Imeandikwa na Baraka Mbolembole
Mtu ‘ mkubwa’ ni mwanafunzi, kwani
huona mbali zaidi na kwa kuona kwake huko hutamani vitu zaidi kuliko watu
wengine. Lakini ukweli ni kwamba mtu huyo hata kama atakuwa na uwezo wa kuona
mbali zaidi, au awe na akili nyingi zaidi, ukweli hawezi kubadili mwendo wa
historia. Kitu ambacho anaweza kufanya ni kubadilisha matukio Fulani. Ni
kutokana na mambo kama haya ndipo viongozi wakubwa hutokea.
Fasihi ni taaluma, Taaluma ni elimu,
na elimu ni maisha. Mtu huzaliwa na akili. Katika makuzi yake, mtu husikia,
huona, huonja, hunusa na hutenda. Vitendo hivi ndiyo msingi wa kutumia akili
ili kupata elimu. Hivyo elimu ya kwanza na sehemu kubwa na sehemu kubwa ya
elimu ya maisha hupatikana nje ya darasa. ‘ Yaani, Maisha kutokana na vionjo
vya mwili’ . Tunajifunza ili tuishi, na katika maisha yetu tunakutana na
marafiki wa kila aina, kwa wanasoka maisha yao mengi hutumia kutengeneza
marafiki wa dhati kutoka katika family ya soka. Urafiki ni Uadui, au Uadui ni
Urafiki?
Dunia hadaa. Kwa mtu ambaye
hajawajhi kufika pwani na kuiona bahari, anaweza kudanganywa kuwa maji ya
bahari ni ‘mekunde’. Kama ni rahisi, mtu huyo anaweza kudanganyika kuwa maji ya
bahari ni mekundu. Hatari ya uongo siku zote iko wazi. Itatokea siku mtu huyo ‘
mjinga’ asiyeijua bahari, akajifunga na kufanya safari ili aje kuhakikisha
uwepo wa maji mekundu ya bahari. Apatapo ukweli na kubaini kuwa alidanywa, mtu
huyo atamuamini tena mtu aliyempatia habari hizo hata kama atakuwa akizungumza
ukweli wakati mwingine.
Usaliti kwetu sisi mashabiki upo siku
zote, Martin Saanya, na aliyekuwa mwamuzi wake msaidizi, Jesse Onesmo wamekutwa
na adhabu ya kufungiwa kutochezesha soka kwa muda wa mwaka mmoja. Waamuzi hao
walichezesha mchezo kati ya Yanga na Coastal Union, septemba 28 na kumalizika
kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.
Waamuzi hao, wenyeji wa mkoani
Morogoro wamefungiwa kwa kuwa walishindwa kuendana na kasi ya mchezo na
kujikuta wakifanya makosa ya mara kwa mara. Adhabu ya kiki ya penati ambayo
Saanya aliitoa kuelekea katika lango la Yanga, dakika ya mwisho ya mchezo na
kutengeneza matokeo ya sare ndiyo iliyowaletea matatizo, na kupelekea wakapata
adhabu kubwa. Sifikirii kama angepewa adhabu hiyo kama angetoa wakati Yanga
wakisaka bao la kusawazisha. Waamuzi hawa ni kweli waliboronga, na mechi
ilikuwa kubwa kwao. Lakini ukichunguza hatua kwa hatua ambazo walizitumia
kufanya maamuzi na kuusimamia mchezo ule, utagundua kuwa makosa waliyofanya
yalikuwa ni ya kibinadamu, na mkwaju wa ' utata' wa penati kwangu mimi nauchukulia kama sehemu
ya kawaida ya mchezo wa soka.
NI,KWELI, SAANYA, ONESMO
WALIBORONGA, lakini adhabu walizopewa ni
kama ziliandaliwa. Sijui ni wapi lakini nakumbuka wakati Fulani nilikutana na
Mwamuzi, Othman Kazi, kiukweli nilitaka kujua kwa nini alifungiwa. Akaniambia
kuwa kuna watu walikuwa hawamtaki kwa sababu wanazozijua wao. Kina, nani hao? “
Nasubiri muda wao madarakani umalizike ndiyo nitarudi kuchezesha tena soka”
aliwahi kuniambia Kazi, ambaye aliwahi kukutwa na adhabu kubwa ya kufungiwa
kwa kosa alilodai kuwa si la kweli. Alifungiwa kwa madai ya kupokea hela kutoka
mahali Fulani waawakati Fulani mjini Bukoba. Aliniambia mambo mengi sana
kuhusu kazi yao ya uamuzi na matatizo ya ubinafsi yaliyopo katika chama
chao.
