Search This Blog

Tuesday, February 26, 2013

KOCHA AZAM AFUNGIWA NA KUPIGWA FAINI KWA KUCHOJOA BUKTA


Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.

Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.

Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.

Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers.

Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita.

Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana.

Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro.

Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea.

Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United.

Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki.

Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

MWAMUZI FIFA, MAHAGI WAONDOLEWA VPL
Mwamuzi Msaidizi wa FIFA, Ferdinand Chacha ameondolewa kuchezesha mechi za VPL baada ya kupata alama za chini kwenye mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa mwezi uliopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Waamuzi wanaopata alama 6.5 au chini ya hapo kati ya 10 zinazohitajika pia wanaondolewa kwenye mechi za VPL na FDL.

Waamuzi wengine walioondolewa kwa kutomudu mechi walizochezesha za VPL ni Mathew Akrama (Yanga vs Simba), Ephrony Ndissa (Yanga vs Simba), Ronald Swai (Yanga vs Mtibwa Sugar).  

Walioondolewa kwa kupata alama za chini ni Alex Mahagi (Simba vs JKT Ruvu), Methusela Musebula (Toto Africans vs Coastal Union), Lingstone Lwiza (Toto Africans vs Coastal Union), Idd Mikongoti (Toto Africans vs Mtibwa Sugar) na Samson Kobe (Toto Africans vs Mtibwa Sugar).

Masoud Mkelemi aliyekuwa mwamuzi wa mezani katika mechi ya FDL kati ya Moro United na Villa Squad ameondolewa kwa kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting) na alichelewa kwa dakika tano kufika uwanjani.

BAADA YA SERIKALI KUIPIGA CHINI KATIBA YAO MPYA - KAMATI YA UTENDAJI TFF KUJADILI TAMKO LA SERIKALI


Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepokea barua ya Serikali ikielezea uamuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kutengua uamuzi wa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo nchini kuidhinisha marekebisho ya Katiba ya TFF toleo la 2012.

Baada ya kupokea barua hiyo jana alasiri (Februari 25 mwaka huu), Sekretarieti iliwasiliana na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye ameagiza kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kujadili tamko hilo.

Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji ya TFF kitafanyika Jumamosi (Machi 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

KAMATI YA UTENDAJI TFF KUJADILI TAMKO LA SERIKALI

Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepokea barua ya Serikali ikielezea uamuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kutengua uamuzi wa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo nchini kuidhinisha marekebisho ya Katiba ya TFF toleo la 2012.

Baada ya kupokea barua hiyo jana alasiri (Februari 25 mwaka huu), Sekretarieti iliwasiliana na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye ameagiza kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kujadili tamko hilo.

Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji ya TFF kitafanyika Jumamosi (Machi 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

KOCHA AZAM AFUNGIWA KWA KUCHOJOA BUKTA
Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.

Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.

Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.

Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers.

Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita.

Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana.

Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro.

Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea.

Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United.

Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki.

Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

MWAMUZI FIFA, MAHAGI WAONDOLEWA VPL
Mwamuzi Msaidizi wa FIFA, Ferdinand Chacha ameondolewa kuchezesha mechi za VPL baada ya kupata alama za chini kwenye mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa mwezi uliopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Waamuzi wanaopata alama 6.5 au chini ya hapo kati ya 10 zinazohitajika pia wanaondolewa kwenye mechi za VPL na FDL.

Waamuzi wengine walioondolewa kwa kutomudu mechi walizochezesha za VPL ni Mathew Akrama (Yanga vs Simba), Ephrony Ndissa (Yanga vs Simba), Ronald Swai (Yanga vs Mtibwa Sugar).  

Walioondolewa kwa kupata alama za chini ni Alex Mahagi (Simba vs JKT Ruvu), Methusela Musebula (Toto Africans vs Coastal Union), Lingstone Lwiza (Toto Africans vs Coastal Union), Idd Mikongoti (Toto Africans vs Mtibwa Sugar) na Samson Kobe (Toto Africans vs Mtibwa Sugar).

Masoud Mkelemi aliyekuwa mwamuzi wa mezani katika mechi ya FDL kati ya Moro United na Villa Squad ameondolewa kwa kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting) na alichelewa kwa dakika tano kufika uwanjani.

MAKAMISHNA VPL/FDL WASIMAMISHWA, WAONYWA
Baadhi ya makamishna wa VPL na FDL wameondolewa na wengine kusimamishwa kusimamia mechi za ligi hizo kutokana na upungufu kwenye ripoti zao au kutowasilisha kabisa ripoti hizo TFF baada ya mechi.

Kamishna Mohamed Jumbe aliyesimamia mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba ameondolewa kwenye orodha ya makamishna kutokana na ripoti yake kuwa na upungufu.

Makamishna wa mechi kati ya JKT Oljoro vs Yanga (Hakim Byemba), JKT Oljoro vs Kagera Sugar (Salum Kikwamba), Toto Africans vs African Lyon (Charles Komba), Coastal Union vs JKT Oljoro (Mohamed Nyange) wamesimamishwa hadi watakapowasilisha ripoti zao TFF.

Kwa upande wa FDL makamishna waliosimamishwa hadi watakapowasilisha ripoti zao TFF ni wa mechi kati ya Kurugenzi vs Polisi Iringa, Morani vs Mwadui, Polisi Mara vs Pamba, Polisi Mara vs Mwadui, Morani vs JKT Kanembwa na Pamba vs Polisi Dodoma.

Wengine ni Mwadui vs JKT Kanembwa, Polisi Tabora vs Morani, Polisi Dodoma vs Polisi Mara, Polisi Tabora vs Mwadui, Polisi Mara vs Morani, JKT Kanembwa vs Polisi Mara, Morani vs Rhino Rangers na Small Kids vs Mkamba Rangers.

