Search This Blog

Thursday, September 12, 2013

TUHUMA ZA KUKAMATWA NA MADAWA KWA WANAMICHEZO, NI MSINGI MBAYA ULIOACHWA NA VIONGOZI WALIOPITA



Na Baraka Mbolembole

Pesa siyo kila kitu katika maisha, ila mwanadamu anatakiwa kuwa na kiasi Fulani cha  pesa ili kumuwezesha kuishi katika jamii yake anayoishi. Mtu anatakiwa kufanya kazi ili apate kipato chake halali, na kumuwezesha kupata mahitaji yake muhimu ( Chakula, Mavazi, na Malazi). Pesa ni sabuni ya roho, lakini Hasara ‘Roho’, pesa ni makaratasi tu. Kila binadamu atakula kutokana na urefu wa kamba yake, na Yule asiyefanya kazi na asile ‘asilani’, ndivyo maandiko ya mwenyezi Mungu.

Tamaa ya kupata kipato cha haraka, ni chukizo kwa mwenyezi Mungu, labda kama matendo yanayokuingizia kipato chako ni ya halali, na yanayompendeza mwenyezi Mungu na kukubalika katika jamii. ‘ Wingu’ zito limetanda katika ‘anga’ ya Tanzania, wiki moja iliyopita kuna meli kubwa iliyokuwa imebeba zaidi ya tani 30 za Bangi, ilikamatwa pembezoni ya nchi ya Italia, bendera waliyokuwa wanaitumia katika meli hiyo ni ya…… Ni aibu kuitaja lakini ndiyo ukweli huo. Na huko inatangazwa kuwa ni…….TANZANIA.

Vita dhidi ya madawa ya kulevya katika miaka michache iliyopita ilikuwa inawahusisha, Polisi na wavutaji, wale mawakala, na wauzaji pamoja na wananuzi wakubwa hawakuwa wakiguswa. Miaka imekwenda, na kuwakamata wavutaji pekee ya kuacha mizizi yake ikiendelea kuchipua imekuwa ni tatizo kubwa kwa nchi yetu. Sasa, serikali za nchi ambazo hazihitaji ‘SEMBE’ katika ardhi ya nchi zao imekuwa ikitusaidia kuwakamata, wasafirishaji na waingizaji ‘ ulevi huo haramu kwa wananchi wao’ kuwakamata na kuwahukumu, Watanzania wenzetu ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao Fulani katika jamii kufanya biashara hiyo haramu.

Kumbuka kuhusu wale mabondia ambao walikamatwa huko Visiwa vya Komoro na kuhumiwa vifungo vya miaka 15. Wanamichezo wamekuwa wakitumia kila sifa zao nzuri wanazozipata kutokana na vipaji vyao kuwaadaa, maafisa wa polisi na kupitisha biashara hiyo haramu. Ni msingi mbaya ambao mimi tangu nikiwa na miaka saba, wakati timu ya Simba ikichezea fainali ya kombe la Caf dhidi ya Stella Abdjan, na kufungwa nimekuwa nikisikia habari za uwepo wa usafirishaji wa  madawa ya kulevya kutumia wanamichezo. Niliwahi kusikia mengi tu, lakini sasa kukamatwa kwa wasanii maarufu nchini, wachezaji maarufu, mabondia maarufu, na wanasoka maarufu wakiwa na ‘ mizigo’ ya mabilioni ya shilingi katika nchi mbalimbali barani Afrika, Asia, ni muendelezo wa ukweli ambao ulikuwa ukifichwa nchini kwetu.

Ni msingi mbaya uliwekwa na viongozi wetu waliopita katika sekta mbambali, na hata kwa wanamichezo hatua ambazo nchi yetu imefika ya kukosa walau medali ya shaba katika michuano ya Olimpiki, Madola, ama ile ya Afrika ni dalili kuwa viongozi wetu waliopita waliacha msingi mbaya. WAlikuwa ni wafanyabiasha wakubwa wa kimataifa ambao muda wote walipanga mipango ya namna ya kuingiza na kutoa biashara zao haramu. Sasa wanakamtwa, nje ya nchi, wanalitia aibu Taifa, wanatia aibu thamani ya bendera ya nchi yetu. Lakini walipata wapi, ujasiri huo? ‘Mtoto wa nyoka ni nyoka. Na ukiishi na mwizi na wewe utakuwa mwizi’’ na ndicho kinachoonekana sasa, kuwa wachezaji ambao walitumia vibaya vipaji vyao na wakati wao wa uchezaji, wameamua kuingia wao wenyewe katika biashara hii, sijui ni kwa ‘mgongo wa nani’ ila ni kutokana na kile ambacho walikuwa wakikiona au  kufanya wakiwa chini ya misingi ambayo viongozi wetu waliijenga.

