Search This Blog

Tuesday, November 8, 2011

GALATASARAY WATHIBITISHA KUVUTIWA NA BERBATOV



Galatasary president Unal Aysal amethibitisha kuwa timu hiyo ya Istanbul wanafikiria kupeleka ofa kwa Manchester United mwezi January kwa ajili ya kumsaini Dimitar Berbatov.


Mkataba wa mbulgaria at OT unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo speculations zinaanza kusambaa kwamba mchezaji huyo mwenye miaka 30 muda wake wa kuwepo Carrington umeisha.


“Hatumuangalii Berbatov peke yake, tunavutiwa na wachezaji wengi. Ndiyo, tunahitaji zaidi washambuliaji, lakini sasa bado mapema.


“Tunaanza tukaanza mazungumzo mwishoni wa December, mpaka sasa tuna machaguo ya wachezaji wane au watano, lakini hatuwezi kusema tutamsajili Fulani kwa sababu bado hatujaamua,” alisema Raisi huyu wa Galatasary.

KALI YA LEO: YANAYOTOKEA USWAZI HATA MBELE YAPO: REFA ALA KIPIGO KUTOKA WACHEZAJI NA MASHABIKI

Monday, November 7, 2011

REAL MADRID WANA NAFASI KUBWA YA KUNYAKUA UBINGWA WA SPAIN MSIMU HUU.


Inawezekana ikawa ni mapema sana, lakini baada ya kuvuka vikwazo kadhaa katika rounds za mwanzo Primera Division, Real Madrid tayari wameanza kuonekana kama mabingwa.

Mapema jumapili, Madrid hawakuonyesha ishara zozote za kusinzia baada ya kuwatandika Osasuna 7-1 at Santiago Bernbeau. Ushindi wa 10 mfululizo kwa vijana wa Mourinho katika mashindano yote – na saba kati ya 10 ni ushindi katika Primera division. Hii ni form ya ubingwa.

Maandalizi ya msimu mpya ya Madrid yalitoa ishara mategemeo mazuri na expectations zimekuwa juu kufuatia performance nzuri dhidi ya Barca katika Spanish supercopa, hata kama Catalans waliishia kushinda kwa mabao 5-4 on aggregate.

Hivi karibuni watani hawa wa jadi watakutana tena – muda huu itakuwa kwenye ligi. Na katika mchezo huu, tofauti ya misimu kadhaa iliyopita, mchezo wa kwanza wa watawala hawa La Liga itafanyika mjini Madrid. Na kama vijana wa Jose Mourinho wataendelea kuwa kileleni kwa tofauti ya pointi 3 mpaka wakati huo, Wakatalani hawapaswi kupoteza mchezo huo.

Chini ya Pep Guardiola , Barca wamepata ushindi mara 5 na kudroo mchezo mmoja, lakini mawimbi yanaweza yakageuka. Barca walifungwa na Madrid katika fainali ya Copa del Rey msimu uliopita, wakati mechi yao ya mabingwa wa ulaya ya nusu fainali iliamuliwa na kutolewa kwa red card kwa Pepe na performance ya kutisha ya Lionel Messi baada ya kutolewa kwa mreno huyo.

Madrid wameongeza pengo la pointi kati yao na Barca kuwa 3 Jumapili wiki iliyopita baada ya mabingwa watetezi kutoa droo na Athletic Bilbao. Na haijawahi kutokea kwa Barca kupitwa pointi 3 na Madrid chini ya Pep Guardiola. Infact inabidi urudi nyuma michezo 125 tangu Madrid walipowaongoza Barca kwa pointi hizo.

BARCELONA & REAL MADRID | Their last five Primera Division results

Athletic Bilbao 2-2 Barcelona
Barcelona 5-0 Mallorca
Granada 0-1 Barcelona
Barcelona 0-0 Sevilla
Barcelona 3-0 Racing

Real Madrid 7-1 Osasuna
R. Sociedad 0-1 Real Madrid
Real Madrid 3-0 Villarreal
Malaga 0-4 Real Madrid
Real Madrid 4-1 Betis

Ndio maana Raisi wa Madrid Florentino Perez alimleta Mourinho, ambaye ameruhusiwa kuchukua majukumu yote ya ufundi ndani ya timu hiyo.Ndio njia pekee kwa Real kuweza kushindana na Barca, ambayo perhaps ndio bora zaidi historia ya timu hiyo.

