Klabu
14 ambazo timu zao zinashiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimesema hazitacheza
hatua ya pili ya Ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 26 mwakani hadi
zitakaporejeshewa fedha zao zilizochukuliwa na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kutoka kwenye moja ya akaunti za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).
Novemba
23 mwaka huu, TRA kwa uwezo ilionao kisheria iliielekeza benki ya NMB
kuilipa fedha hizo (sh. 157,407,968) kutoka kwenye moja ya akaunti za
TFF ikiwa ni Kodi ya Lipa Kama Unavyopata (PAYE) kutoka kwenye mishahara
ya waliokuwa makocha wa timu za Taifa.
Serikali
ndiyo inayolipa mishahara ya makocha hao moja kwa moja kwenye akaunti
zao, lakini ilikuwa haikati PAYE kutoka kwenye mishahara hiyo, hivyo
malimbikizo kufikia sh. 157,407,968.
TFF
bado inaendelea na mazungumzo na pande husika (Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande mmoja na TRA kwa upande
mwingine) ili fedha hizo zirejeshwe kwani zilitolewa na mdhamini wa Ligi
Kuu (kampuni ya Vodacom) kwa ajili ya maandalizi ya timu hizo tayari
kwa mzunguko wa pili wa Ligi hiyo.
OFISA WA CAF KUTUA MWAKANI KUKAGUA VIWANJA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa wake Abbas
Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano
inayoandaliwa na Shirikisho hilo.
Ofisa
huyo kutoka Uganda atawasili nchini Januari 7 mwakani ambapo
anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14 mwakani na baadaye kupeleka
ripoti yake CAF.
Utekelezaji
wa kazi yake nchini utahusisha mwakilishi kutoka TFF, mwakilishi kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mameneja wa viwanja
husika na Ofisa Usalama wa TFF.
No comments:
Post a Comment