Wakati mwingine ni lazima chama
cha waamuzi kiwasemee waamuzi hasa wanapokutana na adhabu ambazo zinakuwa ni
kali zaidi na ambazo zinaweza kuwafanya wakashindwa kuaminiwa tena, hata pindi
watakaporudi uwanjani baada ya adhabu kumalizika.
Kitu, gani ambacho kimemfanya
Saanya, na Onesmo wahukumiwe? Ni kuiadhibu Yanga katika ‘muda mbaya’, nafikiri
tu kama adhabu ile ingetolewa katika lango ya Coastal mambo yangekuwa makubwa
kiasi hiki. Hapana, LAKINI imekuwa tatizo kubwa hadi katika kazi yake, kwa kuwa
aliamua mkwaju wa penati. Katika mechi kama ile, katika muda kama ule, katika
kipindi ambacho timu nzima ya Coastal ilikuwa ikicheza katika eneo la hatari la
Yanga, ilikuwa ni lazima Saanya ‘ afunike mkono wake’ haijalishi mpira
ulimgonga mahali gani Haruna Niyonzima. Yanga walikuwa wakiomba mechi imalizike
na presha ya Coastal ilikuwa juu kuliko muda wowote ule wa mchezo.
Adhabu yake ni fundisho kwa waamuzi
wote ambao huishia kuchezesha mechi kwa namna wanavyopangiwa na watu au vile
watakavyo wao. Soka letu haliwahitaji waamuzi ‘ wazembe’, soka letu
haliwahitaji waamuzi kama Saanya ambao hawawezi kuendana na kasi ya mchezo,
soka letu linawahitaji waamuzi kama Saanya ambao wana uwezo wa kufanya maamuzi
makubwa, na kuyasimamia maamuzi yake. Mechi kubwa tatu, zimemuondoka katika
sifa za mwamuzi bora nchini, hii ni kutokana na uzoefu wake mdogo katika
uchezeshaji mechi kubwa, lakini ana kitu ambacho waamuzi wengi hawana.
Watu
wengi wa mpira nchini hawana ujasiri wake wa kukubali kupoteza kazi yake kwa
sababu alisimamia maamuzi ya kuiadhibu Yanga katika mechi kubwa, tena ikicheza
na timu kutoka mkoani, ndani ya uwanja wa Taifa.
Viongozi wetu ‘wakubwa’ wa soka
wana elimu nzuri ya darasani, lakini ni waongo na wanaosimamia upande mmoja,
tu. Jana niliandika makala kuhusu timu yate ya taifa kuwa na wachezaji wengi wa
Simba, Yanga, na Azam. Nilisema ni sawa tu wala haina tatizo timu hizo kuwa na
wachezaji wengi katika kikosi cha Taifa Stars. Lakini ubora wao hauwezi kuletwa
kwa njia ya upendeleo uwanjani, wanatakiwa wapambane na washinde kwa nguvu zao
wenyewe, kwa mbinu zao wenyewe, na mwisho wa siku mwamuzi anatakiwa kusimamia
mchezo kwa kufuata utaratibu na sheria zake.
Hakuna, mkubwa kuliko mwamuzi
katika mchezo wa soka, ndiyo maana Ufaransa ilifuzu kwa kombe la dunia, 2010
baada ya goli la ‘ mkono la Thierry Hennry, ndiyo maana, Bao la ‘ mkono wa
mungu’ la Diego Maradona dhidi ya England, 1986 litabaki kuwa sehemu ya
kumbukumbu za fainali za kombe la dunia, ni kama shuti kali la Frank Lampard
dhidi ya Ujremani, katika ‘ WOZA 2010’.
Soka linahitaji matokeo yale, ( Yanga v Coastal) “ Niliwaona baadhi ya wachezaji wetu wakiwa walelala chini, niliwaambia ‘ okoteni mpira nyavuni’. Sikuwa tayari, kukata tama. Hutakiwi kukata tama hadi sekunde ya mwisho. HII NDIYO SABABU SOKA NI MCHEZO WA KUVUTIA” aliwahi kusema aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uturuki, Faith Terem mara baada ya timu yake kuitupa nje ya robo fainali ya Euro 2008 timu ya taifa ya Croatia, wakiwa wamefungwa bao dakika ya 119, lakini wakasawzisha dakika ya 1119, lakini wakasawzisha dakika ya 120 na kushinda kwa mikwaju ya penati. Adhabu ya Saanya kwangu mimi ni kuzidi kuthibitisha kuwa ‘ Yanga ni timu ya wananchi’ lakini isiyojua thamani yake.
