Search This Blog

Wednesday, September 11, 2013

BARUA YA WAZI KWA MZEE AKILIMALI KUTOKA KWA MWANANCHAMA WA YANGA.




Kwako Mzee Akilimali,Assalam Alleikhum.

Mimi ni Manachama wa Yanga kadi namba 3005.Napenda kukuandikia waraka huu wa wazi  ikiwa ni fursa pekee ya kuwasilisha ujumbe kwa njia ya masiliano ya waraka kwako wewe na kwa Wana-Yanga wote wenye mtizamo na fikra kama za kwako. Nimekutaja wewe Mzee Akilimali kwa jina kwa sababu moja kubwa kwamba hicho cheo unachokitumia mimi sikitambui na siamini kama kweli unakundi kubwa la wazee wa Yanga nyuma yako.

UTANGULIZI

Klabu ya Yanga  kama inavyojieleza na kama ilivyosajiliwa na msajili wa vyama vya michezo,mbali na kujihusisha na mchezo wa mpira wa miguu,lakini vilevile  inatakiwa iwe na timu zingine za michezo kama Mpira wa pete(Netball),Ngumi(Boxing) na michezo mingineyo.
Kwa hiyo basi ndiyo maana inaiitwa Young Africans Sports Club ama Yanga kama ilivyozoeleka. Kwa maana hiyo basi Yanga kama taasisi ina Katiba yake,ambayo imezaa viongozi wake,ina taratibu na kanuni za kuendesha klabu ambazo zimepitishwa na wanachama na kutambuliwa na Serikali na taasisi zingine ambazo zinasimamia michezo,kitaifa na kimataifa.

MADHUMUNI.

Nia kubwa ya kukuandikia waraka huu ni kukujulisha yafuatayo:-
* Yanga kama klabu yenye wanachama zaidi ya 10,000 Tanzania nzima,inaongozwa kwa  
    kufuata katiba,ambayo imezaa kanuni miongozi na taratibu ,hivyo basi panatokea jambo lolote
    linalohusu klabu ni lazima taratibu zifuatewe,kama vile kuwaona viongozi na kuwaeleza juu
    ya jambo husika,kupitia mikutano ya mwaka ama mikutano ya matawi au hata ikibidi
    kuwaandikia barua.
*  Soka la sasa ni Biashara,na ndiyo maana wafanya biashara wakubwa duniani wanawekeza
    kaika soka,vilabu kama Liverpool,Man United,Chelsea PSG na vinginevyo vimenunuliwa na
    matajiri ili kujiendesha kibiashara huku ufananisi katika usakataji  mpira ukiwa mkubwa.
*  Kwa kuwa  mfumo wa uongozi klabuni ni wa uwakilishi,na viongozi waliopo madarakani
    wamechaguliwa kihali na wanachama,hivyo basi si busara kwa kikundi cha watu wachache
    kujivika isivyo halali madaraka na kufanya kazi za viongozi
*  Klabu inahitaji kubadilika kutoka katika mfumo wa ki –anologia kwenda katika mfumo wa 
    Ki-digitali,nikiwa na  maana kwamba kwa hali ilivyo sasa klabu lazima iongozwe na watu
    wenye upeo,busara na wasomi wataoiwezesha kuondokana na kasumba ya  klabu kuwa omba
    omba ama kumtegemea mtu mmoja.

HITIMISHO ( USHAURI)

Umefika wakati sasa wa Wazee wa Yanga kukubali  mabadiliko,kama ilivyotokea kwenye mifumo ya uongozi wa kisiasa katika nchi ,kutoka katika mfumo wa chama kimoja kwenda kwenye vyama vingi,nasi WANA-YANGA tubadilike,tuwaache tuliowakabidhi dhamana ya uongozi wafanye kazi.

