Search This Blog

Wednesday, October 10, 2012

TENGA AZITAKA KAMATI ZA UCHAGUZI KUSIMAMIA KANUNI



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amezitaka Kamati za Uchaguzi kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki. Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Rais Tenga amesema uongozi wa mpira wa miguu unahitaji uamuzi mgumu, hivyo Kamati za Uchaguzi ambazo zimeundwa kwa mujibu wa Katiba zinatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na si kuangalia sura za watu.

Amepongeza kamati zilizosimamia uchaguzi kwa kufuata kanuni, na ingawa kila mtu ana haki ya kuongoza, jambo lolote lazima liwe na kanuni, kwani hata kwenye mikutano ya hadhara kuna kanuni. “Huwezi kufika kwenye mkutano wa hadhara na wewe unaanzisha mkutano wako. Lazima kanuni ziheshimiwe ili kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki. Nini kimetokea kwenye maeneo ambayo kuna matatizo? Kila mwanachama wetu (mkoa/chama shiriki) ana Kamati ya Uchaguzi ambayo imeundwa kwa mujibu wa kanuni.

 “Zile kamati hazitekelezi majukumu yake, unampitisha mtu unajua hana sifa unasema acha akafie mbele (Kamati ya Uchaguzi ya TFF). Kanuni zinasema jaza fomu mwenyewe, weka nakala za vyeti na si kwamba huyu tunamjua. Kanuni zinatakiwa zifuatwe, ukienda kinyume unaondolewa,” amesema. Amesisitiza kamati zifanye kazi kwa kufuata kanuni ili kusaidia mpira wa miguu kwani zimeundwa kihalali, kwa hiyo zisiogope kuengua hata walioziteua kama hawana sifa. Pia Rais Tenga amezitaka Kamati za Utendaji na Sekretarieti kutoziingilia Kamati za Uchaguzi katika mchakato wa uchaguzi, badala yake zinatakiwa kuziwezesha tu (facilitation).

Amesema baadhi ya wagombea nao ni tatizo kwani wanaingia kwenye uchaguzi bila kuzielewa Katiba za vyama vyao na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo ni vizuri wakazielewa kwanza. Rais Tenga amesema ni vizuri wanachama wote wakafanya uchaguzi kabla ya uchaguzi wa TFF utakaofanyika Desemba mwaka huu ili wapate fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi huo wa shirikisho. Vilevile amewataka wadau kujitokeza kwa wingi kuwania uongozi kwenye chaguzi za vyama wanachama wa TFF, kwani mwitikio umeonekana kuwa mdogo kulinganisha na umaarufu wa mchezo wenyewe. Amepongeza vyama vya mikoa ambavyo tayari vimefanya uchaguzi wao. Baadhi ya vyama hivyo ni Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Morogoro, Mtwara na Singida. Boniface Wambura Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

HUU NI UZALENDO ATOA KALI NYINGINE! AMWAGA CHOZI BAADA YA YANGA KUTOKA SARE NA SIMBA.

GOLI BORA LA SIKU - JESUS MARTINEZ

MCHEZAJI WA AC MILAN AWA WAZIRI MKUU MSAIDIZI NA WAZIRI WA MIUNDOMBINU NCHINI GEORGIA



Mchezaji wa zamani wa AC Milan Kakha Kaladze amethibitishwa kuwa waziri mkuu msaidizi wa nchi ya Georgia.

Mshindi wa mara mbili wa UEFA Champions league  akiwa na Milan, Kaladze amekuwa makamu wa waziri mkuu na pia waziri wa miundo mbinu na maendeleo katika serikali mpya ya Georgia.

Kakha Kaladze baada ya kuwa mwanasiasa
"Nilipotangaza kustaafu kucheza soka, nilisema mechi muhimu zaidi ya maisha yangu ndio imeanza sasa," alisema mlinzi huyo mstaafu mwenye miaka 34 akiongea na shirika la habari la AFP wakati wa kampeni za uchaguzi.

Kampeni za uchaguzi zilizianza kuwa chafu baada ya kituo cha TV cha serikali utoa mikanda ya video ambayo walisema inatoa ushahidi kwamba baadhi wanasiasa, akiwemo Kaladze walikuwa na mahusiano mabosi makundi yanayofanya vitendo vya makosa  - tuhuma ambazo Kaladze aliziita za kijinga. 

“Sina chochote kinachohusiana na Mafia, sio mwanzoni huko nyuma wala sasa," anasema Kaladze.
"Mip[ango yangu kwa sasa ni kutengeneza vizuri barabara na kutoa huduma nzuri za usambazaji wa maji."

