Search This Blog

Monday, January 21, 2013

HATIMAYE KIJANA ALIYETEMBEA KWA MIGUU KUTOKA MORO MPAKA DAR AJIUNGA NA AZAM ACADEMY

Hapa nikiwa na kijana Juma Omary baada ya kufanikiwa kujiunga na Azam Academy. Juma ni kijana ambaye ametokea Mpanda kuja jijini Dar es Salaam kuweza kutimiza ndoto yake ya kwenda kucheza soka la kulipwa barani ulaya. Shukrani sana kwa uongozi wa Azam kwa kuweza kukubali ombi la kipindi bora cha michezo Sports Extra na kumpokea kijana huyu ili aweze kutimiza malengo yake, Azam inampatia mahitaji yote muhimu Juma Omary huku ikimfunza vizuri soka katika kituo chake cha soka kilichopo Chamazi Complex.

12 comments:

  1. bigup Shaffih kwa kujali wengine

    ReplyDelete
  2. Kijana kweli ana nia na Inshaallah atafanikiwa,(Penye nia pana njia).. that's what we say 'determaination'.

    Hongera sana kaka Shaffih, hongera Sports Extra, hongera clouds fm.

    Mohamed de Bebeto.

    ReplyDelete
  3. hongera kwake kwa kupigania ndoto yake, na pia kwako kwa kumsaidia kufikia kufikia malengo naamini atafanikiwa kwani hata kina eto'o walianzia huko huko

    ReplyDelete
  4. kweli hiyo ni radio ya watu, big up sana

    ReplyDelete
  5. hongera sana shaffih, na sports xtra kwa ujumla kwa kumsaidia kija Juma,basi kazi ibaki kwake sas!!

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Shaffih na Sports Xtra kwa ujumla kwa kuweza kusaidia kijana Juma Omary,basi kazi ibaki kwake sasa kuweza kutimiza ndoto zake!!

    ReplyDelete
  7. Napenda kuwapa pongezi timu ya azam japo kuwa mimi ni mpenzi wa simba kwa huyu kijana.kwa kweli ni jambo laa mendeleo kwa nchi yetu hii kwa kusaidia vijana wa taifa lA kesho

    ReplyDelete
  8. mungu azidi kukuzidishia shaffih kwa moyo wako wa kuwajali watanzania wenzako walio maskini na kutimiza ndoto zao wish you luck!!

    ReplyDelete
  9. huyu ameonyesha nia ya dhati,najua kunawengine watatumia njia kama yake,wakifikiri ni rahisi, hii ni kwasababu huyu kijana kaonesha njia.Natoa angalizo kwa wengine wasione hii njia ni rahisi aliyopitia juma. mfano Babu wa loliondo alipoanza kutoa huduma ya kikombe wengine walijitokeza kwa ule ule mfumo, mwishowe kikombe cha babu kilionekana ndicho bora, hivyo basi huamuzi wa kijana juma na clouds fm utabakia kuwa bora zaidi!

    ReplyDelete
  10. Kama mdau mkubwa wa soka hongera sana bro, kule kwetu(mpanda) wapo vijana wakutosha na wadogo sema chance za kuwafanya waonekane ndiyo tatizo. fanya kaza ziara hata ya wiki uende ukajionee mwenyew

    ReplyDelete