Baada ya kufungwa na Lavante mapema mwanzoni mwa msimu na kudroo ugenini kwa Racing Santander katika mechi yao iliyofuata. Madrid chini ya Special wamerudi na kuwa kwenye consistency ya kushinda mechi 7 mfululizo za ligi na kufunga jumla ya mabao 39, matano zaidi ya vijana wa Guardiola.

BARCELONA & REAL MADRID | Their next five Liga fixtures

Nov 19: Zaragoza (h)
Nov 26: Getafe (a)
Dec 3: Levante (h)
Dec 10: Real Madrid (a)
Dec 17: Rayo Vallecano (h)

Nov 19: Valencia (a)
Nov 26: Atletico (h)
Dec 3: Sporting Gijon (a)
Dec 10: Barcelona (h)
Dec 17: Sevilla (a)








Mechi zinazofuata ni ngumu. Madrid watasafiri kucheza na Valencia walio kwenye form baada ya international break, kabla ya derby dhidi ya Atletico na baadae wataenda kucheza na Sporting Gijon, ambao walimaliza kasi ya kushinda mechi 9 mfululizo kwa kuwafunga Real at Santiago Bernebeau msimu uliopita.

After that inafuatia El Classico.

Temu iliyopita, Madrid waliongoza ligi wakiwa wanaenda kucheza the classico @ Nou Camp. Lakini vijana wa Mourinho waliadhiriwa katika mji wa Catalan baada ya kuchapwa 5-0. Kutoka hapo hawaku-recover. This time pande hizi mbili zinakutana in Madrid na na Real iliyofungwa last November ni tofauti sana na ya sasa.

Wakati sasa Real ikionekana kutomtegemea Cristiano Ronaldo, Barca wanaonekana kumtegemea zaidi na zaidi Lionel Messi. Muargentina huyu amecheza kila mechi msimu huu na kwa hakika sasa anahitaji apumzike. Akiwa na mechi ambazo si ngumu sana, dhidi ya Zaragoza, Getafe na Lavante mechi ambazo zinaweza kumruhusu Guardiola ku-rotate kikosi chake kabla ya Clasico, lakini kama Madrid wataendelea kushinda, the catalans itabidi washinde @ Santiago bernabeu ili kuzifikia pointi za Madrid ikizingatiwa pia Barca bado wana mzigo wa mashindano ya klabu bingwa ya dunia yatayoanza December.

Mwezi unaokuja ama kwa hakika unaweza kuwa ndio mwezi muafaka wa kuamua hatma ya msimu wa huu wa la liga. Ingawa imeshaanza kuonekana kuwa Madrid na Mourinho ndio watakaokuwa wakicheka siku ya mwisho.

DERRICK WALULYA KURUDI SIMBA, KUZIBA PENGO LA JERRY SANTO

SIMBA SPORTS CLUB

P.O.BOX 15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330 |MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | EMAIL simbasportsclub@yahoo.com|

WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA

07/11/2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu Wanahabari

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club ilikutana kujadili masuala anuai ya klabu na yafuatayo ni maazimio yaliyofikiwa mara baada ya mkutano huo.

Kuhusu Jerry Santo

Klabu ilikubaliana na ombi la mchezaji wake Jerry Santo aliyeomba aruhusiwe kwenda barani Asia kucheza soka la kulipwa mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa na Simba mwezi huu.

Simba inamtakia heri na fanaka mchezaji huyo kwenye maisha yake ya kisoka.

Nafasi ya Santo itajazwa na mchezaji kutoka nchini Uganda, Derick Walulya, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA).

Moses Basena

Kamati ya Utendaji haikumjadili Moses Basena wala kuchukua maamuzi yoyote kumhusu. Hii inatokana na ukweli kwamba Simba SC ni klabu ya kistaarabu na inafahamu kuwa kocha wake huyo yuko kwenye msiba mzito wa mama yake mzazi.

Klabu ya Simba inapenda kutumia nafasi hii kukanusha habari zote kuhusu kusimamishwa au kufukuzwa kazi kwa Basena katika kipindi hiki kigumu kwake.