Na ilikuwaje kuhusu safari yako ya Ujerumani, tuliambiwa ulikwenda kufanya majaribio ? Kuna mchezaji niliwahi kumuuliza swali hili, naye akanijibu

Bwana Kule kiukweli kuna Siri nzito maana hata aliyenipeleka kanisihi sana nisiseme , lakini nilifanya majaribio kwa mwezi mzima,  ila ikatokea ishu ambayo ile timu hawakupendezwa nayo ikabidi nirudi nyumbani”

Nikamuuliza tena,

Ilikuhusu wewe au, na nani aliyekuwa wakala aliyekusimamia katika safari ile?

“  Haikunihusu mimi, ilimuhusu wakala wangu”

 Nikaendelea kudadisi….

Labda kwa ufupi kitu gani kilitokea kwani ulipata muda mrefu wa kujaribiwa?

“ Kweli nilipata muda mrefu kule, ila Daah! Ila kweli suala lililotokea siwezi  kusema kaka”

 Huyu ni mchezaji wa timu ya taifa na klabu kubwa nchini. Umewahi kuchunguza muda ambao wachezaji wetu huchukuliwa na mawakala na kupekwa nje ya nchi kufanya majaribio? Huwa ni kipindi ambacho dirisha la usajili limekuwa limefungwa, ndiyo hatukatai kuwa mchezaji anaweza kufanya vizuri na baadae akapewa nafasi ya kusajiliwa wakati wa usajili ukufika. Lakini ni wangapi ambao tumekuwa tukiambiwa kuwa wamefuzu, na watarudi tena wakati wa usajili na tunaendelea kuwaona katika viwanja vya Tanzania. Soka la kisasa linaenda kisasa, muda ni muhimu kuzingatiwa, rekodi ni muhimu na video ni muhimu pia.

Tazama tangu safari za Mrisho Ngassa, West Ham, na Seatlle Sounders, Abdulhalim Humud, Afrika ya Kusini, Mussa Hassan Mgosi, India, Shadrack Nsajigwa, Ufaransa, Zahoro Pazi, Ujerumani, na Afrika ya Kusini, wote hawa tuliambiwa wamefuzu majaribio walipokwenda kufanya na wangerudi tena. Kweli, Ngassa karudi Tena Yanga, Humud karudi tena, Simba, Zahoro kahama Azam katua Simba, Mgosi amerudi Mtibwa Sugar tena, kweli majira yanakwenda haraka sana. Biashara kwanza michezo baadae, kwa mwanasoka, kucheza soka la kulipwa hakutakuja kwa maribio bali ni kuonesha kiwango kama Mbwana Samatta na kutoka nje. Labda kama tutawaondoa wafanyabiashara wakubwa katika mpira.

 AFANDE SELE, mwanamuzi mshindi wa tuzo ya mfalme wa mashairi nchini aliwajhi kuimba Pesa, na kusema…..

" Achinjwe binadamu, na pesa ipakazwe damu...., Watu wataifuta, kisha wataitumia...., Watanunulia, misahafu na bibilia, na waumini wataipokeaaa...

 WATU, NAZO PESA... wewe zinakutesaaa,
MIMI ZINANITESAAA, pesaaa....
“Kweli, pesa ni tamu saaana, Ni tamu kwa kila namnaaa..., Kijana akikamata, madingi watamwita bwana... Dingi akikamata anaonekana ni kijanaaa..."

  0714 08 43 08

ROBIN VAN PERSIE AMPITA BERGKAMP KWA MABAO UHOLANZI - BADO MAWILI AMFIKIE KLUIVERT NA KUWA MFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE WA TAIFA HILO


ROBIN VAN PERSIE amemfunika gwiji wa soka wa Uholanzi Denis Bergkamp kwa kufunga mabao mengi katika listi ya washambuliaji wa nchi hiyo walioifungia The Oranje mabao mengi.

Van Persie anakaribia kuwa mfungaji bora wa muda wote kwa taifa lake.

