Siku kadhaa baada ya kuwepo na tetesi kwamba mchezaji Wayne Rooney ameomba kuondoka Manchester United, hatimaye leo hii ALEX FERGUSON amethibitisha kwamba ni kweli mshambuliaji huyo ameondoka kuuzwa.
Rooney alipeleka maombi yake kwa bosi wake wiki hii akiomba kuuzwa mwishoni mwa msimu huu kwa mara ya pili ndani ya miaka 3.Lakini akizungumza baada ya mechi ya Swansea Fergie alisema: “Tumelikataa ombi lake. Nadhani anahitaji kwenda mbali kufikiria kwa kina zaidi.
“Hakuwa amefurahishwa kuwa anatolewa nje mara kwa mara msimu huu. Wayne Rooney wa kiwango cha juu hawezi kutolewa nje mara kwa mara.”
Rooney leo hakuwepo katika kikosi kilichocheza mechi ya mwisho ndani ya Old Trafford msimu huu baada ya kusema kwamba hajisikii kucheza mechi hiyo na anataka kuondoka.
No comments:
Post a Comment