AKINA OZIL, GOMEZ NA PODOLSKI WAAHIDIWA €20,000 KWA KILA MECHI MPAKA WATAKAPOFUZU KUCHEZA WORLD CUP 2014

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani watapokea kiasi cha €20,000 kwa kila mechi ya kufuzu kombe la dunia watakayocheza na ikiwa watafanikiwa kufika nchini Brazil 2014, chama cha soka cha hiyo DFB kimethibitisha.

Kila mchezaji atapata kiasi hicho chote cha fedha kwa kila mechi ya kufuzu, lakini watapokea kiasi hicho mara watakapoweza kufuzu kwenda kwenye michuano ya hiyo ya dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014.

"Nina furaha na uharaka na kutokuwepo kwa matatizo katika makubaliano haya. Hii inaonyesha uaminifu uliopo kati ya shirikisho na wachezaji wa timu ya wakubwa ya soka ya Ujerumani," alisema Raisi wa shirikisho hilo Mr.Wolfgang Niersbach.

Ujerumani tayari wameshashinda mechi zao mbili za kundi C na mpaka sasa wanapewa nafasi kubwa ya kuwa viongozi wa kundi hilo  kwa kuongeza pointi 6 nyingine watakapocheza na Irealnd na Sweden Ijuma na Jumanne ijayo.
 

MTOTO WA MANUTE BOL KATIKA HARAKATI ZA KURITHI UWEZO WA BABA YAKE KATIKA NBA

Tuesday, October 9, 2012

ENGLAND WAZINDUA KITUO CHA ST.GEORGE PARK CHENYE THAMANI YA £100 MILLION


Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William na mkewe Kate wakizindua kituo cha St.George Park





Frank Lampard akitaniana na Duchess of Cambridge - mke wa Prince William ambaye ni Raisi wa FA.

Raisi wa FA Prince William akizungumza na wachezaji wa England

Game for a laugh: Wayne Rooney jokes with England coach Gary Neville
Wayne Rooney akifurahia jambo na kocha wake msaidizi Gary Neville

Prince William akimtania Ashley Cole - Mchezaji ambaye juzi aliwatolea maneno machafu chama cha soka cha FA ambacho mjukuu huyo wa Malkia ndio Raisi.

Wachezaji wa England wakiwa kwenye Jaccuzi wakipumzika baada ya mazoezi

Kituo cha ST.George Park kilivyo

St.George Park

Hostel za kituo cha St.George Park

Uwanja wa ndani wa soka uliopo ndani ya kituo cha St.George Park

KWA USHAHIDI HUU NI KWELI LUIS SUAREZ ANAONEWA AU ANAJIRUSHA KWELI??


BAADA YA MASHABIKI KUGOMA KUINGIA UWANJANI - WACHEZAJI WA DINAMO WATOA MKWANJA MREFU KUWASHAWISHI MASHABIKI KUJAA UWANJANI

Baada ya kuumizwa na kitendo cha kucheza mechi za Champions league katika uwanja uliokaribia kuwa mtupu, wachezaji wa Dinamo Zagreb wameamua kuchanga fedha kwa ajili ya kuchezesha bahati nasibu ili kuwavutia mashabiki kuingia katika mechi yao ya Champions league inayofuatia dhidi ya PSG. Dinamo walicheza mechi yao iliyopita uwanjani kukiwa na watu wasiozidi 15,000 katika uwanja wenye siti zaidi ya 38,000, katika mechi dhidi ya Porto. Mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakiachana na kwenda kwenye mechi wakiwekea mgomo bei za tiketi na kuonyesha kutokubalina na uongozi wa klabu hiyo. Hivyo ili kushawishi mashabiki, wachezaji wa timu hiyo wameamua kutoa ofa ya million moja za kunas ambazo ni sawa na $174,000 katika bahati nasibu kwa wanunuzi wa tiketi wa mechi zao.

Kutoka AFP:
Wazo hilo lilianzishwa na kiungo Mateo Kovac ambaye aliweka video, "Million moja kwa uwanja ukijaa" katika ukurasa wake wa faceboo, kwenye viedo iliyokuwa ikimuonyesha akiongea na wachezaji wenzie.
Katika press conference ya Ijumaa iliyopita wachezaji walisema kiwango cha zawadi ya fedha kitategemeana na namba ya mashabiki watakaoingia kwenye uwanja katika mechi yo dhidi ya PSG itakayofanyika mwezi huu tarehe 24.
Million moja ya kunas otatolewa ikiwa tu zaidi ya mashabiki 25000 watakuja uwanjani.