Mabo yake mawili aliyofunga jzui yamefanya ampite mchezaji mwenzie wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkamp mwenye mabao 38, wakati Van Persie akiwa na mabao 38.

Van Persie sasa anashika nafasi ya pili nyuma ya Patrick Kluivert, ambaye ana mabao 40, na sasa kwa hakika ni suala la muda tu kabla ya Van Persie kumfikia na kumpita mshambuliaji huyo wa zamani wa FC Barcelona.

Mshambuliaji huyu wa Manchester United alifunga goli la kwanza akiwa na jezi ya Uholanzi mnamo mwaka 2005, alipoweka kimiani goli la nne katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Finaldn katika michuano ya kugombea kufuzu kucheza kombe la dunia 2006.

MESUT OZIL AWASILI MAKAO MAKUU YA ARSENAL KWA MARA YA KWANZA TANGU ALIPOSAJILIWA




KALI YA LEO: SAN MARINO WAFUNGA GOLI LA KWANZA KATIKA MIAKA 5 - WASHANGILIA KAMA WAMETWAA UBINGWA WA DUNIA


Kwa nchi inayoshika nafasi ya 207 kwa ubora wa viwango vya soka duniani kama San Marino, soka la kimataifa ni jambo la kujifurahisha kwa kupata nafasi ya kucheza na mstaa wa timu mbalimbali barani humo. Wiki iliyopita, walifungwa 9-0 na Ukraine — matokeo mabovu kwa timu yoyote ile, lakini ulikuwa ni kama mchezo mwingine kwa kikosi cha San Marino.

Wakielekea katika mchezo wa kugombea kufuzu kombe la dunia dhidi ya Poland, timu hiyo ilikuwa haijashinda mchezo wowote wa kugombea kwenda Brazil katika mechi 7 zilizopita huku wakiruhusu wao kuguswa mara 38. Wakati Poland walipofunga katika dakika ya 10, ilionekana ingekuwa kama kawaida, lakini katika dakika ya 22, San Marino walifunga bao lao la kwanza katika mechi ya mashindano ndani ya kipindi cha miaka 5. Goli la kichwa kutokana kwa mchezaji ambaye ni mhasibu wa benki  Alessandro Della Valle. 
Mara ya mwisho San Marino walifunga goli katika mchezo wa kimashindano katika mchezo dhidi ya Slovakia mwaka 2008 katika harakati za kufuzu kucheza kombe dunia dhidi ya Poland ambapo walifungwa  5-1, Poland.
Na sasa timu ambayo inashika nafasi ya 205 Andorra inabaki kuwa ndio pekee iliyocheza mechi 8 za kugombea kufuzu kwenda Brazil 2014 bila kufunga bao.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                               

Wednesday, September 11, 2013

PICHA YA SIKU: CRISTIANO RONALDO NA GARETH BALE WALIPOKUTANA KWA MARA YA KWANZA MAZOEZINI LEO

ADHABU YA MAREFA SAANYA NA ONESMO, YAONYESHA KWAMBA YANGA NI TIMU YA WANANCHI



Imeandikwa na Baraka Mbolembole
Mtu ‘ mkubwa’ ni mwanafunzi, kwani huona mbali zaidi na kwa kuona kwake huko hutamani vitu zaidi kuliko watu wengine. Lakini ukweli ni kwamba mtu huyo hata kama atakuwa na uwezo wa kuona mbali zaidi, au awe na akili nyingi zaidi, ukweli hawezi kubadili mwendo wa historia. Kitu ambacho anaweza kufanya ni kubadilisha matukio Fulani. Ni kutokana na mambo kama haya ndipo viongozi wakubwa hutokea.
Fasihi ni taaluma, Taaluma ni elimu, na elimu ni maisha. Mtu huzaliwa na akili. Katika makuzi yake, mtu husikia, huona, huonja, hunusa na hutenda. Vitendo hivi ndiyo msingi wa kutumia akili ili kupata elimu. Hivyo elimu ya kwanza na sehemu kubwa na sehemu kubwa ya elimu ya maisha hupatikana nje ya darasa. ‘ Yaani, Maisha kutokana na vionjo vya mwili’ . Tunajifunza ili tuishi, na katika maisha yetu tunakutana na marafiki wa kila aina, kwa wanasoka maisha yao mengi hutumia kutengeneza marafiki wa dhati kutoka katika family ya soka. Urafiki ni Uadui, au Uadui ni Urafiki?
Dunia hadaa. Kwa mtu ambaye hajawajhi kufika pwani na kuiona bahari, anaweza kudanganywa kuwa maji ya bahari ni ‘mekunde’. Kama ni rahisi, mtu huyo anaweza kudanganyika kuwa maji ya bahari ni mekundu. Hatari ya uongo siku zote iko wazi. Itatokea siku mtu huyo ‘ mjinga’ asiyeijua bahari, akajifunga na kufanya safari ili aje kuhakikisha uwepo wa maji mekundu ya bahari. Apatapo ukweli na kubaini kuwa alidanywa, mtu huyo atamuamini tena mtu aliyempatia habari hizo hata kama atakuwa akizungumza ukweli wakati mwingine.