Kamati ya Ligi imewakumbusha makamishna wote kuwa ni jukumu lao kuhakikisha ripoti zao zimefika TFF na kurekebisha upungufu wa jinsi ya kuripoti matukio yanayotokea uwanjani. Licha ya kutuma nakala kwa njia ya email, wanatakiwa pia kuwasilisha ripoti halisi (original) TFF.

MECHI YA SIMBA, MTIBWA YAINGIZA MIL 62/-
Mechi namba 121 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Februari 24 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Mtibwa Sugar kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba imeingiza sh. 239,686,000.

Watazamaji 10,669 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,577,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,467,694.92.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 9,491 na kuingiza sh. 47,455,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 105 na kuingiza sh. 2,100,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,412,162.26, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,447,297.36, Kamati ya Ligi sh. 4,447,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,223,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,729,504.53.

VUMBI LA VPL KUENDELEA JUMATANO
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Februari 27 mwaka huu) kwa  mechi tano zitakazochezwa katika viwanja tofauti.

Vinara wa ligi hiyo Yanga wataikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000 (viti vya bluu na kijani), sh. 8,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 (VIP C na B) na sh. 20,000 (VIP A).

Mechi nyingine za ligi hiyo ni Coastal Union vs Ruvu Shooting (Mkwakwani, Tanga), Polisi Morogoro vs Mgambo Shooting (Jamhuri, Morogoro), JKT Ruvu vs Toto Africans (Azam Complex, Dar es Salaam) na Mtibwa Sugar vs Tanzania Prisons (Manungu, Morogoro).

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

HIVI NDIVYO MILAN ILIVYOIFUNGA BARCELONA.


Monday, February 25, 2013

MAKALA: SIFA ZA MCHEZAJI BORA NA SIMBA ILIVYOIKAMATWA LIBOLO PART II


LEO tunaendelea na sifa za mchezaji bora huku tukioanisha sifa hizo na mambo yalivyotokea katika mchezo kati ya Simba na Libolo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa hivi karibuni.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilifungwa ba 1-0, lililofungwa na Joao Martins.

Endelea na sifa za mchezaji bora tukirejea katika mchezo wa Simba dhidi ya Libolo;

NGUVU ZA KISAIKOLOJIA (Mental Toughness)
Kitu cha pili kwa umuhimu baada ya uwezo wa kimwili kwa mchezaji, ni upande wa saikolojia. Ni jinsi gani mchezaji ana nguvu kisaikolojia, siyo mwoga, ana ujasiri na uwezo wa kuhimili mapambano huku akibakia na lengo moja kichwani mwake nalo ni kusaka ushindi.

Katika mchezo wa Simba na Libolo, licha ya mashabiki wa Simba kuwa wengi huku wakiwazomea wale wa Libolo, bado wachezaji wa Libolo walisimama katika lengo lao na kuweza kupambana hadi kupata bao. Hata mashabiki walioaminika kuwa ni kutoka upande wa Yanga waliokuwa wakiishangilia Libolo hawakuwa wengi kulinganisha na wale wa Simba. Libolo waliiva kisaikolojia.

Kuna wakati mashabiki wa Simba waliweza kuwazomea wachezaji wa timu yao pindi wanapokosea na waliweza kuwachanganya zaidi. Hapo wachezaji wengi wa Libolo walikuwa na nguvu ya kisaikolojia kuliko wale wa Simba.

Nguvu za kisaikolojia kwa mchezaji zinasambaa katika wigo mpana wenye vipengele vingi. Moja ya vipengele hivi huonyesha kiwango cha mchezaji kwa wakati uliopo sasa lakini pia huonyesha jinsi mchezaji atakavyoweza au kushindwa kupiga hatua siku za mbeleni na zaidi ya hapo itaonyesha mchezaji husika ni mshindani wa aina gani.

Msingi wa mchezo wa soka ni mapambano ya mmoja dhidi ya mmoja. Na siku zote mchezaji bora unategemea ashinde pambano lolote dhidi ya mchezaji mwingine pale wanapokutana uwanjani.

KUJIAMINI KWA MCHEZAJI
Kisaikolojia kinachochangia ushindi ni hali ya kujiamini kwa mchezaji na si wachezaji wote wanajiamini kwenye mapambano ya mtu mmoja dhidi ya mwingine, baadhi ya wachezaji ni waoga wa hali kama hii, wanaogopa kufanya makosa na kwa sababu hiyo wanaogopa kujaribu.

Lakini mchezaji bora ni yule anayependa changamoto, anayetamani kuwa kwenye aina hii ya mapambano muda wote kwani kichwani mwake anahisi kuwa anapaswa kuwakumbusha kuwa yeye ni bora.

Simba ilikosa wachezaji wazoefu katika nafasi nyeti, wachezaji kama Shomari Kapombe na Haruna Chanongo bado ni chipukizi na wasioweza kucheza dakika zote 90 na timu iliyojiandaa vyema kama Libolo.

Unaweza kushangaa ametajwa Kapombe hapo wakati anaonekana kama mmoja wa wachezaji mahili kwa sasa katika kikosi cha Simba, hapana Kapombe anachezeshwa Simba kwa kuwa tu, hakuna mchezaji mwingine.

Katika mechi moja tu ya nyuma kabla ya kuivaa Libolo, Kapombe alicheza kama beki wa kati, ndani ya siku chache, anachezeshwa kama beki wa kushoto, unategemea nini kwa timu kama Libolo? Lazima atakuwa uchochoro, na hata krosi ya bao ya Libolo ilipitia upande wake. Kapombe ni mchezaji mzuri, lakini tatizo linakuja kuwa, amejiandaa vipi kucheza na timu kama Libolo?

