Source: www.youngafricans.co.tz
Young Africans Sports Club imeanza mazoezi leo asubuhi katika viwanja vya Fame Footballl vilivyopo pemebni kidogo mwa hoteli ya Fame Residence Lara & Spa iliyopo kusini mwa mji wa Antalya ambapo imeweka kambi ya mafunzo ya wiki mbili.
Kocha Brandts akisaidiwa na kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa waliongoza mazoezi hayo yaliyoanza majira ya saa 4 kamili asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na awamu ya pili ilianza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, ambapo timu inapata huduma zote za kambi katika Hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kuanzia chakula, malazi, mazoezi ya viungo (Gym) ufukwe kwa ajili ya mazoezi ya stamina na kujenga mwili.
Mji wa Antalya ni maarufu katika medani ya soka kwani kwa ripoti tuliyopewa timu zaidi ya 200 zimeshafika katika mji huu kipindi cha majira ya baridi kuja kuweka kambi zikitokea katika nchi tofauti duniani.
Wenyeji wa Young Africans Team Travel wameandaa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ambapo wachezaji na viongozi pamoja wenyeji wa mji huu watasherehekea pamoja.
Search This Blog
Monday, December 31, 2012
HIZI NDIO STORY TANO ZILIZOPATA VIEWERS WENGI KATIKA MWAKA 2012 NDANI YA MTANDAO HUU
Story ya mwanadada Lulu kutoa maelezo polisi kuhusu tuhuma za kuhusika na kifo cha Kanumba ndio imeshika nafasi ya kwanza |
LIVE MATCH CENTRE - Mitanange ya Yanga vs Azam na Simba vs Mtibwa ilipata viewers wengi na kushika namba 2 |
Story ya kuhusu kifo cha marehemu Steven Kanumba imeshika nafasi ya 3 |
Nafasi ya nne imekatamatwa na story kuhusiana na kesi ya kifo cha Steven Kanumba |
LIVE MATCH CENTRE ya pili Kati ya Simba na Setif ndio inakamata nafasi ya 5 |
Sunday, December 30, 2012
EXCLUSIVE: KOCHA MPYA WA SIMBA ANATUA KESHO SAA 7 MCHANA
Baada ya kuibuka kwa maswali mengi juu ya lini hasa kocha mpya wa klabu ya Simba mfaransa Patrick Leiwing atakuja nchini Tanzania kuanza kazi, leo hii msemaji rasmi wa klabu bingwa ya Tanzania Ezekiel Kamwaga kupitia ukurasa wake wa Facebook amethibitisha kwamba Leiwing ataingia nchini kesho mchana wa saa saba na dakika kuja kuanza kazi ya kuinoa Simba inayojiandaa kwa ngwe ya pili ya ligi kuu ya Vodacom pamoja na michuano ya kimataifa |
YANGA YAWASILI SALAMA NCHINI UTURUKI
Kikosi cha mabingwa wa kombe la Kagame mara mbili mfululizo timu ya Young Africans imewasili salama katika mji wa Antalya kusini mwa nchi ya Uturuki majira ya saaa 10:30 jioni kwa saa za afrika mashariki na kati na moja kwa moja kupolekewa na wenyeji wake kampuni ya Team Travel.
Young Africans imefikia katika hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kilomita chahce kutoka katika uwanja wa ndege wa antalya, ambapo hoteli ya Fame Residence ipo mwambaoni mwa bahari ya mediteranian.
Mwanzoni Yanga ilikuwa ifikie katika hotel ya Sueno Beach Hotel iliyopo kilometa 70 kutoka uwanja wa ndege lakini jana siku moja kabla ya safari ilifanya mabadiliko na kuamua kuhamia katika hotel ya Fame Residence.
Wachezaji wamefurahi mandhari ya hotel kwani ni miongoni mwa hotel za nyota tano katika mjii huu wa Antalya hivyo wamefariijika na kuupa hongera uongozi kwa hatua waliyofikia ya kukubaliana na mwalimu kuweka kambi ya mafunzo nchini Uturuki.
Timu itaanza mazoezi kesho asubuhi katika viwanja vilivyopo katika eneo la hotel ya fame, ambapo kwa siku timu itakua inafanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.
Kuhusu hali ya hewa ni baridi kiasi na sio baridi kali kama ilivyokuwa inatangazwa na vyombo vya habari hapo awali.
Mtandao wa huu utaendelea kwa hisani ya mtandao wa rasmi wa Yanga (www.youngafricans.co.tz) utaendelea kuwajuza juu ya kila kitu kinachojiri nchini Uturuki.
