Search This Blog

Monday, September 19, 2011

Tottenham 4-0 Liverpool: Tottenham yaitawala Liverpool.




Timu zilizoanza.
Bao la ajabu liliwapa Totenham nafasi ya kutawala mchezo na mengine yalikuja baada ya Tottenham kuwa na faida ya kuwa na watu wengi zaidi ya Liverpool lakini ukiacha hayo yote Tottenham walikuwa timu bora na hilo lilidhihirika kwa matokeo ya mwisho.
Harry Redknapp alitumia mfumo wa 4-4-2 huku Niko Kranjcar akiwa kwenye upande wa kulia na Rafael Van Der Vart alikuwa fit kidogo na alikaa benchi.
Kenny Dalglish alianza na timu ambayo ilikuwa imejibana – Charlie Adam akiwa kwenye upande wa kushoto na Stewart Downing akiwa upande wa kulia –Akiwa amepangwa huko kujaribu kupunguza mashambulizi ya Totenham kwenye upande wa kushoto toka kwa Gareth Bale kuliko upande wa kulia alikokuwa Niko Kranjcar .
Tottenham walianza mchezo kwa kasi ,wakiwasukuma Liverpool kwenye sehemu ya kati ya uwanja huku wakimiliki mpira vizuri . Charlie Adam hakupewa muda wa kumiliki mpira na kupiga pasi kama kawaida yake na kwa sababu hii jana Charlie Adam alikuwa na takwimu mbaya za pasi kuliko wakati wowote kwenye wakati wake kama mchezaji kwenye miaka yote aliyocheza akiwa England. Na pengine ndio maana alikerwa na kuamua kucheza rafu hadi akapewa kadi nyekundu.

Umiliki mpira.
Tottenham walimiliki mpira sana tangu wakati Liverpool wakiwa 11 kwa 11 jambo ambalo lilikuwa zuri kwao hasa ukizingatia ukweli kuwa Liverpool walijaribu kujaza wachezaji katikati ya kiwanja mapema.

Luka Modric alicheza pasi nyingi sana kuelekea pembeni ya uwanja , na Scot Parker naye alitoa mipira mingi toka chini na Kranjcar aliingia kati ambako mara nyingi alijikuta akiwa kwenye nafasi toka kwenye upande wa kulia pembeni.
Washambuliaji wawili ambao walijenga Patnership nzuri tangu kwenye mchezo wa wiki iliyopita Wolves walikuwa na mchezo mzuri kwa mara nyingine.

Defoe alishuka hadi chini kwa muda mrefu akitoa pasi za akili sana huku Adebayor akifanya kazi kwenye nafasi nafasi ambazo zilikuwa zinajitokeza katikati ya mabeki wa kati wa Liverpool.
Wote walikuwa wakija mpaka katikati ya uwanja wakitoa nafasi ya ziada kwa mtu aliyekuwa na mpira ya kutoa pasina ndio maana wote walimaliza na takwimu nzuri sana za pasi baina yao.
Kitu kilichokuwa kinajirudia kwenye kipindi cha kwanza ilikuwa ni nidhamu mbovu ya wachezaji wa Liverpool. Wachezaji wa Liverpool walikuwa wakicheza rafu zisizo na msingi na walikuwa wakigawa faulo za kizembe sana hasa nje ya eneo lao la hatari na kwenye upande wa kushoto na pia tackling mbovu ziliwazulia matatizo makubwa.

Kitu ambacho kilionekana kuja bila kizuizi ni mchezaji wa Liverpool kuonyeshwa kadi nyekundu na pia hali hii iliwapa Tottenham nafasi ya kupiga mashuti nje ya eneo la hatari kutokana na mipira iliyokufa.

11V10.
Mchezo uliongezeka msisimko baada ya Liverpool kubaki 10 uwanjani baada ya Charlie Adam kuonyeshwa kadi nyekundu . Dalglish aliamua kuwaacha wachezaji waliokuwa uwanjani kama wlaivyo pasipo kufanya mabadiliko yoyote.
Cha kushangaza ni maamuzi ya kumuacha uwanjani Andy Carrol huku akicheza kushoto mwa uwanja .
Labda wazo la Kenny Lilikuwa kumpa wakati mgumu beki Kylie Walker hususana kwenye mipira ya juu lakini Caroll alionekana kutokuwa mchezoni na alikosa nguvu za kumkaba ipasavyo Kylie Walker wakati Liverpool walipokuwa hawana mpira. Kumpanga Suarez pembeni ingekuwa jambo la msingi zaidi au kuwachezesha Craig Bellamy na Dirk Kuyt watu ambao ni wachezaji wa pembeni kiasili. Tottenham walicheza vizuri sana katika hali ya wachezaji 11 kwa 10 ,walimiliki mipira na waliwachosha Liverpool. Japo hawakutengeneza nafasi nyingi za wazi na walilazimika kungoja hadi pale Liverpool walipopungua uwanjani ili kupata bao la pili.

11V 9.

Ni vigumu kujenga hoja kuwa Dalgish angeweza kufanya chochote kuirudisha Liverpool mchezoni . Kushindana ukiwa na wachezaji tisa inawezekana ukiwa uko kwenye matokeo ya 0-0 na unaweza kucheza kwa nguvu na kupata sare lakini Liverpool walikuwa wanataka kurudi mchezoni wakiwa nyuma hivyo haikuwezekana kwao.

Mwisho.

Huu ungeweza kuwa mchezo wa kusisimua sana . Dakika za mwanzo Tottenham walikuwa wakicheza kwa kupiga pasina matatizo ya Charlie Adam yalionekana kuwa matatizo ya Liverpool kwa jumla. Wachezaji wa Liverpool walishindwa kutafuta nafasi za kupitisha mipira . Mbinu ya kucheza kwa klupunguza uwanja inaweza kukupa umiliki wa mpira lakini pia inamaanisha kuwa wapinzani wana hatua chache za kukimbia kuutafuta mpira kwa kuwa uwanja umepunguzwa kwa niaba yao na kazi inakuwa nyepesi. Dalglish alikuwa kwenye wakati mgumu akiwa na wachezaji 10 lakini kumtumia Caroll pembeni ya uwanja ilikuwa maamuzi ya ajabu sana na hayakuwa na faida kwa timu yake –Liverpool haikuweza kupeleka mipira pembeni alikokuwa na Caroll hakuwa na msaada kwenye ukabaji . Liverpool walihitaji kufanya mabadiliko wakati walipobaki 10 ila walipobaki 9 kimsingi mchezo ulikuwa umeisha kwao.

1 comment:

  1. Yaa kwa kweli kwa mnazi wa Liverpool tangu miaka ya 1980's bado msimu huu sina matumaini sana. Ila naamini kwa vile Charlie Adams atakosa mechi zijazo ni wakati wa Dalglish kujaribu mtu mwingine ktk position ile. Pia itasaidia kuja na system mpya na wachezaji tofauti labda tutaona mabadiliko.
    In short, pia goli la 3 nadhani Kipa Reina hakuwa katika kiwango siku ile. Ligi bado changa, ninaamini Manchester United ina uwezo wa kutwaa ubingwa ila Man City, bado, Mancini si meneja wa kupata ubingwa, hajui kubalance team. Line up yake always haina balance, na sioni wakiweza kupata ubingwa. Kwa Arsenal, naamini defence itatulia tu na Gervino atakuwa mchezaji gumzo msimu huu.

    ReplyDelete