Search This Blog

Tuesday, May 14, 2013

BREAKING NEWS: ROBERTO MANCINI ATIMULIWA KUIFUNDISHA MANCHESTER CITY - MSAIDIZI WAKE KUBEBA JAHAZI MPAKA MWISHO MWA MSIMU


Roberto Mancini of Manchester City
Tetesi zilianza kusambaa kuhusu hatma ya kocha wa Manchester City Roberto Mancini hata kabla ya mchezo wa fainali wa FA Cup.
Lakini muda mfupi uliopita kocha huyo wa kitaliano amefukuzwa rasmi kazi ya kuifundisha Manchester City huku Manuel Pellegrini, kocha wa Málaga, akitajwa kuwa yupo mbioni kuchukua nafasi ya muitaliano huyo. 

Hatma ya Mancini ilianza kuonekana kwenye mashaka kufuatiwa kuibuka kwa taarifa huko Spain usiku wa kuamkia siku ya fainali ya FA Cup ambapo City walifungwa na Wigan na siku iliyofuata ilionekana wazi kwamba wamiliki wa timu hiyo kutoka Abu Dhabi wamepoteza imani na kocha huyo. 

Mancini ndio kocha aliyewapa City ubingwa wao wa kwanza tangu mwaka 1968, ametimuliwa baada ya timu yake kukosa kikombe hata kimoja msimu huu huku akifanya vibaya katika michuano ya ulaya 
 
Mwenyekiti wa City Khaldoon Al Mubarakalisema: "Rekodi ya Roberto inaongea yenyewe, amekuwa na wakati mzuri hapa na ameweza kupata mapenzi ya mshabiki na heshima pia.
"Amefanya kazi nzuri na kutuletea makombe.
"Tunamtakia mafanikio mema siku za mbele na tunamshukuru kwa yote aliyotufanyia."

Kocha msaidizi Brian Kidd atachukua nafasi ya Mancini mpaka mwishoni mwa msimu - akimalizia mechi mbili zilizobakia za premier league.

Monday, May 13, 2013

BAADA YA KUMWAGIWA POMBE - FRANCK RIBERY AAPA KUTOONGEA TENA NA JEROME BOATENG

Franck Ribery ameapa kutoongea tena na mchezaji mwenzie wa Bayern Munich Jerome Boateng baada ya kulowanishwa kwa pombe wakati wa wakishangilia ubingwa wa Bundesliga wikiendi iliyopita.

Mfaransa huyo ambaye ni muislamu wa swala tano - alijaribu kukimbia ili aepuke ushangiliaji wa kumwagiana pombe wa wachezaji wenzie baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo walioshinda  3-0 dhidi ya Augsburg.
Lakini pamoja na kujaribu sana kukwepa kuguswa na pombe - ambayo ni haramu kwa dini yake - Ribery hatimaye aliogeshwa na na Boateng.

Akiwa amekasirishwa kabisa kwa kitendo hicho cha mjerumani, winga huyo alisema: ‘Sitoongea tena na Boateng, anajua mie muislam. Nimeudhiwa sana na kitendo chake.’
Mlinzi David Alaba na kiungo Anatoliy Tymoshchuk pia walijiunga na Boateng kumlowesha Ribery, ambaye alionekana kutulia kwa wakati huo.
Golikipa Manuel Neuer kwa busara kabisa yeye alijiepusha na suala hilo na kuamua kuwamwagia baadhi ya mashabiki walionekana kupendezewa na ushangiliaji huyo.

PSG WATHIBITISHA REAL MADRID WAMEPELEKA OFA YA KUMTAKA ANCELOTTI - LAKINI WAMEWAKATALIA

Paris St Germain imekataa ofa ya Real Madrid kutaka kumsaini kocha wao Carlo Ancelotti, raisi w klabu hiyo  Nasser al Khelaifi amesema leo Jumatatu.
"Wao (Real) walikuja na tukajadili suala. Carlo ana mkataba na sisi kwa mwaka mmoja zaidi..... kwangu mimi naamini atakuwa hapa msimu ujao," Al Khelaifi aliiambia Reuters.
"Ni mtu mzuri sana na nina uhakika atauheshimu mkataba wake."
Ancelotti amekataa kuthibitisha kwamba ataendela kubaki PSG jana Jumapili wakati waliposhinda kombe lao la kwanza tangu la Ligue 1 tangu msimu 1994.
"Tutaongea na klabu kuhusu suala hili," alisema muitaliano huyo ambaye alijiunga na klabu hiyo December 2011.
Al Khelaifi alielezea kwamba hana haraka yoyote ya kujadili suala hilo na Ancelotti ambaye amekuwa akihusishwa na kujiunga na Real katika wiki kadhaa zilizopita baada ya vyombo vya habari kusema kwamba Jose Mourinho ataondoka kwenye klabu hiyo ya Spain na kurudi kwenye timu yake ya zamani ya Chelsea.
"Kwa sasa sina mpango wowote wa kukutana nae kwa sababu ana mkataba na klabu. Sasa ni muda wa kusherehekea ubingwa" alisema raisi wa PSG.
Al Khelaifi pia aliongeza anataka kuongeza urefu wa mkataba wa David Beckham baada ya nahodha huyo wa zamani wa England kujiunga na klabu hiyo mwezi January.
"David ni mchezaji wa aina yake, mweledi na mtu mzuri sana. Tunataka kuendelea kuwa nae hapa lakini inategemea na atakachoamua mwenyewe," alisema.
"Ana furaha kuwa hapa, niliongea nae jana na wiki iliyopita na ameonyesha kwamba anaweza akabaki."