SIMBA YATANDIKWA 3-0 NA TUSKER - KOCHA MZUNGU BADO KITENDAWILI
Kiungo
wa Simba, Mussa Mudde, akijaribu kupiga shuti mbele ya mchezaji wa
Tusker ya Kenya, katika mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki uliopiga leo
katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo, Simba
walipigwa bao 3-0.
KOCHA Mpya wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig, aliyetarajiwa
kuwapo uwanjani wakati kikosi hicho kilipomenyana na Tusker FC katika mchezo wa
kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ameshindwa kutokea uwanjani hapo
na kuwaacha midomo wazi mashabiki wa timu hiyo.
Awali katika taarifa yake, Simba ilidai kwamba Liewig
angetambulishwa rasmi kuinoa timu hiyo wakati wa mchezo huo, lakini kukosekana
kwake ni jambo lililowaacha njia panda mashabiki wa timu hiyo waliofurika
kwenye kumshuhudia kocha wao mpya.
Mechi hiyo ambayo ilitarajiwa na mashabiki wa timu hiyo
kwamba watashuhudia kikosi kamili kikishuka dimbani ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya duru la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza mwezi ujao,
badala yake ni kikosi B cha timu hiyo ndicho kilichoanzishwa.
Tusker FC ambao siku kadha zilizopita waliinyuka Yanga bao
1-0, waliendeleza makali yao na kuzichapa timu za hapa nchini baada ya kuinyuka
Simba mabao 3-0 katika mchezo wa
kirafiki uliofanyika kwenye dimba la Taifa, Dar es Salaam jana.
Mabao mawili ya Jesse Were na moja la Fredrick Onyango
yalitosha kuitoa kimasomaso Tusker katika mchezo ambao mashabiki wa Simba
walishindwa kupata burudani kutoka kwa nyota wao wa kimataifa kutokana na
kutokuwapo katika mchezo huo.
Katika mchezo huo, Simba ilianza kumtumia tena kiungo wake
mshambuliaji, Haruna Moshi 'Boban', aliyeingia kipindi cha pili kujaribu kuweka
mambo sawa, lakini mambo yaliendelea kuwa magumu kwa kikosi hicho cha Wekundu
wa Msimbazi.
Boban alicheza mechi hiyo akitokea kwenye adhabu ya kufungiwa
mechi kadha za duru la kwanza la Ligi Kuu Bara kwa madai ya kwamba ni utovu wa
nidhamu.
Kama timu tumeona hilo sio tatizo na kwamba kocha wetu
mtu atatua hapa nchini Jumatatu. Kuhusu wachezaji wengi, Okwi (Emmanuel) na
kipa wetu Abel Dhaira na Sunzu (Felix) watatua hapa nchini kesho (leo).
Kuhusu wale wachezaji waliokuwa kwenye timu ya taifa,
Kapombe (Shomari), Ngassa (Mrisho) na wengineo watajiunga rasmi na timu
Jumatatu.
Katika mchezo wa jana, Simba ilijaribu kufanya mabadiliko
kadha ya kuwaingiza wachezaji wake, Boban, Edward Christopher, Nassor Chollo,
Emily Isyaka, Salum Kinje, Jonas Mkude na Ramadhan Singano, lakini hakukuwa na
mabadiliko yoyote na hivyo hadi mwisho wa mchezo, Simba ilikubali kipigo.
Simba: William Mwete, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Hassan
Hatibu, Komain Keita, Mussa Mudde, Haroun Athuman, Abdallah Seseme, Abdallah
Juma, Ramadhan Chomo, Kiggy Makassy.
Tusker FC: Samwel Odhiambo, Luje Ochieng, Jeremiah Bright,
Mana Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Ombasa, Fredrick Onyango,
Jesse Were, Robert Omonuk. Refa: Hashim Abdallah kutoka Dar es Salaam.