MAPAMBANO YA WATU BORA
Washambuliaji bora siku zote wanapenda kukutana na mabeki bora kudhihirisha kuwa wao ni bora na vivyo hivyo kwa mabeki bora, siku zote wanapenda kukabiliana na washambuliaji bora ili wakumbukwe kama watu walioweza kuwanyamazisha na kuwaficha kabisa.

Kujiamini hakuishii kwa mapambano ya mtu mmoja mmoja, wachezaji bora huwafanya wenzao wajiamini, wanaambukiza wenzao ile hali ya kutokuwa waoga.

Kuna wakati wachezaji wa Libolo walikuwa wanauchezea mpira watakavyo baada ya kujiamini na kujiridhisha na kiwango cha wachezaji wengi wa Simba. Hao walipigiana pasi watakavyo na kushambulia kwa muda waliotaka.

Simba kupitia kwa Mrisho Ngassa na Chanongo walikuwa wakifika mara kadhaa katika lango la Libolo, lakini Haruna Moshi ‘Boban’ aliyecheza kama straika hakuwa katika hali ya kujiamin, matokeo yake alikuwa na papara ya kufunga na kujikuta akitumia muda mwingi kuwatoa mchezoni Libolo ambao walikuwa wameshiba kisaikolojia kuhusu mambo yote mabaya uwanjani.

Simba hawakuonyesha kupambana mmoja mmoja katika mchezo huo na mara nyingi walicheza kwa mfumo zaidi huku Libolo wakiwa wameshaudhibiti mfumo wa Simba, ambao ulikuwa 4-4-2.

KUTOKATA TAMAA MAPEMA
Lakini ni yale mapambano ya mtu mmoja mmoja ambayo yanamfanya mchezaji aonyeshe ishara za kutaka kuendelea kujifunza na hivyo kukomaa zaidi katika hali kama hizo za mapambano pamoja na hali ya kujitolea kwa ajili ya timu na kutokukubali kushindwa kwa hali yoyote ile.

Katika hili, kidogo Chanongo na Ngassa ndiyo walionekana kucheza kwa mapambano ya mtu mmoja mmoja uwanjani na kuifanya Simba kukaa na mpira kwa muda mrefu kidogo.

Ni ile ya hali kujitolea kwa imani na dhamira ya kutaka kuwa bora inayomfanya mchezaji awe juu ya wenzie. Kama unakumbuka, Emmanuel Okwi alikuwa na sifa kama hii ya kujituma uwanjani kwani alitumia vyema kipaji chake.

Okwi aliweza kuwalamba chenga mabeki kadhaa kabla ya kutoa pasi na mfungaji akafunga kirahisi. Sasa katika kikosi cha Simba amebaki Ngassa pekee mwenye uwezo wa kufanya hivyo.


MCHEZAJI KIONGOZI
Sifa ya uongozi wa mchezaji kwa wenzie huonekana pale ambapo mchezaji husika analazimika kukumbana na matatizo. Sifa ya mchezaji bora ya uongozi itajionyesha kwenye nyakati kama hizi na ukomavu wao na uwezo wa kubakia na lengo la kutaka kufanikiwa pamoja na matatizo na vikwazo vilivyoko mbele ni vitu vinavyomuonyesha mchezaji kuwa bora.

Siku zote Juma Kaseja amekuwa kiongozi mzuri kwa wenzake kiasi cha kuhamasisha ushindi na kweli hata kama Simba inaonekana ipo nyuma, kipa huyo na nahodha wa Simba atajitahidi kuzungumza na wachezaji wenzake na kusawazisha bao.

Katika mchezo dhidi ya Libolo, ilionekana wazi Simba haikuwa na kiongozi sahihi uwanjani, muda mwingi Kaseja ni kama mtu anayejuta jambo fulani na asiweze tena kuwapigia kelele mabeki wake pindi wakicheza vibaya.


TUJIULIZE MASWALI HAYA KWA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOCHEZA NA LIBOLO;
Je, wachezaji wa Simba walibaki na hali zao za kawaida za kisaikolojia pale walipopambana na vikwazo?

Walitumia mbinu zipi kupambana?

Je, walitumia mbinu chafu kuwaondoa wapinzani wao mchezoni?

Je, walikuwa kwenye hali gani pale walipoonekana kukaribia kupoteza mchezo?

Je, walibakia na lengo moja akilini? waliendelea kupambana au walikata tamaa?

USIKOSE MUENDELEZO WA MAKALA HII…

REVEALED:KIKULACHO KINGUONI MWAKO, KINACHOITAFUNA SIMBA HIKI HAPA-PART 1


Mwenyekiti wa FRIENDS OF SIMBA, Zacharia Hanspope





SIKU KADHAA ZILIZOPITA ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA SC, MSERBIA MILOVAN CIRKOVIC ALIFANYA MAZUNGUMZO YA KINA JUU YA MAMBO YALIYOMUONDOA KWENYE AJIRA YAKE YA KUIKOCHI KLABU BINGWA YA TANZANIA BARA.

 MILOVAN ALIYEKUJA NCHINI KUJA KUDAI FEDHA ALIZOKUWA AKIWADAI SIMBA ALIKUWA NA HAYA KUSEMA NA KITOA SABABU KADHAA ANAZODHANI ZIMEMUONDOA SIMBA NA CHANZO CHA TIMU HIYO KUTOKUFANYA VIZURI..

