Search This Blog

Monday, November 7, 2011

REAL MADRID WANA NAFASI KUBWA YA KUNYAKUA UBINGWA WA SPAIN MSIMU HUU.


Inawezekana ikawa ni mapema sana, lakini baada ya kuvuka vikwazo kadhaa katika rounds za mwanzo Primera Division, Real Madrid tayari wameanza kuonekana kama mabingwa.

Mapema jumapili, Madrid hawakuonyesha ishara zozote za kusinzia baada ya kuwatandika Osasuna 7-1 at Santiago Bernbeau. Ushindi wa 10 mfululizo kwa vijana wa Mourinho katika mashindano yote – na saba kati ya 10 ni ushindi katika Primera division. Hii ni form ya ubingwa.

Maandalizi ya msimu mpya ya Madrid yalitoa ishara mategemeo mazuri na expectations zimekuwa juu kufuatia performance nzuri dhidi ya Barca katika Spanish supercopa, hata kama Catalans waliishia kushinda kwa mabao 5-4 on aggregate.

Hivi karibuni watani hawa wa jadi watakutana tena – muda huu itakuwa kwenye ligi. Na katika mchezo huu, tofauti ya misimu kadhaa iliyopita, mchezo wa kwanza wa watawala hawa La Liga itafanyika mjini Madrid. Na kama vijana wa Jose Mourinho wataendelea kuwa kileleni kwa tofauti ya pointi 3 mpaka wakati huo, Wakatalani hawapaswi kupoteza mchezo huo.

Chini ya Pep Guardiola , Barca wamepata ushindi mara 5 na kudroo mchezo mmoja, lakini mawimbi yanaweza yakageuka. Barca walifungwa na Madrid katika fainali ya Copa del Rey msimu uliopita, wakati mechi yao ya mabingwa wa ulaya ya nusu fainali iliamuliwa na kutolewa kwa red card kwa Pepe na performance ya kutisha ya Lionel Messi baada ya kutolewa kwa mreno huyo.

Madrid wameongeza pengo la pointi kati yao na Barca kuwa 3 Jumapili wiki iliyopita baada ya mabingwa watetezi kutoa droo na Athletic Bilbao. Na haijawahi kutokea kwa Barca kupitwa pointi 3 na Madrid chini ya Pep Guardiola. Infact inabidi urudi nyuma michezo 125 tangu Madrid walipowaongoza Barca kwa pointi hizo.

BARCELONA & REAL MADRID | Their last five Primera Division results

Athletic Bilbao 2-2 Barcelona
Barcelona 5-0 Mallorca
Granada 0-1 Barcelona
Barcelona 0-0 Sevilla
Barcelona 3-0 Racing

Real Madrid 7-1 Osasuna
R. Sociedad 0-1 Real Madrid
Real Madrid 3-0 Villarreal
Malaga 0-4 Real Madrid
Real Madrid 4-1 Betis

Ndio maana Raisi wa Madrid Florentino Perez alimleta Mourinho, ambaye ameruhusiwa kuchukua majukumu yote ya ufundi ndani ya timu hiyo.Ndio njia pekee kwa Real kuweza kushindana na Barca, ambayo perhaps ndio bora zaidi historia ya timu hiyo.

Baada ya kufungwa na Lavante mapema mwanzoni mwa msimu na kudroo ugenini kwa Racing Santander katika mechi yao iliyofuata. Madrid chini ya Special wamerudi na kuwa kwenye consistency ya kushinda mechi 7 mfululizo za ligi na kufunga jumla ya mabao 39, matano zaidi ya vijana wa Guardiola.

BARCELONA & REAL MADRID | Their next five Liga fixtures

Nov 19: Zaragoza (h)
Nov 26: Getafe (a)
Dec 3: Levante (h)
Dec 10: Real Madrid (a)
Dec 17: Rayo Vallecano (h)

Nov 19: Valencia (a)
Nov 26: Atletico (h)
Dec 3: Sporting Gijon (a)
Dec 10: Barcelona (h)
Dec 17: Sevilla (a)








Mechi zinazofuata ni ngumu. Madrid watasafiri kucheza na Valencia walio kwenye form baada ya international break, kabla ya derby dhidi ya Atletico na baadae wataenda kucheza na Sporting Gijon, ambao walimaliza kasi ya kushinda mechi 9 mfululizo kwa kuwafunga Real at Santiago Bernebeau msimu uliopita.

After that inafuatia El Classico.

Temu iliyopita, Madrid waliongoza ligi wakiwa wanaenda kucheza the classico @ Nou Camp. Lakini vijana wa Mourinho waliadhiriwa katika mji wa Catalan baada ya kuchapwa 5-0. Kutoka hapo hawaku-recover. This time pande hizi mbili zinakutana in Madrid na na Real iliyofungwa last November ni tofauti sana na ya sasa.

Wakati sasa Real ikionekana kutomtegemea Cristiano Ronaldo, Barca wanaonekana kumtegemea zaidi na zaidi Lionel Messi. Muargentina huyu amecheza kila mechi msimu huu na kwa hakika sasa anahitaji apumzike. Akiwa na mechi ambazo si ngumu sana, dhidi ya Zaragoza, Getafe na Lavante mechi ambazo zinaweza kumruhusu Guardiola ku-rotate kikosi chake kabla ya Clasico, lakini kama Madrid wataendelea kushinda, the catalans itabidi washinde @ Santiago bernabeu ili kuzifikia pointi za Madrid ikizingatiwa pia Barca bado wana mzigo wa mashindano ya klabu bingwa ya dunia yatayoanza December.

Mwezi unaokuja ama kwa hakika unaweza kuwa ndio mwezi muafaka wa kuamua hatma ya msimu wa huu wa la liga. Ingawa imeshaanza kuonekana kuwa Madrid na Mourinho ndio watakaokuwa wakicheka siku ya mwisho.

No comments:

Post a Comment