KATUNI YA LEO!




TASWIRA YA UWANJA WA SOKOINE JIJINI MBEYA BAADA YA MVUA KUNYESHA.


JASIRI HAACHI ASILI - MARK VAN BOMMEL APEWA KADI NYEKUNDU YA TISA KWENYE MCHEZO WAKE WA MWISHO WA SOKA LA KULIPWA

Waswahili wanasema jasiri haachi asili - ndivyo ilivyotokea kwenye mchezo wa mwisho wa mchezaji Mark Van Bommel, ambaye amedumu kwenye soka kwa misimu 21 huku akiwa anatmbulika kwa mchezo wake wa kutumia nguvu na rafu akiwa na vilabu vya PSV, Barcelona, Bayern Munich na AC Milan.

Kiungo huyo wa Uholanzi, 36, alicheza mechi yake ya 350 ya ligi ya Eredivisie siku jumapili, mechi ambayo PSV walifungwa 3-1 na FC Twente.

Kwenye mchezo huo Van Bommmel alipata kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 70 baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Twente Dusan Tadić, Van Bommel alitangaza kustaafu mara tu baada ya mchezo huo. Hiyo ilikuwa kadi nyekundu ya 9 kwenye maisha yake ya soka la kulipwa.


TWENZETU ndani ya wakazi wa Dodoma,ilikuwa nomaaa...!

PICHA YA SIKU: MBONGO NDANI YA OLD TRAFFORD JANA KUMUAGA SIR ALEX FERGUSON


MESSI AUMIA TENA BARCELONA WAKIICHAPA 2-1 ATLETICO MADRID KUSHEREHEKEA UBINGWA WA LA LIGA

 
 
Atletico Madrid 1-2 Barcelona (All Goals) 12... by ourmatch

VIDEO: SIR ALEX FERGUSON AKITHIBITISHA WAYNE ROONEY KUOMBA KUUZWA

"NILIAMUA KUSTAAFU CHRISTMAS ILIYOPITA BAADA YA KUFIWA NA SHEMEJI YANGU" - FERGIE

Fergie na wajukuu zake
Kocha wa Manchester United amefichua namna alivyoamua kustaafu mapema mwezi Desemba 2012.
Mscotland huyo aliushtua ulimwengu huo jumatano wiki hii kwa kutangaza kwamba ameamua kustaafu mwishoni mwa msimu huu.

Ferguson alisema: “Niliamua kustaafu wakati wa christmas iliyopita. Mambo yalibadilika wakati mke wangu Cathy alipofiwa na dada yake. Alimpoteza rafiki yake kipenzi, ndugu yake. Pia, nilitaka kuondoka nikiwa mshindi. 
“Ilikuwa jambo gumu sana. Tuliwaambia watoto wetu. Kaka yangu hakufahamu lolote mpaka jumanne.
“Kitu muhimu zaidi kilikuwa ni kushinda kombe la kwanza na milango ikafunguka. Tuliendelea kukua na kukua. Tumekuwa na timu nzuri sana kwa muda wote.
“Bado nina vitu vingi vya kufanya. Mtoto wangu Jason amekuwa akipanga vitu vingi. Siwezi kuendelea kukaa tu.

HATIMAYE SIR ALEX FERGUSON ATHIBITISHA WAYNE ROONEY AMEOMBA KUONDOKA KWA MARA PILI - LAKINI AMEKATALIWA OMBI LAKE

Siku kadhaa baada ya kuwepo na tetesi kwamba mchezaji Wayne Rooney ameomba kuondoka Manchester United, hatimaye leo hii ALEX FERGUSON amethibitisha kwamba ni kweli mshambuliaji huyo ameondoka kuuzwa.

Rooney alipeleka maombi yake kwa bosi wake wiki hii akiomba kuuzwa mwishoni mwa msimu huu kwa mara ya pili ndani ya miaka 3.
Lakini akizungumza baada ya mechi ya Swansea Fergie alisema: “Tumelikataa ombi lake. Nadhani anahitaji kwenda mbali kufikiria kwa kina zaidi.
“Hakuwa amefurahishwa kuwa anatolewa nje mara kwa mara msimu huu. Wayne Rooney wa kiwango cha juu hawezi kutolewa nje mara kwa mara.” 
Rooney leo hakuwepo katika kikosi kilichocheza mechi ya mwisho ndani ya Old Trafford msimu huu baada ya kusema kwamba hajisikii kucheza mechi hiyo na anataka kuondoka.

