Search This Blog

Tuesday, January 22, 2013

UCHAGUZI TFF: HAWA NDIO WALIOMBA KUGOMBEA TAYARI KWA PINGAMIZI


Shaffih Dauda mmoja ya watu waliomba kuchaguliwa kwenye uchaguzi wa TFF


1. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepitia Fomu za waombaji uongozi wa TFF na kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 11 (1), (2) na (3), waombaji uongozi wafuatao majina yao na nafasi wanazoomba kugombea yanawekwa wazi kutoa fursa kwa wale wote wenye pingamizi kwa nini mwombaji aliyetajwa hapa chini asiteuliwe kugombea nafasi aliyoomba, wawasilishe pingamizi zao kwa Katibu Mkuu wa TFF, kuanzia tarehe 22 Januari 2013 hadi tarehe 26 Januari 2013 saa 10.00 jioni.


2. Pingamizi sharti liwe kwa maandishi, lieleze kwa uwazi sababu za pingamizi, liambatanishwe na ushahidi wa pingamizi, liwe na jina kamili la mtoa pingamizi, anwani ya kudumu na saini yake.

NAFASI
S/No.
JINA

RAIS WA TFF


1.
Athumani Jumanne Nyamlani
2.
Jamal Emily Malinzi
3.
Omary Mussa Nkwarulo

MAKAMU WA RAIS WA TFF


1.
Michael Richard Wambura
2.
Ramadhan Omar Nassib           
3.
Wallace Karia


MJUMBE WA KAMATI YA
UTENDAJI –
Kanda ya 1 (Kagera, Geita)
1.
Abdallah Hussein Musa 
2.
Kalilo Samson
3.
Salum Hamis Umande Chama


Kanda ya 2 (Mwanza, Mara)
1.
Jumbe Oddessa Magati
2.
Mugisha Galibona
3.
Samuel Nyala
4.
Vedastus F.K Lufano


Kanda ya 3 (Shinyanga, Simiyu)
1.
Epaphra Swai
2.
Mbasha Matutu


Kanda ya 4 (Arusha, Manyara)
1.
Charles Mugondo
2.
Elley Simon Mbise
3.
Omary Walii Ali 


Kanda ya 5 (Tabora, Kigoma)
1.
Ahmed Idd Mgoyi
2.
Yusuf Hamis Kitumbo


Kanda ya 6 (Rukwa, Katavi)
1.
Ayubu Nyaulingo
2.
Blassy Mghube Kiondo
3
Nazarius A.M Kilungeja 
4.
Seleman Bandiho Kameya


Kanda ya 7 (Iringa, Mbeya)
1.
David Samson Lugenge
2.
Eliud Peter Mvella
3.
John Exavery M. Kiteve
4.
Lusekelo E. Mwanjala


Kanda ya 8 (Ruvuma, Njombe)
1.
James Patrick Mhagama
2.
Stanley W. D Lugenge


Kanda ya 9 (Mtwara, Lindi)
1.
Athuman Kingome Kambi
2.
Francis Kumba Ndulane
3.
Zafarani Mzee Damoder


Kanda ya 10 (Dodoma,  Singida)
1.
Hussein Zuberi Mwamba
2.
Stewart Ernest Masima


Kanda ya 11 (Morogoro, Pwani)
1.
Farid Nahdi
2.
Hassan Othuman Hassan
3.
Riziki Juma Majala
4.
Twahil Twaha Njoki


Kanda ya 12 (Kilimanjaro, Tanga)
1.
Davis Elisa Mosha
2.
Khalid Abdallah Mohamed
3.
Kusianga Mohamed Kiata


Kanda ya 13 (Dar es salaam)
1.
Alex Crispine Kamuzelya
2.
Juma Abbas Pinto
3.
Muhsin Said Balhabou   
4.
Omary Isack Abdulkadir
5.
Shafii Kajuna Dauda
3.                   Waombaji uongozi wafuatao  wameondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi:

(i)                   Richard Julius Rukambura; Amevunja Kanuni za Uchaguzi  za TFF Ibara ya 10(8) kwa kuomba nafasi  mbili za Rais na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kwenye uchaguzi  wa TFF.
(ii)                 Titus Osoro; Amejitoa kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.

