Search This Blog

Thursday, May 17, 2012

PICHA: ANGALIA JINSI WACHEZAJI WA SIMBA NA YANGA WANAVYOMLILIA MAFISANGO



Haruna Moshi 'Boban' akiwa na simanzi baada ya kifo cha mwenzake.
Emmanuel Okwi (kulia) nae alifika Muhimbili baada ya tukio hilo.
Uhuru Seleman wa Simba akilia kwa huzuni baada ya kufika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 
Kiungo wa Yanga na mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima akiwa na majonzi kwa kifo cha mwenzake anayetokea Rwanda pia.
Beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa (kushoto) pamoja na Uhuru Seleman wakimlilia mchezaji mwenzao.
Kiungo wa Simba, Patrick Mafisango ‘Mutesa’, amefariki leo alfajiri katika ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya Chang’ombe maeneo ya Chuo cha Ufundi, Veta, jijini Dar es Salaam.
Mtandao huu uliushuhudia mwili wa marehemu ukiwa umetapakaa damu nzito ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mchezaji huyo alipata ajali hiyo akitokea Klabu ya New Maisha kuelekea nyumbani kwake ambapo ndani ya gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Cresta lenye namba za usajili T 387 BMZ kulikuwa na wenzake watatu ambao wote walitoka salama kwenye ajali hiyo.
(PICHA:RICHARD BUKOS/GPL )

HARUNA MOSHI BOBAN AONGOZA MSAFARA WA WACHEZAJI WA SIMBA KWENDA MOCHWARI KUONA MWILI WA MWENZAO MAFISANGO





MASTAA WA TANZANIA WANAZUNGUMZIAJE KIFO CHA MAFISANGO

R.I.P Patrick Mafisango... Simba Sports Club and Rwanda National Team player
Rest in Peace PATRICK MUTEESA MAFISANGO..


R.I.P Patrick Mafisango. What a Loss, you were a very good player for Simba, it is very sad.

PATRICK MAFISANGO KUAGWA KESHO LEADERS CLUB ASUBUHI

Hatimaye kesho wapenzi wa soka nchini watapata kuuaga mwili wa marehemu Patrick Mafisango aliyefariki leo alfajiri wakati akitoka klabu na wenzie wanne, ataagwa kesho asubuhi katika viwanja vya leaders club kinondoni - jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa meneja wa Simba Nico Nyagawa - Mwili wa Mafisango baada ya kuagwa utaondoka na kusafirishwa na ndege ya shirika la KQ kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya mazishi.

Nyagawa amewaomba wapenzi wote wa Simba na soka kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kumuaga kipenzi chao, mchezaji ambaye enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa katika kuisadia Simba kupata mafanikio waliyoyapata msimu huu.


Mafisango aliyekuja nchini mwaka juzi na kujiunga na Azam kabla ya kuhamia Simba mwaka jana, alizaliwa Machi 7, mwaka 1987 mjini Kinshasa, DRC alikoanzia soka kabla ya kuhamia Rwanda, ambako baadaye alichukua uraia wa nchi hiyo.

Kabla ya kuja Tanzania alichezea APR ya Rwanda. Mechi ya mwisho Mafisango kuichezea Simba ilikuwa dhidi ya Al Ahly Shandy nchini Sudan Jumapili katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya jumla ya 3-3.

Hadi anafariki dunia, Mafisango alikuwa ni tegemeo Simba katika safu ya kiungo na jana tu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nange 'Kaburu' alisema kiungo huyo yupo kwenye mpango wa kocha wa kikosi cha msimu ujao. 

Pamoja na kucheza kama kiungo, Mafisango pia anamudu kucheza nafasi ya beki wa kushoto na beki wa kati.

Japokuwa alikuwa kiungo, lakini pia alikuwa hodari wa kufunga mabao na msimu huu imeshuhudiwa akiifungia Simba mabao 11 katika Ligi Kuu na manne kwenye Kombe la Shirikisho.

HII NDIO GARI ILIYOCHUKUA UHAI WA KIPENZI CHETU MAFISANGO - WENZAKE WANNE WANASURIKA

Ndugu yake Mafisango aliekua nae wakati wa ajali amesema Mafisango alifariki dunia hapohapo kwenye ajali wakati wakitoka Club kuelekea nyumbani, walipofika kwenye taa za barabarani Tazara Dar es salaam, Mafisango ambae ndio alikua anaendesha alijaribu kuziwahi taa lakini ghafla akakutana na mwendesha guta ambapo katika kumkwepa gari ilimshinda na kuingia mtaroni leo Alfajiri.
 