ADAM MATUNGA: MAXIMO ALINISHAURI NISIJIUNGE NA YANGA - ATALIA AKIRUDI NCHINI NA KUNIONA




Kwa mchezaji ambaye amezaliwa mwaka 1989 bila shaka bado ni angali kijana hasa ambaye anaweza kutimiza ndoto zake za kimaisha kwa kutumia kipaji chochote ambacho hutokea kujaliwa na mwenyezi Mungu.

 Adam Matunga ni mchezaji wa mpira wa miguuu, na ni kijana ambaye amejaliwa kipaji cha hali ya juu cha mchezo huu, hasa akicheza kama kiungo mshambuliaji, aliwahi mara kadhaa kuitwa na kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha wa Kibrazil, Marcio Maximo. Alikuwa ni mmoja wa vijana wa mwanzo kuingizwa timu ya Taifa kwa nia ya kuendelezwa ili waje waisaidie timu hiyo katika siku za usoni, aliingia hasa katika moyo wa kocha, Maximo na bahati kubwa kwake ni kwamba aliitwa akitokea timu ya moani ya AFC Arusha mwaka 2007. Lakini yupo wapi hivi sasa, ana fanya nini na kwa nini hasisiki tena kama matarajio ya wengi yalivyokuwa yakifikiria? 

Yote haya www.shaffihdauda.com inakuletea baada ya kumkuta kijana huyu wa mwaka 1989 akicheza soka la‘Kiveterani’ na wakongwe kina Sanifu Lazaro ‘Tingisha’ na Sekilojo Johnson Chambua…..

SWALI; Mbona kimya na hausikiki tena katika soka la Tanzania, nini kimekusibu?

MATUNGA; Nilipata matatizo makubwa ya goti nikiwa Mtibwa Sugar mwaka 2008, na kuna wakati nikapatwa na hisia mbaya kuhusiana na mchezo huu, sikuona faida yake kwani viongozi wengi ni waongo, unakaa kambini kwa miezi mingi unarudi nyumbani hata pesa ya likizo hapewi. Nadhani ni wachezaji wachache sana ndiyo wanaofaidika na soka la nchi hii. Ukitazama hata hao waliopo timu kubwa wengi wana maisha mabovu sana Kaka , hilo nalo lilinikatisha sana tamaa. Unajua kuna wachezaji wapo Simba na Yanga wanawaomba wale ambao wapo mitaani msaada, kweli inatakiwa moyo kucheza mpira katika nchi hii.

SWALI; Je, hiyo ndiyo unadhani sababu kubwa ya wewe kukufanya ushindwe kutimiza malengo yako?

MATUNGA; Mimi bado kijana mdogo na bado nina ndoto za kufanikiwa katika soka, lakinmi niliamua kupumzika kidogo ili nitafute kwanza pesa ili nije niucheze pasipo kuwa na mawazo, na hata hilo la ‘usanjo’ wa viongozi wengi wa mpira nchini unachangia kuwaondoa vijana wengi kwenye soka. Mimi najiandaa kurejea uwanjani kwani hivi sasa nitacheza soka bila kuwa na mawazo kwani nilichokuwa nakitafuta ( pesa) nimeshapata.

SWALI; Ipi ni timu yako ya mwisho kuichezea na Je, kwa upande wa kambi ya timu ya Taifa kwa kipindi kifupi ambacho wewe ulikuwa katika kikosi hicho ulikutana na hali hii ya ‘usamjo’ wa viongozi hasa katika masuala ya ulipaji wa posho?

MATUNGA; Manyema Rangers ndiyo timu yangu ya mwisho kuicheza kabla sijaamua kutafuta pesa kwanza, ilikuwa ni mwaka 2010. Kwa upande wa timu ya Taifa kama kulikuwa na matatizo nadhani ni miaka ya nyuma, kwa muda ambao mimi nilibahatika kuingia kikosini sikuona hali hiyo, posho ilikuwa inakuja kwa wakati na ilikuwa imepanda pia, timu ilikuwa inafilkia na kuweka kambi katika hotel kubwa na zenye hadhi. Nadhani yote hii sababu ya kocha, Maximo yeye alikuwa ni zaidi ya kocha, alikuwa ni kama Baba kwa wachezaji wengi nchini, ndiye aliyebadilisha maisha ya wachezaji wengi nchini ‘ per day’ ilikuwa nzuri, mnalala sehemu nzuri , binafsi ninamkubali sana Maximo na kanisaidia sana Kaka.

