Search This Blog

Monday, February 25, 2013

REVEALED:KIKULACHO KINGUONI MWAKO, KINACHOITAFUNA SIMBA HIKI HAPA-PART 1


Mwenyekiti wa FRIENDS OF SIMBA, Zacharia Hanspope





SIKU KADHAA ZILIZOPITA ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA SC, MSERBIA MILOVAN CIRKOVIC ALIFANYA MAZUNGUMZO YA KINA JUU YA MAMBO YALIYOMUONDOA KWENYE AJIRA YAKE YA KUIKOCHI KLABU BINGWA YA TANZANIA BARA.

 MILOVAN ALIYEKUJA NCHINI KUJA KUDAI FEDHA ALIZOKUWA AKIWADAI SIMBA ALIKUWA NA HAYA KUSEMA NA KITOA SABABU KADHAA ANAZODHANI ZIMEMUONDOA SIMBA NA CHANZO CHA TIMU HIYO KUTOKUFANYA VIZURI..

1: FRIENDS OF SIMBA NA KUINGILIA UPANGAJI WA TIMU
Friends of Simba ni kundi la mashabiki wa Simba ambao kwa miaka mingi sasa wamekuwa wakiisaidia timu hii kwenye masuala mbalimbali ya kifedha. Wamekuwa wakisajili wachezaji na kulipa mishahara ya baadhi ya wachezaji. Lakini Kocha Milovan Cirkovic anasema kundi hili ndio mja ya sababu ya yeye kuondolewa Simba.

Anasema Milovan"NAJUA KUWA KUNA WATU KWENYE KLABU HAWANIPENDI, NAJUA KWANINI HAWANIPENDI, NI KWA SABABU MIMI HUWA SIKUBALIANI NA YALE AMBAYO WANANIPANGIA KAMA WACHEZAJI WA KUCHEZA KWENYE MECHI, HUWEZI KUNIAMBIA MCHEZAJI WA KUMPANGA HALAFU BAADA YA MECHI UKAJA KUNIULIZA KWANINI HUKUMPANGA FULANI, HAWA JAMAA WANAJUA KULIKO KOCHA??

"NAKUMBUKA KABLA YA GAME YA PRISONS YA MZUNGUKO WA KWANZA, WALIKUJA ARUSHA NA ZANZIBAR, HAWA JAMAA WA FRIENDS OF SIMBA NI WATU HATARI SANA, WALINIULIZA KWANINI USIMCHEZESHE FULANI, KWANINI UMEMCHEZESHA OKWI AU NGASSA KWANINI USINGEMCHEZESHA MESSI , NIKAMUULIZA HUYU JAMAA, HIVI UNAJUA KUWA MIMI NAMPENDA MESSI NA KUMKUBALI KULIKO NYINYI?? HIVI NI NANI ALIYEMPA MESSI NAFASI YA KUCHEZA KIKOSI CHA KWANZA?? SI MIMI ? ANAELEZEA MILOVAN CIRKOVIC

'UNAKUMBUKA NILIMPANGA MESSI KWENYE MECHI NA AZAM AKACHEZA VIZURI , NAMWAMINI, NIKAENDA NAE RWANDA, KWA KUWA NAMWAMINI, NAJUA KUWA KIYOVU SIO TIMU YA NGUVU KAMA AZAM , NA TUKAWAFUNGA, KWANINI , KWA KUWA NAMWAMINI , NAJUA NINACHOFANYA , .KABURU AKAJA KUNIULIZA KWANINI UMEMPANGA MESSI , NIKAMUULIZA KWANINI , AKAJIBU KUWA BADO NI MDOGO, NIKAMUULIZA MBONA ALIPOCHEZA NA AZAM BADO ALIKUWA MDOGO PIA ALICHEZA VIZURI MBELE YA WATU ELFU SITINI, WANASEMA SI BORA UMCHEZESHE UHURU, NA NIKIMCHEZESHA UHURU WANASEMA KWANINI USIMPANGE MESSI NA NDIO HIVYO HIVYO.




"NIKAMWAMBIA KUWA HATUIFANYI HIVYO, NADHANI HUYU KABURU NDIO MWENYE SHIDA , NIKAMWAMBIA KUWA UNAJUA KUWA MESSI HAJAFANYA MAZOEZI NA SISI KWA MWEZI MMOJA NA NUSU, ALIKUWA KWENYE TIMU YA TAIFA , SASA HUYU KABURU HAJUI KUWA MESSI ANA TATIZO GANI , ANATAKA TUMPANGE TU BILA KUJUA CHOCHOTE, NA ALIPOENDA NATIONAL TEAM HAKUCHEZA VIZURI KAMA ILIVYOKUWA KABLA, LAKINI KWA KUWA YEYE NI FRIENDS OF SIMBA NA WAO WANATOA HELA HIVYO WANADHANI KUWA WANAWEZA KUAMUA CHOCHOTE , MIMI NDIO KOCHA HII NI KAZI YANGU , NATAKA MATOKEO BORA KULIKO MTU YOYOTE , NA MPAKA SASA SIJUI NANI ALINIBADILISHA NA KUMLETA KOCHA MPYA."



TO BE CONTINUED











14 comments:

  1. hamjui kwa kiasi gani mnaongeza vurugu klabuni kwetu,time will come Kaburu will leave our team.

    ReplyDelete
  2. not only kaburu pia hata haya makundi likiwemo friends of simba hawa jamaa wanaiona simba kama Mali yao na haiwez kufka mbali bila wao remember kaburu alimsajili mungusa kwa ahadi kibao akashndwa kumtimizia mungusa alipoulizia haki yake akaishiwa kupigwa bench

    ReplyDelete
    Replies
    1. hakika friends of simba ndio wanatufikisha hapa tulipo na wakiendelea kupewa nafasi simba haitafanya la maana hata ujenzi wa kiwanja cha club wanapiga vita sana ni watu wanaopenda kuabudiwa nawaomba watuachie simba yetu tumechokanao hata mzungu kagundua tatizo la simba ni hao jamaa

      Delete
  3. JAMANI FRIENDS OF SIMBA WANAJULIKANA MIAKA NENDA MIAKA RUDI KUWA NDIYO WANAVURUGA TIMU YA SIMBA.KABURU AKIWA MSTARI WA MBELE KUVURUGA WACHEZAJI,MAKOCHA NA KUJIPATIA PESA ISIVYO HALALI KWA KULALIA WACHEZAJI.MFANO MCHEZAJI ANATAKA MIL 20 KUSAJILIWA,KUBURU HUMWAMBIA MCHEZAJI ATAJE MILIONI 30 THEN ILE 10 WAGAWANE YEYE NA MCHEZAJI NA KUMPA UHAKIKA WA KUMPANGA KWENYE MECHI KAMA VILE YEYE NDIYE KOCHA.MPIRA WA HIZI TIMU KUBWA TUKIWAONDOA HAWA MAMLUKI KAMA KABURU NA RAGE MPIRA UTAENDELEA VIZURI.TUNAOMBA KABURU,RAGE,HANS POPE NA WENGINE WENYE MASLAHI BINAFSI WAJITOE MAPEMA KABLA HATUJAWATOA KWA FIMBO KLABUNI.WACHEZAJI HAWAMTAKI KOCHA MPYA ALIYELETWA NA KINA KABURU,WANAMTAKA MILLOVAN ARUDISHWE AU BASENA(AMBAYE NAYE NI DUKA LA KUJIPATIA PESA KINA KABURU.SASA KAMA FRIENDS OF SIMBA WANAWEZA KUCHEZA NA KUBADILI MATOKEO YA MECHI ,WAOMBE JEZI ILI WAPEWE NAMBA ZA KUOKOA JAHAZI BILA HIVYO SIMBA HATUTASHIKA HATA NAFASI YA TATU MSIMU HUU.

    ReplyDelete
  4. Me nadhani kila mtu afanye kile kinachomuhusu na si kuingilia mamlaka ya mtu mwingine.
    Tupeane nafasi basi watanzania na tuwe serious katika kazi
    we ka umemsajili mchezaji hakikisha ulomwahidi yote unayatimiza ili mchezaji asipate kisingizio chochote
    Na kama mtu awajibiki katika nafasi ake hapo n haki ngazi husika kumwajibibisha mana mambo ya kuoneana aibu na kujuana ndio yanaleta soka la tanzania linakuwa bovu
    Kitu kingine ni kuheshimiana na kila kukicha majungu tu na kama mtu kafanya vizuri mpeni sifa zake,pia unayepewa sifa zisikuleweshe bali uzid kuvuta soksi


    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka hebu wacha jazba, soma mwanzo hadi mwisho wa stori ndio utaelewa! wewe si umeona hapo juu ameandika Part 1, au hujui maana ya part 1...........ina maana hiyo stori itaendelea, sasa wewe unajuaje kama hatoweka mahojiano yake na Friends of Simba???? was upumbavu wewe....nyie ndio mnaharibu simba, mnataka msikie mazuru tu............mabaya hamtaki kusikia, sasa kama ni hivyo watu watajirekebisha vp? wacha ujinga...........mpira haundeshwi kwa kujua positives tu.

      Shaffii, we weka tu kila kitu ili tujue mbivu na mbichi achana na hawa mapoyoyo wenye akili za makopo ya chooni! mi nakukubali ile mbaya hususan unapokosoa uongozi wa hizi timu zetu. We kunguru naomba usirudt tena hapa............kama wewe una uchungu na simba kuliko, jinyonge basi! mpuuzi mkubwa wewe!

      Delete
  5. KIUKWELI NIMEKUWA NIKIFUATILIA SANA BLOG YAKO KWA MUDA MREFU SANA NA NIKUPONGEZE KWA KUWA CHANZO MUHIMU SANA CHA TAARIFA ZA MICHEZO!! LAKINI KITU KIMOJA AMBACHO BLOG YAKO INAENDELEA KUSHUKA HADHI NI MAKALA ZAKO AMBAZO HAZIJENGI TIMU ZETU.