Soka linahitaji matokeo yale, ( Yanga v Coastal) “ Niliwaona baadhi ya wachezaji wetu wakiwa walelala chini, niliwaambia ‘ okoteni mpira nyavuni’. Sikuwa tayari, kukata tama. Hutakiwi kukata tama hadi sekunde ya mwisho. HII NDIYO SABABU SOKA NI MCHEZO WA KUVUTIA” aliwahi kusema aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uturuki, Faith Terem mara baada ya timu yake kuitupa nje ya robo fainali ya Euro 2008 timu ya taifa ya Croatia, wakiwa wamefungwa bao dakika ya 119, lakini wakasawzisha dakika ya 1119, lakini wakasawzisha dakika ya 120 na kushinda kwa mikwaju ya penati. Adhabu ya Saanya kwangu mimi ni kuzidi kuthibitisha kuwa ‘ Yanga ni timu ya wananchi’ lakini isiyojua thamani yake.
Katika watu wanafiki wana didimiza soka la bongo wewe ni mmoja wao,umeacha kufanya taaluma yako unaanza kufanya mipasho,hivi kuna mtu gani ambae hajaona utumbo wa mwamuzi yule(i)kitendo cha kuto oenalt dakika za lala salama wala sio tatizo issue inakuja ni mazingira gani penalt imetolewa,na uzuri walio mfungia wameelezea kuwa alikuwa mbali na eneo la tukio hivyo sio rahisi kwake kuona tukio,mwamuzi wa pembeni alipaswa kumuelekeza refa wake kuwa ile haikuwa penalt lkn alishindwa,alimpa kadi msuva bila kuangalia tukio na ndio maana akampa na odula kadi kwa kuwa hakujua kinacho endelea,hakuwa na ushirikiano na wasaidizi wake.wewe umeandika post yako kishabiki tu kwa kuiona yanga ni timu inayo bebwa,unaacha kusimamia ukweli unaenda kwenye umbea.ninyi waandishi ndio mnaosababisha soka leyu lina shuka coz hamsimamii ukweli,TAMBUA YANGA NI TIMU KUBWA NA ITABAKI HIVYOHIVYO,DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.by Kuntah kinte.
ReplyDeleteaisee nimependa sana huu uchambuzi, adhabu ni kubwa sana kwa hawa marefa vijana! wangeweza kufungiwa hata mechi tatu basi ila mwaka ni kama unawakomoa! shame on you TFF
ReplyDeleteHamna cha kuwa tim ya wananchi wala nini, huwezi ukaamuru penati wakati wewe mwenyewe upo umbali wa zaidi ya mita arobaini. Hao waliofumbia makosa kama ya akina henry, germany v/s england ndo walewale na haimaanishi kwa kuwa wale waliyafumbia ndo basi na sisi ma-tz tuwe tunapotezea tu.Acha UNAZI wewe.
ReplyDeleteBLAH BLAH.....NO CONTENT
ReplyDeleteNakupa hongera kwanza, kwa kutoa mifano mbalimbali za Soka kidunia! Ni kweli adhabu za Waamuzi wa mechi ya Yanga na Coastal union ni uonevu wa hali ya juu sana!? Mimi nilitegemea cha cha Waamuzi kingekaa na kuwapa adhabu stahiki za kimchezo kulikoni kuwa hukumu ki Club kama walivyoonekana ktk mechi hiyo! Inadhihilisha kuwa Yanga ni lazima walistahili kuondoka na ushindi ? kitu amabacho kimchezo dk za mwisho Yanga walifunikwa sana na Coastal union!! anayebisha basi si mzalendo wa kweli kama alikuwepo uwanjani pale wadau! Tunaharibu ligi yetu!!!!! Obrigada,,,,,,Tanzania ktk soka inaongozwa na Yanga na Simba??? ligi itabaki kuwa bovu milele na milele!
