Paris St Germain imekataa ofa ya Real Madrid kutaka kumsaini kocha wao Carlo
Ancelotti, raisi w klabu hiyo Nasser al Khelaifi amesema leo Jumatatu.
"Wao (Real) walikuja na tukajadili suala. Carlo ana mkataba na sisi kwa mwaka mmoja zaidi..... kwangu mimi naamini atakuwa hapa msimu ujao," Al Khelaifi aliiambia
Reuters.
"Ni mtu mzuri sana na nina uhakika atauheshimu mkataba wake."
Ancelotti amekataa kuthibitisha kwamba ataendela kubaki PSG jana Jumapili wakati waliposhinda kombe lao la kwanza tangu la Ligue 1 tangu msimu 1994.
"Tutaongea na klabu kuhusu suala hili," alisema muitaliano huyo ambaye alijiunga na klabu hiyo December 2011.
Al Khelaifi alielezea kwamba hana haraka yoyote ya kujadili suala hilo na Ancelotti ambaye amekuwa akihusishwa na kujiunga na Real katika wiki kadhaa zilizopita baada ya vyombo vya habari kusema kwamba Jose Mourinho ataondoka kwenye klabu hiyo ya Spain na kurudi kwenye timu yake ya zamani ya Chelsea.
"Kwa sasa sina mpango wowote wa kukutana nae kwa sababu ana mkataba na klabu. Sasa ni muda wa kusherehekea ubingwa" alisema raisi wa PSG.
Al Khelaifi pia aliongeza anataka kuongeza urefu wa mkataba wa David Beckham baada ya nahodha huyo wa zamani wa England kujiunga na klabu hiyo mwezi January.
"David ni mchezaji wa aina yake, mweledi na mtu mzuri sana. Tunataka kuendelea kuwa nae hapa lakini inategemea na atakachoamua mwenyewe," alisema.
"Ana furaha kuwa hapa, niliongea nae jana na wiki iliyopita na ameonyesha kwamba anaweza akabaki."
No comments:
Post a Comment