Search This Blog

Tuesday, October 9, 2012

ADAM MATUNGA: MAXIMO ALINISHAURI NISIJIUNGE NA YANGA - ATALIA AKIRUDI NCHINI NA KUNIONA




Kwa mchezaji ambaye amezaliwa mwaka 1989 bila shaka bado ni angali kijana hasa ambaye anaweza kutimiza ndoto zake za kimaisha kwa kutumia kipaji chochote ambacho hutokea kujaliwa na mwenyezi Mungu.

 Adam Matunga ni mchezaji wa mpira wa miguuu, na ni kijana ambaye amejaliwa kipaji cha hali ya juu cha mchezo huu, hasa akicheza kama kiungo mshambuliaji, aliwahi mara kadhaa kuitwa na kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha wa Kibrazil, Marcio Maximo. Alikuwa ni mmoja wa vijana wa mwanzo kuingizwa timu ya Taifa kwa nia ya kuendelezwa ili waje waisaidie timu hiyo katika siku za usoni, aliingia hasa katika moyo wa kocha, Maximo na bahati kubwa kwake ni kwamba aliitwa akitokea timu ya moani ya AFC Arusha mwaka 2007. Lakini yupo wapi hivi sasa, ana fanya nini na kwa nini hasisiki tena kama matarajio ya wengi yalivyokuwa yakifikiria? 

Yote haya www.shaffihdauda.com inakuletea baada ya kumkuta kijana huyu wa mwaka 1989 akicheza soka la‘Kiveterani’ na wakongwe kina Sanifu Lazaro ‘Tingisha’ na Sekilojo Johnson Chambua…..

SWALI; Mbona kimya na hausikiki tena katika soka la Tanzania, nini kimekusibu?

MATUNGA; Nilipata matatizo makubwa ya goti nikiwa Mtibwa Sugar mwaka 2008, na kuna wakati nikapatwa na hisia mbaya kuhusiana na mchezo huu, sikuona faida yake kwani viongozi wengi ni waongo, unakaa kambini kwa miezi mingi unarudi nyumbani hata pesa ya likizo hapewi. Nadhani ni wachezaji wachache sana ndiyo wanaofaidika na soka la nchi hii. Ukitazama hata hao waliopo timu kubwa wengi wana maisha mabovu sana Kaka , hilo nalo lilinikatisha sana tamaa. Unajua kuna wachezaji wapo Simba na Yanga wanawaomba wale ambao wapo mitaani msaada, kweli inatakiwa moyo kucheza mpira katika nchi hii.

SWALI; Je, hiyo ndiyo unadhani sababu kubwa ya wewe kukufanya ushindwe kutimiza malengo yako?

MATUNGA; Mimi bado kijana mdogo na bado nina ndoto za kufanikiwa katika soka, lakinmi niliamua kupumzika kidogo ili nitafute kwanza pesa ili nije niucheze pasipo kuwa na mawazo, na hata hilo la ‘usanjo’ wa viongozi wengi wa mpira nchini unachangia kuwaondoa vijana wengi kwenye soka. Mimi najiandaa kurejea uwanjani kwani hivi sasa nitacheza soka bila kuwa na mawazo kwani nilichokuwa nakitafuta ( pesa) nimeshapata.

SWALI; Ipi ni timu yako ya mwisho kuichezea na Je, kwa upande wa kambi ya timu ya Taifa kwa kipindi kifupi ambacho wewe ulikuwa katika kikosi hicho ulikutana na hali hii ya ‘usamjo’ wa viongozi hasa katika masuala ya ulipaji wa posho?

MATUNGA; Manyema Rangers ndiyo timu yangu ya mwisho kuicheza kabla sijaamua kutafuta pesa kwanza, ilikuwa ni mwaka 2010. Kwa upande wa timu ya Taifa kama kulikuwa na matatizo nadhani ni miaka ya nyuma, kwa muda ambao mimi nilibahatika kuingia kikosini sikuona hali hiyo, posho ilikuwa inakuja kwa wakati na ilikuwa imepanda pia, timu ilikuwa inafilkia na kuweka kambi katika hotel kubwa na zenye hadhi. Nadhani yote hii sababu ya kocha, Maximo yeye alikuwa ni zaidi ya kocha, alikuwa ni kama Baba kwa wachezaji wengi nchini, ndiye aliyebadilisha maisha ya wachezaji wengi nchini ‘ per day’ ilikuwa nzuri, mnalala sehemu nzuri , binafsi ninamkubali sana Maximo na kanisaidia sana Kaka.

SWALI; Unamzungumziaje, Maximo na vitu gani ambavyo alikuwa akikwambia kama msaada wako katika siku za usoni?

