Waamuzi wawili wakubwa nchini Kenya wamechaguliwa kwenda nchini Afrika ya Kusini kwenda kuamua mechi ya Africa Cup of Nations (Afcon) zitakazoanza mwezi ujao huko kusini mwa bara la afrika.
Aden Marwa, ambaye ni mwalimu kutoka Nyanza kusini, amechaguliwa pamoja na refa mwingine Sylvester Kirwa, kutoka Eldoret.
Wawili hao wamechaguliwa kuamua mechi za michuano hiyo baada ya kushiriki katika kozi ya CAF ya marefa iliyofanyika huko Egypt mapema mwezi uliopita.
Marefa hao wa pekee kutoka ukanda huu wa Afrika mashariki wataenda South Africa siku ya jumanne tarehe 15, siku nne kabla ya michuano kuanza.
Marwa – ambaye alishiriki katika 2012 AFCON, zilizofanyika nchini Gabon na
Equatorial Guinea – amesema kuchaguliwa kwao kwenda AFCON ni ishara nzuri kwa soka la Kenya.
Ni changamoto kwa TFF na chama cha marefa,sijui kama kuna kitu wamejifunza kupitia waamuzi hawa au ndio zaidi ya kuwapongeza na kujisifia ukanda wetu umetoa waamuzi tu basi..KWANINI ISIWE TANZANIA...??? Hili ndilo swali ambalo wanapaswa walijadili na kulitolea majibu kwa vitendo..
ReplyDelete