Wachezaji wa Timu ya Vijana ya Simba

Kama inavyofahamika, Simba imesajili wachezaji 26 kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu ingawa Kanuni za TFF zinaruhusu timu kusajili wachezaji wasiozidi 30.

Kamati ya Utendaji imeamua kuwa nafasi nne zilizobaki (ili kufikia 30) zitajazwa na wachezaji kutoka timu za vijana za Simba.

Majina ya wachezaji hao yatapatikana baada ya Kamati ya Ufundi na Benchi la Ufundi kukutana na kujadiliana kuhusu wachezaji watakaofaa kwa ajili hiyo.

Simba ni timu ambayo falsafa yake ya soka inafahamika. Wachezaji ambao wamepikwa ndani ya timu (kama hao wa timu za vijana) wanafundishwa kwenye falsafa hiyo na wanatarajiwa kuwa mabalozi wazuri wa falsafa ya klabu.

Klabu maarufu na zenye mafanikio duniani kama vile Barcelona na Man United zimefanikiwa sana kwa kukuza vipaji kutoka kwenye timu zake za vijana.

Simba inaelekea kwenye njia hiyo.

Vurugu Viwanjani

Kamati ya Utendaji ya Simba imesikitishwa sana na vitendo vya vurugu vilivyofanywa na baadhi ya washabiki wake wakati wa mchezo wa mwisho wa raundi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Moro United.

Washabiki hao wachache walikuwa wakitoa lugha ya matusi, vitisho na vurugu dhidi ya wachezaji na viongozi wa Simba waliokuwapo uwanjani.

Kamati iliazimia kuwa wakati umefika sasa kwa vyombo vya dola kushughulikia washabiki wanaofanya vitendo visivyo vya kiungwana katika viwanja vya soka nchini.

Kwa taarifa hii, Simba inawaomba washabiki wake waendelee kuwa alama ya uungwana na ustaarabu michezoni. Washabiki wa Simba wanafahamika kote duniani kwa sifa hii.

Simba SC haitatetea mpenzi au mwanachama wake yeyote atakayekutwa na hatia ya kufanya vitendo vya vurugu uwanjani.

Kufungwa na Yanga

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji walieleza kusikitishwa kwao na kufungwa na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu msimu huu.

Kamati inafahamu machungu ambayo wapenzi na wanachama wa Simba waliyapata baada ya kipigo hicho.

Hata hivyo, Kamati inasisisitiza kuwa ni vema wapenzi wa Simba wakaanza kuitazama ligi kwa mapana yake. Ligi haipo kwa ajili ya Simba kuifunga Yanga pekee bali kutwaa ubingwa wa Tanzania na kuwakilisha Taifa katika michuano ya kimataifa.

Pamoja na kufungwa na Yanga, Simba inaongoza ligi si kwa kuwa na pointi nyingi pekee bali pia kwa kuwa na idadi kubwa ya magoli ya kufunga na wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Hii ni ishara kuwa Simba ni timu bora Tanzania kwa sasa kwa vigezo vyovyote vile vya kimpira.

Kitendo cha washabiki kutuhumiana, kugombana na kutaka kufanya fujo kwa sababu ya kupoteza mechi moja na kusahau mazuri yote ambayo yamefanywa na timu ni kinyume cha uanamichezo.

Timu kubwa kama Man United ya England zimefungwa hadi mabao sita katika mechi ya watani wa jadi lakini hakuna aliyefanya fujo kwa wachezaji, benchi la ufundi au viongozi wa timu hiyo.

Kamati imehimiza umoja na mshikamano miongoni mwa wana Simba ndani na nje ya nchi. Hakuna sababu ya kuibua migogoro na migongano isiyo na sababu kwa sababu ya timu kupoteza mechi moja.

Naomba kuwasilisha

Ezekiel Kamwaga

Msemaji

Simba Sports Club

MAGOLI YOTE 202 ALIYOWAHI KUFUNGA MESSI NDANI YA BARCELONA

ARSENAL WASHINDA MECHI YA 400 KWENYE PREMIER LEAGUE


4 – Wes Brown sasa ameweka rekodi katika premier league kwa kujifunga magoli mengi zaidi (4 goals).