MATUNGA; Ukweli ni vitu vingi sana ambavyo aliniambia na ndiyo ambavyo nimekuwa nikivitumia hasi leo katika maisha yangu, kama nilivyokwambia awali kuwa Maximo alikuwa zaidi ya kocha hivyo alijua maisha ya wachezaji wa Kitanzania yalivyo hivyo alikuwa akinambia hata mambo ya kufanya kama binadamu ninayehitaji kuwa na maisha mazuri. Kikubwa nachokumbuka aliniambia ‘ Usiichague Yanga, nenda Mtibwa kwa manufaa ya mchezo wako” hakutaka mimi niende Yanga kwa sababu alioniona bado kijana mdogo na nisingeweza kuhimili presha ya timu hiyo, hivyo akaniambia niende Mtibwa na kweli nikafanya hivyo.

SWALI; Unadhani kwa nini alikwambia usiende Yanga na uende Mtibwa wakati wengi huchagua kwanza Yanga ama Simba na si timu za mikoani pale wanapopata ‘ofa’ kama yako?

MATUNGA; Aliniambia nikicheza Mtibwa nitakuwa na kiwango kizuri zaidi kwani nilikuwa bado mdogo na alihitaji kuniona nikikua taratibu, pia aliniambia presha iliyopo Mtibwa ni ndogo tofauti na iliyopo Yanga hivyo kwa umri wangu mahala sahihi aliona ni kule, na kweli nilifurahi sana nilipokuwa katika klabu ile ( Mtibwa)
SWALI; Unadhani, Maximo akija Tanzania hivi sasa na kukuona ukicheza mechi za ‘veterani’ atajisikiaje, kwani alikuwa na matarajio makubwa kukuona ukipata mafaniko katika soka?

MATUNGA; Atasikitika sana kaka. Yaani alikuwa akiniona ni bonge la mchezaji kila nilipokuwa uwanjani, alikuwa anapenda kunitazama, na mara zote alihitaji kuona wachjezaji wenzangu wananipasia mipira mimi. Utamsikia nje akisema “ ADAM, VOMELAA VOMELAA ( Adam zungushaa, zungusha), alikuwa akiniambia nacheza soka la kibrazil, furaha yake ilikuwa kuniona mimi namiliki mpira.

SWALI; Mara ngapi uliiwakilisha Stars chini yake (Maximo) na nini malengo yako sasa?

Chini ya Maximo mara tatu niliichezea Stars na pia nilipata kuicheza Kilimanjaro Srars ( Tanzania Bara). Narudi uwanjani kumuenzi marehemu, Baba yangu ambaye alikuwa akihitaji kuniona mwanae nacheza tena soka , nilimpenda sana Baba yangu lakini mungu amempenda zaidi, narudi uwanjani kwa nguvu zote sina mawazo ya pesa tena itakuwa ni soka tu kwani ndiyo furaha yangu.
SWALI; Unadhani nini kinachangia ugumu wa maisha kwa wachezaji wengi wa ligi kuu nchini?

MATUNGA; Malipo ni madogo sana na maisha yanapanda kila siku, mchezaji huwezi kupata mafanikio kama unaishi maisha ya kubahatisha ni lazima ule vizuri na hata wachezaji wanakimbilia kusaini hovyo mikataba wakati ukweli wa maisha ni tofauti na wanachosaini wachezaji ambao wanapata bahati ya kushika walau vimillioni ni vyema wakakumbuka kuwa kuna maisha nje ya soka, wapunguze kuishi Ki-star waukubali ukweli na wafungue miradi ambayo itawasitiri mara baada ya kumaliza kucheza soka. Pia ni wakati pia kwa viongozi kuwathamini na kuwajali wachezaji, wasiwacheweleshee mishahara yao na watazame pia hata malipo yao ya posho na aina ya maisha ya sasa.

SWALI; Umekuwa ukijumuika na kucheza pamoja na wachezaji ‘veterani’ kina Sekilojo Chambua na Sanifu Lazaro ambao kimsingi tayari wameshashinda mataji makubwa hapa nchini, kitu gani wamekuwa wakikueleza na ambacho kinawauma kukuona ukijumuika nao wao badala ya kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya Taifa?

Wamekuwa waninisisitiza umuhimu wa mimi kurejea uwanjani na kucheza soka la ushindani, kila napokutana na wao hayo maneno lazima waniambie na sitawangusha najiaanda., inshalah Mungu akijalia ‘next season’ nitakuwa uwanjani tena

SWALI; Unacheza kama nani?

MATUNGA; Kama Iniesta Kaka nampenda sana Iniesta anaisadia sana timu yake ya Barcelona na ie ya Hispania

No comments:

Post a Comment