SWALI; Unamzungumziaje, Maximo na vitu gani ambavyo alikuwa akikwambia kama msaada wako katika siku za usoni?

MATUNGA; Ukweli ni vitu vingi sana ambavyo aliniambia na ndiyo ambavyo nimekuwa nikivitumia hasi leo katika maisha yangu, kama nilivyokwambia awali kuwa Maximo alikuwa zaidi ya kocha hivyo alijua maisha ya wachezaji wa Kitanzania yalivyo hivyo alikuwa akinambia hata mambo ya kufanya kama binadamu ninayehitaji kuwa na maisha mazuri. Kikubwa nachokumbuka aliniambia ‘ Usiichague Yanga, nenda Mtibwa kwa manufaa ya mchezo wako” hakutaka mimi niende Yanga kwa sababu alioniona bado kijana mdogo na nisingeweza kuhimili presha ya timu hiyo, hivyo akaniambia niende Mtibwa na kweli nikafanya hivyo.

SWALI; Unadhani kwa nini alikwambia usiende Yanga na uende Mtibwa wakati wengi huchagua kwanza Yanga ama Simba na si timu za mikoani pale wanapopata ‘ofa’ kama yako?

MATUNGA; Aliniambia nikicheza Mtibwa nitakuwa na kiwango kizuri zaidi kwani nilikuwa bado mdogo na alihitaji kuniona nikikua taratibu, pia aliniambia presha iliyopo Mtibwa ni ndogo tofauti na iliyopo Yanga hivyo kwa umri wangu mahala sahihi aliona ni kule, na kweli nilifurahi sana nilipokuwa katika klabu ile ( Mtibwa)
SWALI; Unadhani, Maximo akija Tanzania hivi sasa na kukuona ukicheza mechi za ‘veterani’ atajisikiaje, kwani alikuwa na matarajio makubwa kukuona ukipata mafaniko katika soka?

MATUNGA; Atasikitika sana kaka. Yaani alikuwa akiniona ni bonge la mchezaji kila nilipokuwa uwanjani, alikuwa anapenda kunitazama, na mara zote alihitaji kuona wachjezaji wenzangu wananipasia mipira mimi. Utamsikia nje akisema “ ADAM, VOMELAA VOMELAA ( Adam zungushaa, zungusha), alikuwa akiniambia nacheza soka la kibrazil, furaha yake ilikuwa kuniona mimi namiliki mpira.

SWALI; Mara ngapi uliiwakilisha Stars chini yake (Maximo) na nini malengo yako sasa?

Chini ya Maximo mara tatu niliichezea Stars na pia nilipata kuicheza Kilimanjaro Srars ( Tanzania Bara). Narudi uwanjani kumuenzi marehemu, Baba yangu ambaye alikuwa akihitaji kuniona mwanae nacheza tena soka , nilimpenda sana Baba yangu lakini mungu amempenda zaidi, narudi uwanjani kwa nguvu zote sina mawazo ya pesa tena itakuwa ni soka tu kwani ndiyo furaha yangu.
SWALI; Unadhani nini kinachangia ugumu wa maisha kwa wachezaji wengi wa ligi kuu nchini?

MATUNGA; Malipo ni madogo sana na maisha yanapanda kila siku, mchezaji huwezi kupata mafanikio kama unaishi maisha ya kubahatisha ni lazima ule vizuri na hata wachezaji wanakimbilia kusaini hovyo mikataba wakati ukweli wa maisha ni tofauti na wanachosaini wachezaji ambao wanapata bahati ya kushika walau vimillioni ni vyema wakakumbuka kuwa kuna maisha nje ya soka, wapunguze kuishi Ki-star waukubali ukweli na wafungue miradi ambayo itawasitiri mara baada ya kumaliza kucheza soka. Pia ni wakati pia kwa viongozi kuwathamini na kuwajali wachezaji, wasiwacheweleshee mishahara yao na watazame pia hata malipo yao ya posho na aina ya maisha ya sasa.

SWALI; Umekuwa ukijumuika na kucheza pamoja na wachezaji ‘veterani’ kina Sekilojo Chambua na Sanifu Lazaro ambao kimsingi tayari wameshashinda mataji makubwa hapa nchini, kitu gani wamekuwa wakikueleza na ambacho kinawauma kukuona ukijumuika nao wao badala ya kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya Taifa?