1: FRIENDS OF SIMBA NA KUINGILIA UPANGAJI WA TIMU
Friends of Simba ni kundi la mashabiki wa Simba ambao kwa miaka mingi sasa wamekuwa wakiisaidia timu hii kwenye masuala mbalimbali ya kifedha. Wamekuwa wakisajili wachezaji na kulipa mishahara ya baadhi ya wachezaji. Lakini Kocha Milovan Cirkovic anasema kundi hili ndio mja ya sababu ya yeye kuondolewa Simba.

Anasema Milovan"NAJUA KUWA KUNA WATU KWENYE KLABU HAWANIPENDI, NAJUA KWANINI HAWANIPENDI, NI KWA SABABU MIMI HUWA SIKUBALIANI NA YALE AMBAYO WANANIPANGIA KAMA WACHEZAJI WA KUCHEZA KWENYE MECHI, HUWEZI KUNIAMBIA MCHEZAJI WA KUMPANGA HALAFU BAADA YA MECHI UKAJA KUNIULIZA KWANINI HUKUMPANGA FULANI, HAWA JAMAA WANAJUA KULIKO KOCHA??

"NAKUMBUKA KABLA YA GAME YA PRISONS YA MZUNGUKO WA KWANZA, WALIKUJA ARUSHA NA ZANZIBAR, HAWA JAMAA WA FRIENDS OF SIMBA NI WATU HATARI SANA, WALINIULIZA KWANINI USIMCHEZESHE FULANI, KWANINI UMEMCHEZESHA OKWI AU NGASSA KWANINI USINGEMCHEZESHA MESSI , NIKAMUULIZA HUYU JAMAA, HIVI UNAJUA KUWA MIMI NAMPENDA MESSI NA KUMKUBALI KULIKO NYINYI?? HIVI NI NANI ALIYEMPA MESSI NAFASI YA KUCHEZA KIKOSI CHA KWANZA?? SI MIMI ? ANAELEZEA MILOVAN CIRKOVIC

'UNAKUMBUKA NILIMPANGA MESSI KWENYE MECHI NA AZAM AKACHEZA VIZURI , NAMWAMINI, NIKAENDA NAE RWANDA, KWA KUWA NAMWAMINI, NAJUA KUWA KIYOVU SIO TIMU YA NGUVU KAMA AZAM , NA TUKAWAFUNGA, KWANINI , KWA KUWA NAMWAMINI , NAJUA NINACHOFANYA , .KABURU AKAJA KUNIULIZA KWANINI UMEMPANGA MESSI , NIKAMUULIZA KWANINI , AKAJIBU KUWA BADO NI MDOGO, NIKAMUULIZA MBONA ALIPOCHEZA NA AZAM BADO ALIKUWA MDOGO PIA ALICHEZA VIZURI MBELE YA WATU ELFU SITINI, WANASEMA SI BORA UMCHEZESHE UHURU, NA NIKIMCHEZESHA UHURU WANASEMA KWANINI USIMPANGE MESSI NA NDIO HIVYO HIVYO.




"NIKAMWAMBIA KUWA HATUIFANYI HIVYO, NADHANI HUYU KABURU NDIO MWENYE SHIDA , NIKAMWAMBIA KUWA UNAJUA KUWA MESSI HAJAFANYA MAZOEZI NA SISI KWA MWEZI MMOJA NA NUSU, ALIKUWA KWENYE TIMU YA TAIFA , SASA HUYU KABURU HAJUI KUWA MESSI ANA TATIZO GANI , ANATAKA TUMPANGE TU BILA KUJUA CHOCHOTE, NA ALIPOENDA NATIONAL TEAM HAKUCHEZA VIZURI KAMA ILIVYOKUWA KABLA, LAKINI KWA KUWA YEYE NI FRIENDS OF SIMBA NA WAO WANATOA HELA HIVYO WANADHANI KUWA WANAWEZA KUAMUA CHOCHOTE , MIMI NDIO KOCHA HII NI KAZI YANGU , NATAKA MATOKEO BORA KULIKO MTU YOYOTE , NA MPAKA SASA SIJUI NANI ALINIBADILISHA NA KUMLETA KOCHA MPYA."



TO BE CONTINUED











SERIKALI YAIPIGA CHINI KATIBA YA TFF YA MWAKA 2012,YAAGIZA UCHAGUZI UFANYIKE KWA KATIBA YA MWAKA 2006

HOSPITALI YA BILLIONI 50 YA KANU YAZINDULIWA - KUTOA HUDUMA BURE KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 12

Nahodha wa zamani wa Super Eagles, Kanu Nwankwo, ataizindua hospitali ya kutibu magonjwa wa moyo yenye thamani ya Naira billioni 5, tarehe 14 mwezi March 2012, huko mjini Abuja Nigeria.

Hospitali, kwa majibu wa ripoti itatoa huduma ya magonjwa yanayohusiana na moyo kwa watoto. 

Pia kumekuwepo na ripoti kwamba Raisi wa nchi hiyo, Goodluck Jonathan atawaongoza watu wengine wakubwa kwenye jamii kuizindua hospitali hiyo ya Kanu. 

Inasemekana kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Ajax na Arsenal atatoa ofa ya kutibiwa bure kwa watoto kuanzia umri wa miaka 0 mpaka 12 wenye matatizo ya moyo.
 
Kanu alipatwa na matatizo ya moyo wakati akitokea Inter Milan kujiunga na Arsenal miaka kadhaa iliyopita. Alianzisha Kanu Heart Foundation ambayo imesaidia kutibiwa watoto wengi wenye matatizo ya moyo nje ya nchi ya Nigeria. 

WAZIRI WA MICHEZO MGENI RASMI KILIMANJARO MARATHONI


WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara anatarajiwa kufungua mbio za 11 za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Jumapili hii mjini Moshi.
 

Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions ambao ndiyo waratibu wa mbio hizo, Aggrey Marealle alithibitisha uwepo wa Waziri Mukangara siku hiyo na kueleza kuwa ndiye atazifungua mbio hizo sambamba na kutoa zawadi kwa washindi.                                              
 

Tayari washiriki zaidi ya 6,000 kutoka nchi zaidi ya 40 wamethibitisha kushiriki kwenye mbio hizo zitakazofanyika katika makundi ya mbio ndefu za marathon (km 42), nusu marathoni (km21) na mbio za km 5 za kujifurahisha.
 

"Waziri Mukangara atashiriki pia katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi 10 bora wa mbio za km 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon) kwa wanaume na wanawake,"alisema Marealle.
 

Kwa mujibu wa Marealle, mbali na Waziri Mukangara, viongozi mbalimbali wa Serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama watashiriki kwenye mbio hizo.
 

"Mbio za Kilimanjaro Marathon zinaiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa kila mwaka, pia zinatoa fursa kwa wanariadha wa ndani kukua zaidi, kukuza utalii wa Tanzania na watu kupata nafasi ya kujenga afya zao," alisema Marealle.

Marealle alibainisha kuwa mbio hizo zitakuwa na hadhi ya kimataifa ambapo zitasimamiwa na klabu ya Kilimanjaro Marathon, Chama cha Riadha Tanzania (AT) na kile cha Mkoa wa Kilimanjaro.
 

"Ilikuhakikisha usalama wa wakimbiaji, baadhi ya barabara za ndani na nje ya mji wa Moshi zitafungwa kuanzia saa 12:15 asubuhi hadi 03:30 asubuhi siku hiyo kwa lengo la kuwapa fursa wakimbiaji kupita salama,"alisema Marealle.

Mbio hizo zinadhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chao cha Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania (iliyodhamini mbio za Km 5 Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon kwa Walemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Tanzanite One, New Arusha Hotel, UNFPA, Fastjet na Kilimanjaro Water.

KOCHA WA YANGA AGOMA KUMLAUMU JERRY TEGETE KWA KUKOSA MABAO DHIDI YA AZAM FC

KOCHA wa Yanga, Ernest Brandts amemkingia kifua mshambuliaji wake Jerryson Tegete baada ya mashabiki wa klabu hiyo kumshutumu kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga wakati wa mchezo dhidi ya Azam FC.
 

Yanga iliifunga Azam bao 1-0 katika pambano la mzunguko wa pili wa Ligi Kuu lililopigwa mwishoni mwa wiki kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 

Katika mchezo huo, Tegete alijikuta akipigiwa kelele na mashabiki wa klabu yake huku baadhi yao wakitaka atolewe kwa madai alikuwa akipoteza nafasi za wazi za kufunga.
 

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Brandts alisema kuwa, hawezi kumlaumu Tetege kwa kushindwa kupachika bao kwenye mchezo huo kwa vile kilichotokea ni bahati mbaya ambayo inaweza kumkuta mchezaji nyota yeyote.
 

"Siwezi kumlaumu Tegete kwa kushindwa kupachika mabao kwa sababu wakati mwingine ni mambo ya bahati mbaya ambayo yanaweza kumkuta mchezaji nyota yeyote,"alisema Brandts.
 

Alisema,"Tegete huyu huyu ndiye aliyefunga mabao mawili katika mchezo uliopita na amekuwa anaonyesha juhudi kubwa mazoezini, mimi nasema mambo ya bahati mbaya tu kukosa mabao."
 

Katika hatua nyingine, Brandts alisema kuwa ushindi alioupata dhidi ya Azam unamaanisha
kwamba ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu upo
karibu yao.
 

"Ushindi huu dhidi ya Azam una maana kwamba ubingwa upo karibu yetu, tunachotakiwa kufanya sasa ni kuhakikisha tunaifunga Kagera Sugar katika mchezo ujao ili tuwe katika mazingira mazuri zaidi ya kutimiza kile tunachokifikiria,"alisema Brandts.
 

Katika hatua nyingine baadhi ya mashabiki waliofika kwenye uwanja huo, walimtaka mshambuliaji wa timu ya Yanga, Jerryson Tegete kuwa makini uwanjani kama anataka kupata namba ya uhakika katika kikosi hicho kutokana na kukosa mabao ya wazi kwenye mchezo dhidi ya Azam.
 

Walisema Tegete alikosa umakini kwenye mchezo huo jambo lililofanya aikoseshe timu yake mabao ya wazi. “Yaani huyu Tegete ni haki yake kutoitwa Stars, ona sasa anavyotukosesha mabao ya wazi kabisa hayuko makini kabisa huyu,”alisema Yusuph Salum shabiki wa Yanga.

MDAU WA SOKA NCHINI MOHAMMED BAWAZIR MWENYEKITI MPYA CCM KATA YA JANGWANI


1.MWENYEKITI mpya wa CCM Kata ya Jangwani Mohamed Bawazir, akipeana mkono na aliyekuwa mpinzani wake Abubakar Mzuka katika uchaguzi wa kuwania uenyekiti wa kata hiyo uliofanyika wiki iliyopita katika Ukumbi wa CCM, Ilala, Dar es Salaam.

2.MWENYEKITI Mpya wa CCM Kata ya Jangwani, Mohamed Bawazir, akizungumza na wanachama wa kata ya Jangwani mara baada ya kushinda nafasi hiyo.
3.Bawazir akipongezwa na Diwani wa Kata ya Jangwani Abuu Jumaa mara baada ya kutangazwa mshindi.