Usaliti kwetu sisi mashabiki upo siku zote, Martin Saanya, na aliyekuwa mwamuzi wake msaidizi, Jesse Onesmo wamekutwa na adhabu ya kufungiwa kutochezesha soka kwa muda wa mwaka mmoja. Waamuzi hao walichezesha mchezo kati ya Yanga na Coastal Union, septemba 28 na kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.
Waamuzi hao, wenyeji wa mkoani Morogoro wamefungiwa kwa kuwa walishindwa kuendana na kasi ya mchezo na kujikuta wakifanya makosa ya mara kwa mara. Adhabu ya kiki ya penati ambayo Saanya aliitoa kuelekea katika lango la Yanga, dakika ya mwisho ya mchezo na kutengeneza matokeo ya sare ndiyo iliyowaletea matatizo, na kupelekea wakapata adhabu kubwa. Sifikirii kama angepewa adhabu hiyo kama angetoa wakati Yanga wakisaka bao la kusawazisha. Waamuzi hawa ni kweli waliboronga, na mechi ilikuwa kubwa kwao. Lakini ukichunguza hatua kwa hatua ambazo walizitumia kufanya maamuzi na kuusimamia mchezo ule, utagundua kuwa makosa waliyofanya yalikuwa ni ya kibinadamu, na mkwaju wa ' utata'  wa penati kwangu mimi nauchukulia kama sehemu ya kawaida ya mchezo wa soka.
NI,KWELI, SAANYA, ONESMO WALIBORONGA, lakini  adhabu walizopewa ni kama ziliandaliwa. Sijui ni wapi lakini nakumbuka wakati Fulani nilikutana na Mwamuzi, Othman Kazi, kiukweli nilitaka kujua kwa nini alifungiwa. Akaniambia kuwa kuna watu walikuwa hawamtaki kwa sababu wanazozijua wao. Kina, nani hao? “ Nasubiri muda wao madarakani umalizike ndiyo nitarudi kuchezesha tena soka” aliwahi kuniambia Kazi, ambaye aliwahi kukutwa na adhabu kubwa ya kufungiwa kwa kosa alilodai kuwa si la kweli. Alifungiwa kwa madai ya kupokea hela kutoka mahali Fulani waawakati Fulani mjini Bukoba. Aliniambia mambo mengi sana kuhusu kazi yao ya uamuzi na matatizo ya ubinafsi yaliyopo katika chama chao.  
Wakati mwingine ni lazima chama cha waamuzi kiwasemee waamuzi hasa wanapokutana na adhabu ambazo zinakuwa ni kali zaidi na ambazo zinaweza kuwafanya wakashindwa kuaminiwa tena, hata pindi watakaporudi uwanjani baada ya adhabu kumalizika.
Kitu, gani ambacho kimemfanya Saanya, na Onesmo wahukumiwe? Ni kuiadhibu Yanga katika ‘muda mbaya’, nafikiri tu kama adhabu ile ingetolewa katika lango ya Coastal mambo yangekuwa makubwa kiasi hiki. Hapana, LAKINI imekuwa tatizo kubwa hadi katika kazi yake, kwa kuwa aliamua mkwaju wa penati. Katika mechi kama ile, katika muda kama ule, katika kipindi ambacho timu nzima ya Coastal ilikuwa ikicheza katika eneo la hatari la Yanga, ilikuwa ni lazima Saanya ‘ afunike mkono wake’ haijalishi mpira ulimgonga mahali gani Haruna Niyonzima. Yanga walikuwa wakiomba mechi imalizike na presha ya Coastal ilikuwa juu kuliko muda wowote ule wa mchezo.
Adhabu yake ni fundisho kwa waamuzi wote ambao huishia kuchezesha mechi kwa namna wanavyopangiwa na watu au vile watakavyo wao. Soka letu haliwahitaji waamuzi ‘ wazembe’, soka letu haliwahitaji waamuzi kama Saanya ambao hawawezi kuendana na kasi ya mchezo, soka letu linawahitaji waamuzi kama Saanya ambao wana uwezo wa kufanya maamuzi makubwa, na kuyasimamia maamuzi yake. Mechi kubwa tatu, zimemuondoka katika sifa za mwamuzi bora nchini, hii ni kutokana na uzoefu wake mdogo katika uchezeshaji mechi kubwa, lakini ana kitu ambacho waamuzi wengi hawana. 
Watu wengi wa mpira nchini hawana ujasiri wake wa kukubali kupoteza kazi yake kwa sababu alisimamia maamuzi ya kuiadhibu Yanga katika mechi kubwa, tena ikicheza na timu kutoka mkoani, ndani ya uwanja wa Taifa.
Viongozi wetu ‘wakubwa’ wa soka wana elimu nzuri ya darasani, lakini ni waongo na wanaosimamia upande mmoja, tu. Jana niliandika makala kuhusu timu yate ya taifa kuwa na wachezaji wengi wa Simba, Yanga, na Azam. Nilisema ni sawa tu wala haina tatizo timu hizo kuwa na wachezaji wengi katika kikosi cha Taifa Stars. Lakini ubora wao hauwezi kuletwa kwa njia ya upendeleo uwanjani, wanatakiwa wapambane na washinde kwa nguvu zao wenyewe, kwa mbinu zao wenyewe, na mwisho wa siku mwamuzi anatakiwa kusimamia mchezo kwa kufuata utaratibu na sheria zake. 
Hakuna, mkubwa kuliko mwamuzi katika mchezo wa soka, ndiyo maana Ufaransa ilifuzu kwa kombe la dunia, 2010 baada ya goli la ‘ mkono la Thierry Hennry, ndiyo maana, Bao la ‘ mkono wa mungu’ la Diego Maradona dhidi ya England, 1986 litabaki kuwa sehemu ya kumbukumbu za fainali za kombe la dunia, ni kama shuti kali la Frank Lampard dhidi ya Ujremani, katika ‘ WOZA 2010’.

