Search This Blog

Thursday, September 22, 2011

MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI BARANI ULAYA


SPANISH LA LIGA

FT Atletico Madrid 4 - 0 Sporting Gijon
FT Malaga 1 - 0 Athletic Bilbao
FT Racing Santander 0 - 0 Real Madrid
FT Rayo Vallecano 1 - 2 Levante
22:00 Valencia 2 - 2 Barcelona

ENGLAND CARLING CUP

Brighton 1-2 Liverpool
Cardiff 2-2 Leicester - Cardiff win 7-6 on penalties
Chelsea 0-0 Fulham - Chelsea win 4-3 on penalties
Everton 2-1 West Brom - After Extra Time
Man City 2-0 Birmingham
Southampton 2-1 PrestonArsenal 3-1 Shrewsbury
Aston Villa 0-2 Bolton
Blackburn 3-2 Leyton Orient
Burnley 2-1 MK Dons
Crystal Palace 2-1 Middlesbrough
Leeds 0-3 Man Utd
Nott'm Forest 3-4 Newcastle aet
Stoke 0-0 Tottenham - Stoke win 7-6 on penalties
Wolves 5-0 Millwall

Wednesday, September 21, 2011

MATCH LIVE CENTER: YANGA vs VILLA SQUARD na TOTO AFRICANS vs SIMBA.




YANGA 3:2 VILLA SQUARD ( FT )
Villa: Mohamed Kijuso,KIGGI Luseke
Yanga: Haruna Niyonzima,Asamoah Keneth,Kiiza Hamis


SIMBA 3:3TOTO AFRICANS ( FT )
Felix Sunzu (2 ), Mafisango.
Toto: Idd Mobi,Soud Mohamed.


COASTAL UNION 0:1 AZAM ( FT)
John Bocco.

Tuesday, September 20, 2011

TIKETI YANGA v AZAM,POULSEN KUTAJA TIMU SEPT 26

Mmoja wa wauzaji tiketi kwenye mechi ya Azam na Yanga iliyochezwa Septemba 18 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Seleman Masoud aliripoti kupotelewa kitabu kimoja cha tiketi mara baada ya ugawaji wa vitabu hivyo kwa wauzaji kufanyika asubuhi ya siku ya mchezo kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Tiketi kutoka kwenye kitabu hicho ziliuzwa kwa mashabiki ambao walikamatwa. Walitakiwa kuonesha mahali ambapo wameuziwa tiketi hizo ambapo walionesha kwa muuzaji mwingine Salum Abdallah. Abdallah pia alikuwa mmoja wa wauzaji tiketi katika mechi hiyo.

Wauzaji wote wawili walikamatwa na TFF na tukio kuripotiwa Kituo cha Polisi Chang’ombe. Tukio hilo lilifunguliwa jalada namba CHA/IR/6257/2011 ambapo watuhumiwa wameshachukuliwa maelezo yao. Kitabu kilichoibwa kilikuwa na tiketi 100 zenye thamani ya sh. 300,000. Thamani ya kila tiketi ni sh. 3,000.

POULSEN KUTAJA TIMU SEPT 26
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen anatarajia Septemba 26 mwaka kutaja wachezaji watakaoingia kambini kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Oktoba 9 mwaka huu jijini Casablanca.

Timu inatarajia kuingia kambini Septemba 28 mwaka huu, na inatarajia kuondoka Oktoba 6 mwaka huu kwenda Casablanca. Mechi hiyo ni ya mwisho hatua ya makundi kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatoria Guinea na Gabon.

Poulsen ambaye pia ni Mkufunzi wa Makocha wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) yuko nchini Gambia ambapo anaendesha kozi ya wakufunzi na anatarajia kurejea nchini Septemba 24 mwaka huu.


LIGI DARAJA LA KWANZA
Ligi Daraja la Kwanza inayoshirikisha timu 18 inatarajia kuanza mwezi ujao. Kamati ya Mashindano inayoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Ramadhan Nassib inatarajia kukutana Septemba 24 mwaka huu kuangalia mambo mbalimbali ya ligi hiyo.

Moja ya mambo ambayo kamati hiyo itafanya ni kupitisha tarehe ya kuanza ligi hiyo pamoja na vituo.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Patrick Vieira kuongoza Mradi mpya wa kukuza vipaji Manchester City.



Based on 80-acre site in east Manchester next to stadium
•15 full-size pitches, two half-size pitches, all with undersoil heating and floodlights
•A 7,000-seat mini-stadium
•Capable of training 400 young players, with an education centre for 200
•Accommodation for 32 first-team players and 40 youth players
•Staff offices and a media centre
•A first-team building with changing rooms, state-of-the-art gym, refectory and injury and rehabilitation centre
•5.5-acre area reserved for community use including a sixth-form college and swimming pool
•A pedestrian bridge linking the campus to Etihad Stadium

ANGALIA UNYAMA WA KICHAA WA REAL MADRID "PEPE" DIMBANI

JOSEPH OWINO AKITIA SAINI MKATABA WA KUICHEZEA AZAM


Aliyekuwa beki wa Simba Joseph Owino ( kushoto ) akisaini Form za kuichezea Azam Fc,anayeshuhudia ni katibu mkuu wa Azam Nassor Idrissa. ( Blog hii ndo ilkuwa ya kwanza kutoa taarifa za Mchezaji huyo kujiunga na Azam )

JE BAO LA ALILOKOSA TORRES NI ZAIDI YA MASTAA HAWA








MBINU ZA KOCHA TIMBE HAZIPO SAHIHI....HAKUMTENDEA HAKI SHAMTE ALLY...