FIFA KUCHUNGUZA KWA KINA MCHAKATO WA UCHAGUZI TFF


OFISA Maendeleo wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Kusini mwa Afrika, Ashford Mamelodi amewahakikishia Watanzania kuwa ujumbe wa Shirikisho hilo utakaokuja nchini mwezi ujao, utafanya uchunguzi wa kina kuhusu mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA) na kutoa uamuzi kwa maslahi ya mchezo huo.

“Ninafurahi kwamba hali ya utulivu imefikia kiwango hiki na nina uhakika FIFA itafanya uchunguzi wa kina na kufanya uamuzi kwa maslahi ya mpira wa miguu,” amesema Mamelodi alipokuwa akizungumzia uchaguzi mkuu wa TFF ambao ulikuwa ufanyike Februari 24 mwaka huu lakini ukasimamishwa kutokana na matatizo kadhaa baada ya baadhi ya wagombea kuenguliwa.

Mbali na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa TFF na uchaguzi, safari ya Mamelodi nchini pia ilihusisha kumtambulisha msaidizi wake, Patrick Onyango ambaye amejiunga na ofisi hiyo ya FIFA kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, kufuatilia miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na GOAL Project 4 ambayo ni uwekaji wa nyasi bandia kwenye Uwanja wa Nyamagana na maendeleo ya Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba, mikakati ya mwaka 2013 na kozi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa TFF jana, Mamelodi alisema uamuzi wa Shirikisho hilo kutuma wajumbe katikati ya mwezi ujao unatokana na mawasiliano baina ya Rais wa TFF, Leodegar Tenga na FIFA ambayo ilitaarifiwa hali halisi ilivyo na kama inaweza kusaidia kutatua matatizo yaliyopo.

“FIFA haitakuja kuingilia mchakato wa uchaguzi, itakuja kutatua matatizo,” amesema Mamelodi. “Masuala ya uchaguzi ni ya ndani ya nchi. FIFA haiji kuichagulia Tanzania rais. Wajumbe wanaweza kumchagua mtu yeyote wanayeona kuwa anafaa kuwa rais,” amesema Mamelodi.

“Lakini katiba ya FIFA iko wazi kwamba mwanachama wake ni lazima akubaliane na sheria za Shirikisho kuwa wanachama ni lazima wabanwe na Katiba ya FIFA. Kwa hiyo mara tu unapopata uanachama wa FIFA, ni lazima ujue kuwa utabanwa na katiba ya FIFA na mojawapo ya mambo haya.

“Lakini kuna tofauti na kitendo cha Serikali kusimamisha uchaguzi kwa kuwa hiyo inakuwa ni Serikali kuingilia moja kwa moja masuala ya mpira wa miguu, kitu ambacho katiba ya FIFA inakataza.”

Mamelodi, ambaye alitumia muda mwingi kuelezea umuhimu wa hali ya utulivu iliyotawala kwa muda mrefu nchini, amesema anajua kuwa uongozi wa Rais wa sasa wa TFF, Leodegar Tenga umefanya mengi katika kuhakikisha unajenga mazingira mazuri ya maendeleo ya mpira wa miguu, lakini kuna wakati ni lazima uheshimu uamuzi wa mtu.

“Tenga amesema imetosha anaondoka na hatuna budi kuheshimu uamuzi wake. Hiyo ni kauli inayotoka kwa kiongozi wa kweli, kiongozi anayewajibika. Lakini kwa kuangalia misingi ambayo uongozi wake umeijenga, ni wazi kuwa kiongozi mpya ataendeleza taasisi bila ya matatizo.

“Tanzania haikufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, lakini kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo ilifanyika, mingine ambayo ilijaribiwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na ikafanikiwa. Kuna Azimio la Bagamoyo, Semina ya Mawasiliano ya Jamii (Comm-Unity) ya Wanawake, Futuro III na mingine. Yote hii ilifanyika kwa sababu kulikuwa na utulivu.

“Hivi sasa TFF ina sekretarieti ina Mkurugenzi wa Ufundi; ina programu za maendeleo na kuna utulivu. Cha msingi ni kuendeleza haya. Kama mambo haya yataendelezwa baada ya uchaguzi, ni dhahiri kuwa mpira utazidi kuendelea. Hakuna njia ya mkato katika maendeleo.”

Uchaguzi wa TFF ulihusisha nafasi za rais, makamu wa rais na wajumbe wa Kamati ya Utendaji kutoka Kanda 13 za Shirikisho.

Sunday, February 24, 2013

RYAN GIGGS NA REKODI YA KIPEKEE KWENYE SOKA: WAKATI ANAANZA KUICHEZEA MAN UNITED WACHEZAJI WA KIKOSI CHA SASA WALIKUWA NA UMRI GANI?


Siku ya jana Ryan Giggs alitimiza mechi ya 999 kukichezea kikosi cha wakubwa cha Manchester United. Katika kikosi cha sasa cha United, Giggs ndio mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi. Wakati alipoanza kuichezea Man United kwenye mechi dhidi ya Everton ambayo kikosi cha Fergie kilifungwa 2-0 mwezi March 2, 1991. Wakati huo wachezaji wote wa kikosi cha sasa United walikuwa na umri huu.