Soka linahitaji matokeo yale, ( Yanga v Coastal) “ Niliwaona baadhi ya wachezaji wetu wakiwa walelala chini, niliwaambia ‘ okoteni mpira nyavuni’. Sikuwa tayari, kukata tama. Hutakiwi kukata tama hadi sekunde ya mwisho. HII NDIYO SABABU SOKA NI MCHEZO WA KUVUTIA” aliwahi kusema aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uturuki, Faith Terem mara baada ya timu yake kuitupa nje ya robo fainali ya Euro 2008 timu ya taifa ya Croatia, wakiwa wamefungwa bao dakika ya 119, lakini wakasawzisha dakika ya 
1119, lakini wakasawzisha dakika ya 120 na kushinda kwa mikwaju ya penati. Adhabu ya Saanya kwangu mimi ni kuzidi kuthibitisha kuwa ‘ Yanga ni timu ya wananchi’ lakini isiyojua thamani yake.

SAKATA KUKAMATWA NA UNGA: RASHID MATUMLA AZUNGUMZA KUHUSU TUHUMA ZINAZOMKABILI MDOGO WAKE



Bondia Rashid ‘Snake man’ Matumla amedai endapo itathibitika mdogo wake, Mkwanda anajihusisha kusafirisha dawa za kulevya atakuwa ameipa fedheha familia yao.
“Mkwanda ameipa fedhea familia yetu, hii ni aibu kubwa ukizingatia vitendo hivyo vinakatazwa si Tanzania tu bali na kwenye nchi nyingine,” alisema Matumla jana katika mahojiano na gazeti hili.
Mkwanda ambaye kwa mujibu wa Rashid alipumzika kucheza ngumi miaka kadhaa iliyopita kutokana na kusumbuliwa na  maradhi alikamatwa wiki iliyopita nchini Ethiopia akiwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Joseph Kaniki na leo watapandishwa kizimbani nchini humo kwa tuhuma hiyo.
“Mimi mwenyewe nashangaa ni lini amejiingiza kwenye kazi hiyo, hata wakati anaondoka hakuniaga, mimi kaka yao na familia hatuelewi chochote,” alisema Matumla.
Alisema mdogo wake huyo alikuwa amebadilisha uraia na kuchukua uraia wa Sweden na kuoa hukohuko Sweden licha ya kwamba hapa Tanzania alikuwa amepanga Mbagala, Dar es Salaam na alikuwa anakuja na kukaa kwa muda na kisha kuondoka.
“Ni mwezi sasa umepita sina taarifa naye na hata wakati anaondoka hakuniaga, nimesikia kupitia vyombo vya habari kitendo cha mdogo wangu kukamatwa kimenisikitisha mno, siyo siri nimekwazika na ninarudia kusema hii ni fedheha kwenye familia yetu,” alisema bingwa huyo wa zamani wa dunia wa WBU. Rekodi zinaonyesha kabla ya kupumzika kwa muda kucheza ngumi, Mkwanda alishinda mapambano manane (sita kwa KO) alipigwa mara tatu zote kwa KO alitoka sare mara moja tangu 2004.
SOURCE: MWANANCHI

LISTI YA WACHEZAJI WANAOLIPWA FEDHA NYINGI SERIE A: DANIELE DE ROSSI AWAFUNIKA - HIGUAIN ASHIKA NAFASI YA PILI


