Fergie na wajukuu zake |
Mscotland huyo aliushtua ulimwengu huo jumatano wiki hii kwa kutangaza kwamba ameamua kustaafu mwishoni mwa msimu huu.
Ferguson alisema: “Niliamua kustaafu wakati wa christmas iliyopita. Mambo yalibadilika wakati mke wangu Cathy alipofiwa na dada yake. Alimpoteza rafiki yake kipenzi, ndugu yake. Pia, nilitaka kuondoka nikiwa mshindi.
“Ilikuwa jambo gumu sana. Tuliwaambia watoto wetu. Kaka yangu hakufahamu lolote mpaka jumanne.
“Kitu muhimu zaidi kilikuwa ni kushinda kombe la kwanza na milango ikafunguka. Tuliendelea kukua na kukua. Tumekuwa na timu nzuri sana kwa muda wote.
“Bado nina vitu vingi vya kufanya. Mtoto wangu Jason amekuwa akipanga vitu vingi. Siwezi kuendelea kukaa tu.”
No comments:
Post a Comment