Mabingwa watetezi wa ligi ya Vodacom Yanga wamefungwa kwenye mchezo wao dhidi ya Azam Fc . Huu ni mchezo wa pili kwa wanajangwani kupoteza na hadi sasa wanajikuta kwenye hali ngumu baada ya kufungwa michezo miwili na kutoka sare miwili huku wakishinda kwenye mchezo mmoja.
Kwa kuutazama kwa jicho la kiufundi mchezo kati ya Yanga na Azam kuna kila sababu ya kusema kuwa mbinu za kocha wa Yanga hazikuwa sahihi.
Kwa kuitazama Yanga iliyoanza mchezo dhidi ya Azam ilikuwa na washambuliaji wawili Davis Mwape na Kiiza Hamis,basi utagundua hakukuwepo na uhusiano wa kuwapanga wote pamoja na ndiyo maana kocha Timbe alilazimika kumtoa mapema Mwape.



Pointi B ndio mahala alitakiwa awepo mshambuliaji wa Yanga lakini matokeo yake krosi zote za Shamte Ally zilikuwa zinapita tu kama unavyoona kwenye mchoro hapo juu, Mwape na Kiiza mara nyingi walikuwa 'OFF POSITION '.



Zamani ukisikia namba 9 basi jukumu lake lilikuwa ni kusimama mbele huku namba 10 akiwa na jukumu la kumkaba namba 8 wa timu pinzani ili kumfanya namba 8 wenu kuwa huru ili aichezeshe timu,
Siku hizi mpira umebadilika sana hasa mbinu za kucheza uwanjani,mifumo imekuwa ikitumika sana siku hizi kuliko wachezaji kujipanga kwa namba kama ilivyokuwa zamani.
Ili kupata mfumo husika basi huna budi kufahamu tabia za wachezaji wako wawapo nje na ndani ya uwanja,kuwachezesha Mwape na Kiiza kwa wakati mmoja hakukua na tija kwa aina ya viungo waliokuwa wanawazunguka hasa hasa Shamte Ally.

Pointi A ni krosi ya Shamte tena...hii inakuonyesha tena 'POOR POSITIONING' ya washambuliaji wa Yanga,




Shamte alikuwa mchezaji bora kwa Yanga kwenye kipindi cha kwanza . Alipiga mipira mingi sana toka eneo lake na alikuwa akiindesha timu na upande wake uliokuwa ‘active’ hasa kipindi cha kwanza.
Tatizo ni kwamba mipira yote ya Shamte haikukutana na mtu yoyote kati ya Kiiza na Mwape na hivyo haikuwa na madhara yoyote kwa wapinzani ( kumbuka aina ya mabao aliyokuwa akiyafunga Boniface Ambani )
Ndiyo maana nasema Timbe hakumtendea haki Shamte kwa kumpangia Mwape na Kiiza,
Kwa jinsi walivyopangwa ilionekana kama Kiiza na Mwape wanacheza kama ‘mapacha’ ambao walikuwa wanatakiwa kusaidiana wao kwa wao. Ingeleta maana kama Mwape angesimama mbele kama mshale na Kiiiza angecheza nyuma yake kidogo lakini haikuwa hivyo.
Mwape ni mshambuliaji mwenye nguvu ambaye anatakiwa kucheza kwenye eneo la 18 na si zaidi ya hapo .
Hakuna anayeelewa kwanini Mwape huwa anaelekezwa kucheza nje ya eneo la hatari . Kimsingi mwape akiwa nje ya eneo la hatari utamlaumu tu kwa kuwa hana ‘first touch’ nzuri na zaidi ya hapo hana mahesabu ya ‘dribbling’ yaani hajui ni mara ngapi mchezaji anatakiwa kuendesha mpira kabla hajatoa pasi na ndio maana Mwape ataonekana kuwa mzigo akiwa nje ya 18.
Kwa jinsi Shamte Ally alivyocheza hakuna shaka Yanga walihitaji sana huduma ya Jerry Tegete kwa kuwa aina ya mipira ambayo ilikuwa inatumwa kwenye mchezo wa Azam ni mipira ambayo Jerry Huwa anafunga.
Haya yatabaki kwa Viongozi wa Yanga lakini ukweli ni kwamba Yanga watakosa huduma ya mabao ya Tegete ( si kwasababu ya kufungiwa tu bali hata kwa namna ambavyo walikuwa wanamtumia akicheza zaidi nje ya box wakati yeye ni ‘Goal pocher’ ).
Pius Kisambale kwa upande wake alikuwa na umuhimu sana kwa timu yake lakini hilo halikuwa linaonekana na benchi la ufundi . Kisambale alikuwa anawa-occupy mabeki wa Azam hususan Erasto Nyoni ambaye muda mwingi alikuwa analazimika kuondoka kwenye eneo lake na kumkaba Kisambale.
Pengine makocha wa Yanga walikuwa wanaona kuwa Kisambale hana msaada kwa kuwa Yanga walikuwa wanashambulia sana kupitia upande wa Shamte ambao kimsingi ulikuwa unasaidiwa na wachezaji watatu Shamte,Niyonzima na Nsajigwa.