Kiungo wa kimataifa wa Italy na klabu ya AS Roma Daniele De Rossi ndio mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika ligi kuu ya Italia, hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa na La Gazzetta dello Sport. 
Kiungo huyo mwenye miaka 30 analipwa kiasi cha 6.5 million euros kwa mwaka, akimzidi Euro millioni 1 mchezaji anayeshika nafasi ya pili Gonzalo Higuain - na millioni 2 zaidi ya nahodha wa Roma Francesco Totti.

Uchumi m'baya wa Serie unaweza kuonekana vizuri kwa namba za mishahara ya wachezaji. Ni wachezaji 12 tu katika ligi nzima ambao wamefikia au kuzidi kiwango cha mshahara wa 4 million kwa mwaka, ukilinganisha na wachezaji 13 tu wa Chelsea ambao wanairpotiwa kulipwa kiwango cha namna hiyo. 


Hakuna mchezaji yoyote kutoka kwenye ligi ya Serie A aliyeweza kuingia kwenye listi ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi barani ulaya, huku De Rossi akifunikwa kabisa na wachezaji wanaolipwa fedha nyingi katika vilabu vya ligi za nchi nyingine.  Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic na mshambuliaji wa Monaco Radamel Falcao wote wawili wanalipwa kiasi cha 14 million euros baada ya kodi, wakati Lionel Messi anachukua 13 million kutoka Barca, dili jipya la Gareth Bale na Madrid limemfanya mchezaji huyo kushika nafasi ya tisa miongoni mwa 10 wanaolipwa fedh nyingi zaidi.

BARUA YA WAZI KWA MZEE AKILIMALI KUTOKA KWA MWANANCHAMA WA YANGA.




Kwako Mzee Akilimali,Assalam Alleikhum.

Mimi ni Manachama wa Yanga kadi namba 3005.Napenda kukuandikia waraka huu wa wazi  ikiwa ni fursa pekee ya kuwasilisha ujumbe kwa njia ya masiliano ya waraka kwako wewe na kwa Wana-Yanga wote wenye mtizamo na fikra kama za kwako. Nimekutaja wewe Mzee Akilimali kwa jina kwa sababu moja kubwa kwamba hicho cheo unachokitumia mimi sikitambui na siamini kama kweli unakundi kubwa la wazee wa Yanga nyuma yako.

UTANGULIZI

Klabu ya Yanga  kama inavyojieleza na kama ilivyosajiliwa na msajili wa vyama vya michezo,mbali na kujihusisha na mchezo wa mpira wa miguu,lakini vilevile  inatakiwa iwe na timu zingine za michezo kama Mpira wa pete(Netball),Ngumi(Boxing) na michezo mingineyo.
Kwa hiyo basi ndiyo maana inaiitwa Young Africans Sports Club ama Yanga kama ilivyozoeleka. Kwa maana hiyo basi Yanga kama taasisi ina Katiba yake,ambayo imezaa viongozi wake,ina taratibu na kanuni za kuendesha klabu ambazo zimepitishwa na wanachama na kutambuliwa na Serikali na taasisi zingine ambazo zinasimamia michezo,kitaifa na kimataifa.

