Search This Blog
Monday, February 25, 2013
MAKALA: SIFA ZA MCHEZAJI BORA NA SIMBA ILIVYOIKAMATWA LIBOLO PART II
LEO tunaendelea na sifa za mchezaji bora huku tukioanisha sifa hizo na mambo yalivyotokea katika mchezo kati ya Simba na Libolo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa hivi karibuni.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilifungwa ba 1-0, lililofungwa na Joao Martins.
Endelea na sifa za mchezaji bora tukirejea katika mchezo wa Simba dhidi ya Libolo;
NGUVU ZA KISAIKOLOJIA (Mental Toughness)
Kitu cha pili kwa umuhimu baada ya uwezo wa kimwili kwa mchezaji, ni upande wa saikolojia. Ni jinsi gani mchezaji ana nguvu kisaikolojia, siyo mwoga, ana ujasiri na uwezo wa kuhimili mapambano huku akibakia na lengo moja kichwani mwake nalo ni kusaka ushindi.
Katika mchezo wa Simba na Libolo, licha ya mashabiki wa Simba kuwa wengi huku wakiwazomea wale wa Libolo, bado wachezaji wa Libolo walisimama katika lengo lao na kuweza kupambana hadi kupata bao. Hata mashabiki walioaminika kuwa ni kutoka upande wa Yanga waliokuwa wakiishangilia Libolo hawakuwa wengi kulinganisha na wale wa Simba. Libolo waliiva kisaikolojia.
Kuna wakati mashabiki wa Simba waliweza kuwazomea wachezaji wa timu yao pindi wanapokosea na waliweza kuwachanganya zaidi. Hapo wachezaji wengi wa Libolo walikuwa na nguvu ya kisaikolojia kuliko wale wa Simba.
Nguvu za kisaikolojia kwa mchezaji zinasambaa katika wigo mpana wenye vipengele vingi. Moja ya vipengele hivi huonyesha kiwango cha mchezaji kwa wakati uliopo sasa lakini pia huonyesha jinsi mchezaji atakavyoweza au kushindwa kupiga hatua siku za mbeleni na zaidi ya hapo itaonyesha mchezaji husika ni mshindani wa aina gani.
Msingi wa mchezo wa soka ni mapambano ya mmoja dhidi ya mmoja. Na siku zote mchezaji bora unategemea ashinde pambano lolote dhidi ya mchezaji mwingine pale wanapokutana uwanjani.
KUJIAMINI KWA MCHEZAJI
Kisaikolojia kinachochangia ushindi ni hali ya kujiamini kwa mchezaji na si wachezaji wote wanajiamini kwenye mapambano ya mtu mmoja dhidi ya mwingine, baadhi ya wachezaji ni waoga wa hali kama hii, wanaogopa kufanya makosa na kwa sababu hiyo wanaogopa kujaribu.
Lakini mchezaji bora ni yule anayependa changamoto, anayetamani kuwa kwenye aina hii ya mapambano muda wote kwani kichwani mwake anahisi kuwa anapaswa kuwakumbusha kuwa yeye ni bora.
Simba ilikosa wachezaji wazoefu katika nafasi nyeti, wachezaji kama Shomari Kapombe na Haruna Chanongo bado ni chipukizi na wasioweza kucheza dakika zote 90 na timu iliyojiandaa vyema kama Libolo.
Unaweza kushangaa ametajwa Kapombe hapo wakati anaonekana kama mmoja wa wachezaji mahili kwa sasa katika kikosi cha Simba, hapana Kapombe anachezeshwa Simba kwa kuwa tu, hakuna mchezaji mwingine.
Katika mechi moja tu ya nyuma kabla ya kuivaa Libolo, Kapombe alicheza kama beki wa kati, ndani ya siku chache, anachezeshwa kama beki wa kushoto, unategemea nini kwa timu kama Libolo? Lazima atakuwa uchochoro, na hata krosi ya bao ya Libolo ilipitia upande wake. Kapombe ni mchezaji mzuri, lakini tatizo linakuja kuwa, amejiandaa vipi kucheza na timu kama Libolo?
