Search This Blog

Thursday, May 17, 2012

SIMBA KUWAPUMZISHA BAADHI YA WACHEZAJI KWENYE KAGAME

SIMBA imesema itatumia michuano ya Kombe la Kagame kupumzisha baadhi ya wachezaji
wake waliotumika sana kwenye michuano mbalimbali msimu huu.

Michuano ya Kombe la Kagame inatarajiwa kuanza kutimua vumbi jijini Dar es Salaam Juni 13, ambapo Tanzania itawakilishwa na Simba, Yanga na Azam.


Akizungumza jijini jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kikosi chake kiko imara na kwamba watatumia michuano hiyo kuwapumzisha nyota wake na nafasi zao zitachukuliwa na wale ambao hawakupata nafasi msimu huu.


“Sisi tuko sawasawa, tutashiriki michuano ya Kombe la Kagame na tutatumia sana wachezaji wetu wapya tunaowasajili pamoja na wale ambao hawakupata nafasi msimu huu, unajua kuna wachezaji wametumika sana safari hii,” alisema.


Simba ambayo ilikuwa mwakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa,

mwishoni mwa wiki ilishindwa kufurukuta mbele ya Al Ahly Shendi ya Sudan baada ya
kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho kwa mikwaju ya penati 9-8.

“Tumeondolewa shirikisho tunaelekeza nguvu kwenye Kagame tutashiriki, tunaiheshimu

sana michuano hiyo na tutaitumia kuwapa nafasi wachezaji wapya pamoja na wale ambao walikuwa hawapati nafasi, unajua kuna wachezaji walitumika sana.

“Hivyo wachezaji wote wako sawa na tunajiandaa kufanya maandalizi ya Kombe la Kagame ambalo tunaamini tutafanya vizuri,”alisema Kamwaga.


Simba mwaka jana ilicheza fainali za michuano ya Kombe la Kagame ambapo ilishindwa

kumtambia mtani wake wa jadi Yanga baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika muda wa
nyongeza baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa hazijafungana.

3 comments:

  1. kwa hilo simba mmeona mbele sana,na soka liko hivyo!

    ReplyDelete
  2. simba wamecheza mechi za kimashindano ambazo hazidi 30,collect me if am wrong...leo unasema unataka kuwapumzisha wachezaji kweli hi ni sahihi?tutaweza kweli kucheza ulaya kama mechi 22 za ligi na 6 za kimataifa wachezaji wanachoka?

    ReplyDelete
  3. Jamani mafisangoooooooooooooooooooooooooooo, rest in peace brother, tulikupenda sana, lakini mungu kakupenda zaidi,hata simba tulikutegemea sana kaka. MUNGUailaze mahali pema peponi roho yako

    ReplyDelete