Alikua na wenzake watano kwenye gari ambapo wengine wanne wamepona japoa walipata majeraha madogo madogo akiwemo mdogo wake ambae amesajiliwa na club ya Simba.
 
Haruna Niyonzima mchezaji wa Yanga alikua mchezaji wa mwisho kubadilishana jezi na Mafisango Tanzania, katika mechi ambayo Mafisango alifunga goli lake la mwisho.
 
Anasema Ijumaa ndio Mafisango alimwambia atasafiri kwenda Rwanda kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, hili ni pigo kwa Tanzania, Rwanda na hata Congo DRC.

HILI NDILO GOLI LA MWISHO LA MAFISANGO KABLA YA KUFA - RIP MUTESA

BREAKING NEWS: PATRICK MAFISANGO AFARIKI DUNIA KWA AJALI

Amini usiamini Patrick Mafisango Mutesa hatunae tena duniani. Habari nilizozipata zinasema kiungo huyo wa Simba amepata ajali ya ajali maeneno ya Tazara wakati akijaribu kumkwepa mwenye pikipiki na kwa bahati mbaya gari lake likakosa balance na kuingia mtaroni na hapo ndipo alipopeteza maisha.


Kwa taarifa zaidi endelea kutembea www.shaffihdauda.com

SIMBA KUWAPUMZISHA BAADHI YA WACHEZAJI KWENYE KAGAME

SIMBA imesema itatumia michuano ya Kombe la Kagame kupumzisha baadhi ya wachezaji
wake waliotumika sana kwenye michuano mbalimbali msimu huu.

Michuano ya Kombe la Kagame inatarajiwa kuanza kutimua vumbi jijini Dar es Salaam Juni 13, ambapo Tanzania itawakilishwa na Simba, Yanga na Azam.


Akizungumza jijini jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kikosi chake kiko imara na kwamba watatumia michuano hiyo kuwapumzisha nyota wake na nafasi zao zitachukuliwa na wale ambao hawakupata nafasi msimu huu.


“Sisi tuko sawasawa, tutashiriki michuano ya Kombe la Kagame na tutatumia sana wachezaji wetu wapya tunaowasajili pamoja na wale ambao hawakupata nafasi msimu huu, unajua kuna wachezaji wametumika sana safari hii,” alisema.


Simba ambayo ilikuwa mwakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa,

mwishoni mwa wiki ilishindwa kufurukuta mbele ya Al Ahly Shendi ya Sudan baada ya
kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho kwa mikwaju ya penati 9-8.

“Tumeondolewa shirikisho tunaelekeza nguvu kwenye Kagame tutashiriki, tunaiheshimu

sana michuano hiyo na tutaitumia kuwapa nafasi wachezaji wapya pamoja na wale ambao walikuwa hawapati nafasi, unajua kuna wachezaji walitumika sana.

“Hivyo wachezaji wote wako sawa na tunajiandaa kufanya maandalizi ya Kombe la Kagame ambalo tunaamini tutafanya vizuri,”alisema Kamwaga.


Simba mwaka jana ilicheza fainali za michuano ya Kombe la Kagame ambapo ilishindwa

kumtambia mtani wake wa jadi Yanga baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika muda wa
nyongeza baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa hazijafungana.