MAPAMBANO YA WATU BORA
Washambuliaji bora siku zote wanapenda kukutana na mabeki bora kudhihirisha kuwa wao ni bora na vivyo hivyo kwa mabeki bora, siku zote wanapenda kukabiliana na washambuliaji bora ili wakumbukwe kama watu walioweza kuwanyamazisha na kuwaficha kabisa.
Kujiamini hakuishii kwa mapambano ya mtu mmoja mmoja, wachezaji bora huwafanya wenzao wajiamini, wanaambukiza wenzao ile hali ya kutokuwa waoga.
Kuna wakati wachezaji wa Libolo walikuwa wanauchezea mpira watakavyo baada ya kujiamini na kujiridhisha na kiwango cha wachezaji wengi wa Simba. Hao walipigiana pasi watakavyo na kushambulia kwa muda waliotaka.
Simba kupitia kwa Mrisho Ngassa na Chanongo walikuwa wakifika mara kadhaa katika lango la Libolo, lakini Haruna Moshi ‘Boban’ aliyecheza kama straika hakuwa katika hali ya kujiamin, matokeo yake alikuwa na papara ya kufunga na kujikuta akitumia muda mwingi kuwatoa mchezoni Libolo ambao walikuwa wameshiba kisaikolojia kuhusu mambo yote mabaya uwanjani.
Simba hawakuonyesha kupambana mmoja mmoja katika mchezo huo na mara nyingi walicheza kwa mfumo zaidi huku Libolo wakiwa wameshaudhibiti mfumo wa Simba, ambao ulikuwa 4-4-2.
KUTOKATA TAMAA MAPEMA
Lakini ni yale mapambano ya mtu mmoja mmoja ambayo yanamfanya mchezaji aonyeshe ishara za kutaka kuendelea kujifunza na hivyo kukomaa zaidi katika hali kama hizo za mapambano pamoja na hali ya kujitolea kwa ajili ya timu na kutokukubali kushindwa kwa hali yoyote ile.
Katika hili, kidogo Chanongo na Ngassa ndiyo walionekana kucheza kwa mapambano ya mtu mmoja mmoja uwanjani na kuifanya Simba kukaa na mpira kwa muda mrefu kidogo.
Ni ile ya hali kujitolea kwa imani na dhamira ya kutaka kuwa bora inayomfanya mchezaji awe juu ya wenzie. Kama unakumbuka, Emmanuel Okwi alikuwa na sifa kama hii ya kujituma uwanjani kwani alitumia vyema kipaji chake.
Okwi aliweza kuwalamba chenga mabeki kadhaa kabla ya kutoa pasi na mfungaji akafunga kirahisi. Sasa katika kikosi cha Simba amebaki Ngassa pekee mwenye uwezo wa kufanya hivyo.
MCHEZAJI KIONGOZI
Sifa ya uongozi wa mchezaji kwa wenzie huonekana pale ambapo mchezaji husika analazimika kukumbana na matatizo. Sifa ya mchezaji bora ya uongozi itajionyesha kwenye nyakati kama hizi na ukomavu wao na uwezo wa kubakia na lengo la kutaka kufanikiwa pamoja na matatizo na vikwazo vilivyoko mbele ni vitu vinavyomuonyesha mchezaji kuwa bora.
Siku zote Juma Kaseja amekuwa kiongozi mzuri kwa wenzake kiasi cha kuhamasisha ushindi na kweli hata kama Simba inaonekana ipo nyuma, kipa huyo na nahodha wa Simba atajitahidi kuzungumza na wachezaji wenzake na kusawazisha bao.
Katika mchezo dhidi ya Libolo, ilionekana wazi Simba haikuwa na kiongozi sahihi uwanjani, muda mwingi Kaseja ni kama mtu anayejuta jambo fulani na asiweze tena kuwapigia kelele mabeki wake pindi wakicheza vibaya.
TUJIULIZE MASWALI HAYA KWA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOCHEZA NA LIBOLO;
Je, wachezaji wa Simba walibaki na hali zao za kawaida za kisaikolojia pale walipopambana na vikwazo?
Walitumia mbinu zipi kupambana?