UCHAGUZI WA TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD
(TPL BOARD)

1.                   Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepitia Fomu za waombaji uongozi wa TPL Board na kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 11(1), (2) na (3), waombaji uongozi wafuatao majina yao na nafasi wanazoomba kugombea yanawekwa wazi kutoa fursa kwa wale wote wenye pingamizi kwa nini mwombaji aliyetajwa hapa chini asiteuliwe kugombea nafasi aliyoomba, wawasilishe pingamizi zao kwa Katibu  Mkuu wa TFF, kuanzia tarehe 22 Januari 2013 hadi tarehe 26 Januari 2013 saa 10.00 jioni.

2.    Pingamizi sharti liwe kwa maandishi, lieleze kwa uwazi sababu za pingamizi, liambatanishwe na ushahidi wa pingamizi, liwe na jina kamili la mtoa pingamizi, anwani ya kudumu na saini yake.



NAFASI INAYOGOMBEWA
S/No.
JINA

MWENYEKITI WA TPL BOARD


1.
Hamad Yahya Juma
2.
Yusufali Manji


MAKAMU MWENYEKITI WA TPL BOARD
1.
Said Mohamed 



MJUMBE –KAMATI YA UENDESHAJI (Management Committee)
1.
Christopher Peter Lukombe

2.
Kazimoto Miraji Muzo

3.
Omary Khatibu Mwindadi

YANGA YAWASILI SALAMA MWANZA TAYARI KUWANYOOSHA WASAUZI KESHO KIRUMBA


Baadhi ya wachezaji wa timu ya Young Africans wakisubiri usafiri wa ndani ya Uwanja wa ndege Mwanza uweze kuwachukua baada ya kushuka kwenye ndege leo asubuhi


Timu Young Africans Sports Club tayari imewasili salama jijini Mwanza asubuhi ya leo tayari kabisa kwa mchezo wake wa kirafiki hapo kesho dhidi ya timu ya Black Leopard kutoka nchini Afrika Kusini mchezo utakaochezwa katika dimba la Uwanja wa CCM Kirumba majira ya saa 10 jioni.
Msafara wa watu 37, wachezaji 27 na viongozi 10 uliwasili majira ya saa 2 kamili asubuhi kwa shirika la ndge la Fast Jet ambapo leo jioni timu inatarajiwa kufanya mazoezi mepesi katika Uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya mchezo wa kesho.
Young Africans inacheza mchezo huo wa marudiano dhidi ya timu ya Black Leopard ikiwa ni mchezo wa pili wa kirafiki wa kujipima uwezo kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom mwishoni mwa wiki.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mwishoni wa wiki,Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Black Leopard huku mabao yake yakifungwa na Jerson Tegete mawili na Frank Domayo.
Black Leopard amabyo inajiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya PSL nchini Afrika Kusini iliomba kupata mchezo mwingine wa kirafiki ambapo kampuni ya Prime Time Promotions walioandaa ziara ya timu hii walikubaliana na Yanga mchezo huu ufanyike jijini Mwanza ili kutoa fursa kwa wakazi wa kanda ya ziwa kuweza kupata burudani ya soka kutoka kwa timu hizi mbili.
Viiongillio vya mnchezo ni Tsh 10,000/= kwa Jukwaa Kuu na Tsh 3,500/= kwa mzunguko.

Monday, January 21, 2013

ZAMBIA YATOLEWA JASHO NA ETHIOPIA - ANGALIA HIGHLIGHTS


Mabingwa watatezi wa kombe la mataifa ya Afrika Chipolopolo ya Zambia wameanza kampeni ya kutetea kombe hilo waliloshinda mwaka uliopita kwa kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya Kundi C nchini Afrika Kusini.
Kinyume na matarajio ya wengi Ethiopia ilionyesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo na mara nyingi wachezaji wake wakionekana kuwathibiti wachezaji wa Chipolopolo.
Kwa mara nyingine tena timu hiyo ya Zambia, imeonyesha kuwa kwa sasa haipo katika hali nzuri kama ilivyokuwa mwaka uliopita.
Wakati wa mechi hiyo beki wake Chisamba Lungu alimuangusha mshambulizi wa Ethiopia Saladin Seid, kwenye eneo la hatari na bila kusita refa wa mechi hiyo akatoa adhabu ya penalti.
Lakini kipa wa Zambia Kennedy Mweene aliokoa mkwaju uliopigwa na Seid na hivyoi kufufua matumaini ya mabingwa hao watatezi.
Dakika chache baadaye, kipa wa Ethiopia, Jemal Tassew alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Chisamba Lungu.
Licha ya kuwa alikuwa akiondolewa uwanjani kwa machela refa wa mechi hiyo alimpa kipa huyo kadi nyekundu kutokana na mchezo mbaya na hatari aliouonyesha.
Dakika chache baada ya tukio hilo mabingwa hao watetezi wakafunga bao lao la kwanza kupitia kwa mchezaji Collins Mbesuma kunako dakika ya 45 kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili licha ya kucheza wachezaji kumi pekee kwa muda mrefu, Ethiopia ilisawazisha kunako dakika ya 65 kupitia kwa mchezaji Adane Girma.
Ithiopia ilithibiti mpira wa asilimia kubwa katika kipindi cha pili na hivyo kuzima matumaini ya mabingwa hao watatezi.
Mechi hiyo ilimalizika huku timu hizo mbili zikitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja.

