Hatimaye michuano ya Fainali za Kombe la Afrika, AFCON inayofanyika
nchini Afrika Kusini imeanza kuzaa magoli. Mechi ya kwanza ya kundi B
kati ya Ghana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, imemalizika kwa
kufungana magoli 2-2.
Ghana ilianza kufunga kupitia kwa Emmanuel Agyemang Badu katika
dakika ya 40. Kipindi cha pili kilianza kwa Ghana tena kuongeza goli la
pili likifungwa na Kwadwo Asamoah katika dakika ya 49.
Tresor Mputu ambaye ni ni nahodha wa timu ya DRC
alifunga bao la kwanza katika dakika ya 53. Goli la pili la DRC
limepatikana kwa njia ya mkwaju wa penalti ukifungwa na Dieumerci
Mbokani dakika ya 69. Kwa matokeo hayo timu hizo zimegawana pointi moja
moja.
Mechi ya pili ya kundi B inazikutanisha Mali na Niger.
No comments:
Post a Comment