Je, walitumia mbinu chafu kuwaondoa wapinzani wao mchezoni?
Je, walikuwa kwenye hali gani pale walipoonekana kukaribia kupoteza mchezo?
Je, walibakia na lengo moja akilini? waliendelea kupambana au walikata tamaa?
USIKOSE MUENDELEZO WA MAKALA HII…
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
tatizo lililopo ni kuwa hakuna viongozi wa soka katika klabu zetu hawana misingi ya uongozi zaid i ya kuwa na ujanja ujanja wa kuongea na kuonekana kuwa wanajua. Na hili litatupa shida sana tanzania kusonga mbele. iweje kiongozi ambaye si kocha awe mstali wa mbele kupanga timu na si kocha!!!! hakina simba haitatulia mpaka friends of simba wajue wajibu wao katika timu.
ReplyDeleteNI MUENDELEZO WA KUHUJUMU SOKA LETU!! SIKU ZOTE KUBOMOA NI RAHISI KULIKO KUJENGA.
ReplyDeleteMAKALA YAKO UTAFIKIRI IMEANDIKWA NA MWANDISHI WA ANGOLA ILIKOTOKA LIBOLO!! UNAJUA KABISA SIMBA NA LIBOLO WATACHEZA MECHI YA MARUDIANO SIKU CHACHE ZIJAZO LAKINI WEWE BADALA YA KUTOA MAKALA ZENYE KUWAJENGA SIMBA UMEKUWA MTU WA KUWAKOSOA,
MAKALA YAKO KIUKWELI HAINA TAFAKULI YA KUTOSHA ZAIDI YA PROPAGANDA ZA SOKA LA SIMBA NA YANGA!!
CHANGE MY FRIEND!!
Tatizo si uyanga na simba, tatizo misingi mibovu ya soka letu.Tatizo hatutaki kuambiwa Ukweli.Soka ni kama taaluma nyingine ambazo zina miiko na taratibu zake za utendaji wa kila siku, soka siyo kuchezea mpira uwanjani tu na kushinda magoli basi ndio imeishia hapo. Leo tunashabikia sana timu za nje,mfano man u, chelsea au real madrid, kule kuna mipango thabiti katika uendeshaji wake, hakuna siasa au longolongo.Leo niulize katika klabu zetu viongozi wengi ni hawa wanaosemasema sana au wenye senti zao za kulipa kocha mshahara, lakini nani ana dira ya maendeleo ya klabu kwa miaka mingi ijayo??.
ReplyDeleteTunataka kujenga soka letu lakini tunajengaje? hapo ndio tatizo lililopo!Uongozi tatizo, wachezaji hawana njia sahihi ya kufika kwenye mafanikio! nani hasa atuongoze njia!!!
Mechi ya Simaba na Lobolo inakuja! leo kuna nn cha maana kwenye maandalizi ya kitaalamu yamefanyika!!mambo ya vikao yanasaidia nn!!! jamani jifunzeni toka kwa libolo walipofika hapa walifanya nn kuanzia kwenye mazoezi mpaka kwenye mechi.!!Mm naamini kabisa tuna wachezaji wazuri tu lakini hatuna mipango ya maana katika soka letu, limejaaa ujanja ujanja tu.
Simba amkeni ili tusonge mbele, kwani bila maandalizi ya maana, angola tutafungwa tu na hilo ni uhakika wa asilimia mia.
makala nzuri ila timing sio, tusubiri mechi ya marudiano kwanza,kweli ni mkubwa ambao ni lazima wajaribu kuupanda, inawezekana. wanae ngasa
ReplyDeleteShaffih try to be constructive....!
ReplyDeleteWe Kocha wenu si alishasema jamaa wana hela kuliko Simba? Sasa sababu nyingine za nini tena?
ReplyDeleteAzam pia wana hela kuliko Simba, kwa hiyo kaeni kimya kabisa!!
Mzozaji.
acheni unafiki simba kufungwa tu mechi hiyo imekuwa gumzo go and ask barcelona nou camp against madrid hivyo basi ninaamini simba atampiga tu libolo
ReplyDelete