Kama wachezaji wa Yanga wangekuwa na mlengo tofauti wangeona umuhimu wa Kisambale na kuutumia lakini haikuwa hivyo .
Mwisho wa siku Kisambale baada ya kuonekana hana faida alitolewa nje.
Tatizo moja kwenye soka la Tanzania ni kuwa na maamuzi yasiyozingatia ufundi,Makocha wengi hupenda kufanya mabadiliko kwa kusikiliza presha za mashabiki na nadhani ndio kilichotokea kwa Kisambale.
Nafasi ya Kisambale ilichukuliwa na Rashid Gumbo ( nilicheza naye pale Temeke,kwahiyo namfahamu vizuri Chidy Gumbo ) kimsingi si mchezaji wa pembeni bali kiungo wa kati tena akiwa na sifa kubwa ya kupiga mashuti na pia kutoa pasi za mwisho.
Kwa wenzetu duniani huko ambao wachezaji wao ni mahiri hili sio tatizo kwa kuwa mchezaji amejengwa kuwa na mazingira ya kucheza nafasi zaidi ya moja kuendana na mechi na mifumo mbali mbali. Alipoingia Gumbo hakuwa anacheza pembeni kama Kisambale na ni kama alishurutishwa kucheza nafasi ile nafasi ambayo si yake . Gumbo alikuwa akilazimika kugeuka na kuuleta mpira kwenye mguu wake wa kulia aliouzoea na pia alikuwa akiingia kati alikozoea badala ya kucheza pembeni kama mchezaji anayetokea pembeni.
Ingekuwa busara kwa kocha kufanya ‘tactical switch’ ya kumpeleka Gumbo katikati na kumleta Nurdin Bakari/Haruna Niyonzima pembeni kwa kuwa wana uwezo wa kucheza huko.
Matokeo yake upande wa kulia ukafa kabisa kwa kukosa huduma na matokeo yake Shamte Ally akaonekana amepwaya,akatolewa na nafasi yake akaingia Godfrey Taita mchezaji ambaye ana mentality ya ulinzi na si ushambuliaji.
Ubovu wa mabadiliko haya ulikuwa kwenye ukweli kuwa Yanga walikuwa nyuma na walikuwa wakihitaji bao ili kuokoa mchezo.
Kimsingi mchezo kwa Yanga uliishia hapo na ndio walipofungwa. Kama Yanga wataendelea kucheza kwa ufundi mbovu kama hivi hali itakuwa ngumu sana kwa wao kutetea ubingwa wao hasa ukizingatia ukweli kuwa wanaendelea kuangusha pointi kila leo.
Kwa upande wa Azam sio kwamba walicheza vizuri sana lakini walitengenezewa mazingira ya kupata ushindi na jinsi Yanga walivyocheza hovyo.

Monday, September 19, 2011

Tottenham 4-0 Liverpool: Tottenham yaitawala Liverpool.




Timu zilizoanza.
Bao la ajabu liliwapa Totenham nafasi ya kutawala mchezo na mengine yalikuja baada ya Tottenham kuwa na faida ya kuwa na watu wengi zaidi ya Liverpool lakini ukiacha hayo yote Tottenham walikuwa timu bora na hilo lilidhihirika kwa matokeo ya mwisho.
Harry Redknapp alitumia mfumo wa 4-4-2 huku Niko Kranjcar akiwa kwenye upande wa kulia na Rafael Van Der Vart alikuwa fit kidogo na alikaa benchi.
Kenny Dalglish alianza na timu ambayo ilikuwa imejibana – Charlie Adam akiwa kwenye upande wa kushoto na Stewart Downing akiwa upande wa kulia –Akiwa amepangwa huko kujaribu kupunguza mashambulizi ya Totenham kwenye upande wa kushoto toka kwa Gareth Bale kuliko upande wa kulia alikokuwa Niko Kranjcar .
Tottenham walianza mchezo kwa kasi ,wakiwasukuma Liverpool kwenye sehemu ya kati ya uwanja huku wakimiliki mpira vizuri . Charlie Adam hakupewa muda wa kumiliki mpira na kupiga pasi kama kawaida yake na kwa sababu hii jana Charlie Adam alikuwa na takwimu mbaya za pasi kuliko wakati wowote kwenye wakati wake kama mchezaji kwenye miaka yote aliyocheza akiwa England. Na pengine ndio maana alikerwa na kuamua kucheza rafu hadi akapewa kadi nyekundu.

Umiliki mpira.
Tottenham walimiliki mpira sana tangu wakati Liverpool wakiwa 11 kwa 11 jambo ambalo lilikuwa zuri kwao hasa ukizingatia ukweli kuwa Liverpool walijaribu kujaza wachezaji katikati ya kiwanja mapema.

Luka Modric alicheza pasi nyingi sana kuelekea pembeni ya uwanja , na Scot Parker naye alitoa mipira mingi toka chini na Kranjcar aliingia kati ambako mara nyingi alijikuta akiwa kwenye nafasi toka kwenye upande wa kulia pembeni.
Washambuliaji wawili ambao walijenga Patnership nzuri tangu kwenye mchezo wa wiki iliyopita Wolves walikuwa na mchezo mzuri kwa mara nyingine.

Defoe alishuka hadi chini kwa muda mrefu akitoa pasi za akili sana huku Adebayor akifanya kazi kwenye nafasi nafasi ambazo zilikuwa zinajitokeza katikati ya mabeki wa kati wa Liverpool.
Wote walikuwa wakija mpaka katikati ya uwanja wakitoa nafasi ya ziada kwa mtu aliyekuwa na mpira ya kutoa pasina ndio maana wote walimaliza na takwimu nzuri sana za pasi baina yao.
Kitu kilichokuwa kinajirudia kwenye kipindi cha kwanza ilikuwa ni nidhamu mbovu ya wachezaji wa Liverpool. Wachezaji wa Liverpool walikuwa wakicheza rafu zisizo na msingi na walikuwa wakigawa faulo za kizembe sana hasa nje ya eneo lao la hatari na kwenye upande wa kushoto na pia tackling mbovu ziliwazulia matatizo makubwa.