5 – Bolton Wanderers waliifunga Stoke City 5-0 kulipiza kisasi kwa kipigo kama hicho katika nusu fainali ya FA Cup iliyopita. Ushindi huo ndio ulikuwa wa kwanza ndani ya msimu huu na mkubwa zaidi katika premier league.


8 – Wigan Athletic sasa wamepoteza mechi ya nane mfululizo in Barclays premier league, ndio timu ya kwanza kuandika historia hiyo katika vipindi vitatu tofauti in Premier league.


10 – Ushindi wa Chelsea 1-0 dhidi ya Blackburn Rovers ulimaanisha walipata clean sheet kwa mara ya kwanza ndani ya mechi 10 tangu kuanza kwa msimu huu.


14 – Ushindi wa Newcastle United wa 2-1 dhidi ya Everton unaamnisha kwamba sasa hawajafungwa katika 14 za Barclays premier league, wakiifikia rekodi yao waliyoiweka mwaka 1950.


18 – Steve Bruce hajawahi kumfunika mwalimu wake Sir Alex Ferguson katika majaribio 18 baada ya timu yake ya Sunderland kufungwa 1-0 at Old Trafford.


24 – Arsenal hawajawahi kufungwa mchezo wowote kati ya 24 ya premier league ambayo Robin Van Persie alianza kufunga.

25 – Sir Alex Ferguson alisherehekea miaka 25 ndani ya Manchester United na ushindi wa 1-0 dhidi ya Sunderland.


46 – Magoli mawili ya Darren Bent dhidi ya Norwich City yalimfanya afikishe jumla ya magoli 46 in Barclays premier league tangu msimu wa 2009/10, magoli mengi zaidi kuliko mchezaji yeyote.


400 – Ushindi wa Arsenal wa 3-0 dhidi ya West Bromwich Albion ulikuwa ushindi wao wa 400 in premier league.

CANNAVARO: SUNZU KANIONDOA STARS...... KAPOMBE ARITHI NAFASI YAKE


Beki wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kuwa mechi dhidi ya mahasimu wao Simba ambayo walishinda 1-0 ndiyo iliyomtoa kwenye timu ya taifa kutokana na majeraha ya kuvimba enka.

Akizungumza jana, Cannavaro, alisema kuwa aliumia wakati akiwania mpira dhidi ya mshambuliaji wa Simba, Mzambia Felix Sunzu, na si kweli kwamba aliumia wakati wa mazoezi ya timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa na mechi dhidi ya Chad ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014.

Alisema kwamba kilichotokea juzi akiwa kwenye kikosi cha Stars ni kutonesha jeraha hilo ambalo litamweka nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki moja.

"Sunzu ndiye aliyenipa maumivu haya, Stars nimejitonesha tu, mwanzo wa kuumia ilikuwa ni mechi yetu na Simba," alisema beki huyo tegemeo katika ngome ya Stars na klabu yake ya Yanga.

Maumivu hayo ya Cannavaro yamemfanya aondolewe Stars na pia hataweza kuambatana na timu yake ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, ambayo inatarajia kuelekea Misri leo kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Chalenji yatakayofanyika kuanzia Novemba 25 jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, kocha mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen, hajaita beki mwingine kwa ajili ya kuziba pengo la Cannavaro na badala yake huenda akamtumia mchezaji 'kiraka' Shomary Kapombe wa Simba katika nafasi hiyo.

THREE DAYS REMAINING CAST YOUR VOTE NOW FOR SWAHILI FASHION WEEK 2001 AWARDS / ZIMESALIA SIKU TATU PIGA KURA YAKO SASA KTK TUZO ZA SWAHILI FASHION





FEW DAYS HAVE REMAINED FOR THE VOTING LINES OF SWAHILI FASHION WEEK AWARDS 2011 TO BE CLOSED, VOTE FOR YOUR FAVORITE TIME RUNS OUT SO QUICKLY. DON'T EVER TRY MISS THIS FASHION EVENT AS IT IS BEING THE BIGGEST FASHION EVENT OVER EAST AND CENTRAL AFRICA

ZIKIWA ZIMESALIA SIKU CHACHE HADI KUFUNGWA KWA NJIA ZA KUPIGA KURA KWA AJILI YA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK 2011 WEWE KAMA MUWEZASHAJI WA TUZO HIZI MPIGIE KURA YULE UMPENDAYE NA UNAYEONA ANAFAA KUSHINDA. USIJARIBU KUTOKUWA MMOJA WA WASIOPIGA KURA JIVUNIE MAVAZI YA KIAFRIKA KWANI HILI NI ONESHO KUBWA LA MAVAZI AFRIKA MASHARIKI NA KATI


PIGA KURA YAKO SASA HAPA: www.swahilifashionweekawards.blogspot.com

KUFANYIKA KWA MAFUNZO YA KIMATAIFA KWAWALIMU WA MCHEZO WA NGUMI ZA RIDHAATANZANIA 12-20 Nov 2011 KIBAHA PWANI.

Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) wameandaa mafunzo kwa walimu wa mchezo wa ngumi Tanzania.
Kozi hiyo itafanyika kuanzia tarehe 12-20 Nov 2011 Kibaha, Pwani katika shule ya Filbert Bayi.
Mkufunzi katika kozi hiyo ni kutoka Algeria,aliyeteuliwa na Chama cha ngumi cha Dunia (AIBA)
Jumla ya washiriki ni 30 wamechaguliwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara kuja kuhudhuria mafunzo hayo, kwa kuzingatia mchango wao katika ushiriki wa matukio mbali mbali ya BFT hasa mashindano kwa kuleta timu au mikoa yao kama makocha na kujihusisha kikamilifu katika shughuri mbalimbali zinazohusu kuendeleza mchezo wa ngumi Tanzania
Zaidi makocha hao tayari walishapata mafunzo ya awali yaliyoandaliwa na BFT.
Baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo washiriki watakaofuzu watatambuliwa na kuingizwa katika data base za Chama cha ngumi cha Dunia [AIBA]
Pia wataweza kufundisha mchezo wa ngumi popote Duniani na kuruhusiwa kushiriki mashindano yote ya kimataifa kama makocha kwa mashindano yote yatakayo andaliwa kwa kufata sheria za AIBA.
Kwa uzoefu sisi kama BFT tunategemea mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo,tunategemea kupata ushindani wa uhakika kutoka katika mikoa iliyopata nafasi ya ushiriki,na tunategemea kupata timu ya Taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa tofauti na awali ambapo wachezaji wengi walitokea DAR ES SALAAM na hasa katika vyombo vya ULINZI NA USALAMA.
Kwa msingi huo sasa tutategemea kupata ushiriki wenye tija katika mashindano mbalimbali ya kimataifa hasa kufuzu katika ushiriki wa timu yetu ya Tanzania katika mashindano ya Olimpiki 2012 London Uingereza.Na mashindano mengine ya kimatafa.
Makore Mashaga.
KATIBU MKUU BFT.
Mob; 0713588818.
Email;mashagam@yahoo.com

HATIMAYE TIMBE ALIPWA MIL.36 NA KUONDOKA BONGO


Hatimaye aliyekuwa Kocha Mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Sam Timbe, ametimka jana jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Uganda, baada ya kulipwa stahiki zake alizokuwa akiudai uongozi wa klabu hiyo baada kusitisha naye mkataba wa kuinoa timu hiyo.

Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema jana kuwa tayari wameshamlipa stahiki zake Timbe ambaye alisitishiwa ghafla mkataba na uongozi wa klabu hiyo hivi karibuni na kumrejesha kocha wake wa zamani Mserbia Kostadin Papic.

“Tumeshamalizana na Timbe kwa kumlipa kilicho chake na ameondoka jana kwenda kwao tayari kwa masuala yake binafsi,” alisema Sendeu.

Kabla ya kuondoka, juzi Timbe alikaririwa kwenye vyombo vya habari akiapa kutoondoka mpaka atakapolipwa fedha zake baada ya kuona akizungushwa kulipwa malipo yake ambayo ni mishahara ya miezi saba na fidia ya kuvunja naye mkataba, ambao ulikuwa unatarajiwa kumalizika Mei mwakani.

Hata hivyo, Sendeu hakuwa tayari kuweka wazi kiasi alicholipwa kocha huyo kwa madai kuwa ni siri baina ya uongozi na kocha huyo mwenye rekodi ya mafanikio ya kufundisha soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa mabingwa hao wa TZ Bara na afrika mashariki na kati kimesema kuwa, Timbe amelipwa shilingi milioni 36 ambazo zimejumuisha mishahara yake na fidia ya kuvunjiwa mkataba wake.

