Search This Blog

Monday, November 7, 2011

ARSENAL WASHINDA MECHI YA 400 KWENYE PREMIER LEAGUE


4 – Wes Brown sasa ameweka rekodi katika premier league kwa kujifunga magoli mengi zaidi (4 goals).


5 – Bolton Wanderers waliifunga Stoke City 5-0 kulipiza kisasi kwa kipigo kama hicho katika nusu fainali ya FA Cup iliyopita. Ushindi huo ndio ulikuwa wa kwanza ndani ya msimu huu na mkubwa zaidi katika premier league.


8 – Wigan Athletic sasa wamepoteza mechi ya nane mfululizo in Barclays premier league, ndio timu ya kwanza kuandika historia hiyo katika vipindi vitatu tofauti in Premier league.


10 – Ushindi wa Chelsea 1-0 dhidi ya Blackburn Rovers ulimaanisha walipata clean sheet kwa mara ya kwanza ndani ya mechi 10 tangu kuanza kwa msimu huu.


14 – Ushindi wa Newcastle United wa 2-1 dhidi ya Everton unaamnisha kwamba sasa hawajafungwa katika 14 za Barclays premier league, wakiifikia rekodi yao waliyoiweka mwaka 1950.


18 – Steve Bruce hajawahi kumfunika mwalimu wake Sir Alex Ferguson katika majaribio 18 baada ya timu yake ya Sunderland kufungwa 1-0 at Old Trafford.


24 – Arsenal hawajawahi kufungwa mchezo wowote kati ya 24 ya premier league ambayo Robin Van Persie alianza kufunga.

25 – Sir Alex Ferguson alisherehekea miaka 25 ndani ya Manchester United na ushindi wa 1-0 dhidi ya Sunderland.


46 – Magoli mawili ya Darren Bent dhidi ya Norwich City yalimfanya afikishe jumla ya magoli 46 in Barclays premier league tangu msimu wa 2009/10, magoli mengi zaidi kuliko mchezaji yeyote.


400 – Ushindi wa Arsenal wa 3-0 dhidi ya West Bromwich Albion ulikuwa ushindi wao wa 400 in premier league.

No comments:

Post a Comment