SIMBA YANG'ARA OMAN YAITANDIKA 2-1 ALHI SIDAB

Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ahli Sidab ya daraja la kwanza hapa Oman. Wenyeji hao walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mbrazil, Lopez lakini Kiggi Makasi akasawazisha na kipindi cha pili Amri Kiemba akapachika bao la pili...Wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza Boban, Mwinyi na Kazimoto walikuwa nje, Sunzu hakucheza, pia Abel Dhaira....
Baada ya mechi, mdhamini wa safari hiyo hapa Oman, Rahma Al Kharusi aliwapongeza wachezaji na benchi la ufundi na kuahidi kuja kuzungumza nao Jumatatu mchana na kula nao chakula cha mchana. Kambi ya Simba inafikia tamati keshokutwa Jumatano...



Kocha wa Simba Patrick Leiwing akisalimiana na mdhamini wa safari ya Simba nchini Oman Rahma Al Kharusi



BAADA YA KUWANYOOSHA WASAUZI DAR - YANGA KURUDIANA NAO MWANZA JUMATANO



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Timu ya Young Africans Sports Club kesho alfajiri inatarajiwa kusafiri kuelekea jijini Mwanza ambapo siku ya jumatano itacheza mchezo wa kirafiki wa marudiano dhidi ya timu ya Black leopard kutoka nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa CCM Kirumba.
 
Mchezo huo wa jumatano utakua ni fursa kwa wakazi, wapenzi wa soka wa kanda ya ziwa kuweza kuiona timu yao kwani tangu irejee nchini kutoka Uturuki imecheza mchezo mmoja tu wa kirafiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hivyo ni fursa nzuri kwa wapenzi wa soka kanda ziwa kuiona timu yao.
 
Katika mchezo wa kwanza Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Black leopard huku mabao ya Yanga yakifungwa na Jerson Tegete mabao mawili na Frank Domayo akifunga bao moja na pia kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
 
Kocha Mkuu Ernest aliomba kupata michezo miwili ya kirafiki kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa wikii hii katika viwanja tofauti, Yanga ikianza na timu ya Prisons siku ya jumapili.
 
Aidha Black Leopard ambayo iko nchini Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini Afrika kusini PSL imesifia mchezo wa juzi dhidi ya Yanga na kusema ulikuwa mchezo mzuri na wakuvutia japokuwa walifungwa, lakini watajitahid kupata ushindi katika mchezo wao wa marudiano siku ya jumamosi.
 
Young Africans ambayo itatumia mchezo huo kama maandalizi yake ya mwisho, itaondoka kesho alfajiri na msafara wa watu 37, wachezaji 27, benchi la ufundi 7 na viongozi 3. 
 
Timu itarejea Dar es salaam siku ya alhamis jion tayari kabisa kwa kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa ligi Kuu ya Vodacpm dhidi ya timu ya Prisons ya Mbeya.
 
Kuhusu viingilo vya mchezo huo ni vitakua ni Jukwaa Kuu Tshs 10,000/=,  na mzunguko Tshs 3,500/= (source: http://www.youngafricans.co.tz)

ALLIANCE AUTOS YASAIDIA TIMU YA DAR LEOPARDS RUGBY CLUB

Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja akikabidhi jezi kwa timu mchezo wa raga (Rugby) ya Dar Leopards jijini Dar es Salaam. Anayepokea ni Mwenyekiti wa Dar Leopards Rugby Club,Bw. Phillippe Poinsot. Minja amesema kuwa wameamua kuunga mkono mchezo wa raga(Rugby) kwani ni miongoni mwa michezo iliyosahaulika nchini. Alliance Auto wameshirikiana na HSE Solutions kudhamini jezi Dar Leopards Club. Wanaoshuhudia tukio hilo ni baadhi wachezaji wa Dar Leopards Rugby Club.

