iondoe gharama za kutumia Uwanja wa Taifa ambazo ni fixed kwenye mechi kati ya Twiga Stars na Namibia. Lengo la maombi hayo ni kusaidia kupunguza gharama za kuandaa mechi hiyo ambayo bajeti nzima ni sh . 74,660,000. Hiyo inajumuisha usafiri, posho kwa wachezaji, posho kwa benchi la ufundi, gharama za kambi, dawa na maji ya kunywa wakati wa mazoezi na mechi kwa Twiga Stars. Maeneo mengine ni usafiri wa ndege, usafiri wa ndani (magari mawili), posho na hoteli kwa kamishna na waamuzi. Nyingine ni gharama za timu ya Namibia itakayokuwa na watu 25 ambazo ni usafiri wa ndani (magari matatu), hoteli (malazi na chakula) na maji ya kunywa wakati wa mazoezi na mechi. Gharama ambazo ni fixed kwa matumizi ya Uwanja wa Taifa ni pamoja na usafi na ulinzi, umeme, maandalizi ya sehemu ya kuchezea, malipo kwa kampuni ya Wachina na asilimia kumi ya mapato.

AFCON: MANUCHO AIONGOZA ANGOLA KUITANDIKA BURKINA FASO

AFCON: DROGBA AWAUA WASUDAN

JIJI LA MANCHESTER LAENDELEZA UBABE MBELE YA LONDON: CITY NAYO WAITANDIKA SPURS

MAN UNITED WAENDELEZA UBABE KWA ARSENAL

BALOTELLI HAISHI KWA VITUKO!

AFCON 2012 YAANZA NA MATOKEO YA KUSHANGAZA!







LA LIGA: MESSI AFUNGA HAT TRICK,RONALDO NAYE ATUPIA KAMBANI MARA MBILI