Wamekuwa waninisisitiza umuhimu wa mimi kurejea uwanjani na kucheza soka la ushindani, kila napokutana na wao hayo maneno lazima waniambie na sitawangusha najiaanda., inshalah Mungu akijalia ‘next season’ nitakuwa uwanjani tena

SWALI; Unacheza kama nani?

MATUNGA; Kama Iniesta Kaka nampenda sana Iniesta anaisadia sana timu yake ya Barcelona na ie ya Hispania

SHABIKI WA YANGA AFARIKI BAADA YA KUSHINDA KWENYE SHINDANO LA KULA MENDE MAREKANI


Edward akila mende
Mshindi wa shindano la kula mende amefariki dunia muda mfupi  kula mende wazima huko Florida -Marekani, polisi wamesema.

Edward Archbold, 32, ambaye alisema kwamba ameshawahi kula wadudu hao huko nyumbani kwao Dar es Salaam, Tanzania alianza kuumwa na hatimaye kuanguka katika duka la wadudu mahala ambapo shindano hilo lilikuwa likifanyika katika mji wa Deerfield Beach Ijumaa iliyopita.

Kuna zaidi ya watu 30 walioshiriki shindano hilo katika duka la Ben Siegel Reptile Store.
Mamalka zinasubiri matokeo ya vipimo vya hosptali ili kujua chanzo cha kifo cha Archbold.

Hakuna mtu yoyote aliyeshiriki kwenye shindano hilo aliyeumwa baada ya kumalizika kwa shindano hilo, walisema polisi.
"Tumesikitika sana juu ya tukio hili," alisema Ben Siegel , mmiliki wa duka la wadudu.
""Alionekana kama alitaka kujionyesha na alikuwa mtu mzuri sana," alisema, akiongeza kwamba Archbold hakuonekana kuwa anaumwa kabisa.

Mwanasheria wa Mr.Siegel  alisema kwamba washiriki wote walisaini maelezo kwamba "wanakubaliana na matokeo yoyote yatakayotokea kutokana na kushiriki mchezo huo wa ajabu.

Mr.Archbold ambaye alikuwa anajulikana kwa mapenzi yake makubwa kwa timu ya Young Africans ya nchini Tanzania, alishinda shindano hilo lakini badae kidogo akadondoka na kufa.
 

PHOTOS: YANGA WALIPOLAMBISHWA SUKARI NA KAGERA MJINI BUKOBA

 Ligi kuu ya Tanzania Bara imeendelea hii leo katika uwanja wa kaitaba Mjini Bukoba ambapo timu ya Yanga imeambulia kichapo cha bao 1-0 Kutoka kwa wakata miwa wa Kagera Sugar. (Picha kwa hisani ya bukobawadau blog))
 Mfungaji wa bao la  Kagera Sugar Temmy Alphonce pichani kulia.
Bao la Kagera Sugar limepatikana dk ya 40 kipindi cha pili cha mchezo, Bao hilo limefungwa na mchezaji mahiri mzaliwa wa Kimbugu Muleba Temmy Alfonce.
 Kocha wa Kagera Abdallah King Kibadeni




 Benchi la wachezaji wa timu ya Yanga katika hali ya sintofahamu
 Safu imara ya Kagera Sugar ikiongozwa na goli kipa Andrew Ntalla na walinzi wake wa karibu kama Juma Nade na Kanoni Salim wanastahili pongezi.
 Hekaheka  kuelekea langoni mwa Yanga.
 Mchezaji wa Yanga Said Bahanzi aumia  vibaya baada ya kuangka mnamo dakika ya 22 kipindi cha kwanza cha mchezo.

 Bahanzi akipata matibaba kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na  Jeryson Tegete
 Jeryson Tegete akijiandaa kuingia uwanjani
Wachezaji wa Kagera Sugar wakielekea mapumziko baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.
 Sehemu ya mashabiki wa Kagera Sugar Jukwaani
 Wadau wa soka na habari  kutoka Kasibante Fm Radio
 Kamisaa wa mchezo
 Waandishi wa habari
 Sehemu ya mashabiki wa soka Jukwaa la mchanganyiko
 Jukwaa la Golani

Monday, October 8, 2012

LIVE MATCH CENTRE: KAGERA SUGAR 1 - 0 YANGA -FULL TIME


Dakika ya 86, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Nurdin Bakari anatoka Stephano Mwasika
Dakika ya 70, Kagera Sugar 1 - 0 Young Africans
Dakika ya 68, Themi Felix anaipatia Kagera Sugar bao la kwanza