YANGA KWAZIDI KUCHAFUKA: MINZIRO NAIDAI YANGA MSHAHARA WA MIEZI MINNE

Kocha  msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro amesema hataifundisha timu hiyo inayojiandaa kutetea taji la michuano ya Kombe la Kagame kama uongozi wa klabu hiyo hautamlipa malimbizo yake ya mishahara ya miezi minne.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Minziro alisema hajalipwa mishahara tangu mwezi Februari na juhudi zake za kudai hazionyeshi matumaini kutokana na kutopata jibu la kuridhisha.
Minziro alisema majibu anayopata ni ya kukatisha tamaa na pamoja na uongozi kutangaza kuwa atasimamia mazoezi kwa ajili ya kombe la Kagame.
Kocha huyo, alisema pamoja na mapenzi makubwa aliyonayo kwenye klabu hiyo, hatakuwa tayari kuendelea kufanya kazi katika mazingira magumu ya kutolipwa mshahara.“Uzalendo umenishinda, binadamu wa kawaida hawezi kuishi maisha ya bila mshahara na hakuna matarajio ya kupata fedha hizo kutokana na hali halisi ya klabu hiyo,” alisema Minziro.
Alisema kuwa alipata matumaini ya kulipwa fedha zao mara baada ya mechi ya Zamalek, lakini wakapewa hadithi na baadaye akaambiwa atalipwa baada ya mchezo dhidi ya Simba, lakini mpaka sasa hajalipwa.
“Hali hii ni ya muda mrefu, benchi lote la ufundi tunadai mishahara ya miezi mitatu. Kukosekana pesa kwa wakati kumechangia kwa kiasi kikubwa kushusha morali ya wachezaji na hata sisi wenyewe,” alisema.
Alisema pia anashangaa kuona tangu ligi ilipomalizika hakuna kikao chochote cha kufanya tathmini kilichofanyika ikiwemo maandalizi ya usajili wakati yeye sasa ndiye Mkuu wa Benchi la Ufundi.
Kocha huyo alisema mbali na mishahara yake ya miezi minne, pia anadai posho za mechi 15 na kuweka wazi kwamba kila mechi hulipwa Sh. 100,000.
Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo na kusema ni masuala binafsi ya makocha hao.

Wednesday, May 16, 2012

DENILSON - MCHAWI WA CHENGA ALIYEPATA KUTOKEA KWENYE SOKA

NIPO NJIANI KUELEKEA JIJINI MUNICH KUANGALIA FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE

Nikiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuelekea jijini Munich Ujerumani kupita Dubai kwa ajili ya kuwaletea coverage ya live kutoka Allianz Arena kwenye mtanange wa fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya kati ya Chelsea na Bayern Munich. Endelea kuwa nami kwa uhondo zaidi.
Allianz Arena Dressing Room

BREAKING NEWS: KING KENNY DALGLISH ATIMULIWA LIVERPOOL

Masaa machache baada ya kutoka Marekani kuzungumza na wamiliki wa klabu ya Liverpool, leo kocha King Kenny Dalglish ametimuliwa kazi ya ukocha pale Anfield.

Kenny Dalglish anaondoka Liverpool miezi 16 baada ya kuichukua timu hiyo baada ya kuondoka kwa kocha Roy Hodgson mwezi January 2011. Dalglish ambaye ameiongoza Liverpool kubeba kombe la Carling Cup msimu huu kabla hawajafungwa na kwenye fainali ya FA Cup dhidi ya Chelsea.

Lakini kushika nafasi ya nane kwenye premier league kulikuwa chini ya mategemeo ya wamiliki waliotumia kiasi kingi cha pesa wakitegemea angalau kupata nafasi ya kushiriki kwenye ligi ya mabingwa ya ulaya.


EXCLUSIVE: KELVIN YONDAN AONGEZA MKATABA WA MIAKA 2 KUICHEZEA SIMBA - AWAKANA YANGA

Siku moja baada ya kutua Tanzania akitokea Sudan na klabu yake ya Simba katika michuano ya kombe la shirikisho na kuzuka kwa habari kwamba amejiunga na klabu Yanga, Kelvin Yondani ameongea exclusively na www.shaffihdauda.com na kukanusha taarifa kwamba anahamia mitaa ya jangwani kutoka Msimbazi.

Kelvin ambaye mwaka jana pia alikuwa akihusishwa na taarifa za kujiunga na Yanga amesema yeye bado ni mchezaji halali wa mabingwa wa Tanzania na ataendelea kuwepo Msimbazi kwa misimu miwili zaidi, "Jana nilivyorudi kutoka Sudan nimekuwa nikipokea simu nyingi za waandishi wakiulizia ukweli juu ya taarifa za kujiunga na Yanga lakini sikuwa nimepata wakati mzuri wa kuwajibu. Leo kupitia www.shaffihdauda.com natangaza rasmi kwamba mie ni mchezaji wa na nitakuwa hivyo kwa misimu miwili ijayo kwa sababu nimeongeza mkataba wa kuitumikia klabu yangu kwa miaka zaidi. Hivyo hizo taarifa si za kweli mie bado nipo kwenye winning team."

