Search This Blog

Thursday, January 26, 2012

JE MANCHESTER UNITED INAPASWA KUMREJESHA OLD TRAFFORD CARLOS QUEIROZ?




Carlos Queiroz amekuwa akionekana mtu ambaye hafai katika siku za hivi karibuni. Amefeli akiwa timu ya taifa ya Ureno, pamoja na kupata matatizo ya kisheria nchini kwao, amekuwa akifukuzwa kazi mapema. Hana yale mafanikio kama kocha mkuu, ni mtu ambaye amekuwa underrated hata na baadhi ya washabiki wa Man United. Mafanikio pekee kama kocha mkuu ni pale aliposhinda kombe la vijana na kikosi cha vijana cha Ureno, pamoja na kushinda kombe la Super Cup akiwa na Los Blancos Real Madrid. Queiroz anasifika kwa kuendeleza kizazi cha dhahabu cha wachezaji wa Ureno, ambacho Luis Figo alikuwa mmoja wao.

Wakati wake akiwa kocha msaidizi @Old Trafford huwa hauongelewi mara kwa mara; kutokana na nature ya nafasi ya ukocha msaidizi. Ambayo ni mara chache sana kutokea kuona wasaidizi wa makocha wakuu kuwa wanatambuliwa na kupewa heshima kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Queiroz alikuwa moja ya makocha bora kabisa wasaidizi at United. Anakumbukwa na wachezaji kwa mapinduzi yake ya mbinu za ufundishaji. Gary Neville anakumbuka moja ya training sessions kupitia makala anazoandika.

“Routine za kila siku za Queiroz kabla ya Champions league semifinal dhidi ya Barcelona mwaka 2008 ilikuwa ni kuweka sit-ups mats (vitambaa vigumu vya kufanyiwa mazoezi ya kukata tumbo) uwanjani ili kuweka alama kwenye sehemu ambapo alitaka mabeki wawe wanasimama kwa ukaribu zaidi.

“Hatukuwahi kuona attention ya namna ile. Tulifanya mazoezi kwa utaratibu ule na baadae tukawa tunatembea na mipira kwa kufuata namna zoezi lile lilivyokuwa linapaswa kuwa.

“Matokeo yake United tuliwatoa Barcelona na katika michezo yote miwili Barca hawakufanikiwa kugusa nyavu zetu.”

Of course, haya yote hayakuwa yakijulikana na mashabiki wa United,.

Ingawa, mashabiki wa United wanapaswa kujua kwamba Queiroz alikuwa msaidizi wa Fergie katika kipindi muhimu zaidi katika klabu yao. Alipokuja , Manchester United walikuwa wameachwa nyuma wakikimbiza upepo wa kikosi kisichofungika cha Arsenal kwa pointi 15. Kikosi cha United kilikuwa kimeanza kudhoofika, huku Ruud Van Nistelrooy na Paul Scholes hawapo kwenye form baada ya kuwa na msimu mzuri wa nyuma yake. Keane alikuwa anakaribia kustaafu, na matumaini pekee yalikuwa winga mchanga aliyeitwa Cristiano Ronaldo (ambaye aliletwa na Queiroz, alipokuwa Old Trafford kwa mara ya kwanza, in 2002-03, msimu ambao United pia walichukua ubingwa).

Tangu kuja kwa Queiroz, United walifanya usajili wa wachezaji mablimbali, lakini wengine wanaweza kuwa wamestuck kwenye minds zaidi ya wengine.

MSIMU WA 2004-05 :

DatePos.NameFromFee
1 July 2004DF Gerard PiquéSpain BarcelonaUndisclosed
6 July 2004FW Giuseppe RossiItaly ParmaUndisclosed
31 August 2004FW Wayne RooneyEngland Everton£27m

Wachezaji wote hawa sasa hivi ni maarufu sana ulimwenguni. Pique sasa anatajwa kama moja ya mabeki bora wa kati. Giuseppe Rossi ambaye kwa sasa yupo nje ya uwanja kwa majeraha alikuwa lulu katika dirisha usajili summer iliyopita. Rooney ndio kafunika kabisa, mchezaji bora England pamoja na Manchester United.

MSIMU WA 2005-06:

DatePos.NameFromFee
1 July 2005GKNetherlands Edwin van der SarEngland FulhamUndisclosed
8 July 2005MFSouth Korea Park Ji-SungNetherlands PSV Eindhoven£4m
19 September 2005GKEngland Ben FosterEngland Stoke CityUndisclosed
5 January 2006DFSerbia and Montenegro Nemanja VidićRussia Spartak MoscowUndisclosed
10 January 2006DFFrance Patrice EvraFrance AS Monaco

Undisclosed

Edwin Van Der Sar sasa anafikiriwa kuwa golikipa bora wa pili au tatu kuwahi kuichezea United katika historia, akitoa mchango mkubwa ambao uliisadia United kucheza fainali 3 za Champions league. Park Ji Sung ni moja ya wachezaji bora wa United leo hii, na siku zote amekuwa akisifika kwa kazi kubwa anayoifanya ndani ya squad ya United. Vidic leo anatajwa kuwa ndio beki wa kati duniani. Evra pia anatajwa kwamba ndio beki bora wa kushoto duniani. Ben Foster ni mchezaji ambaye ameweka historia ya kuwa man of tha match mara 2 katika fainali tofauti za Carling cup.

During the 2007-08 season (Queiroz's last):

DatePos.NameFromFee
1 July 2007MFEngland Owen HargreavesGermany Bayern MunichUndisclosed
2 July 2007MFBrazil AndersonPortugal Porto£30m
(combined)
2 July 2007MFPortugal NaniPortugal Sporting
2 July 2007GKPoland Tomasz KuszczakEngland West Bromwich AlbionUndisclosed
1 January 2008FWAngola ManuchoAngola Petro AtléticoUndisclosed
30 January 2008MFBrazil Rodrigo PossebonBrazil InternacionalUndisclosed
13 June 2008FWItaly Davide PetrucciItaly Roma£200k

Ndio, Manucho na Rodrigo Possebon na pia Petrucci hawakuwa good signings, lakini Anderson, Nani na Owen Hargreaves wamekuwa wachezaji wazuri ndani ya United. Anderson bado ni mchezaji mzuri akiwa katika form, na Nani sasa ni moja ya mawinga bora katika dunia ya soka. Hargreaves alikuwa ndio nguzo na kiunganishi cha safu ya ulinzi na usahmbuliaji katika kikosi cha United kipindi akiwa ahajapatwa na majeruhi.

MAKOMBE WALIYOCHUKUA UNITED CHINI QUEIROZ

Makombe matatu ya Ligi kuu

Makombe mawili ya Ngao za Hisani

Kombe la champions league

Ama kwa hakika unapoangalia na kusoma kwa umakini unagundua umuhimu wa mreno katika jopo la makocha pale Old Trafford. Je sasa ni wakati muafaka kwa United kumrudisha Theatre OF Dreams Carlos Queiroz ambaye kwasasa ni jobless ili kuweza kupambana na Barcelona na timu nyingine zinazotishia utawala wa Manchester United katika soka la vilabu barani ulaya?

1 comment:

  1. as man utd fan, i would like to see the return of queiroz at OT

    ReplyDelete