Kitu ambacho kilionekana kuja bila kizuizi ni mchezaji wa Liverpool kuonyeshwa kadi nyekundu na pia hali hii iliwapa Tottenham nafasi ya kupiga mashuti nje ya eneo la hatari kutokana na mipira iliyokufa.

11V10.
Mchezo uliongezeka msisimko baada ya Liverpool kubaki 10 uwanjani baada ya Charlie Adam kuonyeshwa kadi nyekundu . Dalglish aliamua kuwaacha wachezaji waliokuwa uwanjani kama wlaivyo pasipo kufanya mabadiliko yoyote.
Cha kushangaza ni maamuzi ya kumuacha uwanjani Andy Carrol huku akicheza kushoto mwa uwanja .
Labda wazo la Kenny Lilikuwa kumpa wakati mgumu beki Kylie Walker hususana kwenye mipira ya juu lakini Caroll alionekana kutokuwa mchezoni na alikosa nguvu za kumkaba ipasavyo Kylie Walker wakati Liverpool walipokuwa hawana mpira. Kumpanga Suarez pembeni ingekuwa jambo la msingi zaidi au kuwachezesha Craig Bellamy na Dirk Kuyt watu ambao ni wachezaji wa pembeni kiasili. Tottenham walicheza vizuri sana katika hali ya wachezaji 11 kwa 10 ,walimiliki mipira na waliwachosha Liverpool. Japo hawakutengeneza nafasi nyingi za wazi na walilazimika kungoja hadi pale Liverpool walipopungua uwanjani ili kupata bao la pili.

11V 9.

Ni vigumu kujenga hoja kuwa Dalgish angeweza kufanya chochote kuirudisha Liverpool mchezoni . Kushindana ukiwa na wachezaji tisa inawezekana ukiwa uko kwenye matokeo ya 0-0 na unaweza kucheza kwa nguvu na kupata sare lakini Liverpool walikuwa wanataka kurudi mchezoni wakiwa nyuma hivyo haikuwezekana kwao.

Mwisho.

Huu ungeweza kuwa mchezo wa kusisimua sana . Dakika za mwanzo Tottenham walikuwa wakicheza kwa kupiga pasina matatizo ya Charlie Adam yalionekana kuwa matatizo ya Liverpool kwa jumla. Wachezaji wa Liverpool walishindwa kutafuta nafasi za kupitisha mipira . Mbinu ya kucheza kwa klupunguza uwanja inaweza kukupa umiliki wa mpira lakini pia inamaanisha kuwa wapinzani wana hatua chache za kukimbia kuutafuta mpira kwa kuwa uwanja umepunguzwa kwa niaba yao na kazi inakuwa nyepesi. Dalglish alikuwa kwenye wakati mgumu akiwa na wachezaji 10 lakini kumtumia Caroll pembeni ya uwanja ilikuwa maamuzi ya ajabu sana na hayakuwa na faida kwa timu yake –Liverpool haikuweza kupeleka mipira pembeni alikokuwa na Caroll hakuwa na msaada kwenye ukabaji . Liverpool walihitaji kufanya mabadiliko wakati walipobaki 10 ila walipobaki 9 kimsingi mchezo ulikuwa umeisha kwao.

Pointi 10 katika ushindi wa mabao 3-1 wa Manchester United dhidi ya Chelsea.


Ulikuwa mchezo wa wazi ambao haukuwa na mbinu wala mfumo wa aina moja na yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea

1. Mwanzoni kulikuwa ni kama hakuna presha hasa pale ambapo wachezaji walipokuwa wanamiliki mpira hasa kwa wachezaji wa United Anderson na Fletcher.Huu umekuwa kama mtindo wa soka la Ulaya kwa sasa ambapo viungo huwa wanawaruhusu viungo wa timu pinzani kumiliki mpira mwanzoni.

2. Wakati Man United ilipocheza na Chelsea mara nne msimu uliopita suala la msingi kwa upande wao lilikuwa mchezaji mwenye nguvu ambaye angeweza kucheza dhidi ya Wayne Rooney kwani anaposogea kucheza kwenye ‘shimoni’ anakuwa tishio sana.
Andre Villas Boas kwa uzoefu wake mdogo asingeweza kwenda vitani bila ya kiungo mlinzi lakini alimchezesha Raul Meireles. Mreno huyu ni mchezaji ambaye anachangamsha timu na anao uwezo wa kucheza kwenye eneo la kiungo mkabaji (kimsingi meireles ni aina ya mchezaji ambaye hucheza kadri anavyoelekezwa hivyo angelekezwa kucheza sehemu Fulani ndio ambacho angefanya)

lakini hana ufanisi wa kucheza nafasi ya ukabaji kwenye kiungo dhidi ya aina ya mchezaji kama Rooney. Jon Obi Mikel angeweza kucheza vyema dhidi ya Rooney.

3. United wamekuwa wepesi sana kwenye safu ya ushambuliaji msimu huu lakini dhidi ya Chelsea walikuwa wamejipanga zaidi .Wachezaji wa pembeni walikuwa wakaa zaidi pembeni na si kwenda mahali kwingine.

Mfano mzuri ni Ashley Young ambaye mara nyingi hupnda kuingia kati japo yeye ni mchezaji wa pembeni lakini dhidi ya Chelsea hakuondoka kwenye winga yake hata mara moja.