Sunday, November 6, 2011

EMMANUEL OKWI : SIMJUI RIDHIWAN NA SIKUPIGWA NA BOBAN








HAPA ILIKUA NI BAADA YA MAHOJIANO YETU......


BAADA YA MAHOJIANO TULIJIMWAGA KWENYE DUKA LA VIFAA VYA MICHEZO LA ADIDAS PALE QUALITY PLAZZA...


HIKI NDO KIATU AMBACHO HUPENDA KUKITUMIA...NI CHEPESI SANA...


BAADA YA MAHOJIANO NA MSHAMBULIAJI EMMANUEL OKWI MASAA MACHACHE KABLA YA KUKWEA PIPA KWENDA KWAO UGANDA KUJIUNGA NA KAMBI YA TIMU YA TAIFA INAYOJIANDAA NA MASHINDANO YA LG CUP YATAKAYOFANYIKA NCHINI MOROCCO HIVI KARIBUNI..







OKWI AKIWA NA MASHABIKI WAKE AMBAO NI WAFANYAKAZI WA MGAHAWA WA SUBWAY PALE QUALITY PLAZZA.













MSHAMBULIAJI EMANUEL OKWI AMEYAJIBU BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA MASHABIKI KUPITIA KWENYE UKURASA WANGU WA FACEBOOK. ( RANGI YA BLUE NI MAJINA YA WALIOULIZA NA RANGI NYEKUNDU NI MASWALI YAO )






Joseph Fredie ‎
Ni kwel alipigwa na boban kisa aliuza mech ya juzi na yanga?
Vanmedy Bakari
‎amejiskiaje baada ya kuskia tuhuma za yeye kupigwa na boban!?, kisakolojia zaidi.. Je hazijamuathiri kivyovyote..
Adan Abdul,BUGURUNI DSM
Yapoje mahusiano ya kikazi kati yako na haruna moshi?
Fazzy Phyzzo
likuaje mpaka boban akampga au kuna ugomvi wa siku nyng kwan wachezaj weng walkosea mbona hakuwaga au ana ugomv na wewe?
Alex Mayoge,KILIMANJARO

Ni mchezaj gan wa mpira ambaye anamkubal sana wa hapa bongo na ligi za ulaya?

Joe Sailas
je ni kweli alipigwa na Boban na nini mipango yake ya baadae, anaendelea na Simba au anatafuta timu nyingine na kuna tetesi kua anaenda Yanga ni kweli?

Sam Abdul

ni kweli okwi alipigwa na boban?
Leonard Kasanjala

Ni kweli. Alipigwa na. Boban.

EMANUEL OKWI:Binafsi nilishangazwa na hizo tuhuma za mimi kupigwa na Boban,labda walivyomuona boban anatoka ndo wakapata hisia hizo,mi pia wakati naelekea nyumbani nilishangazwa na hizo story nilizozisikia toka kwa mashabiki waliokua bado wamejazana pale uwanjani,ukweli upo hivi Boban hakunifanya chochote na sidhani anaweza kufanya kitendo kama hicho,Boban ni mchezaji mkubwa ambaye pia ni rafiki yangu sana.

Tullo Chambo
UHUSIANO WAKE NA RIZ ONE
Issah Mahiki
Je unaukaribu na Ridhiwan Kikwete? kama kweli ulianza lni na wa nn?
Halber Bin Ambary
riz one ni nani kwake.?je kweli amenunuliwa gar na riz one...!?ni hayo 2..

Othman Famau
hv Okwi na Ridhwan Kikwete wana urafiki wowote
Kiamu Nahar
Je ana ukaribu wowote na ridhwani kwikwete?

Emmanuel Okwi:Kwanza kabisa huyo Ridhiwan ni nani hasa,maana simjui huyo mtu anaitwa Ridhiwan na hata nikikutana naye barabarani siwezi kumtambua,nimekua nazisikia hizo story lakini ninachoweza kukwambia sina mawasiliano wala mahusiano sasa atawezaje kuninunulia hilo gari ?

kwa taarifa zaidi ya mahojiano haya fuatilia vipindi vya Sports Xtra kwenye Clouds fm , Sports Bar kwenye Clouds TV na Jarida namba moja la mpira wa miguu Tanzania NUMBER 10.

MPAMBANO WA BOOM FC NA ASHANTI KWENYE PICHA..


PETER TINO PIA ALIKUEPO...KWENYE MPAMBANO ULIOPIGWA KWENYE UWANJA WA SHULE YA SEKONDARI YA BENJAMIN MKAPA MAENEO YA ILALA...



NAJEEM MANAGER WA COSMOPOLITAN




SHOTO NI JAMAL AKIJULIKANA KWA JINA LA SEKI ENZI HIZO AKIWA NA COSMO, UBWA ( KATI ) MCHEZAJI WA ZAMANI WA DAR FIRE NA OMARI




CHAMBEGA MZEE WA LIVERTONE




SEHEMU YA MASHABIKI WA BOOM FC WAKIUFATILIA MCHEZO DHIDI YA MAHASIMU WAO ASHANTI..











MWAMUZI HAMIS CHANG'WALU ALIUMUDU VYEMA MCHEZO HUO..



MAPACHA ! MAPACHA ! KUSHOTO NI CISSE MSHAMBULIAJI WA BOOM FC





HUYU NI SHABIKI MAARUFU WA BOOM FC.....



MANEJA WA BENDI YA MUZIKI YA MAPACHA WATATU HAMIS DA COSTA PIA ALIKUEPO KUIPA SUPPORT TIMU YAKE YA ASHANTI....



















HAROUB AONDOLEWA TAIFA STARS


Beki wa kati wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Nadir Haroub ameondolewa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena. Haroub ameondolewa baada ya kuumia kifundo cha mguu wa kulia (right ankle) akiwa mazoezini jana asubuhi (Novemba 5 mwaka huu). Kwa mujibu wa daktari wa Stars, Dk. Juma Mwankemwa, mchezaji huyo hakuvunjika isipokuwa amepata mshtuko mkubwa wa kifundo hicho ambapo itamchukua wiki mbili kupona sawa sawa. Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amesema kutokana na hali hiyo Haroub hatakuwemo kwenye kikosi hicho kwa ajili ya mechi hiyo na ile ya marudiano ambayo itachezwa Novemba 15 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Poulsen amesema kwa muda uliobaki hataita mchezaji mwingine kwa ajili ya kuziba pengo la Haroub, hivyo kwa sasa atabaki na kikosi cha wachezaji 21 alionao kambini hoteli ya New Africa.



LESENI ZA UKOCHA ZA CAF DARAJA C

Kozi ya ukocha kwa ajili ya kupata leseni za daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanzia kesho (Novemba 7 mwaka huu) hadi Novemba 20 mwaka huu. Makocha 30 ndiyo wanaoshiriki kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi wanne; Jan Poulsen kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Kasimawo Laloko (Nigeria) na Sunday Kayuni wanaotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Kim Poulsen kutoka Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU).Washiriki wa kozi hiyo ni Abdul Nyumba, Absolom Mwakyonde, Ahmed Mumba, Christopher Eliakim, Dismas Haonga, Edward Hiza, Eliasa Thabit, Emmanuel Massawe, Fulgence Novatus, Gabriel Gunda, Gideon Kolongo, Haji Amir na Hassan Banyai. Wengine ni Juma Mgunda, Jumanne Ntambi, Keneth Mkapa, Leonard Jima, Maarufu Yassin, Maka Mwalwisi, Mecky Maxime, Mohamed Tajdin, Mussa Furutuni, Mussa Kamtande, Peter Mhina, Richard Kabudi, Sebastian Nkoma, Stephen Matata, Tiba Mlesa, Wane Mkisi na Wilfred Kidau.

STARS KWENDA CHAD NOVEMBA 9

Taifa Stars itaondoka nchini Novemba 9 mwaka huu kwenda N’Djamena, Chad kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayochezwa nchini humo Novemba 11 mwaka huu. Msafara wa timu hiyo utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Eliud Mvella utaondoka saa 9 kamili alasiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ambapo utawasili N’Djamena saa 1 jioni ambapo Tanzania itakuwa saa 3 usiku. Timu itarejea nchini Novemba 12 mwaka huu kwa ndege ya Ethiopian Airlines na kwenda moja kwa moja kambini kujiandaa kwa mechi ya marudiano itakayochezwa Novemba 15 mwaka huu.