Kocha wa timu ya Dar Leopards Rugby Club Bw. Jonathan Taylor (kushoto) akipozi na baadhi ya wachezaji wa Club hiyo huku wakiwa wamevalia jezi hizo.

Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Dar Leopards Rugby Club,Bw. Phillippe Poinsot.

Kocha wa timu ya Dar Leopards Rugby Club Bw. Jonathan Taylor akipozi na baadhi ya wachezaji wa Club hiyo kwenye moja ya Brand ya magari ya Alliance Autos aina ya 'Volks Wagon AMAROK' huku wakiwa wamevalia Jezi walizokabidhiwa leo katika makao makuu ya kampuni hiyo.

ZAIDI YA MILLION 31.9 ZAGHARAMIA VIFAA LIGI YA MOHAMMED DEWJI, SINGIDA

Mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa tawi la Mitunduruni.

Foleni ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa kuanza Januari 20 mwaka huu.

Baadhi ya wa viongozi ngazi za matawi jimbo la Singida mjini,wakimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida, Hamisi Nguli (hayupo kwenye picha) wakati akitoa nasaha zake muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo.

Baadhi ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa soka jimboni kwake. (Picha zote na Nathaniel Limu).

Mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9 vitakavyotumika kwenye ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi januari 20 mwaka huu.

Vifaa hivyo ni pamoja na jezi pea 854,mipira 122,soksi pea 854 na cloves za magolikipa 61.Vifaa hivyo ni kwa ajili ya timu zitakazoshiriki ligi ngazi ya kitongoji katika jimbo la Singida mjini.Baada ya ligi hiyo,itafuatwa na ligi ngazi ya kata ambayo atakuwa na vifaa vyake pia.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli amepongeza mbunge Dewji kwa kuendelea kutoa misaada mikubwa mbalimbali katika jimbo lake kwa lengo la kuendeleza wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.

“Dewji toka awe mbunge wa jimbo la Singida mjini,siku zote yupo karibu zaidi na vijana. Amewasaidia mambo mengi makubwa ikiwemo kuwaendeleza kimichezo na pia ametoa pikipiki kwa ajili ya vijana wa bodaboda watakaojiunga katika vikundi”,alisema.

Awali msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni mwendelezo wa Dewji kuhakikisha vijana wanatumia michezo kujiendeleza kimaisha.

HATIMAYE KIJANA ALIYETEMBEA KWA MIGUU KUTOKA MORO MPAKA DAR AJIUNGA NA AZAM ACADEMY

Hapa nikiwa na kijana Juma Omary baada ya kufanikiwa kujiunga na Azam Academy. Juma ni kijana ambaye ametokea Mpanda kuja jijini Dar es Salaam kuweza kutimiza ndoto yake ya kwenda kucheza soka la kulipwa barani ulaya. Shukrani sana kwa uongozi wa Azam kwa kuweza kukubali ombi la kipindi bora cha michezo Sports Extra na kumpokea kijana huyu ili aweze kutimiza malengo yake, Azam inampatia mahitaji yote muhimu Juma Omary huku ikimfunza vizuri soka katika kituo chake cha soka kilichopo Chamazi Complex.

LAMPARD NA MATA WAIADHIBU ARSENAL LIGI KUU YA ENGLAND


تشيلسي 2 - 1 آرسنال by kooralive

CLINT DEMPSEY AOKOA JAHAZI LA SPURS KUZAMA DHIDI YA MAN UNITED


توتنهام 1 : 1 مانشستر يونايتد by kooralive

RONALDO, HIGUAIN, DI MARIA WANG'ARA MADRID IKIIUA 5-0 VALENCIA


فالنسيا 0 : 5 ريال مدريد by kooralive

MJADALA: JE ROONEY ALICHEZEWA FAULO KWELI AU ALIJIRUSHA ??

iwF8L3mw9STHf GIF: Wayne Rooney penalty shout (or dive?) v Spurs

OFFICIAL: WESLEY SNEIJDER NDANI YA UZI WA GALATASARY


SEYDOU KEITA AIPA MALI USHINDI WA DAKIKA ZA MWISHO DHIDI YA NIGER


Mali inayopewa nafasi ya kusonga katika hatua ya makundi, ya michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika, mwaka huu, imeandikisha ushindi wake wa kwanza katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Niger.
Mali iliilaza Niger bao moja kwa bila katika mechi hiyo ya pili ya kundi B.
Seydou Keita, nahodha wa timu ya Mali, alifunga bao hilo la ushindi katika dakika ya 84 baada ya mlinda mlango wa Niger, Daouda Kassaly, kuutema mpira wa adhabu na kumfikia mfungaji.
Kwa matokeo hayo Mali, sasa inaongoza kundi B ikiwa na pointi tatu na goli moja.
Timu za DRC na Ghana zinafuatia katika msimamo wa kundi B, zikiwa na pointi moja kila moja baada ya timu hizo mbili kutoshana nguvu ya kufunga magoli mawili kwa mawili.
Hapo kesho mechi za kundi C, zinaanza huku mabingwa watetezi Zambia wakimenyana na Ethiopia, nayo Nigeria ikivaana na Burkina Faso.

TRESOR MPUTU AIONGOZA CONGO KUISHANGAZA GHANA MATAIFA HURU YA AFRIKA

Hatimaye michuano ya Fainali za Kombe la Afrika, AFCON inayofanyika nchini Afrika Kusini imeanza kuzaa magoli. Mechi ya kwanza ya kundi B kati ya Ghana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, imemalizika kwa kufungana magoli 2-2.

Ghana ilianza kufunga kupitia kwa Emmanuel Agyemang Badu katika dakika ya 40. Kipindi cha pili kilianza kwa Ghana tena kuongeza goli la pili likifungwa na Kwadwo Asamoah katika dakika ya 49.
Tresor Mputu ambaye ni ni nahodha wa timu ya DRC alifunga bao la kwanza katika dakika ya 53. Goli la pili la DRC limepatikana kwa njia ya mkwaju wa penalti ukifungwa na Dieumerci Mbokani dakika ya 69. Kwa matokeo hayo timu hizo zimegawana pointi moja moja.
Mechi ya pili ya kundi B inazikutanisha Mali na Niger.

Sunday, January 20, 2013

MKUTANO MKUU WA YANGA WAMALIZIKA SALAMA JIJINI DAR - UONGOZI WAAHIDI MAKUBWA JANGWANI


Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji (katikati) akielezea jambo mbele ya wanachama waliohudhuria mkutano mkuu leo katika Ukumbi wa bwalo la Polisi - Oysterbay , Lawrence Mwalusako katibu mkuu (kushoto) na Clement Sanga makamu mwenyekiti (kulia)
Klabu ya Young Africans Sports Club leo imefanya mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi eneo la Oysterbay, huku mkutano huo ukiendeshwa kisasa kwa kuonyeshwa moja kwa moja (live) na kituo cha Luninga cha Clouds nchini kote.
Mkutano ulianza majira ya saa 5 kasoro, huku wanachama wakijitokeza kwa wingi katika mkutano huo ambao ulikuwa haujafanyika kwa kipindi kirefu katika Klabu ya Yanga.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji alifugua mkutano kisha makamu mwenyekiti aliongoza sara kwa upande wa wakristo na mzee Ibrahim Akilimali alisoma dua kwa upande wa dini ya Kiisalamu.
Katika mkutano huo wanachama wameridhia kuongezewa muda wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mama Fatma Karume na Francis Kifukwe huku wanachama wakipitisha majina ya Captain George Mkuchika na Balozi Ameir Mpumbwe kuwa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini.
Uongozi unaandaa taratibu nzuri kwa kadi za uanachama na kwa sasa wapo katika maongezi na baadhi ya taasisi za fedha ili waweze kufanya hivyo, pia katiba inabidi iboreshwe na mkutano mkuu wa wanachama uwe kila baada ya miezi sita (6) badala ya miezi mitatu (3) y ahivi sasa.
Ifuatayo ni vipengele ambavyo wanachama wamevipisha katika mkutano wa leo;
Katiba - Uchaguzi mgombea nafasi ya mwenyekiti awe namgombea mwenza ili wapate fursa ya kutekeleza mipango/malengo kwa pamoja, tofauti na sasa ambapo kila mgombea anakuwa na mawazo na malengo yake.
Pia Mwneyekiti na makamu mwenyekiti watakua na fursa ya kuchagua wajumbe wa kamati ya utendaji kulingana na mahitaji ya kipindi hicho.