4. Jambo la kufurahisha wiki hii limekuwa hadithi ya Fernando Torresakiwalaumu wachezaji wenzie wa Chelsea hasa viungo kwa kushindwa kumpa huduma ya kutosha .
Torres alienda mbali zaidi na kueleza kuwa akiwa Liverpool alikuwa anafunga sana kwa kuwa alikuwa akipewa mipira ya kupenyezewa na viungo wake na kwa maneno yake mwenyewe anadai kuwa anapenda kuletewa mipira ya moja kwa moja na viungo ambao ni wabunifu ambao hupitisha mipira haraka zaidi.
Lakini hilo halitoi sababu ya umaliziaji wake ambao kiukweli umekuwa mbovu siku hadi siku . Suala la msingi ambalo unaweza kulielewa hapa kwa Torres ni kwamba yeye si mchezaji sahihi kwa Chelsea na Chelsea si timu sahihi kwake.
Torres alicheza vizuri dhidi ya United kwa kuwa viungo wa timu yake walijaribu kupitisha mipira katikati ya mabeki wa United na bao alilofunga ni mfano mzuri wa hili.

5. Huu haukuwa mchezo ambao unamfaa Frank Lampard . John Obi Mikel angeweza kummudu Rooney nah ii ingemaanisha kuwa Chelsea wangeweza kufanya ‘pressing’ kwa uzuri zaidi pamoja na hilo pia wangeweza kumsaidia Fernando Torres zaidi kwa viungo wawili Raul Meireles na Ramires huku Juan Mata akicheza mbele yao kidogo.
Lampard amekuwa mchezaji mzuri sana kwa Chelsea kwa muda mrefu pasipo kuwa na kipaji – kwa miaka mingi nah ii ni kwa sababu alikuwa mchezaji wa kucheza eneo husika akitimiza jukumu husika.
Villas Boas amebadili mfumo aliokuta Chelsea na majukumu kwa wachezaji yamebadilika , inawezekana ni mapema sana kusema kuwa Lampard amekwisha lakini anapaswa kuzoea majukumu Fulani ili kupata nafasi.

6. Kama Vilas Boas anajaribu kuifanya Chelsea icheze kisasa zaidi na kutengeneza timu inayocheza mchezo wa pasi zaidi anapaswa kuwatazama kwa umakini mabeki wake wa kati hasa kwenye uwezo wao wa kucheza wakati mpira uko mguuni. Johhny Evans alikuwa na wastani wa kutoa pasi kwa asilimia 95% ,Phil Jones alifikia 88% ila John Terry na Branislav Ivanovic wote hakuna aliyezidi 77% na hiyo ni hatari.


7. Ukizitazama timu zote za Sir Alex Ferguson kitu pekee ambacho kimefanana ni matumizi ya sehemu ya pembeni ya uwanja na pia matumizi ya mipira mirefu . Hilo lilionekana kwenye mchezo dhidi ya Chelsea-Johny Evans alitoa mpira mmoja wa hatari katikati ya uwanja kwa Nani na Anderson naye alifanya hivyo hivyo kabla Nani hajampa pasi Javier Hernandez mwanzoni. Mara nyingi Wayne Rooney alikuwa akishuka na kucheza pasi fupi na wenzie .

Wakati timu inayotumia mifumo ya 4-4-2 /4-4-1-1 inapokutana na timu inayotumia 4-3-3 faida inayokuwepo kwa timu ya 4-4-2 ni kwamba mawinga wanawapa sana tabu mabeki wa pembeni –mshambuliaji wa pembeni wa timu inayotumia 4-3-3 anakuwa na jukumu la kumtazama beki wa pembeni wa timu pinzani na anamuacha wa timu yake na mara mbili sasa kwenye mchezo wa United na Chelsea wameweza kumpa tabu Ashley Cole na ni kwa sababu ya mfumo huu.

8.Wakati timu ikiwa mbele wachezaji wanaoingia na kutoa pasi rahisi rahisi ili kumiliki mpira wanakuwa hawana thamani . Mfano mzuri ni Michael Carrick ila Dimitar Berbatov alifanya kazi nzuri kwa kutopoteza mpira wowote katika pasi 14 alizopata.

9. Iliruhusu mashuti 22 kwenye mechi hii,ikaruhusu mashuti 22 kwenye mchezo dhidi ya Bolton na 20 kwenye mechi dhidi ya Arsenal na mengine 16 dhidi ya West Brom. Hizi ni takwimu za ajabu kwa timu inayocheza kwa falasafa ya ulinzi kama United.
Kwa kifupi United imeruhusu mashuti mengi kuliko timu zote kwenye ligi hadi sasa-Swali la kujiuliza ni je mashuti haya ni kwa sababu ya ubovu wa beki inayovuja na au wapinzani ambao wanatambua udhaifu wa kipa David De Gea kwenye mashuti ya mbali?

10. Pamoja na makosa kadhaa , kocha Andre Villas Boas ameonekana kuwa anafanya kazi nzuri Chelsea . Hii ni timu iliyokuwa inahitaji mabadiliko makubwa hasa kwenye kikosi cha kwanza na falasafa nzima ya soka lake na hadi sasa inaonekana kufanya kazi kwani timu inaonekana ikicheza kimbinu zaidi.