ReplyDeleteofcoz katka hili spot extra wanahusika, mana siku ile walishikia bango, sana kuwa mwaamuzi hakuwa sahihi lakin kwenye spoti bar hao hao wakamuunga mkono mwaamuzi kuwa ilikuwa rafu ya kweli
ReplyDeleteUzuri hayo ni maoni yako tuu. kama vp pia teua timu yako ya Taifa kama unaona makocha hawajui. Mbona hulalamiki Spain wachezaji wengi wanatoka klab ya Barcelona? Nakushangaa sana kuwa na mdomo kama chuchunge. Halafu sioni sababu ya kuchonga ngenga badala ya kwenda kutoa mawazo yako kwa uongozi pamoja na kamati husika kama kweli una nia njema
ReplyDeleteShafii value ur reputation to the public uwezi kuruhusu mtu aandike crap opinion zisizo na mashiko kwny blog yako ni UNAFIKI na upuuz cjaona alichokiandika hamna maelezo ya maana zaid ya misemo ya vijiwen tu..
ReplyDeleteMaamuzi mangapi yanafanywa in favour of yanga na simba na marefa hawafungiwi kiasi hiki?suala hili halihitaji msomi kuliona,hiyo ndo point ya jamaa.ni kosa lakin wangeadhibiwa hiv isingekua yanga!?TFF haina consistence ya maamuzi,unadhan siku ingine refa gani ataenda against big teams?very good artical,
ReplyDeletembona kama manu tu. refa anapendelea tu. na kama hapendelei . hachezeshi tena. kila ligi ina boss wake. .afadhali bongo hatuwalaumu sana yanga na simba hakuna replay. kila mtu anasema analotaka na alivyoona yeye. subirini karibu replay zitaanza toka azam tv. sasa hivi nyamazeni tu. hakuna ushahidi. ila mtu msianze kama epl. manu wanavyobebwaga mpaka mgongo unauma. ukiwaliza ma pundit wanasema human error. sasa mnalalamika nini. yanga timu kubwa ndio mpira ulivyo duniani kote. na nyie mtaanza kusema makosa ya kibinadam. sisi tunaopenda yanga na manu tunapeta tu. mpende msipende marefa lazima watutumikie. ukitaka mipira ya halali hkuna
ReplyDeleteNadhani tuna Tatizo kubwa la kuwa wajuaji wa kila Jambo, na tunadhani kuwa kila linalofanyika lazima tulitolee kasoro na kulaumu: Hivi, ni nani aliyekuwa uwanjani siku ile hajui kama Martin Saanya alishindwa kwenda na kasi ya mchezo?, ni nani asiyejua kama Martin Saanya ameadhibiwa kwa kanuni zilizopo?.
ReplyDeleteIssue siyo kuwa Yanga ni Timu kubwa au ni Timu ya wananchi, jambo la msingi ni makosa gani aliyotenda Martin Saanya na adhabu aliyopewa kulingana na kiwango chake cha uamuzi alicho onyesha uwanjani yanalingana?.
Tuachane na suala la Penalt tata waliyopata Coastal union dakika za majeruhi, je Tunalidhika na jinsi kadi za njano zilivyo tolewa bila kuwa na sababu?, kadi nyekundu ya Odula na Ile ya Msuva zilitoka katika mazingira gani?. Hivi ni wapi umeona ligi yenye waamuzi wabovu kama Martin Saanya inakuwa na Bingwa anaye Stahili na kutoa nafasi za wachezaji wenye uwezo na kuonekana na waalimu wa Timu ya Taifa ili Kisaidia nchi?.
Waamuzi makini ni muhimu katika maendeleo ya soka letu, Tukiwa na Waamuzi wabovu katika ligi yetu, tutaendelea kuwalemaza wachezaji wetu na kuigharimu Timu ya Taifa inapocheza katika mechi za kimataifa na Waamuzi wenye weledi na kuimudu kazi yao.
Niwakumbushe yaliyotokea timu ya taifa iliposhindwa kufunzu kwenda Kombe la Dunia, Tumefungwa magoli ya kizembe kwa mabeki wetu kucheza offside trap wakidhani waamuzi ni wabovu kama Martin Saanya watatubeba.
Tunajua kuwa Timu yetu huwa tunafungwa magoli ya fauls (set pieces)kwa makosa ambayo wachezaji wetu wamezoea kucheza fauls kwenye ligi bila waamuzi kuchukuliwa hatua, Mazoea haya yalitugharimu hata mechi na Ivory coast na Yaya Toure akatufunga goli rahisi kwa faul ya kizembe.
Tuliona Martin Saanya na waamuzi wengine wanaposhindwa kumudu mechi kwa kushindwa kuwa makini mchezoni.
Huu ni mwanzo, tuache ushabiki, Tuipongeze kamati ya waamuzi kwa kutoa adhabu stahiki kwa Martin Saanya na mwenzake , lakini tusi ishie tu kwenye mechi ya Yanga na Coast, Madudu Mengi yanafanyika Mikoani