Kiungo Nurdin Bakar ameshapona majeraha yake ambayo yalimfanya kuwa
nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitano. Nurdin ambaye anaingia katika
msimu wake wa kumi katika ligi kuu Tanzania Bara, huku akiwa amezichezea
klabu mbili tu za Simba na Yanga, alikutana na mwandishi wa mtandao huu
na kukutana na maswali kadhaa ambayo www.shaffihdauda.com imeonani vyema ikikupatia sehemu ya mazungumzo hayo.
NURDIN; Hivi sasa naendelea vizuri na naweza kucheza mechi pale nitakapopata nafasi.
SWALI;
Kwa kipindi chote hicho ni namna gani umeumiss mchezo huu na ulikuwa
ukijisikiaje binafsi kujiona upo nje ya mchezo kutokana na majeraha?
NURDIN; Sidhani kama kuna mtu anafurahia kuumwa kaka, Iliniuma sana kutokana na kwamba soka ndiyo kazi yangu, nategemea
uzima huku miguu yangu ikifanya kazi ili niweze kuishi, lakini kila
jambo hupangwa na mungu kwani ndiye hupanga kila kitu hapa duniani.
SWALI; Unadhani unafuraha hivi sasa na nini umepanga kufanya mara baada ya kupata nafasi kikosini?
NURDIN;
Ndiyo, nina furaha kubwa kurejea uwanjani kwani kutanisaidia kuonekana
tena mbele ya watu, huwezi kujua naweza kupata bahati ya kupata timu nje
ya nchi
SWALI; Je, klabu yako ina imani gani na wewe?
NURDIN;
Klabu ina niamini kama mchezaji mzuri na bora aliyepo katika kikosi,
ndiyo maana nipo hapa na wamekuwa wakinisaidia kuhakikisha narejea tena
uwanjani na kucheza soka
SWALI; Umefanya kazi na makocha kama Dusan Kondic,
Kostadin Papic na Sam Timbe na wote walikuamini sana, hukupata bahati
ya kufanya kazi ndani ya uwanjani Tom Saintfiet.... Unamzungumziaje
kocha, Tom ambaye ameondolewa ndani ya timu muda mfupi baada ya kuingia?
NURDIN; Nashukuru nilikuwa na mahusiano mazuri tu na
makocha wote ambao nimewahi kufanya nao kazi, si hao tu wapo wengi
Kaka. Siwezi kumzungumzia, Tom mimi nahitaji kufanya kazi inayotakiwa na
kocha yoyote yule.
SWALI; Kuna maingizo mengi ya viungo vijana katika
kikosi chenu, unazungumziaje sasa uwepo wako katika kikosi cha kwanza ,
kwani kwa misimu minne ambayo umecheza Yanga inaonekana msimu huu ukawa
na ushindani mkubwa kwa kila nafasi ndani ya timu yenu?
NURDIN; Na imani kwa jitihada zangu na mafundisho ya
makocha wangu nitacheza, ila kocha ndiye mwenye uamuzi wa mwisho, kwani
ana muono wake . Viungo wote Yanga ni 'moto' na ushindani wa nafasi ni
mkubwa sana
SWALI; Unaonekana kuwa na uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani, nini siri ya hili?
NURDIN;
Wakati nacheza mpira wa utotoni nilikuwa na tabia ya kuhama hama namba
mchezoni. Kikubwa nakuwa msikivu sana na kufanya ambacho nakuwa
nafundishwa na makocha wangu na mimi mwenyewe kuongeza jitihada zangu
binafsi.
SWALI; Unawezaje kuibuka na kufunga mabao muhimu
katika michezo mikubwa na migumu, unawezaje kufunga mabao ya vicha
wakati huna kimo kirefu?
NURDIN; Huwa najipanga
vizuri kutokana na uelekeo wa mpira unapokwenda, hivyo huwa najipanga
vizuri kusubiri mipira na mara nyingi nimefanikiwa kufunga baada ya
kujipanga vizuri
SWALI; Unamzungumiaje, Said Sued ambaye mlitokea
kuwa mabeki bora wa pembeni mnaoshirikiana vizuri kila mmoja
akibadilisha nafasi na mwenzake, nini siri ya uchezaji wenu ule ambao
haupo tena na wala hauonekani kwa timu nyingine?
NURDIN; Yaani, huyo Sued mimi ndiye alikuwa
akinielekeza jinsi ya kucheza, tulikuwa na ushirikiano mzuri sana na
tulikuwa tukiishi pamoja katika nyumba moja. Ushirikiano wetu ndani ya
Simba ulikuwa ni mzuri, tulikuwa tukiishi kama familia moja nadhani
ushirikiano ule ulianzia ndani ya nyumba yetu na kuupeleka uwanjani na
tulifanikiwa sana.
SWALI; Kwa nini uliondoka Simba SC?
NURDIN; Sifahamu, kwa nini waliniacha kwani nilikuwa bado kijana mbichi.
SWALI; Kwa nini ulichagua Yanga na si timu nyingine mara baada ya kuondoka Simba?
NURDIN; Niliichagua Yanga kwa sababu ndioyo klabu iliyonihitaji, na nina furaha kuwa ndani ya timu hii.
SWALI;
Nini malengo yako sasa mara baada ya kupona majeraha yako, umecheza
Simba na Yanga kwa miaka tisa mfululizo sasa, nini umejifunza?
NURDIN; Malengo yangu bado hayajatimia, nahitaji
kucheza zaidi nje ya nchi katika siku za usoni. Nafurahi tu kuwa nimeweza
kucheza katika vilabu vikubwa vya Tanzania kwa miaka tisa mfululizo nje
ya mafanikio nimejifunza mengi sana kama binadamu, kuwa na nidhamu na
jinsi ya kuishi vizuri na kila mtu imekuwa ni sehemu iliyochangia kwa
kiasi kikubwa kuwa hapa nilipo
No comments:
Post a Comment