 Dakika ya 55, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Shamte Ally anatoka Nizar Khalfani 

DK ya 50 Kagera Sugar 0 - 0 Young Africans 

 Kipindi cha pili cha mchezo ndio kimeanza, Kagera Sugar 0 - 0 Young Africans 

Mpira ni mapumziko, Kagera Sugar 0 - 0 Young Africans
Dakika ya 30, Kagera Sugar 0 - 0 Young Africans

 Dakika ya 22, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Jeryson Tegete kuchukua nafasi ya Said Bahanunzi aliyeumia.

 Dakika ya 15, Kagera Sugar 0 - 0 Young Africans
 
DK 10: Yanga 0 - 0 Kagera Sugar 

DK 1: Mpira umeanza hapa uwanja wa Kaitaba.

KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA
1.Yaw Berko
2.Juma Abdul
3.Stephano Mwasika
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (C)
5.Mbuyu Twite
6.Athuman Idd 'Chuji'
7.Nizar Khalfan
8.Frank Domayo
9.Said Bahanunzi

10.Didier Kavumbagu
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Ally Mustapha 'Barthez'
2.Oscar Joshua
3.Ladislaus Mbogo
4.Omega Seme
5.Shamte Ally
6.Nurdin Bakari
7.Jeryson Tegete

EXCLUSIVE: NURDIN BAKARY - SAID SUED NDIO ALIYENIFUNDISHA VIZURI SOKA - USHIRIKIANO WETU NDANI YA SIMBA ULIKUWA NOMA





Kiungo Nurdin Bakar ameshapona majeraha yake ambayo yalimfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitano. Nurdin ambaye anaingia katika msimu wake wa kumi katika ligi kuu Tanzania Bara, huku akiwa amezichezea klabu mbili tu za Simba na Yanga, alikutana na mwandishi wa mtandao huu na kukutana na maswali kadhaa ambayo www.shaffihdauda.com imeonani vyema ikikupatia sehemu ya mazungumzo hayo.


SWALI; Kwa muda mrefu umekuwa ukisumbuliwa na majeraha na mechi yako ya mwisho kucheza ilikuwa ni ile dhidi ya Simba msimu uliopita na baada ya hapo ukapata nafasi ya kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya Taifa, lakini ukaumia na tangu, Juni mwaka huu hujacheza mchezo wowote, vipi hali yako kwa sasa?

NURDIN; Hivi sasa naendelea vizuri na naweza kucheza mechi pale nitakapopata nafasi.

SWALI; Kwa kipindi chote hicho ni namna gani umeumiss mchezo huu na ulikuwa ukijisikiaje binafsi kujiona upo nje ya mchezo kutokana na majeraha?

NURDIN; Sidhani kama kuna mtu anafurahia kuumwa kaka, Iliniuma sana kutokana na kwamba soka ndiyo kazi yangu, nategemea uzima huku miguu yangu ikifanya kazi ili niweze kuishi, lakini kila jambo hupangwa na mungu  kwani ndiye hupanga kila kitu hapa duniani.

SWALI; Unadhani unafuraha hivi sasa na nini umepanga kufanya  mara baada ya kupata nafasi kikosini?

NURDIN; Ndiyo, nina furaha kubwa kurejea uwanjani kwani kutanisaidia kuonekana tena mbele ya watu, huwezi kujua naweza kupata bahati ya kupata timu nje ya nchi

SWALI; Je, klabu yako ina imani gani na wewe?

NURDIN; Klabu ina niamini  kama mchezaji mzuri na bora aliyepo katika kikosi, ndiyo maana nipo hapa na wamekuwa wakinisaidia kuhakikisha narejea tena uwanjani na kucheza soka

SWALI; Umefanya kazi na makocha kama Dusan Kondic, Kostadin Papic na Sam Timbe na wote walikuamini sana, hukupata bahati ya kufanya kazi ndani ya uwanjani Tom Saintfiet.... Unamzungumziaje kocha, Tom ambaye ameondolewa ndani ya timu muda mfupi baada ya kuingia?

NURDIN; Nashukuru nilikuwa na mahusiano mazuri tu na makocha wote ambao nimewahi kufanya nao kazi, si hao tu wapo wengi Kaka. Siwezi kumzungumzia, Tom mimi nahitaji kufanya kazi inayotakiwa na kocha yoyote yule.