SOURCE:http://handenikwetu.blogspot.com
YANGA WAPAA KWENDA UTURUKI USIKU HUU - WAPATA CHAKULA CHA USIKU PAMOJA KABLA YA KUONDOKA
Nizar Khalfan akiwa kwenye foleni ya kwenda kuchukua msosi kabla ya safari ya kwenda Uturuki leo usiku |
Seif Ahmed 'magari' kulia akiteta jambo na Abdallah Bin Kleb wakati wa chakula cha jioni na wachezaji katika Hotel ya Protea Oysterbay |
Kocha Mkuu Brandts, kocha wa makipa Razaki Siwa kulia na makmu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga aliyeipa camera mgongo |
HAMISI KIIZA |
JERRY TEGETE NA DOMAYO |
Ladislaus Mbogo akiwa na Nadir Haroub Canavaro Uwanja wa Ndege JK Nyerere — |
Meneja wa timu Hafidh Saleh — in Dar es Salam. |
Viongozi wa Yanga wakiwa uwanja wa ndege |
MKUTANO MKUU WA TASWA - RIDHIWANI APONDA UENDESHWAJI WA VILABU - ASISITIZA MAFUNZO ZAIDI KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO
Ridhiwani Kikwete, akizungumza wakati akifungua rasmi mkutano Mkuu wa
Chama cha Waandishi wa habari za michzo Tanzania TASWA, uliofanyika
kwenye Hoteli ya Kiromo, mjini Bagamoyo leo mchana.
Katibu Mkuu wa TASWA Amir Mhando akizungumza kwenye mkutano huo |
Shafii Dauda akiwa na Asha Muhaji. |
Baadhi ya wanachama wakifuatilia mkutano huo wakati ukiendelea katika Hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo leo mchana. |
Amir Mhando, akichangia mada..... PICHA ZOTE KWA HISANI YA http://bashir-nkoromo.blogspot.com/
Saturday, December 29, 2012
WENGER: SITOMSAJILI DEMBA BA - SIJAKATA TAMAA KUMRUDISHA HENRY
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema, hana nia ya kumsajili mshambulizi wa Newcastle Demba Ba.
Ba, 27, ameonyesha mchezo mzuri msimu huu na tayari amefunga magoli 11 msimu huu.Mshambulizi huyo kutoka Senegal alifunga magoli kumi na sita msimu uliopita.
Kocha wa Newcastle Alan Pardew amekiri kuwa Ba, huenda akauzwa ikiwa hataondoa kipengee kimoja katika mkataba wake unaosema klabu yeyote inaweza kumsajili mchezaji huyo mradi ilipe pauni milioni saba.
''Namkubali sana Demba Ba'' alisema Wenger.'' lakini ukiniuliza ikiwa tutamsajili Demba Ba basi jibu langu ni hapana''
Wenger aliongeza kusema kuwa huu sio wakati muafaka wa kuzungumzia suala hilo, kwa kuwa yeye ni mpinzani wetu kwa sasa.
Arsenal ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimehusishwa na mchezaji huyo ambaye alijiunga na Newcastle kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka klabu ya West Ham, Juni mwaka uliopita.
Wakati huo huo, Wenger amesema hajakata tamaa ya kumsajili mshambulizi wake wa zamani kutoka Ufaransa Thierry Henry, kwa mara ya tatu kwa mkataba wa muda mfupi.
Thiery ambaye aliifungia Arsenal Magoli mawili msimu uliopita, amekuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo tangu kumalizika kwa ligi kuu ya Marekani MLS.
KABANGE TWITE AZUIWA KUCHEZA YANGA NA TFF
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemzuia kiraka Kabange Twite kuchezea Yanga hadi pale suala lake litakapoamuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba,aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kuwa Kabange hatacheza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwani suala lake liko mikononi mwa Fifa baada ya Yanga kushindwa kupata idhini ya FC Lupopo ya kumsajili mchezaji huyo aliyesaini mkataba wa miaka miwili Jangwani.
Kamati ya Haki za Wachezaji ya Fifa ndio itatakiwa kumuidhinisha kwani muda wa mwisho wa kuwasajili wachezaji wa kigeni ulikuwa Desemba 15 ilivyokuwa imepangwa na TFF.
Licha ya kwamba atakuwapo kwenye msafara wa Yanga utakaoondoka kesho Jumapili alfajiri kwenda kambini Uturuki, Tekinolojia ya Uhamisho wa Wachezaji kwa Kompyuta (TMS) ndio imetibua mipango ya Kabange kujiunga na pacha wake Mbuyu Twite, ambaye alijiunga na Yanga mwezi Agosti mwaka huu.
Kawemba alisema kuwa viongozi wa Yanga walifanya mawasiliano na watu wa Lupopo kwa TMS, lakini hawakupata majibu yoyote.
Yanga waliwasiliana na Lupopo masaa mawili kabla ya dirisha dogo la usajili wa wachezaji wa kigeni kufungwa Desemba 15, alisema Kawemba.
Hata hivyo walikwama kwani hawakupata majibu yoyote kutoka kwa watu wa Lupopo.
Fifa ilianzisha utaratibu wa uhamisho wa wachezaji kwa njia ya TMS, ambayo husaidia klabu kuwasiliana moja kwa moja
na pia vyama vya soka vya nchi husika vikifuatilia mawasiliano hayo kwa ukaribu.
Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndio ilikuwa inammiliki mchezaji huyo kama ilivyokuwa kwa pacha wake, Mbuyu.
Kawemba alisema kufuatia hali hiyo, Yanga wanapaswa kusubiri mawasiliano kutoka kwenye klabu hiyo kwenye TMS.
Alisema, hata hivyo, pale watakapopata majibu ya Lupopo ndio taratibu zitaanza kushughulikiwa na TFF lakini wenye maamuzi ya mwisho watakuwa Fifa.
Yanga wakipata mawasiliano na Lupopo watapaswa kurudi kwetu ili tupeleke suala lao Fifa, alisema.
Itabidi tuwaeleza sababu za kuridhisha Fifa kuwa kwanini Yanga waliingia TMS muda mfupi kabla ya muda wa mwisho wa usajili, pia (Fifa) watapenda kujua sababu za Lupopo kuchelewa kujibu.
Kawemba alidokeza ikiwa Kamati ya Haki za Wachezaji itaridhika na maelezo ya pande hizo mbili basi watatoa kibali lakini wasiporidhika basi watamzuia Kabange kuchezea Yanga.
Aliongeza kuwa Kamati ya Haki na Uhamisho Wachezaji ndio yenye uamuzi wa mwisho na kuongeza ikiwa Yanga watanyimwa kibali basi hawatakuwa na ubavu wa kukata rufaa kokote.
Hakuna chombo chenye mamlaka juu ya Kamati ya
Haki na Usajili ya Fifa. Kwa hiyo Yanga wanapaswa kuelewa hilo, aliongeza.
Ninawashauri Yanga wafanye kila njia wawapate Lupopo kwani kadiri watakavyochelewa ndio watakuwa wanajiweka pabaya zaidi.
Hatua hiyo itakuwa pigo kwa Yanga kwani ilikuwa inamtegemea Kabange angeimarisha kikosi chao kutokana na umahiri wake wa kucheza nafasi nyingi.
Kama ilivyokuwa Mbuyu, kiraka huyo alikuwa ametolewa kwa mkopo kwenye timu ya APR ya Rwanda na Lupopo.
Lupopo ndio ilikuwa inatakiwa kuidhinisha uhamisho wa nyota huyo kwa njia ya TMS lakini bahati mbaya utaratibu huo umekuwa ukitumika kwa nadra nchini Congo kwa kuwa timu zao nyingi ni za ridhaa.
Kama ikishindikana, Yanga itakuwa ina wachezaji wanne tu wa kigeni baada ya kumwachia kipa Yaw Berko, ambaye amejiunga na Lupopo.
Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano na usajili wa Yanga Abdallah Binkleb aliiambia Mwanaspoti jana akisema: Sisi tulikamilisha kila kitu, tatizo liko kwao Lupopo na tumeshawaeleza TFF tunasubiri jibu nadhani kesho (leo Jumamosi) tutapata ufafanuzi zaidi.
SAMSON MFALILA - MWANASPOTI
Friday, December 28, 2012
MEIRELES APUNGUZIWA ADHABU YA KUFUNGIWA MECHI 11 MPAKA MECHI 4 - YATHIBITIKA HAKUMTEMEA MATE MWAMUZI
Mchezaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea kiungo Raul Meireles amepata nafuu ya kupunguziwa adhabu ya kutocheza mechi 11 mpaka kufikia mechi 4.
Shirikisho la soka la Uturuki limesema ilikuwa ni vigumu kwa mchezaji kutema mate kwa kuwa alikuwa anaongea wakati wote wa tukio hilo, hata hivyo bado atakabiliwa na adhabu ya kukosa mechi nne kwa kumtukana mwamuzi.
JINA LA ZLATAN LAONGEZWA KATIKA KAMUSI YA SWEDEN
Hii imekuja kama kumtunuku mchezaji huyo ambaye amekuwa akiletea sifa nchi hiyo ndani na nje ya nchi hiyo kwa miaka takribani 10 sasa.
Neno 'Zlatanera' limetokana na neno la kifaransa 'zlataner' lenye maana ya kutawala, hivyo wasweden wakalinyambua na kuongeza herufi 'a' katika 'zlataner'.