EXCLUSIVE: NIZAR KHALFAN _ SIJASAINI YANGA WALA PENGINE POPOTE ACHENI KUZUSHA

Siku mbili baada ya magazeti na baadhi ya vyombo vya habari kueneza story kwamba kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar ambaye alikuwa nje akicheza Vancouver Whitecaps kabla ya kuhamia Philadephia - Nizar Khalfan kwamba amesaini miaka 2 kuichezea Yanga, leo nimeongea na Nizar mwenyewe ambaye amekana kutia saini ya aina yoyote na klabu ya jangwani.
"Kiukweli nimesikitishwa sana na hizi taarifa kwamba sijui nimesaini kuichezea Yanga kwa sababu ni mambo ambayo hayana ukweli kabisa. Mwanzoni ilisemekana nimesaini Simba lakini haikuwa ukweli, sikatai nimeshafuatwa na baadhi ya timu hapa Tanzania nijiunge nazo lakini na mimi naangalia vigezo vyangu ndipo nitakapochukua maamuzi. Lengo langu ni bado niende nikacheze nje ya nchi katika soka la kulipwa, hivyo hata kama ikitokea nimejiunga na timu yoyote ni lazima mkataba uwe wa muda mfupi ambao utakuwa na vipengele ambavyo havitakuwa na vikwazo vinavyoweza kunifanya nisitimize malengo yangu ya kwenda kucheza nje. Hali halisi kwa sasa ipo hivyo, sina timu kwa sasa hata mazoezi nafanya pale muhimbili na timu ya Binslum." - alisema Nizar Khalfan

STEVEN GERRARD NAHODHA MPYA WA ENGLAND


ZANTEL YATOA SIMU 75 KWA MANISPAA YA ILALA

Afisa Mkuu wa Biashara wa Zantel Ahmed Mokhles (kushoto) akikabidhi Meya wa Ilala Mhe. Jerry Slaa moja ya simu 75 zilizotolewa na kampuni ya Zantel kuisaidia Manispaa ya Ilala kurahisisha mawasiliano kati ya madiwani na watendajikazi wote wa manispaa. Makabidhiano haya yalifanyika ofisini kwa Meya jijini Dar es Salaam.

KIKOSI CHA ENGLAND EURO: RIO FERDINAND ATOSWA: CARROLL NA CHAMBERLAIN NDANI

Joe Hart gives instructions during the International Friendly match between England and the Netherlands at Wembley
Joe Hart (Manchester City)

England squad:

Goalkeepers: Joe Hart (Man City), Rob Green (West Ham), John Ruddy (Norwich)

Defenders: Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Man Utd), John Terry (Chelsea), Joleon Lescott (Man City), Gary Cahill (Chelsea), Ashley Cole (Chelsea), Leighton Baines (Everton)

Midfielders: Theo Walcott (Arsenal), Stewart Downing (Liverpool), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Steven Gerrard (Liverpool), Gareth Barry (Man City), Frank Lampard (Chelsea), Scott Parker (Tottenham), Ashley Young (Man Utd), James Milner (Man City)

Forwards: Jermain Defoe (Tottenham), Wayne Rooney (Man Utd), Danny Welbeck (Man Utd), Andy Carroll (Liverpool)

Robert Green in action for England
Robert Green (West Ham)

Getty

John Ruddy
John Ruddy ()Norwich)

Getty

Glen Johnson prepares to take a throw in during the international friendly match between England and Spain at Wembley
Glen Johnson (Liverpool)

Getty

Ashley Cole in action for England
Ashley Cole (Chelsea)

Getty

Phil Jones in action for England
Phil Jones (Manchester United)

Getty

Gary Cahill in action for England
Gary Cahill (Chelsea)

Getty

John Terry in action for England
John Terry (Chelsea)

Getty

Joleon Lescott of England in action
Joleon Lescott (Manchester City)

Getty

Leighton Baines in action for England
Leighton Baines (Everton)

Getty

Frank Lampard
Frank Lampard (Chelsea)

Mirror

Gareth Barry in action for England
Gareth Barry (Manchester City)

Action

Steve Gerrard in action for England
Steven Gerrard (Liverpool)

Getty

Scott Parker in action for England
Scott Parker (Tottenham)

Getty

James Milner in action for England
James Milner (Manchester City)

Getty

Ashley Young in action for England
Ashley Young (Manchester United)

Getty

Theo Walcott in action for England
Theo Walcott (Arsenal)

Getty

Stewart Downing of England
Stewart Downing (Liverpool)
Alex Oxlade-Chamberlain in action for the Under 21s
Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal)

Getty

Jermain Defoe in action for England
Jermain Defoe (Tottenham)

Getty

Andy Carroll in action for England
Andy Carroll (Liverpool)

Getty

Wayne Rooney in action for England
Wayne Rooney (Manchester United)

Getty

Danny Welbeck in action for England
Daniel Welbeck (England)