Search This Blog
Monday, September 19, 2011
Pointi 10 katika ushindi wa mabao 3-1 wa Manchester United dhidi ya Chelsea.
Ulikuwa mchezo wa wazi ambao haukuwa na mbinu wala mfumo wa aina moja na yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea
1. Mwanzoni kulikuwa ni kama hakuna presha hasa pale ambapo wachezaji walipokuwa wanamiliki mpira hasa kwa wachezaji wa United Anderson na Fletcher.Huu umekuwa kama mtindo wa soka la Ulaya kwa sasa ambapo viungo huwa wanawaruhusu viungo wa timu pinzani kumiliki mpira mwanzoni.
2. Wakati Man United ilipocheza na Chelsea mara nne msimu uliopita suala la msingi kwa upande wao lilikuwa mchezaji mwenye nguvu ambaye angeweza kucheza dhidi ya Wayne Rooney kwani anaposogea kucheza kwenye ‘shimoni’ anakuwa tishio sana.
Andre Villas Boas kwa uzoefu wake mdogo asingeweza kwenda vitani bila ya kiungo mlinzi lakini alimchezesha Raul Meireles. Mreno huyu ni mchezaji ambaye anachangamsha timu na anao uwezo wa kucheza kwenye eneo la kiungo mkabaji (kimsingi meireles ni aina ya mchezaji ambaye hucheza kadri anavyoelekezwa hivyo angelekezwa kucheza sehemu Fulani ndio ambacho angefanya)
lakini hana ufanisi wa kucheza nafasi ya ukabaji kwenye kiungo dhidi ya aina ya mchezaji kama Rooney. Jon Obi Mikel angeweza kucheza vyema dhidi ya Rooney.
3. United wamekuwa wepesi sana kwenye safu ya ushambuliaji msimu huu lakini dhidi ya Chelsea walikuwa wamejipanga zaidi .Wachezaji wa pembeni walikuwa wakaa zaidi pembeni na si kwenda mahali kwingine.
Mfano mzuri ni Ashley Young ambaye mara nyingi hupnda kuingia kati japo yeye ni mchezaji wa pembeni lakini dhidi ya Chelsea hakuondoka kwenye winga yake hata mara moja.
4. Jambo la kufurahisha wiki hii limekuwa hadithi ya Fernando Torresakiwalaumu wachezaji wenzie wa Chelsea hasa viungo kwa kushindwa kumpa huduma ya kutosha .
Torres alienda mbali zaidi na kueleza kuwa akiwa Liverpool alikuwa anafunga sana kwa kuwa alikuwa akipewa mipira ya kupenyezewa na viungo wake na kwa maneno yake mwenyewe anadai kuwa anapenda kuletewa mipira ya moja kwa moja na viungo ambao ni wabunifu ambao hupitisha mipira haraka zaidi.
Lakini hilo halitoi sababu ya umaliziaji wake ambao kiukweli umekuwa mbovu siku hadi siku . Suala la msingi ambalo unaweza kulielewa hapa kwa Torres ni kwamba yeye si mchezaji sahihi kwa Chelsea na Chelsea si timu sahihi kwake.
Torres alicheza vizuri dhidi ya United kwa kuwa viungo wa timu yake walijaribu kupitisha mipira katikati ya mabeki wa United na bao alilofunga ni mfano mzuri wa hili.
5. Huu haukuwa mchezo ambao unamfaa Frank Lampard . John Obi Mikel angeweza kummudu Rooney nah ii ingemaanisha kuwa Chelsea wangeweza kufanya ‘pressing’ kwa uzuri zaidi pamoja na hilo pia wangeweza kumsaidia Fernando Torres zaidi kwa viungo wawili Raul Meireles na Ramires huku Juan Mata akicheza mbele yao kidogo.
Lampard amekuwa mchezaji mzuri sana kwa Chelsea kwa muda mrefu pasipo kuwa na kipaji – kwa miaka mingi nah ii ni kwa sababu alikuwa mchezaji wa kucheza eneo husika akitimiza jukumu husika.