MADHUMUNI.

Nia kubwa ya kukuandikia waraka huu ni kukujulisha yafuatayo:-
* Yanga kama klabu yenye wanachama zaidi ya 10,000 Tanzania nzima,inaongozwa kwa  
    kufuata katiba,ambayo imezaa kanuni miongozi na taratibu ,hivyo basi panatokea jambo lolote
    linalohusu klabu ni lazima taratibu zifuatewe,kama vile kuwaona viongozi na kuwaeleza juu
    ya jambo husika,kupitia mikutano ya mwaka ama mikutano ya matawi au hata ikibidi
    kuwaandikia barua.
*  Soka la sasa ni Biashara,na ndiyo maana wafanya biashara wakubwa duniani wanawekeza
    kaika soka,vilabu kama Liverpool,Man United,Chelsea PSG na vinginevyo vimenunuliwa na
    matajiri ili kujiendesha kibiashara huku ufananisi katika usakataji  mpira ukiwa mkubwa.
*  Kwa kuwa  mfumo wa uongozi klabuni ni wa uwakilishi,na viongozi waliopo madarakani
    wamechaguliwa kihali na wanachama,hivyo basi si busara kwa kikundi cha watu wachache
    kujivika isivyo halali madaraka na kufanya kazi za viongozi
*  Klabu inahitaji kubadilika kutoka katika mfumo wa ki –anologia kwenda katika mfumo wa 
    Ki-digitali,nikiwa na  maana kwamba kwa hali ilivyo sasa klabu lazima iongozwe na watu
    wenye upeo,busara na wasomi wataoiwezesha kuondokana na kasumba ya  klabu kuwa omba
    omba ama kumtegemea mtu mmoja.

HITIMISHO ( USHAURI)

Umefika wakati sasa wa Wazee wa Yanga kukubali  mabadiliko,kama ilivyotokea kwenye mifumo ya uongozi wa kisiasa katika nchi ,kutoka katika mfumo wa chama kimoja kwenda kwenye vyama vingi,nasi WANA-YANGA tubadilike,tuwaache tuliowakabidhi dhamana ya uongozi wafanye kazi.

Inatakiwa tukubali yafuatayo:

UWEPO wa Yanga si kwa ajili ya mahasimu wetu Simba,yaani tujielekeza katika fikra za kuibadili klabu yetu kutoka mfumo wa sasa wa kuomba omba  ili kuiendesha klabu badala yake klabu ijitegemee kiuchumi,kwani ikishajitegemea kiuchumi ndipo hapo tutakoweza kuwa na Timu imara itakayojengwa kutoka chini (Grass root),yaani vijana miaka 14,17,na timu ya wakubwa ambayo inaweza kuleta ushindani kitaifa na kimataifa.
Kauli mbiu kuwa tunampa uongozi mtu eti kwa kuwa ana mbinu ,mikati na uwezo wa kuifunga Simba ,kwa mtizamo wangu-naona imepitwa na wakati.

TUSIITEGEMEE klabu kuendesha maisha ya kila siku,bali tuisaidie klabu kwa michango ya hali na mali,iwe fedha ,ushauri ama mawazo mbadala kupitia vikao halali.

BARAZA LA WAZEE,Katika katiba ya Yanga  haionyeshi mahali ambapo inalitambua baraza la Wazee,ingawa Wazee wanaweza kuwa na mchango mkubwa katika klabu,kama watatumia busara zao kuwashauri viongozi.Hivi kwa mfano nyie mna Baraza lenu,Vijana nao wakiwa na Baraza lao,Wa kina mama nao wakiwa na Baraza lao,halafu kila kukicha wanatoa matamko yao kupitia mikutano na Waandishi wa habari si itakuwa fujo ?

PRESS CONFERENCE.
 Kama wewe si kiongozi wa klabu basi siyo sahihi ukiwa na jambo linalohusu klabu ukakurupuka na kuitisha mkutano na Waandshi wa Habari.Busara ni kuwasiliana na viongozi.
Ni hayo tu kwa leo
      
Mikidadi Sadiki Mikongolo.P.O BOX 12378, DSM,Email.mickmiko@hotmail.com
                                   Mwanachama-Young Africans Sports Club,