    UMEKUWA MKOSOAJI SANA WA MFUMO WA UENDESHAJI WA VILABU VYETU LAKINI WAKATI MWINGINE MAKALA UNAZOAINDIKA NI KAMA KUZIUA NA KUZIBOMOA BADALA YA KUZIJENGA. UMEFANYA MAHOJIANO NA CIRKOVIC LAKINI HUJA-BALANCE KABISA STORY UWATAFUTE BASI FRIENDS OF SIMBA UWAULIZE KWANINI TIMU YAO INAYUMBA.

    LEO UNAMFANYA CIRKOVIC KAMA SOURCE MUHIMU WA KUJUA MATATIZO YA SIMBA. UNACHOFANYA SI SAHIHI UNAHARIBU!! UKO BIAS SANA NA SIMBA!!! NAONA UNATUHARIBIA TU BADALA YA KUTUJENGA!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. me nafikir hjamuelewa shaffih vzuri na pia me nna wacwac na we inawezekana kabsa nawe ukawa ni mmojawapo friends of simba!nafikir cjui kama unamkumbuka m2 mmoja anitwa kaduguda ambaye aliwafukuza hawa friends of simba coz alishawah kutamka kuwa ndio maadui wa simba wakawa hawampendi wakawa wanampiga vita coz alikuwa muwazi juu yao.na hwa ndio wanaaribu timu.

      Delete
    2. Tatizo liko wapi, na wao friends of simba si watajibu, ila wao ndo wanaiua simba miaka yooote

      Delete
  6. hUYO JAMAA ALIESEMA UNAHARIBU , NINAWASIWASI NAE KUWA NAE NI MOJA KATI WA FRIEND OF SIMBA!! UKWELI SIKU ZOTEUKIAMBIA HUUMA SANA!! JIULIZE BASI KWA NINI KOCHA AYASEME YOTE HAYA?? NA JE WACHEZAJI NI NANI ANAPENDA KUNYANYASWA KTK HAKI ZAKE NA JE ANGEKUWA YEYE NI KWELI ANGAKUBALI KUNYIMWA HAKI YAKE ?? KAMA NI MIONGONI AKAEE KIMYA NA ASICHANGIE MAANA HANA HOJA YA MSINGI NA YA KUSAIDIA CLUB YETU YA SIMBA! UKWELI NI HUU, SIMBA HATUNA VIONGOZI WAWAZI BALI TUNAWATAFUNA FEDHA NA JASHO LA WACHEZAJI TUU! M/K NA K/B WOTE HAWA NDIO CHANZO CHA TIMU KUTOFANYA VIZURI, HAWA WATU MIMI NINGEKUWA NA UWEZO NINGEWAFUKUZA KABISA NA KUWAFUNGIA KUJIHUSISHA NA MPIRA TZ! LABDA WAENDE YANGA , MAANA YANGA NI WAWAZI NA UKWELI TU! ASIPOTOKA RAGE NA KABURU SIMBA BADO TATIZO LA MILELE NA MILELE TU!

    ReplyDelete
  7. ukiacha hela ya chakula nyumbani, huitaji kupongezwa sababu ni wajibu wako kama baba, mi nampongeza sana kifukwe kwa kuwafutilia mbali marafiki wa yanga naona migogoro ingezidi pale, lakini sasa migogoro inayokuwepo inakuwa ni ya uongozi na wanachama bila kuhusisha kundifulani la nje, huu utaratibu wa kusajili na kulipa mshahra mchezaji kivyako haukubaliki na ndo unaua timu,na ndio maana mpaka sasa hatuwezi ona hela za kina okwi na wenzake waliouzwa sababu walikuwa wana mikataba na watu na sio klabu. Milovani ni proper source usibabaike komaa na kazi nzuri hizi, hao friends of simba ni kina nani katika katiba ya simba?

    ReplyDelete
  8. Ueledi wa Milovan,msimamo wake na ukweli wake + siasa za chuki za viongozi wa simba,na uongozi mbaya= simba ya sasa,ambayo ni simba mbovu labda ktk kipindi cha miaka kumi sasa haijawahi tokea hivi.

    ReplyDelete
  9. MATHIAS DANIEL26/2/2013

    mie nadhan kuna umhim mkubwa ma kuendelea na kocha Milovan pia viongozi waache habari za kutuambia ooh sijui Nyoso kashuka kiwango kama uongozi ulimshusha akapandishe kiwango hivi kiwango cha Ocheng na Nyoso ni nani alistahir kushuswa, tusikate tamaa bado tuna nafasi ya kuwafunga Libolo kwao na kuutetea ubingwa wa VPL

    ReplyDelete
  10. Niko
    Nilikuwa na bendela ya Simba, nimeitoa. Kwa kwaeli simba inasikitisha sana. Sio Rage, Kaburu wote ni wezi tu. Ebu angalia, lile wazo la kujenga uwanja limeishia wapi? Klabu ya simba si timu ndogo mpaka tukose pa kufanyia mazoezi. Inaniuma sana, Kaburu na Rage wote ni wezi tu. Hivi zile hela zilizokwapuliwa kwenye mechi kesi imeishia wapi? Aliye na taarifa ni vibaya akatujuza.

    ReplyDelete