Dhidi ya United walipambana kwa ukomavu na walikuwa na bahati mbaya kuwa nyuma kwa mabao matatu hadi kufikia half-time. Makocha wengine wangehofia kupewa kipigo cha Arsenal na hivyo wangebaki nyuma kwa kipindi cha pili laki Boas alikuwa na ujasiri wa kufanya mabadiliko yaliyolenga kushambulia zaidi na akabadili mfumo kuwa 4-2-1-3 na kwa asilimia Fulani alifanikiwa kwenye hili.

Vodacom kutoongeza mkataba wa kuidhamini Ligi Kuu


KAMPUNI ya Utoaji Huduma za Simu za Mikononi ya Vodacom huenda ikajitoa katika udhamini wa Ligi Kuu ya Bara mara baada ya kukamilika kwa mkataba wake wa miaka mitano ya udhamini wa ligi hiyo.

Hali hiyo inakuja kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoridhika na mchakato wa Vodacom kuiruhusu Yanga kutumia nembo yenye rangi nyeusi badala ya nyekundu inayotumiwa na kampuni hiyo katika jezi zake.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema baada ya Vodacom kuingia mkataba kienyeji na Yanga wa kubadili rangi ya nembo, wao kama shirikisho wameiandikia kampuni hiyo ya simu na kuieleza klabu yoyote itakayobadili rangi ya nembo, hawatowajibika kwa lolote.

“Tumewaambia Vodacom, sasa klabu yoyote ikitaka kubadili rangi za nembo ya Vodacom wafanye watakavyo kwani walivyofanya na Yanga (kuingia mkataba kienyeji) si jambo la kiungwana,” alisema Tenga.

Hata hivyo katika hali ya kawaida, si jambo rahisi kwa Vodacom kukubali nembo yake ibadilishwe rangi na klabu zitakazoshiriki ligi hiyo kwani nafasi yake kibiashara inaweza kuyumba.

Mambo yote ya mkataba pia yatategemea na faida iliyopata Vodacom kutokana na ushiriki wake katika udhamini wa ligi hiyo kubwa kwa ngazi ya klabu hapa nchini.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa mwezi huu na Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Vodacom ndiyo kampuni inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi wanaotumia simu za mikononi ikifuatiwa na kampuni nyingine
.

TP MAZEMBE WANUNUA NDEGE YAO WENYEWE, SIMBA NA YANGA VIPI?










TIMBE: NAISUKA UPYA SAFU YA USHAMBULIAJI, VILLA SUBIRINI KIPIGO.



Kocha mkuu wa Yanga, Sam Timbe amepanga kuifanyia kazi safu yake ya ushambuliaji kwa ajili ya kupata ushindi katika mechi ijayo dhidi ya Villa Squard itakayochezwa kesho kutwa kwenye uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Dar es Salaam.
Hiyo, imetokana na safu ya ushambuliaji inayoongozwa na wachezaji wa kulipwa Davies Mwape, Kenneth Asamoah na Hamis Kiiza kushindwa kutumia nafasi wanazopata kutoka kwa viungo wake.
Timbe alisema, amepanga kutumia siku mbili kuwanoa washambuliaji wake kwa kuwapa mbinu za kufumania nyavu katika mechi hiyo ya keshokutwa kwa kuanza na leo na kesho.
Kocha huyo aliendelea kusema, hilo linawezekana kutokana na wachezaji kuhitaji kuongezewa vitu vichache ambayo muhimu kama wakivizingatia watapa matokeo mazuri .
“Safu ya Ushambuliaji ndiyo inaangusha, wameshindwa kutumia pasi na krosi wanazopata kutoka kwa viungo wangu,” alisema Timbe raia wa Uganda.
Mapungufu hayo Timbe aliyona wakati timu hiyo ilipocheza na Azam FC, matokeo yaliyomalizika kwa Yanga kukubali kipigo cha bao 1-0 kupitia kwa mshambuliaji wake, John Bocco.

KIPRE TCHETCHE NJE YA DIMBA WIKI 3


Mshambuliaji toka Cote D’Ivoire anayeichezea Azam FC, Kipre Tchetche atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki 3 mpaka 4 baada ya kuumia hapo juzi.

Kipre ambaye alitazamiwa kuanza hapo jana katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Yanga lakini hakuonekana uwanjani na nafasi yake ikachukuliwa na Khamisi Mcha Vuai.
Kocha wa Azam FC, Stewart Hall akizungumza baada ya mchezo huo uliokwisha kwa ushindi wa goli moja kwa Azam FC alisema kuwa Kipre alikuwa katika mipango yake katika mchezo huo lakini maumivu aliyoyapata juzi ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa wiki tatu ndio umefanya kubadili mbinu na mipango kwenye mchezo huo dhidi ya Yanga.

BREAKING NEWZ: VODACOM KUTOONGEZA MKATABA WA KUIDHAMINI LIGI KUU


Kampuni ya Vodacom haitoongeza mkataba wa kuendelea kuidhamini ligi kuu ya Tanzqania Bara baada ya mkataba uliopo kumalizika.Taarifa zaidi zitakujia baadae kidogo.

BARCLAYS PREMIER LEAGUE KWENYE NAMBA


1: Goli la Franco di Santos kwa Wigan Athletic lilikuwa ndio shuti pekee kwenye target katika kipigo chao cha 3-1 kutoka kwa Everton.

2: Sunderland walipata ushindi wao wa 3 ndani ya mwaka huu wakiwa nyumbani, baada ya kuwafunga Stoke City 4-0 @ Stadium Of Light.

5: Norwich City wameadhibiwa penati katika kila mechi 5 za mwanzo waliyocheza katika msimu huu wa Barclays premier league, ikiwa ni rekodi kwenye EPL.