SWALI; Kuna maingizo mengi ya viungo vijana katika kikosi chenu, unazungumziaje sasa uwepo wako katika kikosi cha kwanza , kwani kwa misimu minne ambayo umecheza Yanga inaonekana msimu huu ukawa na ushindani mkubwa kwa kila nafasi ndani ya timu yenu?

NURDIN; Na imani kwa jitihada zangu na mafundisho ya makocha wangu nitacheza, ila kocha ndiye mwenye uamuzi wa mwisho, kwani ana muono wake . Viungo wote Yanga ni 'moto' na ushindani wa nafasi ni mkubwa sana

SWALI; Unaonekana kuwa na uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani, nini siri ya hili?

NURDIN; Wakati nacheza mpira wa utotoni nilikuwa na tabia ya kuhama hama namba mchezoni. Kikubwa nakuwa msikivu sana  na kufanya ambacho nakuwa nafundishwa na makocha wangu  na mimi mwenyewe kuongeza jitihada zangu binafsi.

SWALI; Unawezaje kuibuka na kufunga mabao muhimu katika michezo mikubwa na migumu, unawezaje kufunga mabao ya vicha wakati huna kimo kirefu?

NURDIN; Huwa najipanga vizuri kutokana na uelekeo wa mpira unapokwenda, hivyo huwa najipanga vizuri kusubiri mipira na mara nyingi nimefanikiwa kufunga baada ya kujipanga vizuri

SWALI; Unamzungumiaje, Said Sued ambaye mlitokea kuwa mabeki bora wa pembeni mnaoshirikiana vizuri kila mmoja akibadilisha nafasi na mwenzake, nini siri ya uchezaji wenu ule ambao haupo tena na wala hauonekani kwa timu nyingine?

NURDIN; Yaani, huyo Sued mimi ndiye alikuwa akinielekeza  jinsi ya kucheza, tulikuwa na ushirikiano mzuri sana na tulikuwa tukiishi pamoja katika nyumba moja. Ushirikiano wetu ndani ya Simba ulikuwa ni mzuri, tulikuwa tukiishi kama familia moja nadhani ushirikiano ule ulianzia ndani ya nyumba yetu na kuupeleka uwanjani na tulifanikiwa sana.

SWALI; Kwa nini uliondoka Simba SC?

NURDIN; Sifahamu, kwa nini waliniacha kwani nilikuwa bado kijana mbichi.

SWALI; Kwa nini ulichagua Yanga na si timu nyingine mara baada ya kuondoka Simba?

NURDIN; Niliichagua Yanga kwa sababu ndioyo klabu iliyonihitaji, na nina furaha kuwa ndani ya timu hii.

SWALI; Nini malengo yako sasa mara baada ya kupona majeraha yako, umecheza Simba na Yanga kwa miaka tisa mfululizo sasa, nini umejifunza?

NURDIN; Malengo yangu bado hayajatimia, nahitaji kucheza zaidi nje ya nchi katika siku za usoni. Nafurahi tu kuwa nimeweza kucheza katika vilabu vikubwa vya Tanzania kwa miaka tisa mfululizo nje ya mafanikio nimejifunza mengi sana kama binadamu, kuwa na nidhamu na jinsi  ya kuishi vizuri na kila mtu imekuwa ni sehemu iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuwa hapa nilipo

SIMBA NA OLJORO WAINGIZA MIL.40 - TIMU ZAGAWANA MIL. 16

Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Oljoro JKT ya Arusha lililochezwa jana (Oktoba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 limeingiza sh. 46,680,000.
 
Watazamaji 8,081 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 8,172,396.61 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 7,120,677.97.
 
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 193,000, waamuzi sh. 210,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,175,000. Gharama za mchezo sh. 2,724,132.20, uwanja sh. 2,724,132.20, Kamati ya Ligi sh. 2,724,132.20, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,634,479.32 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,089,652.88.

Airtel na msanii AY waanza kampeni za kusaidia shule nchini

Na Mwandishi wetu

 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii imeanza mchakato wa kutembelea baadhi ya shule zitakazonufaika na mradi maalum wa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum ili kujionea changamoto zinazowakabili pamoja na kuwahimiza watanzania kuweza kuchangia mradi huo unaoendeshwa kwa ushirikiano na Baraza la maendeleo ya vitabu Tanzania (BAMVITA).Afisa mawasiliano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki amesema kampuni hiyo ikiwa na Balozi wake msanii Maarufu AY itatembelea shule zote zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubaiunisha matatizo wanaoyokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia.Amesema shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum zinahitaji vitendea kazi vingi ili kuwafanya wanafunzi hao kuweza kupatiwa elimu inayostahili.