FEDHA ZILIZOCHUKULIWA NA TRA KWENYE AKAUNTI YA TFF NI ZA VILABU VYA LIGI KUU - VYATISHIA KUGOMEA LIGI WASIPORUDISHIWA
Klabu
14 ambazo timu zao zinashiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimesema hazitacheza
hatua ya pili ya Ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 26 mwakani hadi
zitakaporejeshewa fedha zao zilizochukuliwa na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kutoka kwenye moja ya akaunti za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).
Novemba
23 mwaka huu, TRA kwa uwezo ilionao kisheria iliielekeza benki ya NMB
kuilipa fedha hizo (sh. 157,407,968) kutoka kwenye moja ya akaunti za
TFF ikiwa ni Kodi ya Lipa Kama Unavyopata (PAYE) kutoka kwenye mishahara
ya waliokuwa makocha wa timu za Taifa.
Serikali
ndiyo inayolipa mishahara ya makocha hao moja kwa moja kwenye akaunti
zao, lakini ilikuwa haikati PAYE kutoka kwenye mishahara hiyo, hivyo
malimbikizo kufikia sh. 157,407,968.
TFF
bado inaendelea na mazungumzo na pande husika (Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande mmoja na TRA kwa upande
mwingine) ili fedha hizo zirejeshwe kwani zilitolewa na mdhamini wa Ligi
Kuu (kampuni ya Vodacom) kwa ajili ya maandalizi ya timu hizo tayari
kwa mzunguko wa pili wa Ligi hiyo.
OFISA WA CAF KUTUA MWAKANI KUKAGUA VIWANJA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa wake Abbas
Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano
inayoandaliwa na Shirikisho hilo.
Ofisa
huyo kutoka Uganda atawasili nchini Januari 7 mwakani ambapo
anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14 mwakani na baadaye kupeleka
ripoti yake CAF.
Utekelezaji
wa kazi yake nchini utahusisha mwakilishi kutoka TFF, mwakilishi kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mameneja wa viwanja
husika na Ofisa Usalama wa TFF.
HAWA NDIO WACHEZAJI WANAOENDA NA YANGA UTURUKI JUMAPILI - NANI KATOSWA??
Mabingwa mara mbili mfululizo wa Kombe la Vilabu Bingwa Afrika
Mashariki al maarufu(Kagame Cup )timu ya Young Africans inatarajia
kuondoka alfajiri ya jumapili kuelekea nchini Uturuki ambako itaweka
kambi ya mazoezi kwa muda wa wiki mbili.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga/Jangwani, Afisa Habari wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema timu itaondoka alfajiri ya jumapili kwa shirika la ndege la Turkish Airline, ambapo itakua na msafara wa watu 34, wachezaji 27 na viongozi 7.
Timu itaondoka majira ya saa 10:30 alfajiri na itafika katika mji wa Instabul majira ya saa 5 kasoro dakika 10, kisha baadae majira ya saa 9 alasiri itaondoka kwenda katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa nchi ya Uturuki ambapo itafika saa 10 ndio haswa itakapokuwa kambi ya timu alisema 'Kizuguto'
Kizuguto amesema timu itafikia katika hotel ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Majina ya watakosafiri keshokutwa alfajri ni:
Walinda Mlango: Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul
Walinzi wa Pemebeni: Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stephano Mwasika na Oscar Joshua
Walinzi wa kati: Mbuyu Twite, Nadir Haroub, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani
Viungo: Athumani Idd, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari na Omega Seme
Viungo wa Pembeni: Saimon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerson Tegete, George Banda na Hamis Kiiza
Viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni
Kocha Mkuu: Ernest Brandts,
Kocha msaidizi: Fred Felix Minziro,
Kocha wa makipa: Razaki Siwa,
Daktari wa timu: Dr.Suphian Juma,
Meneja wa timu: Hafidh Saleh,
Afisa wa Habari : Baraka Kizuguto
na kiongozi mkuu wa msafara: Mohamed Nyenge ambae ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga/Jangwani, Afisa Habari wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema timu itaondoka alfajiri ya jumapili kwa shirika la ndege la Turkish Airline, ambapo itakua na msafara wa watu 34, wachezaji 27 na viongozi 7.