9: Magoli mawili ya Yakubu Ayegben kwa Blackburn dhidi ya Arsenal, inamaanisha kuwa amefunga katika misimu 9 mfulululizo ya premier league.

9: Mshambuliaji wa Newcastle Leon Best sasa amefunga magoli 9 katika mechi 15 za Barclays premier league tangu kuondoka kwa Andy Carroll.

9: Bolton Wanderers sasa watakuwa wamefungwa katika mechi zao 9 za mwisho kati ya 10 za EPL.

18: Manchester United wamepata ushindi wao wa 18 mfulululizo baada ya kuwafunga Chelsea 3-1 hivyo kuwafanikiwa kuifikia rekodi ya klabu hiyo ambayo imekuwepo tangu 1904/05 walipokuwa ligi ya daraja la pili.

55: Timu tatu zote zilizopanda daraja msimu huu zimeshinda mechi zao kwa mara kwanza kwenye pemier league tangu February 2007, miezi 55 iliyopita.

374: Scott Sinclair amefunga goli la kwanza la Swansea City kwenye Barclays Premier League baada ya dakika 374 za msimu,katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya West Bromwich Albion.

Abdallah Idrisa Majura apokea Leseni ya umiliki wa SPORTS FM.


Mmiliki wa SPORT Fm 91.2 Abdallah Idrisa Majura leo tarehe 16/09/2011
akipokea leseni ya umiliki wa kituo hicho
kutoka kwa Mkurugrnzi Mkuu wa mawasilianao Tanzania (TCRA) Pr. John
Nkoma.
Majura ambaye amewahi kufanya kazi
Radio Tanzania, ITV/Radio one na BBC ni mtangazaji na mwandishi wa
habari Tanzania kumiliki kituo cha Radio

MAN UNITED WAENDELEZA UBABE ENGLAND, YAITANDIKA CHELSEA 3.


manchester united 3-1 chelsea by Royalfootyuk

MAJOGOO WA JIJI WAKANDAMIZWA 4-0 NA SPURS

LAVANTE YAITANDIKA REAL MADRID

EDSON CAVANI APIGA HAT TRICK, NAPOLI IKIUA AC MILAN

YANGA CHALI, BOCCO APELEKA MSIBA JANGWANI


Magiants wa ligi kuu ya Tanzania Simba na Yanga leo wameshindwa kufurukuta katika mechi zao za VPL.

Katika uwanja wa taifa wakicheza na matajiri wa ligi kuu a.k.a Manchester City ya Bongo-Azam FC, mabingwa wa watetezi VPL, Dar Young African walipokea kichapo cha goli 1-0.Goli la Azam liligungwa na mshambuliaji hatari John Bocco.

Katika uwanja wa Kaitaba, Said Sued alikatisha sherehe ya ushindi kwa Simba baada ya kufunga bao la kusawazisha katika dk.30 kipindi cha pili, goli la Simba lilifungwa na Patrick Mafisango.

Kwa Matokeo haya Simba imeendelea kukaa kileleni wakiwa wamecheza mechi 6 na kupata pointi 14, wakiwa fuatiwa na Mtibwa wenye pointi 11,Azam mechi 6 na pointi 11.Yanga wapo nafasi ya 8 na pointi zao 6 katika michezo 6.Anayeshikilia mkia wa ligi ni maafande kutoka Dodoma walio na pointi 3 ndani ya mechi 5.


Sunday, September 18, 2011

THOMAS ULIMWENGU NJIANI KUELEKA TP MAZEMBE NA DILI LA MIAKA 3


Thomas Ulimwengu anatarajiwa kuondoka kesho kuelekea nchini Kongo kwenda kujiunga na klabu ya TP MAZEMBE kwa mkataba wa miaka 3.

Mayweather amtandika Ortiz kwa KO

BARCELONA WAILIPA MAN UNITED

Saturday, September 17, 2011

REDONDO AIPANIA YANGA KESHO


Kiungo Ramadhani Chombo ‘Redondo’ amewatoa hofu mashabiki wa Azam FC kwa kuwa hakikishia ushindi katika mechi zijazo za ligi kuu ukiwepo mchezo wa kesho dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na tovuti ya Azam,Redondo amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kupambana na timu yoyote watakayokutana nayo.

“Timu ina hali nzuri, na kwa kuwa tumekuwa pamoja muda mrefu, tunahitaji ushindi kwa kila mechi tunayokutana nayo ili kufikia malengo yetu, hata kama ni Yanga kwetu ushindi lazima” alisema Redondo.

Redondo ameongeza kuwa baada ya kucheza michezo iliyopita, timu inapigana kadri iwezavyo ili kukaa katika nafasi nzuri. Naye nahodha msaidizi wa timu hiyo, Aggrey Morris amesema wapo katika maandalizi mazuri na mechi dhidi ya Yanga ni sawa na mechi ya kawaida hivyo ushindi utapatikana.

Amesema wapenzi wa Azam FC wasiwe na mashaka, wachezaji wote wapo makini na wajitokeze kwa wingi kwani hawatawaangusha.

Kocha mkuu Stewart Hall amezungumzia mchezo huo kama ni moja ya mechi muhimu kwao ya kupata pointi tatu, kwakuamini kuwa kutokana na wachezaji kuonyesha hali ya kupatikana kwa ushindi.

“Wachezaji wapo kamili, MrishoNgassa na Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ wameshamaliza adhabu zao hivyo watakuwepo katika mchezo huo” alisema Stewart.

