Search This Blog

Wednesday, January 25, 2012

MTOTO WA RAISI WA EQUATORIAL GUINEA - AIPA TIMU YA TAIFA ZAIDI BILLIONI 1 KWA USHINDI DHIDI YA LIBYA.


Teodoro Nguema Obiang Mangue, mtoto wa raisi wa Equatorial Guinea, ametimiza ahadi yake ya kutoa kiasi cha dolla million 1 ambayo ni zaidi ya billion moja ya kibongo kwa timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya timu hiyo kuifunga Libya katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika.

Obiang, ambaye pia ni waziri wa kilimo wan chi hiyo, alitoa ahadi ya kutoa kiasi hicho cha pesa kwa wachezaji ikiwa wangeshinda mechi yao ya ufunguzi.

E Guinea walishinda kwa goli 1-0, goli likifungwa na Javier Balboa ambaye katika hafla ya makabidhiano ya zawadi kutoka mtoto wa raisi, yeye pekee alipewa pesa ya ziada $20,000 kwa kufunga bao la ushindi.

Pia mchezaji mwingine Ivan Bolado ambaye alifunga goli kipindi cha kwanza na likakataliwa nae alipewa $20,000 na mtoto huyo wa raisin a waziri wa kilimo wan chi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta lakini wananchi wakikabiliwa na umaskini wa kutupwa.

No comments:

Post a Comment