Inatakiwa tukubali yafuatayo:

UWEPO wa Yanga si kwa ajili ya mahasimu wetu Simba,yaani tujielekeza katika fikra za kuibadili klabu yetu kutoka mfumo wa sasa wa kuomba omba  ili kuiendesha klabu badala yake klabu ijitegemee kiuchumi,kwani ikishajitegemea kiuchumi ndipo hapo tutakoweza kuwa na Timu imara itakayojengwa kutoka chini (Grass root),yaani vijana miaka 14,17,na timu ya wakubwa ambayo inaweza kuleta ushindani kitaifa na kimataifa.
Kauli mbiu kuwa tunampa uongozi mtu eti kwa kuwa ana mbinu ,mikati na uwezo wa kuifunga Simba ,kwa mtizamo wangu-naona imepitwa na wakati.

TUSIITEGEMEE klabu kuendesha maisha ya kila siku,bali tuisaidie klabu kwa michango ya hali na mali,iwe fedha ,ushauri ama mawazo mbadala kupitia vikao halali.

BARAZA LA WAZEE,Katika katiba ya Yanga  haionyeshi mahali ambapo inalitambua baraza la Wazee,ingawa Wazee wanaweza kuwa na mchango mkubwa katika klabu,kama watatumia busara zao kuwashauri viongozi.Hivi kwa mfano nyie mna Baraza lenu,Vijana nao wakiwa na Baraza lao,Wa kina mama nao wakiwa na Baraza lao,halafu kila kukicha wanatoa matamko yao kupitia mikutano na Waandishi wa habari si itakuwa fujo ?

PRESS CONFERENCE.
 Kama wewe si kiongozi wa klabu basi siyo sahihi ukiwa na jambo linalohusu klabu ukakurupuka na kuitisha mkutano na Waandshi wa Habari.Busara ni kuwasiliana na viongozi.
Ni hayo tu kwa leo
      
Mikidadi Sadiki Mikongolo.P.O BOX 12378, DSM,Email.mickmiko@hotmail.com
                                   Mwanachama-Young Africans Sports Club,

3 comments:

  1. KAKA DAUDA HUYU JAMAA ANA AKILI SANA MIM NI MSHABIKI WA SIMBA ILA HIYO MSG INAZIHUSU HIZI TIMU ZETU, JAMANI WANA SIMBA NA YANGA KULE ULAYA PIA KUNA UTANI WA JADI UWANJANII ILA SIO KAMA HUU WETU USIO NA MAENDELEO YA KIUCHUMI..!!! TUNAJISIFU KUSHANGILIA TIMU ZA ULAYA ILA MBONA TUNAKUWA WANAFIKI WA KUJUA MENGINEYO JINSI TIMU ZA ULAYA ZINAVYOENDESHWAAA ILI HATA UKIMCHAGUA KIONGOZI UJUE HUYU ATAKUWA NA MIPANGO YA MBELE NA SIO ISHU YA KUIFUNGA YANGA AU SIMBAA.... ANGALIZOOO WALE MNAOJIITA WANACHAMA SIO VIBAYA ILA HUO UANACHAMA WENU WENGI NDIO UNARUDISHA MAENDELEO NYUMAA... TUCHEZE MPIRA WENYE MIPANGO ENDELEVU NA WENYE KUNUFAISHA TAIFA NA KIZAZI KIJACHO ....

    ReplyDelete
  2. KAKA MICK I LIKE U R MASSAGE TO MZEE AKILIMALI AND HIS TEAM MZEE AMETUAIBISHA SANA ANAPOSEMA HATAKI KUONGOZWA NA MKENYA MBONA MZEE ANATAKA KUUENDESHA KILA UONGOZI UNOINGIA MADARAKANI...?

    BASI NA WACHEZAJI WA NJE WAONDOKE C NDIYO WANATUSAIDIA KWENYE MAFANIKIO YA TIMU...?

    I FAIL TO UNDERSTAND THIS SO CALLED MZEE AKILIMALI.........

    ReplyDelete
  3. Umesema vema mwanachama.

    ReplyDelete