Search This Blog

Wednesday, January 25, 2012

KWANINI MOURINHO ALINYIMWA KAZI YA KUIFUNDISHA BARCA: SIRI ZAFICHULIWA



Jose Mourinho angekuwa kocha wa Barcelona leo hii - kama isingekuwa ukorofi, ujeuri na tabia yake ya kutopenda kusikiliza.

The special one alikataliwa na mabosi wa Barca baada ya kufanyiwa interview in 2008 na hatimaye Barca wakamteua Pep Guardiola.

Na leo kupitia blog hii utafahamu kwanini usiku huu anaiongoza Real Madrdi na sio wapinzani wao wakubwa katika mchezo wa kombe la Copa De Relay.

Kitabu kipya cha kusisimua kiitwacho, “Barca: The Making of the Greatest Team in the World” kinaelezea namna ambavyo ilikuwa Mourinho alivyokosa kazi @Nou Camp baada ya kufanya mkutano wa siri wan a viongozi wa Barca.

Makamu wa raisi wa zamani wa Barca Marc Ingla na mkurugenzi wa Michezo Txiki Begiristian walikuwa wapo radhi kumpa kazi lakini Jose aliharibu mwenyewe nafasi ya kukaa katika benchi la Catalan giants.

Ingla anasema: “January 2008 tulikuwa katika presha kubwa ya kumuona Jose kutokana na msukumo tulioupata kutoka kwa wakala wake.

“Alikuwa anatuambia, ‘Jose anaijua klabu hii, na amejiandaa, anaelewa style na uwezo mkubwa wa kufundisha.

“Txiki na mimi tulichagua mji wa Lisbon kuwa eneo la kufanyia mkutano wetu na Mourinho

“Kufikia kipindi hicho tulikuwa tumeshamfuata Pep, ambaye alikuwa tayari amefundisha nusu msimu katika kikosi cha Barca B, ili kujua kama atapenda kuifundisha timu ya wakubwa. Lakini ilikuwa ni lazima kumpambanisha na Mourinho.”

Chelsea walimfukuza Mourinho in September 2007 lakini Ingla na Begiristain walikuwa wamevutiwa na uwezo wake aliounyesha.

Pia Jose alifanya kazi @Nou Camp kama mkarimani chini ya Bobby Robson katika miaka ya 1990s.

Lakini Ingla akaongeza: “Nilimwambia Jose, tatizo lako ni kwamba pamoja na ufundishaji mzuri lakini una tabia ya kulumbana na vyombo vya habari na kutokea ukorofi mkubwa ndani yake.

“Nilimwambia, kocha ni nembo ya klabu, huwezi kuanzisha vita kila mahala, hii ni kinyume na utamaduni wetu.

“Mourinho alijibu, ‘Nafahamu, hii ndio staili yangu. Siwezi kubadilika. Alikuwa ndio chaguo letu namba 1 lakini hakuwa msikivu.”

Makamu wa raisi wa sasa Ferran Soriano alielezea mood waliyorudi nayo Ingla na Begiristian waliporudi kutoka Ureno. Alisema: “Walitumia masaa matatu kuongea na Jose, na mwishowe wote walikubaliana kwamba hakuwa mtu sahihi.

“Ingla alisema Mourinho alikuwa anaongea muda wote yeye, asilimia 90 ya maongezi ilitaliwa na Jose na hakuwa akisikiliza. Aliniambia , hakumpenda Mourinho’.”

Watu wa catulunya walimtaka Mourinho - lakini viongozi wa Barca wakafanya maamuzi ya kumchagua Pep Guardiola mchezaji wa zamani wa klabu hiyo.

Ingla alisema: “Mwisho wa mazungumzo yetu na Pep alituambia: “Kwanini msimuajili Mourinho? Ingekuwa kazi rahisi kwenu.”

Nilimjibu: “Hapana, kuna vigezo Fulani yule jamaa hakuwa navyo na tabia yake haikuwa inatufaa kabisa.”

Baada ya hapo Mourinho alienda na akashinda kombe la mabingwa wa ulaya akiwa na Inter Milan – akiwafunga Barca katika nusu fainali.

Tangu Mourinho alipojiunga na Madrid in 2010, kumekuwepo na kadi za njano 66 na nyekundu 9 katika michezo ya El classico.

Uadui unaendelea leo huku Madrid wakiwa wanautetea ubingwa wao wa Spanish Cup – walioupata kwa kuwafunga Barca last April – wanaenda Nou camp wakiwa nyuma kwa goli 2-1 kutoka katika mchezo wa kwanza.

Lakini Barca wameshinda mara makombe 13 kati ya 16 tangu walipomuajiri Guardiola na wamefungwa mara 1 tu kati ya michezo 9 waliyokutana na Madrid ya Mourinho.

Je Mourinho leo atafanikiwa kuwatoa Barcelona katika Spanish Cup na kuweza kulipiza kisasi kwa kunyimwa kazi na Barcelona maiak 3 iliyopita.

1 comment:

  1. Hata hivyo bado ureuri wake umemsaidia kufanya makubwa haya hapa chini.

    Honours
    - Champions League: 2003/04, 2009/10
    - UEFA Cup: 2002/03
    - Portuguese league: 2002/03, 2003/04
    - Premier League: 2004/05, 2005/06
    - Scudetto: 2008/09, 2009/10
    - Copa del Rey: 2011
    - Cup of Portugal: 2002/03
    - FA Cup: 2006/07
    - Carling Cup: 2004/05, 2006/07
    - Cup of Italy: 2009/10
    - Portuguese Super Cup: 2003
    - Community Shield: 2005
    - Italian Super Cup: 2008

    Individual accolades
    - FIFA World Coach of the Year: 2010
    - IFFHS World's Best Coach: 2004, 2005, 2010
    - UEFA Coach of the Year: 2002/03, 2003/04
    - Best Coach of the Portuguese League: 2002/03, 2003/04
    - Best Coach of the Premiership: 2004/05, 2005/06
    - Best Coach of the Italian League: 2009

    ReplyDelete