Ameongeza kuwa watatumia mapungufu walionayo Yanga kupata ushindi, anaamini safu yake ya ulinzi iliyoko chini ya nahodha Aggrey Morris watahakikisha hakuna madhara katika lango lao litakalosimamiwa na makipa Mwadini Ally na Obren Cuckovic.

Azam FC kesho itacheza mchezo wake wa saba wa ligi kuu dhidi ya Yanga, Azam itashuka katika mchezo huo ikiwa na pointi nane, ikishinda michezo miwili, sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja, wakati Yanga inapointi 6.

MTIBWA YAITANDIKA 2-0 VILLA SQUAD

MTIBWA SUGAR YA MOROGORO LEO IMEIFUNGA VILLA SQUAD YA DAR MABAO MAWILI KWA BILA KATIKA MCHEZO WA LIGI KUU YA TZ.BARA .MAGOLI YA MTIBWA YAMEFUNGWA NA THOMAS MORRIS, NA SAID RASHID.

MATOKEO MENGINE YA VODACOM PREMIER LEAGUE

TOTO AFRICA 0-0 JKT RUVU

RUVU SHOOTING 2-1 COASTAL UNION

BLACKBURN 4 - ARSENAL

MAGOLI MATANO YALIYOFUNGWA NA WACHEZAJI WA ARSENAL HAYAKUTOSHA KUWAOKOA THE GUNNERS NA KIPIGO KUTOKA KWA BLACKBURN LEO KWENYE EPL. MAGOLI MAWILI YA KUJIFUNGA YA ALEX SONG NA LAURENT KOSCIENLY NA MENGINE MAWILI KUTOKA YAKUBU YAKITOSHA KUPELEKA MSIBA EMIRATES STADIUM.

YAKUBU AKIPEWA "GWALA" NA KOCHA WAKE STEVE KEAN BAADA YA KUFUNGA BAO

MIKAEL ARTETA AKIFUNGA BAO LA KWANZA KWENYE MECHI DHIDI YA BLACKBURN


MASHABIKI WA BLACKBURN WAKIANDAMANA KWA MADAI KUMTAKA KOCHA "STEVE KEAN" AJIUZULU.


MECHI ZA LEO VODACOM PREMIER LEAGUE


TOTO AFRICAN Vs JKT RUVU
Mchezo huu utapigwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


VILLA SQUAD Vs MTIBWA SUGAR.
Baada ya kufungwa na Simba na Azam FC, Villa squad itakuwa kibaruani kuwakabili wakatamiwa wa Morogoro, Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Azam uliopo Chamanzi Mbande nnje kidogo ya jiji la Dar es salaam.



RUVU SHOOTING Vs COASTAL UNION.
Coastal union leo watakuwa wanatafuta namna ya kujifariji pale watakapo karibishwa Ruvu Shooting katika dimba la Mlandizi mkoani Pwani.
VILLA SQUAD Vs MTIBWA SUGAR.
Baada ya kufungwa na Simba na Azam FC, Villa squad itakuwa kibaruani kuwakabili wakatamiwa wa Morogoro, Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Azam uliopo Chamanzi Mbande nnje kidogo ya jiji la Dar es salaam.


RUVU SHOOTING Vs COASTAL UNION.
Coastal union leo watakuwa wanatafuta namna ya kujifariji pale watakapo karibishwa Ruvu Shooting katika dimba la Mlandizi mkoani Pwani.

MTIHANI WA KWANZA KWA ANDRE VILLAS-BOAS

Kocha Andre Villas-Boas anakutana na mtihani wa kwanza mgumu akiwa kocha kesho jumapili, na nafikiri tutaona na kujua mengi kuhusu falsafa zake kwenye soka.

Chelsea hawajafungwa tangu mreno huyo mwenye miaka 33 alipowasili Stamford Bridge akitokea Porto.

Na nafikiri trip ya Chelsea kwenda Old Trafford itatuthibitishia ubora wa mbinu za Villas Boas.

Tunafahamu nini tutegemee kutoka kwa Manchester united ambao hawajawahi kucheza defensively dhidi ya timu yoyote iwe Barcelona au Wigan.

United hawatobadilisha mchezo wao dhidi ya Chelsea lakini kitachokuwa kinavutiwa zaidi ni kuona jinsi gani wageni watakavyocheza.

Vilas-Boas alipokuwa Porto alikuwa akitegemea kushinda kila mchezo lakini sasa yupo katika sehemu nyingine.

Anai-manage timu kubwa ambayo kesho inasafiri kwenda Theatre of Dreams ambako mwaka huu timu yao ipo katika form nzuri.

Hivyo nafikiri mchezo utatueleza na kutufanya kumjua vizuri Villas-Boas.

Je atafahamu kuwa ni vigumu sana kucheza na United kwa open game?

Au anaweza kwenda na akacheza aina ya mchezo huo na akafanikiwa.?

Nafahamu nini Jose Mourinho ambaye siku zote amekuwa akifananishwa na Villas-Boas-angeenda kufanya kama bado angekuwa kocha wa Chelsea.

Kama Mourinho angekutana na United ambayo ipo kwenye form nzuri, basi ni dhahiri angecheza mchezo wa kuzuia zaidi.

Hivyo natamani kuona je Villas Boas atacheza mtingdo wa 4-3-3 au 4-5-1 au 4-4-2 @ old Trafford.

Kesho naamini AVB atachagua kikosi chake bora kabisa kwa mara ya kwanza kitu ambacho tena kitakuwa cha kutazamwa ili kujua his assessment of his squad.

Haijalishi matokeo ya kesho, nina uhakika AVB atakuwa manager mzuri sana.