“Shule hizi zinamahitaji mengi sana, Airtel tumeona ni vyema kumtumia pia Balozi wetu huyu msanii maarufu nchini A Y kuendea kuwafikishia jamiii ujumbe waendelee kuchangia katika mradi huu wenye lengo la kuendeleza jamii” alisema Bi DANGIO KANIKI Afisa mawasiliano na matukio wa AirtelAkizungumza mara baada ya kutembelea shule ya msingi Sinza Maalum Balozi wa Airtel AMBWENE YESAYA (A.Y) amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuongeza kiwango cha elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.

“Watoto hawa wenye uhitaji maalum nimejionea mwenyewe kuwa wakiwezeshwa wanaweza, ndio maana naona ni vyema zaidi kushirikiana na Airtel pamoja na jamii kwa ujumla kuhakikisha tunawachangia vijana wetu hawa nao waweze kuendeleza hata vipaji vyao pamoja na elimu yao Ninaomba kuwakubusha watanzania kuchangia katika kuwapatia vijana hawa vifaa mbalimbali ambavyo ni changamoto kwao, unaweza kuchangia kwa kupitia Airtel Money ambapo unaandika jina la fumbo VITABU na utatuma kiasi chochote au kwa kutuma SMS yenye neno VITABU kwenda namba 15626 na atakuwa amechangia shilingi 200 tu.Watanzania naomba tusaidiane katika elimu kwa kuwa tuanaamini Tanzania itajengwa na sisi wenyewe. Alimalizia kusema

AMBWENE YESAYA ---Balozi wa AirtelWakati wa ziara hio mwuishoni mwa wiki hii Mwalimu Mkuu wa shule ya Sinza Maalum, SIMON Milobo alibainisha kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia pamoja na mafuta ya kuendeshea gari la wanafunzi.Kampeni ya Airtel kwa kushirikiana na Bamvita itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu , na Watanzania wataweza kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS utakayotuma utakuwa umechangia shilingi 200 itakayoingizwa katika mradi huu”

 Mwananafunzi wa shule ya Sinza Maalum akiimba wimbo wa mwanamuzi Ambwene Yesaya (AY) walipotembelewa na mwanamuzi huyo mwishoni mwa wiki hii wakiongozana na wafanyakazi wa Airtel, kushoto ni meneja mahusiano wa jamii  wa Airtel Hawa Bayumi, watatu kutoka kulia Ambwene  Yessaya (AY) akifwatiwa na Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki.  Student of Sinza Maalum performing a song of R&B artist Ambwene Yessaya known as AY, when he visited the school accompanied by Airtel staffs  end of this week, left is Corporate Social Responsibility Manager of Airtel Hawa Bayumi,, third from right is Airtel ambassador Ambwene  Yessaya followed by Public Relations and Events officer  of Airtel Dangio Kaniki
 Wafanyakazi wa Airtel wakiwa na balozi wao Ambwene Yesaya  katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sinza Maalum iliyopo jijini Dar Es Salaam walipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii kama mwendelezo wao wa kusaidia jamii kwa watoto wenye mahitaji maalum kupitia mradi wao wa kuchangia Elimu  kwa kushirikiana na BAMVITA.Staff s from Airtel with their ambassador Ambwene Yessaya (AY) on a group picture with students from Sinza Maalum in Dar Es Salaam when visited the school at the end of this week as part of supporting  schools with special needs in education through their project who are working together with Bamvita.
Balozi wa Airtel Ambwene Yesaya (AY) wakiimba kwa pamoja na mwanafunzi wa shule ya Sinza Maalum (Kushoto) mwishoni mwa wiki hii walipotembelewa na mwanamuzi huyu aliyeongozana na wafanyakazi wa Airtel kama mwendelezo wao wa kusaidia jamii kwa watoto wenye mahitaji maalum kupitia mradi wao wakishirikiana na Bamvita wa kuchangia Elimu. Airtel ambassador Ambwene Yessaya (AY) singing together  with a student of Sinza Maalum (left) the end of this week when they had a visit from him followed by Airtel staff as continuation of Airtel supporting education to this country  with children with special needs who are working together  with Bamvita .

SIMBA NA YANGA TWAMBIENI HUU MCHONGO WA NANI ?