Vice-chairman wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Juma Nkamia amekitaka Chama cha Netiboli Tanzania, Chaneta kuelezea umma wa wacheza netiboli hatma ya aliyekuwa katibu wa chama hicho, Anna Kibira.
Mwenyekiti wa Chaneta, Anna Bayi alikaririwa akisema kuwa chama kimemsimamisha Kibira kutokana na kutoa maamuzi binafsi bila kuishirikisha kamati ya utendaji.
Alisema kuwa Kibira alijichukulia madaraka binafsi na kuandika barua kwa njia ya siri kwa wadau kuhusiana na mambo mbalimbali ya chama hicho.
Nkamia aliyeongeza kamati hiyo katika ziara ya kutembelea taasisi za michezo ikiwemo Baeaza la Michezo la Taifa, BMT katikati ya wiki, aliitaka BMT kufuatilia suala la Kibira ambaye anatumikia mwaka wa tatu sasa.
"Nashangaa kwanini BMT wamekaa kimya wakati Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli amesimamishwa mwaka wa tatu huu sasa kana kwamba hakuna jambo linaloendelea na kubakia wakigawa bendera tu wachezaji wanaokwenda kuwakilisha nje ya nchi."
No comments:
Post a Comment