Franck Ribery ameapa kutoongea tena na mchezaji mwenzie wa Bayern Munich Jerome Boateng baada ya kulowanishwa kwa pombe wakati wa wakishangilia ubingwa wa Bundesliga wikiendi iliyopita.
Mfaransa huyo ambaye ni muislamu wa swala tano - alijaribu kukimbia ili aepuke ushangiliaji wa kumwagiana pombe wa wachezaji wenzie baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo walioshinda 3-0 dhidi ya Augsburg.
Lakini pamoja na kujaribu sana kukwepa kuguswa na pombe - ambayo ni haramu kwa dini yake - Ribery hatimaye aliogeshwa na na Boateng.
Akiwa amekasirishwa kabisa kwa kitendo hicho cha mjerumani, winga huyo alisema: ‘Sitoongea tena na Boateng, anajua mie muislam. Nimeudhiwa sana na kitendo chake.’
Mlinzi David Alaba na kiungo Anatoliy Tymoshchuk
pia walijiunga na Boateng kumlowesha Ribery, ambaye alionekana kutulia kwa wakati huo.
Golikipa Manuel Neuer kwa busara kabisa yeye alijiepusha na suala hilo na kuamua kuwamwagia baadhi ya mashabiki walionekana kupendezewa na ushangiliaji huyo.
duu!!!pole ustadh ribery
ReplyDeletekweli
ReplyDelete