Timu itaondoka majira ya saa 10:30 alfajiri na itafika katika mji wa Instabul majira ya saa 5 kasoro dakika 10, kisha baadae majira ya saa 9 alasiri itaondoka kwenda katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa nchi ya Uturuki ambapo itafika saa 10 ndio haswa itakapokuwa kambi ya timu alisema 'Kizuguto'
Kizuguto amesema timu itafikia katika hotel ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Majina ya watakosafiri keshokutwa alfajri ni:
Walinda Mlango: Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul
Walinzi wa Pemebeni: Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stephano Mwasika na Oscar Joshua
Walinzi wa kati: Mbuyu Twite, Nadir Haroub, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani
Viungo: Athumani Idd, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari na Omega Seme
Viungo wa Pembeni: Saimon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerson Tegete, George Banda na Hamis Kiiza
Viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni
Kocha Mkuu: Ernest Brandts,
Kocha msaidizi: Fred Felix Minziro,
Kocha wa makipa: Razaki Siwa,
Daktari wa timu: Dr.Suphian Juma,
Meneja wa timu: Hafidh Saleh,
Afisa wa Habari : Baraka Kizuguto
na kiongozi mkuu wa msafara: Mohamed Nyenge ambae ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya
Thursday, December 27, 2012
KENYA YATOA MAREFA WAWILI KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA - TANZANIA, UGANDA MMMMMMH
Waamuzi wawili wakubwa nchini Kenya wamechaguliwa kwenda nchini Afrika ya Kusini kwenda kuamua mechi ya Africa Cup of Nations (Afcon) zitakazoanza mwezi ujao huko kusini mwa bara la afrika.
Aden Marwa, ambaye ni mwalimu kutoka Nyanza kusini, amechaguliwa pamoja na refa mwingine Sylvester Kirwa, kutoka Eldoret.
Wawili hao wamechaguliwa kuamua mechi za michuano hiyo baada ya kushiriki katika kozi ya CAF ya marefa iliyofanyika huko Egypt mapema mwezi uliopita.
Marefa hao wa pekee kutoka ukanda huu wa Afrika mashariki wataenda South Africa siku ya jumanne tarehe 15, siku nne kabla ya michuano kuanza.
Marwa – ambaye alishiriki katika 2012 AFCON, zilizofanyika nchini Gabon na Equatorial Guinea – amesema kuchaguliwa kwao kwenda AFCON ni ishara nzuri kwa soka la Kenya.
Aden Marwa, ambaye ni mwalimu kutoka Nyanza kusini, amechaguliwa pamoja na refa mwingine Sylvester Kirwa, kutoka Eldoret.
Wawili hao wamechaguliwa kuamua mechi za michuano hiyo baada ya kushiriki katika kozi ya CAF ya marefa iliyofanyika huko Egypt mapema mwezi uliopita.
Marefa hao wa pekee kutoka ukanda huu wa Afrika mashariki wataenda South Africa siku ya jumanne tarehe 15, siku nne kabla ya michuano kuanza.
Marwa – ambaye alishiriki katika 2012 AFCON, zilizofanyika nchini Gabon na Equatorial Guinea – amesema kuchaguliwa kwao kwenda AFCON ni ishara nzuri kwa soka la Kenya.
CHRIS KATONGO ATUNUKIWA NA WANAJESHI WENZAKE ZAMBIA
Nahodha wa mabingwa wa Afrika Chris Katongo ametunukiwa na jeshi la Zambia.
Katongo, ambaye ni ofisa wa jeshi la nchi hiyo, alitunukiwa tuzo ya heshima ya jeshi la Zambia na meja jenerali Toply Lubaya katika sherehe zilizofanyika huko Arakan barracks mwanzoni mwa wiki hii.
Tuzo hii ya heshima imekuja baada ya mshambuliaji huyo wa Zambia kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa BBC African Footballer of the Year award.
Jeshi la nchi hiyo pia lilitoa tuzo na maua kwa wachezaji wengine wa Chipolopolo ambao ni maofisa wa jeshi - Felix Katongo na Nathan Sinkala.
Katongo, ambaye ni ofisa wa jeshi la nchi hiyo, alitunukiwa tuzo ya heshima ya jeshi la Zambia na meja jenerali Toply Lubaya katika sherehe zilizofanyika huko Arakan barracks mwanzoni mwa wiki hii.
Tuzo hii ya heshima imekuja baada ya mshambuliaji huyo wa Zambia kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa BBC African Footballer of the Year award.
Jeshi la nchi hiyo pia lilitoa tuzo na maua kwa wachezaji wengine wa Chipolopolo ambao ni maofisa wa jeshi - Felix Katongo na Nathan Sinkala.
Subscribe to:
Posts (Atom)