Sunday, May 12, 2013

UKIONA MWENZAKO AMECHUKUA KIJITI USILALAMIKE KWA MEDIA JIPANGE-MRISHO MPOTO.

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA NDANI YA DODOMA KATIKA UZINDUZI MPYA WA CLOUDS FM

 

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Snura akiimba jukwaani wimbo wake unaotamba kwa sasa katika vituo vingi vya redio,uitwao Majanga,mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uwanja wa Jamuhuiri jioni ya leo wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM ilipokuwa ikizindua msimu wake mpya kwa wasikilizaji wake,uzinduzi huo ulikwenda sambamba na kufanyika kwa semina ya fursa kwa Watanzania.

Aidha msimu huo umekwenda sambamba na kaulimbiu inayofuatia harakati za MADE IN TANZANIA,ambapo msukumo wake ni kuwashawishi Watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa hizo kwa umoja wa maendeleo,huku neno TWENZETU likitumika kama neno rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi uzinduzi huo utabeba harakati rasmi za vita dhidi ya Uharamia wa kazi za wasanii,Wabunifu na wavumbuzi mbalimbali.Kesho kutakuwepo na matembezi ya kampeni ya kupinda uharamia wa kazi za sanii yatakayoanzia uwanja wa Jamuhuri mapema asubuhi na kupolewa na Waziri Mkuu Mh. Pinda.
 Msanii mahiri wa Mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akiwakuna vilivyo wakazi wa mji wa Dodoma jioni ya leo.alipowaangushia maneno kadhaa na umati kulipukw ana mayowe kila kona,ambapo Clouds FM wamezindua msimu wao mpya.
 Maelfu ya Watu wakiwa ndani ya uwanja wa jamuhuri jioni ya leo wakijumuika kwa pamoja na wana Clouds FM walipokuwa wakizindua msimu wao mpya.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop,Izzo Bizziness akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Madee akitumbuiza mbele ya umati mkubwa wa watu ndani ya uwanja wa jamuhuri,wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM kilipokuwa kikizindua msimu wake mpya.
Pichani shoto ni Mkurugenzi wa vipindi na Utafiti,Ruge Mutahaba akizungumza na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ndani ya Uwanja wa Jamuhuri jioni ya leo,wakati tamasha la uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM likiendelea,Nape alifika uwanjani hapo kujionea shamrashamra mbalimbali zilizojumuisha maelfu ya watu.
 Palikuwa hapatoshi uwanja wa jamuhuri Dodoma jioni ya leo.

Shaffih Dauda akicheza kiduku


  Msanii wa mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop,Afande Sele a.k.a Baba Tunda  akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.











INTERVIEW YA PAUL SCHOLES AKIHOJIWA NA GARY NEVILLE KUHUSU KUSTAAFU KUICHEZEA MAN UNITED

REAL MADRID WATOA SARE NA ESPANYOL - BARCELONA BINGWA MPYA LA LIGA


Espanyol 1-1 Real Madrid by fasthighlights-2012

WIGAN WAIDHALILISHA MAN CITY - WAIPIGA 1-0 NA KUBEBA UBINGWA WA FA


w1-0mc Footyroom.com by Futbol2101

BAADA YA FERGUSON SASA NI ZAMU SCHOLES: NAE ATANGAZA KUSTAAFU KUICHEZEA MAN UNITED



Wiki hii imeendelea kuwa mbaya kwa mashabiki wa Manchester United, siku chache baada ya Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu, leo hii kiungo wa timu hiyo Paul Scholes nae ameamua kumfuata kocha wake kwa kutundika daluga kuitumikia klabu yake pekee katika soka la kulipwa.

Gwiji huyo wa Manchester United mwanzoni alistaafu wakati wa mwisho mwa msimu wa 2010/2011, lakini akaamua kubadili maamuzi na kurejea kwenye timu mwezi January mwaka jana. 
 
Katika taarifa yake Scholes, 38, alisema:Hatimaye ninatundika daluga zangu kabisa!
"Kucheza soka ndio ilikuwa kila kitu kwangu, na kuwa na na mafanikio kwa muda mrefu kwenye soka ndani ya Manchester United, chini ya meneja bora kabisa wa muda wote, ni heshima kubwa. 

“Timu ipo kwenye hali nzuri na itaendelea kufanikiwa chini ya uongozi wa David Moyes.”
  Scholes amecheza zaidi ya mechi 700 akiwa na jezi ya United na kesho atakusanya medali yake ya 11 ya kombe la premier league watakapocheza dhidi ya Swansea.