Search This Blog

Sunday, November 6, 2011

VIONGOZI WA VILABU WAIPIGA CHINI TENA KAMATI YA TENGA YA KUONGOZA LIGI.




Vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka Tanzania Bara kwa kauli moja vimeikataa kamati ya kusimamia mchakato wa kuanzishwa kwa kampuni ya kusimamia ligi hiyo na ligi daraja la kwanza ,iliyoteuliwa na shirikisho la soka Tanzania (TFF).



Maazimio hayo yalifikiwa katika kikao baina ya wawakilishi wa vilabu hivyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam jana na badala yake kuliachia Shirikisho hilo limalizie kuendesha ligi hiyo katika mzunguko wa pili na baada ya hapo kuwa katika mikono ya kampuni.



Mwenyekiti wa kamati ya mpito ya mchakato wa kuazishwa kampuni ya kusimamia ligi ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alisema jana kwamba wamefikia hatua hiyo baada kuona mapungufu makubwa chini ya usimamizi wa TFF.



“Tunataka tuwe na mafanikio kama wenzetu Kenya na Uganda ambao ligi yao imekuwa ikiendeshwa na kampuni, hivyo tumewaachia kusimamia na mzunguko wa pili, kabla ya msimu ujao ambao utaendeshwa na kampuni,” Alisema.


Wakati huo huo baadhi ya viongozi wa vilabu vya ligi kuu walioteuliwa kwenye kamati ya Tenga, akiwemo Nyange Kaburu wamesema pamoja na kuikataa kamati hiyo ligi pia wameomba TFF iwaombe msamaha kwa kuwateua bila kuwapa taarifa juu ya uteuzi huo waliouita wa magazetini.

No comments:

Post a Comment