Paul Scholes, 16 years, four months                           
Rio Ferdinand, 12 years, four months                        
Michael Carrick, nine years, eight months                  
Nemanja Vidic, nine years, five months                       
Patrice Evra, nine years, two months                          
Robin van Persie, seven years, seven months         
Darren Fletcher, seven years, one month                  
Anders Lindegaard, six years, 11 months                 
Ashley Young, five years, eight months                      
Antonio Valencia, five years, seven months               
Wayne Rooney, five years, five months                        
Nani, four years, four months                                       
Jonny Evans, four years two months

Anderson, two years, 11 months
Javier Hernandez, two years, eight months

Alexander Buttner, two years, one month
 Shinji Kagawa, one year, 11 months
Tom Cleverley, one year, seven months
Chris Smalling, one year, four months
 Ben Amos, 11 months
Rafael, nine months
David de Gea, three months
Danny Welbeck, three months
Phil Jones, not born (D.O.B 21 Feb 1992)
Nick Powell, not born (D.O.B 23 Mar 1994)

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 0 -1 MTIBWA SUGAR FULL TIME

Dk 90+5 FULL TIME! SIMBA 0-1 MTIBWA.

Dk 85 RED CARD....! Juma Nyosso wa Simba anaonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vincent Barnabas wa Mtibwa. Simba 0-1 Mtibwa.

Dk 84 Mtibwa imefanya mabadiliko, ametoka Hussein Javu ameingia Juma Liuzio

Dk 82 Sunzu anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kuingilia mpira wa Mtibwa uliokuwa unaanza.

Dk 69 Said Mkopi wa Mtibwa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Mrisho Ngassa wa Simba.

Dk 65 Simba imecharuka inalishambulia zaidi lango la Mtibwa. Simba 0-1 Mtibwa.

Dk 58 Simba imefanya mabadiliko, ametoka Chanongo ameingia Mrisho Ngassa.

Dk 58 Simba imefanya mabadiliko, ametoka Chanongo ameingia Mrisho Ngassa.

Dk 51 Nditi anaonyeshwa kadi ya njano baada kumlalamikia mwamuzi kupita kiasi baada ya kugongana na Chollo.

Dk 51 Beki wa kulia wa Simba, Nassor Masoud 'Chollo' anaumia mkono baada ya kugongana na Shaaban Nditi wa Mtibwa. Mpira unasimama kwa muda. Simba 0-1 Mtibwa.

Dk 50 Simba imefanya mabadiliko, ametoka Haruna Moshi 'Boban' ameingia Amri Kiemba.

Dk 49 Mtibwa inafanya mabadiliko, ametoka Mnyate, ameingia Ally Mohamed.

Dk 48 Chanongo wa Simba anaichambua ngome ya Mtibwa na kupiga shuti kali nje ya lango la Mtibwa.

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!

Dk 45 HALF TIME! SIMBA 0-1 MTIBWA.

Dk 45 Jamal Mnyate wa Mtibwa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kulumbana na mwamuzi kuhusu faulo aliyochezewa Kiggi.

Dk 45 Kiggi Makassy wa Simba anaangushwa nje kidogo ya eneo la hatari la Mtibwa. Faulo inapigwa na mpira unatoka nje.

Dk 41 Simba imefanya mabadiliko, ametoka Ramadhan Chombo ameingia Kiggi Makassy. Chombo anatoka moja kwa moja kwenda vyumba vya kubadilishia nguo bila ya kwenda benchi.

Dk 40 Kipa wa Mtibwa, Hussein Sharrif 'Cassilas' anaumia baada ya kugongwa na Haruna Chanongo wa Simba.

Dk 28 Sunzu anashindwa kuunganisha kwa kichwa krosi ya Haruna Chanongo. Mpira anaopiga unatoka nje. Simba 0-1 Mtibwa

Dk 23 Mshambuliaji wa Mtibwa, Hussein Javu anapiga shuti kali langoni kwa Simba baada ya kuwazidi mbio mabeki Juma Nyosso na Komanbil Keita.

Dk 18 Kipa wa Simba, Juma Kaseja anaumia baada ya kugongana na Jamal Mnyate wa Mtibwa.

Dk 17 GOOO....! Salvatory Ntebe anaipatia Mtibwa bao la kwanza akimalizia pasi ya Vincent Barnabas. Simba 0-1 Mtibwa.

Dk 13 Kiungo wa Mtibwa, Rashid Gumbo anakumbana na mchezaji wa Simba na kuumia. Anatibiwa na mpira unaendelea.

Dk 10 Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu anaonekana hayupo katika kiwango chake kwani anaonekana hana kasi pia anapoteza pasi nyingi anazopewa.

Dk 7 Mpira umepooza sana, timu bado zinasomana.

Dk 2 Beki Shomari Kapombe wa Simba anapiga shuti kali linalotoka juu ya lango la Mtibwa baada ya kupokea pasi ya Amir Maftah. Simba 0-0 Mtibwa.

Dk 00 MPIRA UMEANZA!

Simba Line Up: Juma Kaseja, Nassoro Masoud 'Chollo', Amir Maftah, Juma Nyosso, Komanbil Keita, Shomari Kapombe, Ramadhan Chombo, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi 'Boban', Haruna Chanongo

Mtibwa Line Up: Hussein Sharrif 'Cassilas', Said Mkopi, Issa Rashid, Salvatory Ntebe, Salum Sued, Shaaban Nditi (C), Jamal Mnyate, Rashid Gumbo, Hussein Javu, Shaaban Kisiga, Vincent Barnabas.

Saturday, February 23, 2013

YANGA WALIVYOKATA NGEBE ZA AZAM FC LEO JIONI

 Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, akijilaumu baada ya kukosa bao la wazi.
 Mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete (kuli) akijaribu kumchambua kipa wa Azam Fc, Mwadin Ally, wakati wa mchezo huo, ambapo Tegete alikosa baada ya kipa huyo kuudaka mpira huo.
 WATANI WA JADI BWANA!!!!, Mashabiki wa Yanga, wakiwakebehi watani wao Mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia Azam Fc, kwa Bango lenye Ujumbe huu. ''Msomaji soma mwenyewe''.
 Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichoanza.
 Sehemu ya mashabiki wa Yanga, waliojitokeza kuishangilia timu yao leo, ambao wanakadiliwa kuwa kama 25,0000 hivi.
Kikosi cha Azam Fc kilichoanza. 
 
 Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akimkabili mshambuliaji wa Azam, Kipre Tchetche, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara
 
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Niyonzima baada ya kutupia bao.(PICHA KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO)

HIVI NDIVYO CLOUDS THE DREAM TEAM ILIVYOPOKEA KIPIGO CHA 4-1















LIVE MATCH CENTRE: AZAM FC 0 - 1 YANGA FULL TIME

Dk 90+5 FULL TIME! YANGA 1-0 AZAM.

Dk 90+4 Kavumbagu anaangushwa ndani ya eneo la hatari lakini mwamuzi anapeta. Kavumbagu na Mwantika wanaumia baada ya tukio hilo.

Dk 87 Cannavaro wa Yanga anaonyeshwa kadi ya njano.

Dk 87 Azam imefanya mabadiliko, ametoka Bolou ameingia Jabir Azizi. Yanga 1-0 Azam.

Dk 86, Seif Abdallah wa Azam anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Niyonzima.

Dk 85 Beki wa Yanga, Kelvin Yondan anaumia na kutibiwa kwa muda baada ya kuchezewa vibaya na viungo wa Azam.

Dk 82 Yanga inafanya mabadiliko, ametoka Kiiza ameingia Said Bahanunzi. Yanga 1-0 Azam.

Dk 80 Mustapha anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kutibiwa. Anaonekana alikuwa anapoteza muda.

Dk 77 Kipa wa Yanga, Ali Mustapha anaumia baada ya kukanyagwa na Seif Abdallah. Mpira umesimama na Mustapha anatibiwa. Yanga 1-0 Azam.

Dk 72 Azam imefanya mabadiliko, ametoka Mcha ameingia Seif Abdallah.

Dk 71 Tchetche anakosa bao la wazi kwa shuti lake kupanguliwa na kipa wa Yanga.

Dk 65 Kavumbagu anakosa bao baada ya kugongana na kipa wa Azam.

Dk 64 Yanga inafanya mabadiliko anatoka Tegete anaingia Didier Kavumbagu.

Dk 62 Tcheche anapiga shuti kali langoni kwa Yanga lakini mpira unagonga mwamba wa juu na kutoka nje.

Dk 57 Tegete anafunga bao lakini mwamuzi anakataa na kusema mfungaji aliotea.

Dk 55 Azam wamebadilika na sasa wanacheza soka la kasi na kufika langoni kwa Yanga mara kadhaa.

Dk 50 Mcha wa Azam anaichambua ngome ya Yanga lakini anapiga shuti linalopaa juu ya lango.

Dk 45 Azam imefanya mabadiliko, ametoka Ibrahim Mwaipopo ameingia Himid Mao. Yanga 1-0 Azam.

Dk 45 HALF TIME! YANGA 1-0 AZAM.

Dk 44 Tegete anakosa tena bao la wazi akiwa amebaki na kipa wa Azam. Alikuwa amepewa pasi safi na Hamis Kiiza. Yanga 1-0 Azam.

Dk 41 Tegete anakosa bao la wazi baada ya mpira wa kichwa alioupiga kutoka nje ya lango.

Dk 33 Bocco anaifungia Azam, lakini mwamuzi anakataa bao kwa kuwa kipa wa Yanga Ali Mustapha alichezewa faulo. Bocco analalamikia hali hiyo na mwamuzi anamuonyesha kadi ya njano. Yanga 1-0 Azam.

Dk 31 GOOO....! Niyonzima anaipatia Yanga bao la kwanza kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya Tegete. Yanga 1-0 Azam.

Dk 26 Beki wa Azam, David Mwantika anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Tegete. Yanga 0-0 Azam.

Dk 24 Beki ya Azam inaonekana haijatulia na inajichanganya katika kuokoa.

Dk 20 Atudo wa Azam anaushika mpira na kuutoa nje, mwamuzi Hashim Abdallah anapeta kwa kuwa hajaona.

Dk 19 Timu zinashambuliana kwa zamu.

Dk 16 Jerry Tegete wa Yanga anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa wa Azam, Mwadini. Anapiga mpira hafifu unaodakwa. Yanga 0-0 Azam.

Dk 12 Beki Jockins Atudo wa Azam anamchezea vibaya Haruna Niyonzima wa Yanga nje kidogo ya eneo la hatari la Azam. Faulo isiyo na madhara inapigwa.

Dk 9 Kipre Tchetche wa Azam anapiga shuti kali langoni kwa Yanga lakini mpira unatoka nje kidogo ya lango.

Dk 4 Hamis Kiiza wa Yanga anakosa bao la wazi baada ya shuti lake kudakwa na kipa wa Azam, Mwadin Ali. Awali mabeki wa Azam walijichanganya katika kuokoa.

Mpira umeanza hapa uwanja wa taifa timu zote zikicheza soka la kasi sana.


KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA AZAM
1.Ally Mustafa 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Athumani Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Jerson Tegete
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Said Mohamed
2.Juma Abdul
3.David Luhende
4.Nurdin Bakari
5.Nizar Khalfani
6.Didier Kavumbagu
7.Said Bahanuzi


KIKOSI CHA AZAM FC

1: Mwadini Ally, Balou Kipre, Kipre Tchetche, Waziri Salum, Jockins Atudo, David Mwantika, Ibrahim Mwaipopo, Salaum Aboubakar, John Bocco, Humphrey Mieno, Mcha Khamis