Villas Boas amebadili mfumo aliokuta Chelsea na majukumu kwa wachezaji yamebadilika , inawezekana ni mapema sana kusema kuwa Lampard amekwisha lakini anapaswa kuzoea majukumu Fulani ili kupata nafasi.
6. Kama Vilas Boas anajaribu kuifanya Chelsea icheze kisasa zaidi na kutengeneza timu inayocheza mchezo wa pasi zaidi anapaswa kuwatazama kwa umakini mabeki wake wa kati hasa kwenye uwezo wao wa kucheza wakati mpira uko mguuni. Johhny Evans alikuwa na wastani wa kutoa pasi kwa asilimia 95% ,Phil Jones alifikia 88% ila John Terry na Branislav Ivanovic wote hakuna aliyezidi 77% na hiyo ni hatari.
7. Ukizitazama timu zote za Sir Alex Ferguson kitu pekee ambacho kimefanana ni matumizi ya sehemu ya pembeni ya uwanja na pia matumizi ya mipira mirefu . Hilo lilionekana kwenye mchezo dhidi ya Chelsea-Johny Evans alitoa mpira mmoja wa hatari katikati ya uwanja kwa Nani na Anderson naye alifanya hivyo hivyo kabla Nani hajampa pasi Javier Hernandez mwanzoni. Mara nyingi Wayne Rooney alikuwa akishuka na kucheza pasi fupi na wenzie .
Wakati timu inayotumia mifumo ya 4-4-2 /4-4-1-1 inapokutana na timu inayotumia 4-3-3 faida inayokuwepo kwa timu ya 4-4-2 ni kwamba mawinga wanawapa sana tabu mabeki wa pembeni –mshambuliaji wa pembeni wa timu inayotumia 4-3-3 anakuwa na jukumu la kumtazama beki wa pembeni wa timu pinzani na anamuacha wa timu yake na mara mbili sasa kwenye mchezo wa United na Chelsea wameweza kumpa tabu Ashley Cole na ni kwa sababu ya mfumo huu.
8.Wakati timu ikiwa mbele wachezaji wanaoingia na kutoa pasi rahisi rahisi ili kumiliki mpira wanakuwa hawana thamani . Mfano mzuri ni Michael Carrick ila Dimitar Berbatov alifanya kazi nzuri kwa kutopoteza mpira wowote katika pasi 14 alizopata.
9. Iliruhusu mashuti 22 kwenye mechi hii,ikaruhusu mashuti 22 kwenye mchezo dhidi ya Bolton na 20 kwenye mechi dhidi ya Arsenal na mengine 16 dhidi ya West Brom. Hizi ni takwimu za ajabu kwa timu inayocheza kwa falasafa ya ulinzi kama United.
Kwa kifupi United imeruhusu mashuti mengi kuliko timu zote kwenye ligi hadi sasa-Swali la kujiuliza ni je mashuti haya ni kwa sababu ya ubovu wa beki inayovuja na au wapinzani ambao wanatambua udhaifu wa kipa David De Gea kwenye mashuti ya mbali?
10. Pamoja na makosa kadhaa , kocha Andre Villas Boas ameonekana kuwa anafanya kazi nzuri Chelsea . Hii ni timu iliyokuwa inahitaji mabadiliko makubwa hasa kwenye kikosi cha kwanza na falasafa nzima ya soka lake na hadi sasa inaonekana kufanya kazi kwani timu inaonekana ikicheza kimbinu zaidi.
Dhidi ya United walipambana kwa ukomavu na walikuwa na bahati mbaya kuwa nyuma kwa mabao matatu hadi kufikia half-time. Makocha wengine wangehofia kupewa kipigo cha Arsenal na hivyo wangebaki nyuma kwa kipindi cha pili laki Boas alikuwa na ujasiri wa kufanya mabadiliko yaliyolenga kushambulia zaidi na akabadili mfumo kuwa 4-2-1-3 na kwa asilimia Fulani alifanikiwa kwenye hili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment