Search This Blog

Monday, January 21, 2013

ZAMBIA YATOLEWA JASHO NA ETHIOPIA - ANGALIA HIGHLIGHTS


Mabingwa watatezi wa kombe la mataifa ya Afrika Chipolopolo ya Zambia wameanza kampeni ya kutetea kombe hilo waliloshinda mwaka uliopita kwa kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya Kundi C nchini Afrika Kusini.
Kinyume na matarajio ya wengi Ethiopia ilionyesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo na mara nyingi wachezaji wake wakionekana kuwathibiti wachezaji wa Chipolopolo.
Kwa mara nyingine tena timu hiyo ya Zambia, imeonyesha kuwa kwa sasa haipo katika hali nzuri kama ilivyokuwa mwaka uliopita.
Wakati wa mechi hiyo beki wake Chisamba Lungu alimuangusha mshambulizi wa Ethiopia Saladin Seid, kwenye eneo la hatari na bila kusita refa wa mechi hiyo akatoa adhabu ya penalti.
Lakini kipa wa Zambia Kennedy Mweene aliokoa mkwaju uliopigwa na Seid na hivyoi kufufua matumaini ya mabingwa hao watatezi.
Dakika chache baadaye, kipa wa Ethiopia, Jemal Tassew alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Chisamba Lungu.
Licha ya kuwa alikuwa akiondolewa uwanjani kwa machela refa wa mechi hiyo alimpa kipa huyo kadi nyekundu kutokana na mchezo mbaya na hatari aliouonyesha.
Dakika chache baada ya tukio hilo mabingwa hao watetezi wakafunga bao lao la kwanza kupitia kwa mchezaji Collins Mbesuma kunako dakika ya 45 kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili licha ya kucheza wachezaji kumi pekee kwa muda mrefu, Ethiopia ilisawazisha kunako dakika ya 65 kupitia kwa mchezaji Adane Girma.
Ithiopia ilithibiti mpira wa asilimia kubwa katika kipindi cha pili na hivyo kuzima matumaini ya mabingwa hao watatezi.
Mechi hiyo ilimalizika huku timu hizo mbili zikitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment