Na Baraka Mbolembole
Pesa siyo kila kitu katika maisha, ila mwanadamu anatakiwa
kuwa na kiasi Fulani cha pesa ili
kumuwezesha kuishi katika jamii yake anayoishi. Mtu anatakiwa kufanya kazi ili
apate kipato chake halali, na kumuwezesha kupata mahitaji yake muhimu (
Chakula, Mavazi, na Malazi). Pesa ni sabuni ya roho, lakini Hasara ‘Roho’, pesa
ni makaratasi tu. Kila binadamu atakula kutokana na urefu wa kamba yake, na
Yule asiyefanya kazi na asile ‘asilani’, ndivyo maandiko ya mwenyezi Mungu.
Tamaa ya kupata kipato cha haraka, ni chukizo kwa mwenyezi
Mungu, labda kama matendo yanayokuingizia kipato chako ni ya halali, na
yanayompendeza mwenyezi Mungu na kukubalika katika jamii. ‘ Wingu’ zito
limetanda katika ‘anga’ ya Tanzania, wiki moja iliyopita kuna meli kubwa
iliyokuwa imebeba zaidi ya tani 30 za Bangi, ilikamatwa pembezoni ya nchi ya
Italia, bendera waliyokuwa wanaitumia katika meli hiyo ni ya…… Ni aibu kuitaja
lakini ndiyo ukweli huo. Na huko inatangazwa kuwa ni…….TANZANIA.
Vita dhidi ya madawa ya kulevya katika miaka michache
iliyopita ilikuwa inawahusisha, Polisi na wavutaji, wale mawakala, na wauzaji
pamoja na wananuzi wakubwa hawakuwa wakiguswa. Miaka imekwenda, na kuwakamata
wavutaji pekee ya kuacha mizizi yake ikiendelea kuchipua imekuwa ni tatizo
kubwa kwa nchi yetu. Sasa, serikali za nchi ambazo hazihitaji ‘SEMBE’ katika
ardhi ya nchi zao imekuwa ikitusaidia kuwakamata, wasafirishaji na waingizaji ‘
ulevi huo haramu kwa wananchi wao’ kuwakamata na kuwahukumu, Watanzania wenzetu
ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao Fulani katika jamii kufanya biashara hiyo
haramu.
Kumbuka kuhusu wale mabondia ambao walikamatwa huko Visiwa
vya Komoro na kuhumiwa vifungo vya miaka 15. Wanamichezo wamekuwa wakitumia
kila sifa zao nzuri wanazozipata kutokana na vipaji vyao kuwaadaa, maafisa wa
polisi na kupitisha biashara hiyo haramu. Ni msingi mbaya ambao mimi tangu
nikiwa na miaka saba, wakati timu ya Simba ikichezea fainali ya kombe la Caf
dhidi ya Stella Abdjan, na kufungwa nimekuwa nikisikia habari za uwepo wa
usafirishaji wa madawa ya kulevya
kutumia wanamichezo. Niliwahi kusikia mengi tu, lakini sasa kukamatwa kwa
wasanii maarufu nchini, wachezaji maarufu, mabondia maarufu, na wanasoka
maarufu wakiwa na ‘ mizigo’ ya mabilioni ya shilingi katika nchi mbalimbali
barani Afrika, Asia, ni muendelezo wa ukweli ambao ulikuwa ukifichwa nchini
kwetu.
Ni msingi mbaya uliwekwa na viongozi wetu waliopita katika
sekta mbambali, na hata kwa wanamichezo hatua ambazo nchi yetu imefika ya
kukosa walau medali ya shaba katika michuano ya Olimpiki, Madola, ama ile ya
Afrika ni dalili kuwa viongozi wetu waliopita waliacha msingi mbaya. WAlikuwa
ni wafanyabiasha wakubwa wa kimataifa ambao muda wote walipanga mipango ya
namna ya kuingiza na kutoa biashara zao haramu. Sasa wanakamtwa, nje ya nchi,
wanalitia aibu Taifa, wanatia aibu thamani ya bendera ya nchi yetu. Lakini
walipata wapi, ujasiri huo? ‘Mtoto wa nyoka ni nyoka. Na ukiishi na mwizi na
wewe utakuwa mwizi’’ na ndicho kinachoonekana sasa, kuwa wachezaji ambao
walitumia vibaya vipaji vyao na wakati wao wa uchezaji, wameamua kuingia wao
wenyewe katika biashara hii, sijui ni kwa ‘mgongo wa nani’ ila ni kutokana na
kile ambacho walikuwa wakikiona au
kufanya wakiwa chini ya misingi ambayo viongozi wetu waliijenga.
Na ilikuwaje kuhusu safari yako ya Ujerumani, tuliambiwa
ulikwenda kufanya majaribio ? Kuna mchezaji niliwahi kumuuliza swali hili, naye
akanijibu
Bwana Kule kiukweli kuna Siri nzito maana hata aliyenipeleka
kanisihi sana nisiseme , lakini nilifanya majaribio kwa mwezi mzima, ila ikatokea ishu ambayo ile timu hawakupendezwa
nayo ikabidi nirudi nyumbani”
Nikamuuliza tena,
Ilikuhusu wewe au, na nani aliyekuwa wakala aliyekusimamia
katika safari ile?
“ Haikunihusu mimi,
ilimuhusu wakala wangu”
Nikaendelea kudadisi….
Labda kwa ufupi kitu gani kilitokea kwani ulipata muda mrefu
wa kujaribiwa?
“ Kweli nilipata muda mrefu kule, ila Daah! Ila kweli suala
lililotokea siwezi kusema kaka”
Huyu ni mchezaji wa
timu ya taifa na klabu kubwa nchini. Umewahi kuchunguza muda ambao wachezaji
wetu huchukuliwa na mawakala na kupekwa nje ya nchi kufanya majaribio? Huwa ni
kipindi ambacho dirisha la usajili limekuwa limefungwa, ndiyo hatukatai kuwa
mchezaji anaweza kufanya vizuri na baadae akapewa nafasi ya kusajiliwa wakati
wa usajili ukufika. Lakini ni wangapi ambao tumekuwa tukiambiwa kuwa wamefuzu,
na watarudi tena wakati wa usajili na tunaendelea kuwaona katika viwanja vya Tanzania.
Soka la kisasa linaenda kisasa, muda ni muhimu kuzingatiwa, rekodi ni muhimu na
video ni muhimu pia.
Tazama tangu safari za Mrisho Ngassa, West Ham, na Seatlle
Sounders, Abdulhalim Humud, Afrika ya Kusini, Mussa Hassan Mgosi, India,
Shadrack Nsajigwa, Ufaransa, Zahoro Pazi, Ujerumani, na Afrika ya Kusini, wote
hawa tuliambiwa wamefuzu majaribio walipokwenda kufanya na wangerudi tena.
Kweli, Ngassa karudi Tena Yanga, Humud karudi tena, Simba, Zahoro kahama Azam
katua Simba, Mgosi amerudi Mtibwa Sugar tena, kweli majira yanakwenda haraka
sana. Biashara kwanza michezo baadae, kwa mwanasoka, kucheza soka la kulipwa
hakutakuja kwa maribio bali ni kuonesha kiwango kama Mbwana Samatta na kutoka
nje. Labda kama tutawaondoa wafanyabiashara wakubwa katika mpira.
AFANDE SELE,
mwanamuzi mshindi wa tuzo ya mfalme wa mashairi nchini aliwajhi kuimba Pesa, na
kusema…..
" Achinjwe binadamu, na pesa ipakazwe damu...., Watu
wataifuta, kisha wataitumia...., Watanunulia, misahafu na bibilia, na waumini
wataipokeaaa...
WATU, NAZO PESA...
wewe zinakutesaaa,
MIMI ZINANITESAAA, pesaaa....
“
“Kweli, pesa ni tamu saaana, Ni tamu kwa kila namnaaa...,
Kijana akikamata, madingi watamwita bwana... Dingi akikamata anaonekana ni
kijanaaa..."
0714 08 43 08
Hali inatisha kaka,leo umeandika kitu cha maana sana,hongera kwa hilo.
ReplyDeletelkn mimi nikupinge kidogo kwa kuwalaumu viongozi,ifike wakati tuwe wakweli,tamaa ndio inayo wasukuma vijana kufanya mambo hayo kwani hakuna anaye shikwa mkono ila wao wenyewe pia wanazitaka hizo safari kwani wanajua wanacho pata.