QPR 2-3 MAN CITY


szólj hozzá: MAN

MANCHESTER UNITED 1-0 SUNDERLAND


szólj hozzá: Man United 1-0 Sunderland

ARSENAL 3-1 WEST BROMWICH ALBION


szólj hozzá: arsewbmotd

JUMA NKAMIA ALIVALIA NJUGA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA KIBIRA


Vice-chairman wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Juma Nkamia amekitaka Chama cha Netiboli Tanzania, Chaneta kuelezea umma wa wacheza netiboli hatma ya aliyekuwa katibu wa chama hicho, Anna Kibira.

Kibira ambaye pia ni mwamuzi wa mchezo huo, alisimamishwa na Kamati ya Utendaji ya Chaneta kujihusisha na chama hicho mwishoni mwa Agosti 2009.

Mwenyekiti wa Chaneta, Anna Bayi alikaririwa akisema kuwa chama kimemsimamisha Kibira kutokana na kutoa maamuzi binafsi bila kuishirikisha kamati ya utendaji.

Alisema kuwa Kibira alijichukulia madaraka binafsi na kuandika barua kwa njia ya siri kwa wadau kuhusiana na mambo mbalimbali ya chama hicho.

Nkamia aliyeongeza kamati hiyo katika ziara ya kutembelea taasisi za michezo ikiwemo Baeaza la Michezo la Taifa, BMT katikati ya wiki, aliitaka BMT kufuatilia suala la Kibira ambaye anatumikia mwaka wa tatu sasa.

"Nashangaa kwanini BMT wamekaa kimya wakati Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli amesimamishwa mwaka wa tatu huu sasa kana kwamba hakuna jambo linaloendelea na kubakia wakigawa bendera tu wachezaji wanaokwenda kuwakilisha nje ya nchi."

VIONGOZI WA VILABU WAIPIGA CHINI TENA KAMATI YA TENGA YA KUONGOZA LIGI.




Vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka Tanzania Bara kwa kauli moja vimeikataa kamati ya kusimamia mchakato wa kuanzishwa kwa kampuni ya kusimamia ligi hiyo na ligi daraja la kwanza ,iliyoteuliwa na shirikisho la soka Tanzania (TFF).



Maazimio hayo yalifikiwa katika kikao baina ya wawakilishi wa vilabu hivyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam jana na badala yake kuliachia Shirikisho hilo limalizie kuendesha ligi hiyo katika mzunguko wa pili na baada ya hapo kuwa katika mikono ya kampuni.



Mwenyekiti wa kamati ya mpito ya mchakato wa kuazishwa kampuni ya kusimamia ligi ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alisema jana kwamba wamefikia hatua hiyo baada kuona mapungufu makubwa chini ya usimamizi wa TFF.



“Tunataka tuwe na mafanikio kama wenzetu Kenya na Uganda ambao ligi yao imekuwa ikiendeshwa na kampuni, hivyo tumewaachia kusimamia na mzunguko wa pili, kabla ya msimu ujao ambao utaendeshwa na kampuni,” Alisema.


Wakati huo huo baadhi ya viongozi wa vilabu vya ligi kuu walioteuliwa kwenye kamati ya Tenga, akiwemo Nyange Kaburu wamesema pamoja na kuikataa kamati hiyo ligi pia wameomba TFF iwaombe msamaha kwa kuwateua bila kuwapa taarifa juu ya uteuzi huo waliouita wa magazetini.

BOMU FC WAIFUNGA ASHANTI UTD KATIKA ILALA DERBY


Mpambano wa watani wa jadi wa Ilala Bom FC na Ashanti United ulipigwa leo katika uwanja wa shule ya sekondari Benjamin Mkapa.

Mchezo huo wa Ngao ya jamii unaoashiria kuanza kwa ligi ya mkoa wakisoka Ilala ulizishuhudia timu hizo zikimaliza dakika 90 bila kufungana huku mchezo ukiwa na burudani ya kipekee, kwa mashabiki waliojitokeza.

Changamoto za Mikwaju ya Penati ndiyo iliyoamua matokeo ya leo, ambapo Bom FC waliibuka kidedea kwa mikwaju 4 dhidi ya 3 ya Ashanti United.