Ujenzi wa Uwanja - Kamati ya utendaji inaendelea na mchakato wa kutafuta njia ya kuweza kupata pesa ya kujenga uwanja na eneo la mafia

Mkadirio ya uwanja ni bli 32, ambapo uwanja utakua na uwezo wa kubeba watu elfu arobaini (40,000) ukiwa na eneo la kuegeshea magari na huduma zote za muhimu katika viwanja vya michezo.
Makamu mwenyekiti alipata fursa ya kuwaonyesha wanachama ramani na michoro ya uwanja mpya unaontarajiwa kuanza ujenzi wake mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu, ambapo uwanja unatazamiwa kujengwa kwa kipindi cha miaka miwili na kampuni ya ujenzi ya BCCG iliyojenga uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Aidha katika mkutano huo Mwesigwa Selestine, Lousi Sendeu na Godwin Muganyizi wamefutiwa uanachama baada ya kuwa wamefungua kesi za madai dhidi ya klabu yao ya Young Africans. 
Manji alisema pia kuahitajika maboresho katika baadhi ya mikataba kama ya TBL, Push Mobile, Pecha (kalenda) na vifaa vya Yanga (jezi,kofia,kalamu,skafu,suaruali za mazoezi nk) ili viweze kuisadia klabu kuweza kujiendesha kulingana na kipato kinachopatikana.
Katika kitengo cha fedha kuna madeni ambayo Yanga inadaiwa na uongozi bado unahitaji kuyafuatilia ili kuweza kujua uhalali wa madeni hayo:
(i)Cross Road - U$1600 (gharama ya ndege kutoka Zambia)
(ii)Holiday Dreamer - U$ 5079 (gharama za ndege kwenda Cairo) 
(iii)Mwesigwa Selestine - milioni 183.4
(iv)Louis Sendeu - milioni 79 
Pia kuna fedha ambazo zimetumika bila ya idhini ya kamati ya utendaji millioni 288 hazina maelezo, milioni 85.6 bila ya idhini ya kamati ya utendaji na milioni 8.6 hazina ushaidi wa matumizi. 
Mwisho Uongozi uliweza kutoa vyeti vya utambuzi kwa baadhi ya wanachama na wachezaji/viongozi kwa mchango wao katika Klabu ya Yanga, waliopewa vyeti hivyo ni:
1.Abdallah Bin Kleb - kongozi anayejitolea sana katika kuhakikisha timu inafanya vizuri na kushinda michezo inayoikabili
2.Shadrack Nsajigwa - mchezaji aliyechezea Yanga kwa muda mrefu (barua na fedha taslimu tsh 1,000,000/=) 
3.Mahmoud Momar - (mtunza vifaa) mfanyakazi wa siku nyingi katika benchi la ufundi (barua na fedha taslimu tsh 1,000,000/=)
4.Stephen Samuel - mwanachama bora na mwenye uchungu na timu ya Yanga (barua na zawadi ya pikipiki mpya)
5.Hayati Isamail Rashid - mwanachama aliyesaidia kupatikana kwa muafaka (barua)
Mwiesho mwenyekiti alifunga mkutano kwa kuwashukuru wanachama wote waliojitokeza katika mkutano huo wa leo, ambapo wanachama waliouhudhuria mkutano ni 1440 huku mkutano ukiendeshwa kwa masaa matatu tu (live) moja kwa moja na kituo cha runinga cha Clouds Tv ambayo kupitia kampuni yake ya Prime Time Promotions ndio walikuwa waandaji wa mkutano huo.

VIDEO: DAVID SILVA ON FIRE MAN CITY WAKIPUNGUZA PENGO LA POINTI NYUMA MAN UNITED


Manchester City vs Fulham 2:0 GOALS HIGHLIGHTS by UCL2410

VIDEO: BARCELONA WAPIGWA KWA MARA YA KWANZA KWENYE LA LIGA MSIMU HUU


Real Sociedad 3-2 Barcelona 19.01... by ourmatch

LUIS SUAREZ, GERRARD NA STURRIDGE WAIONGOZA LIVERPOOL KUIFANYIA MAUJI NORWICH



L5-0N by ourmatch