Search This Blog

Wednesday, January 25, 2012

BARCA VS MADRID: KIPIGO KUTOKA KWA BARCA KUTAWAHARIBU SANA KISAIKOLOJIA REAL MADRID.


Utawala wa Barcelona wa siku za hivi karibuni mbele ya wapinzani wao wa kihistoria Real Madrid utazidi kuwa mbaya kwa Los Blancos ikiwa wakatalunya watawatoa leo katika kombe la Copa del Rey.

Madrid watakuwa katika wakati mgumu kisaikolojia kama Barcelona atawafunga leo katika mechi hii muhimu, na kitu kibaya kibaya zaidi Los Blancos wanaweza kuchukua muda mrefu sana ku-recover.

Barcelona hawajafungwa katika mechi 6 za mwisho za ligi dhidi Real Madrid, huku wakifunga Madrid na kuwatoa katika michuano ya UEFA Champions league katika hatua ya nusu fainali msimu uliopita.

Kufungwa tena na Barcelona na kutolewa katika mashindano muhimu kutaendelea kuwatesa sana Madrid. Klabu itahitaji kufanya mabadiliko makubwa, ambayo mengine yalipaswa kuwa tayari yameshafanyika.

Sehemu ya ulinzi ya Real inahitaji kuwa stronger zaidi, hasa katikati na upande wa kushoto. Marcelo ni overrated na hana uwezo wa kuzuia kama ambavyo anajua kushambulia. Sure, uwezo wake wa kushambulia na kuipandisha timu upo very effective, lakini katika upande wa kukaba na kuzuia hayupo vizuri. Ricardo Carvalho alikuwa ni world –class player, lakini sio sasa.

Kipindi Los Blancos wakiwa busy kusajili watu wakali wa kushambulia kuanzia summer 2009 wakiwajumuisha kundini Cristiano Ronaldo, Kaka na Karim Benzema, walisahau kabisa kuhusu kuimarisha ukuta wao.

Kwa mtu ambaye alikuwa anategemea zaidi kuwa ukuta mgumu akiwa Inter kabla ya kujiunga na Real Madrid last season, manager Jose Mourinho bado hajafanya usajili wa maana na wenye tija uliomletea mafanikio makubwa katika klabu za nyuma alizofundisha.

Ikiwa Madrid watafungwa na Bacelona na kutolewa leo katika mashindano haya ambayo waliwafunga Barca msimu uliopita, kujiamini kwao kutashuka sana na kusababisha matatizo ya kisaikolojia. Mapambano ya kuondoa utawala wa Barca sasa hayatopiganwa uwanjani tu, lakini pia katika minds za wachezaji wa Real, kitu ambacho sio kizuri kwa Los Blancos.

1 comment:

  1. Shaffih,mimi ni shabiki wa madrid kwa upande wa hispania,leo najua tunapigwa na cha muhimu ni kuanza kutengeneza saikolojia za wachezaji wetu coz kutoka salama camp Now ni miujiza
    Chela wa Dom

    ReplyDelete